The Book of Common Prayer
United States England Scotland Ireland Wales Canada World

    Kitabu cha Sala za Kanuni (1918)
The Zanzibar Book of Common Prayer in Swahili

 

SALA ZA SIKUKUU ZA WATAKATIFU

Nov. 29.   Mkesha wa Andrea, Mtume.

Yote ya Siku ya Kazi, isipokuwa, SALA 1. Bali Wakati wa Majilio isemwe sala ya siku ya kazi ya Majilio.
 

Prayers for Saints' Days

Vigil of St. Andrew

Nov. 30.   Andrea, Mtume. 2

Kawaida ya Mtume

Sala

Mwenyezi Mungu, ulimpa neema Andrea, Mtume wako Mtakatifu, asiwe na shaka wala kukawia alipoitwa na Mwana wako Yesu Kristo: Utujalie sisi sote, tunaoitwa kwa Neno lako takatifu; tujitoe nafsi zetu mara, na kuzifuata amri zako takatifu. Kwa Yeye.
 

St. Andrew

Des. 3.   Fransisi Zavieri, K. Mu. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 54.

Sala

Mwenyezi Mungu, ulipenda kuliongezea Kanisa lako watu wa Bara Hindi kwa mahubiri ya Fransisi Zavieri Mbarikiwa na kwa miujiza yake: Utujalie kwa rehema; sisi tunaomheshimu kwa ajili ya kazi yake, tuifuatishe tabia yake njema. Kwa.
 

Francis Xavier

Des. 4.   Klementi wa Iskanderia, K. Mu. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 54.

Sala

Mwenyezi Mungu, umelifundisha Kanisa lako mwenendo mtakatifu kwa elimu ya Klementi Mbarikiwa wa Iskanderia: Utujalie, tunakuomba; huko mbinguni atuombee sisi tunaomfuatisha yeye hapa duniani. Kwa.
 

Clement of Alexandria

Des. 6.   Nikolao, A. Mu. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 51.   SALA 7.
 

Nicholas

Des. 7.   Ambrosio, A. Mw. 3

Kawaida ya Mtakatifu

Q.   WIMBO 53.

Sala

Ee Mungu, ulimweka Ambrosio, Askofu, katika Kanisa lako awe mlinzi wa Imani Katholiko, na Shujaa mwenye nguvu kwa mfano wa Mitume: Tunakusihi tusaidiwe leo kwa sala zake; ili tuziepuke hatari za uzushi, wala tusione haya kwa ajili ya Dini yetu iliyo kweli. Kwa.
 

Ambrose

Des. 8.   Kuchukuliwa Mimba kwa Mariamu B. Mb. 1

Kawaida ya Mariamu Mb. isipokuwa,

Sala

Bwana Mungu, tunakuomba: Utujalie tuifurahie afya ya mwili na ya roho; ili, kwa msaada wa sala za Mariamu Mbarikiwa, Bikira Mtukufu wa daima, tuokoke katika huzuni ya dunia hii na kuifikia furaha ya milele. Kwa.
 

Immaculate Conception

Des. 13.   Luchia, B. Sh. 3

Kawaida ya Mtakatifu  

WIMBO 56.

Sala

Mwenyezi Mungu, uliye Wokovu wetu: Utusikie sisi tunaoifurahia Sikukuu hii ya Luchia, Bikira na Shahidi wako; tuwe na moyo katika Dini yetu takatifu, tuka zidi kukamilika. Kwa.
 

Lucy

Des. 20.   Mkesha wa Tomaso, Mtume

Yote ya Siku ya Kazi, Wakati wa Majilio
 

Vigil of St. Thomas

Des. 21.   Tomaso, Mtume. 2

Kawaida ya Mtume

ANT. MAG. Antifona kuu.

Sala

Mwenyezi Mungu, wa milele, ulikubali Mtume wako Mtakatifu, Tomaso, aingiwe na shaka kwa habari ya kufufuka kwake Mwana wako, ili kusudi imani yetu izidi kuthibitika: Utujalie sisi tumwamini Mwana wako Yesu Kristo pasipo shaka; imani yetu mbele zako isilaumiwe. Kwa Yeye.
 

St. Thomas

Jan. 9.   Adriano, Mtauwa

Ukumbusho tu

SALA 11.
 

Adrian (of Canterbury)

Jan. 14.   Hilario, A. Mw. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 52.   SALA 8.
 

Hilary (of Poitiers)

Jan. 17.   Antonio, Mtauwa. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 55.   SALA 11.
 

Anthony (of Egypt)

Jan. 18.   Priska, B. Sh. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 56.

Sala

Mwenyezi Mungu, tunashangilia kushinda kwake Priska Mtakatifu, Bikira na Shahidi wako: Utujalie, tunakusihi; tuifurahie Sikukuu yake, na kuufuatisha wingi wa imani yake. Kwa.
 

 
Prisca

Jan. 20.   Fabiano na Sebastiano, Mash. 3

Kawaida ya Mtakatifu

NYIMBO 48, 49.

Sala

Mwenyezi Mungu, uuangalie udhaifu wetu: Tulindwe kwa maombezi yao Fabiano na Sebastiano, Mashahidi wako Wabarikiwa; kwa maana tunalemewa na mzigo wa makosa yetu. Kwa.
 

 
Fabian & Sebastian

Jan. 21.   Agnese, B. Sh. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 56.

Sala

Mwenyezi Mungu wa milele, umewachagua walio dhaifu wa dunia hii ili wenye nguvu watahayarike: Utujalie, tunakusihi; tumwadhimishe Agnese Mbarikiwa, Bikira na Shahidi wako, na kuuona msaada wa sala zake. Kwa.
 

Agnes

Jan. 22.   Vinsenti, Shem. Sh. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 46.   SALA 3.
 

Vioncent (of Saragossa)

Jan. 24.   Timotheo, A. Sh. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 46.

Sala

Ee Mungu, ulimchagua Timotheo Mtakatifu awe Mtenda kazi mashuhuri, na Mhudumu mwema wa Yesu Kristo: Utujalie, tunakuomba, tuzifuate nyayo zake; ili tuzishike amri zako takatifu, na kuupata uzima wa milele. Kwa Yeye.
 

Timothy

Jan. 25.   Kuongoka kwa Paulo. Mtume. 2

Kawaida ya Mtume

WIMBO 58.

Sala

Ee Mungu, uliuletea ulimwengu wote nuru ya Injili kwa mahubiri yake Paulo, Mtume wako Mbarikiwa : Utupe sisi, tunakusihi, tukushangilie kuongoka kwake kwa ajabu; na kuonyesha shukrani yetu kwa kuyafuata mafundisho yake. Kwa.
 

Conversion of St. Paul

Jan. 26.   Polikapo, A. Sh. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 46.

Sala

Ee Bwana, uyafikilize maombi yetu: Utupokee kama kafara mbele zako; pamoja na Polikapo Mtakatifu, Shahidi wako na Askofu, ambaye tunamkumbuka leo kwa heshima na utukufu wako. Kwa.
 

Polycarp

Jan. 27.   Yohana Krisostomo, A. Mw. 3

Kawaida ya Mtakatifu

Q.   WIMBO 53.

Sala

Ee Bwana, Yohana Krisostomo, Mtakatifu wako, hakuacha kuwaonya wenye dhambi, bali alishinda taabu zake nyingi kwa ajili ya kulipenda Jina lako: Tunakusihi kwa unyenyekevu; uwajalie wote wanaohudumia mambo matakatifu wapewe roho ya akili na moyo thabiti. Kwa.
 

John Chrysostom

Jan. 29.   Fransisi wa Sale, A. Mw. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 52.   SALA 8.
 

Francis de Sales

Feb. 1.   Ignatio, A. Sh. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 46.   SALA 2.
 

Ignatius (of Antioch)

Feb. 2.   Kutakaswa kwa Mariamu B. Mb. 2

Kawaida ya Mariamu Mb. isipokuwa,

Sala

Mwenyezi Mungu wa milele, tunaisihi Enzi yako ya Uungu: Utujalie tusafishwe mioyo na kuletwa mbele zako; kama vile Mwana wako pekee alivyoletwa hekaluni kwako, mwenye utu wetu. Kwa Yeye.
 

Purification of Mary

Feb. 3.   Blasio, A. Sh. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 46.   SALA 2.
 

Blaise

Feb. 5.   Agatha, B. Sh. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 56.   SALA 12.
 

Agatha

Feb. 6.   Tito, A. Mu. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 51.

Sala

Ee Mungu, ulimpamba Tito Mtakatifu, Mwungamaji wako na Askofu, karama za utume: Utujalie, tunakuomba; tumfuate katika mwenendo wa haki na utauwa, na kukufikia kwetu mbinguni. Kwa.
 

Titus

Feb. 9.   Sirili wa Iskanderia, A. Mw. 3

Kawaida ya Mtakatifu

Q.   WIMBO 52.   SALA 8.
 

Cyril of Alexandria

Feb. 10.   Skolastika, B. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 56.   SALA 13.
 

Scholastica

Feb. 14.   Valentino, K. Sh. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 46.   SALA 3.
 

Valentine

Feb.23 (au 24).   Mkesha wa Mathiya, Mtume

Yote ya Siku ya Kazi, isipokuwa, SALA 1. Bali Wakati wa Kwaresima isemwe sala ya siku ya kazi ya Kwaresima.
 

Vigil of St. Matthias

Feb. 24 (au 25).   Mathiya, Mtume. 2

Kawaida ya Mtume

Sala

Mwenyezi Mungu, ulimchagua Mathiya, mtumishi wako amini, mahali pa Yuda haini, ahesabiwe katika jamaa ya Mitume: Ulijalie Kanisa lako lisiwe na mitume wa uongo; bali liongozwe na wachungaji wa kweli na uaminifu. Kwa.
 

St. Matthias

Ma. 1.   Daudi, A. Mu. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 51.   SALA 7.
 

David

Ma. 2.   Chadi, A. Mu. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 51.   SALA 7.
 

Chad

Ma. 6.   Pepetua na Wenzake, Mash. 3

Kawaida ya Mtakatifu

NYIMBO 48, 49.   SALA 4.
 

Perpetua & her Companions

Ma. 7.   Tomaso wa Akwino, K. Mw. 3

Kawaida ya Mtakatifu

Q.   WIMBO 53.

Sala

Ee Mungu, uliangaza Kanisa lako kwa hekima ya ajabu aliyopewa Tomaso wa Akwino, Mwalimu mkuu wako: Utujalie, tunakusihi; tuyafahamu yale aliyotufundisha, na kuufuatisha mwenendo wake safi. Kwa.
 

Thomas Aquinas

Ma. 9.   Gregorio wa Nisa, A. Mu. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 51.   SALA 7.
 

Gregory of Nyssa

Ma. 12.   Gregorio wa Rumi, A. Mw. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 53.   SALA 9.
 

Gregory of Rome (the Great)

Ma. 17.   Patriki, A. Mu. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 51.

Sala

Ee Mungu, ulimweka Patriki Mtakatifu, Mwungamaji wako na Askofu, ili awahubiri mataifa utukufu wako: Utujalie kusaidiwa kwa maombi yake; na kwa huruma zako utuwezeshe kuyatenda yote uliyotuagiza. Kwa.
 

Patrick

Ma. 18.   Sirili wa Yerusalemu, A. Mw. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 53.   SALA 9.
 

Cyril of Jerusalem

Ma. 19.   Yusufu, Mtunza Bwana wetu, Mu. 1

Sala ya Jioni (ya 1 na ya 2)

    ANT. ZAB. Malaika wa Bwana alimtokea Yusufu, akisema, Yusufu, Mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo.
    ZABURI. Sehemu C.
    WIMBO 59.

Sala

Ee Bwana, tunakuomba: Utusikilize sisi tunaomfurahia Yusufu Mtakatifu aliyemposa Mama Mbarikiwa wa Mwana wako Yesu Kristo; ili tumfuatishe nia yake ya kujinyima, na kusaidiwa kwa sala zake. Kwa Yeye.

Sala ya Asubuhi

    ANT. ZAB. Yesu alishuka pamoja nao mpaka Nazareti, Naye alikuwa akiwatii.
    WIMBO 59.

Sala ya Adhuhuri

    SOMO. Mtu aliyependwa na Mungu na watu kumbukumbu lake li heri. Mungu alimtukuza katika uaminifu wake na upole wake, akamchagua kuliko wanadamu wote pia.
    R. Tumshukuru Mungu.
    V. Utukufu wake ni mkuu kwa wokovu wako.
    R. Utukufu wake ni mkuu kwa wokovu wako.
    V. Heshima na adhama waweka juu yake.
    R. Kwa wokovu wako.
    V. Atukuzwe, etc.
    R. Utukufu wake ni mkuu kwa wokovu wako.
    V. Mwenye haki atachanua kama nyinyoro,
    R. Atasitawi mbele za BWANA milele.

WAKATI WA PASAKA

ANT. ZAB. Haleluya, Haleluya, Haleluya.

Sala ya Adhuhuri

    Ubeti wa mwisho wa Wimbo

Ahimidiwe Mungu Baba,
    Na Mwana mwenye kufufuka,
Na Roho Mfariji naye,
    Zamani, leo, na milele. Amin.

VIITIKIO hivi,
V. Utukufu wake ni mkuu kwa wokovu wako. Haleluya. Haleluya.
R. Utukufu wake ni mkuu kwa wokovu wako. Haleluya. Haleluya.
V. Heshima na adhama waweka juu yake.
R. Haleluya. Haleluya.
V. Atukuzwe, etc.
R. Utukufu wake ni mkuu kwa wokovu wako. Haleluya. Haleluya.
V. Mwenye haki atachanua kama nyinyoro. Haleluya.
R. Atasitawi mbele za BWANA milele. Haleluya.
 

Joseph, Protector of our Lord

Ma. 20.   Kuthbeti, A. Mu. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 51.   SALA 7.
 

Cuthbert (of Lindisfarne)

Ma. 21.   Benedikto, Mtauwa. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 55.   SALA 11.
 

Benedict (of Nursia)

Ma. 24.   Gabrieli, Malaika Mkuu. 3

Kawaida ya Malaika

WIMBO 69.

Sala

Ee Mungu, ulimchagua Gabrieli, Malaika Mkuu Mbarikiwa, aihubiri siri ya Kutwaa mwili kwake Mwana wako Mpendwa: Utujalie, tunakusihi; tuifurahie Sikukuu yake, na kusaidiwa kwa ulinzi wake. Kwa Yeye.
 

The Angel Gabriel

Ma. 25.   Kuhubiriwa kwa Mariamu B. Mb. 1

Kawaida ya Mariamu Mb. isipokuwa,

Sala

Ee Mungu, ulipenda Neno lako atwae mwili katika tumbo la Mariamu Bikira Mbarikiwa, na kuhubiriwa na Malaika: Utujalie tuzidi kumwamini mama yake kuwa ni mama yake aliye Mungu; na kusaidiwa kwa sala zake. Kwa Yeye.
 

Annuniciation to Mary

Ma. 27.   Yohana wa Dameski, K. Mw. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 53.   SALA 9.
 

John of Damascus

Apr. 11.   Leo, A. Mw. 3

Kawaida ya Mtakatifu

Q.   WIMBO 52.

Sala

Ee Mungu, ulimwinua Leo Mtakatifu, Askofu wako, ili awazuie adui za kweli yako kwa maneno na matendo yake: Utujalie kuongozwa kwa nuru ya maandiko yake; ili na sisi tuendelee kwa amani katika njia aliyotuonyesha. Kwa.
 

Leo

Apr. 14.   Yustino, Sh. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 47.

Sala

Ee Mungu, ulimfundisha kwa ajabu Yustino, Shahidi wako, ya kwamba upumbavu wa Msalaba ni hekima yako: Utujalie msaada wa kuombewa naye; ili tujitenge na mazunguko ya kukisia, na kuyafuata yaliyo kweli kwa nia moja. Kwa.
 

Justin (Martyr)

Apr. 21.   Anselmu, A. Mw. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 52.   SALA 8.
 

Anselm

Apr. 23.   George, Sh. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 47.   SALA 3.
 

 

Apr. 24.   Mnyang'anyi mwenye toba. 3

(aitwaye Dismas)
Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 60.

Sala

Mwenyezi Mungu, mwenye rehema, ulimvuta mnyang'anyi mmoja wa Kalvari akuangukie: Tunakuomba ututubishe na sisi tulio wenye dhambi; ukatulete kwenye utukufu alioahidiwa msalabani na Mwana wako pekee. Kwa Yeye.
 

The penitent Robber

(formerly called Dismas)

Apr. 25.   Marko, Mtunga Injili 2

Kawaida ya Mtume, Wakati wa Pasaka

Sala

Mwenyezi Mungu, ulilifundisha Kanisa lako takatifu kwa elimu ya mbinguni ya Mtunga Injili wako, Marko Mtakatifu: Utujalie tusichukuliwe, kama watoto, kwa kila upepo wa elimu isiyofaa; bali tukae imara katika kweli ya Injili yako takatifu. Kwa.
 

St. Mark

Apr.30.   Katharina wa Siena, B. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 56.   SALA 13.
 

Catherine of Siena

Mei. 1.   Filipo na Yakobo bin Alfayo, Mitume, 2

Kawaida ya Mtume, Wakati wa Pasaka

Sala

Mwenyezi Mungu watufurahisha kila mwaka kwa Sikukuu ya Filipo na Yakobo, Mitume wako Watakatifu: Utufundishe tumjue Mwana wako kuwa ni njia, na kweli, na uzima; ili tuzifuate nyayo zao, na kuenenda kwa furaha hata uzima wa milele. Kwa Yeye.
 

St. Philip & St. James

Mei. 2.   Athanasio, A. Mw. 3

Kawaida ya Mtakatifu

Q.   WIMBO 52.

Sala

Mwenyezi Mungu wa milele, ulimwita Athanasio Mtakatifu ili apigane kwa ushujaa na adui za kweli yako: Tunakusihi utuondolee shaka zote za moyoni; ili tumjue Yesu Kristo uliyemtuma, na kwa kumwamini tuwe na uzima wa milele. Kwa Yeye.
 

Athanasius (of Alexandria)

Mei. 4.   Monika, Mjane. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 57.

Sala

Ee Mungu, Mfariji wao wenye huzuni, Mwokozi wao wakutumainio: Ulikubali machozi yake Monika Mtakatifu, aliyotoka kwa ajili ya mwanawe Agostino ili aongoke; utujalie na sisi tujililie dhambi zetu, na kukugeukia kwa mioyo yetu yote. Kwa.
 

Monnica

Mei. 6.   Kushinda kwake Yohana, Mtume. 3

ANT. ZAB. Haleluya, Haleluya, Haleluya.
ZABURI za kawaida.
WIMBO 45.

Sala

Ee Mungu, unatuona tuna songwa na mabaya mengi sana: Ututazame tunapoishangilia Sikukuu ya kushinda kwake Yohana, Mtume Mbarikiwa; utuokoe na maovu yote, huku tukisaidiwa kwa sala zake. Kwa.

Sala ya Adhuhuri

Kama Kawaida ya Mtume, Wakati wa Pasaka
 

St. John before the Latin Gate

Mei. 9.   Gregorio wa Nazianzum, A. Mw. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 52.   SALA 8
 

Gregory of Nazianzus

Mei. 26.   Agostino wa Canterbury, A. Mu. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 51.

Sala

Ee Mungu, uliwapa Waingereza nuru ya Imani ya kweli kwa mahubiri yake Agostino wa Canterbury, Mwungamaji wako na Askofu: Utuunganishe daima katika umoja wa Imani hii; ili tuyatimize mapenzi yako, Kwa.
 

Augustine of Canterbury

Mei. 27.   Beda, K. Mw. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 53.   SALA 9.
 

Bede (the Venerable)

Mei. 30.   Yoana, B. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 56.   SALA 13.
 

Joanna

Mei. 31.   Anjela, B. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 56.   SALA 13.
 

Angela (Merici, founder of the Urselines)

Jun.2.   Blandina na Wenzake, Mash. 3

Kawaida ya Mtakatifu

NYIMBO 48, 49.   SALA 4.

Wakati wa Pasaka, WIMBO 50.
 

Blandina & her Companions (Martyrs of Lyons)

Jun. 3.   Mashahidi wa Uganda. 3

Kawaida ya Mtakatifu

NYIMBO 48, 49.   SALA 4.

Wakati wa Pasaka, WIMBO 50.
 

Martyrs of Uganda

Jun. 5.   Bonifasio, A. Sh. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 46.   SALA 2.

Wakati wa Pasaka, WIMBO 47.
 

Boniface (of Mainz)

Jun. 9.   Kolumba, Mtauwa. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 55.   SALA 11.
 

Columba

Jun. 10.   Magarita, Mjane. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 57.   SALA 15.
 

Margaret (of Scotland)

Jun. 11.   Barnaba, Mtume. 2

Kawaida ya Mtume

Sala

Bwana Mungu Mwenyezi, ulimpamba Mtume wako Mbarikiwa, Barnaba, kwa karama kubwa za Roho Mtakatifu: Tunakusihi, usitunyime karama zako nyingi; wala neema ya kuzitumia kwa heshima na utukufu wako. Kwa Bwana wetu Yesu Kristo Mwana wako; Aishiye na kumiliki pamoja nawe, katika umoja wake Yeye huyo Roho Mtakatifu, Mungu daima milele na milele. Amin.
 

St. Barnabas

Jun. 13.   Antonio wa Padua, K. Mu. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 54.   SALA 10.
 

Anthony of Padua

Jun. 14.   Basileo, A. Mw. 3

Kawaida ya Mtakatifu

Q.   WIMBO 52.

Sala

Ee Bwana, tunamshangilia Basileo Mtakatifu, Mwalimu wako mashuhuri: Uiamshe katika Kanisa lako roho ile ya hekima aliyokuwa nayo; ili sisi tuelimishwe naye na kuyatekeleza yale aliyotufundisha. Kwa.
 

Basil the Great

Jun. 22.   Albano, Sh. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 46.   SALA 3.
 

Alban

Jun. 23.   Mkesha wa Yohana Mbatizaji

Yote ya Siku ya Kazi, isipokuwa,

Sala

Mwenyezi Mungu, tunakusihi: Utujalie sisi watoto wako tuishike njia ya wokovu; ili tuyafuatishe maonyo ya Kiongozi wetu, Yohana Mbatizaji, tukamfikie Yeye aliyemtabiri, Bwana wetu Yesu Kristo Mwana wako; Aishiye na kumiliki pamoja nawe, katika umoja wa Roho Mtakatifu, Mungu daima milele na milele. Amin.
 

Vigil of St. John the Baptist

Jun. 24.   Kuzaliwa kwa Yohana Mbatizaji. 1

Sala ya Jioni (ya 1 na ya 2)

    ANT. ZAB. Atatangulia mbele za uso wa Bwana, katika roho ya Eliya, na nguvu zake, Ili kumwekea Bwana tayari watu waliotengenezwa.
    ZABURI. Sehemu C. (Sikukuu tu).
    WIMBO 61.

Sala

Ee Mungu, umeitukuza siku hii ya leo kwa kuzaliwa kwake Yohana Mbatizaji: Uwajalie watu wako wote neema ya furaha za rohoni; na kuielekeza mioyo yetu katika njia ya wokovu wa milele. Kwa.

Sala ya Asubuhi

    ANT. ZAB. Wakamwashiria babaye wajue atakavyo kumwita; Akaandika ya kwamba jina lake ni Yohana.
    WIMBO 61.

Sala ya Adhuhuri

    SOMO. Nisikilizeni, enyi visiwa; enyi kabila za watu mlioko mbali sana, tegeni masikio yenu. Bwana ameniita tangu tumboni, toka tumbo la mama yangu amelitaja jina langu.
    R. Tumshukuru Mungu.
    V. Palitokea mtu ametumwa kutoka kwa Mungu.
    R. Palitokea mtu ametumwa kutoka kwa Mungu.
    V. Jina lake Yohana.
    R. Ametumwa kutoka kwa Mungu.
    V. Atukuzwe, etc,
    R. Palitokea mtu ametumwa kutoka kwa Mungu.
    V. Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake.
    R. Aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji.

Sala ya Ukumbusho

    Ant. Mtoto aliyezaliwa kwetu ni mkuu kuliko nabii; kwa habari zake Mwokozi alisema, Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji.
    V. Mtoto huyu ni mkuu mbele za Mungu.
    R. Kwa sababu mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye.
 

Birth of St. John the Baptist

Jun.28.   Irenio, A. Sh. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 46.   SALA 2.

Ukumbusho wa Oktavo; na, Asubuhi, wa Mkesha wa Mitume.

Sala

Mwenyezi Mungu, umependa kutuweka katika mwamba wa Imani ya Mitume wako: Utujalie, tunakuomba; tusiangushwe kwa mabaya yo yote. Kwa.
 

Irenaeus

Jun. 29.   Petro na Paulo, Mitume. 1

Sala ya Jioni (ya 1 na ya 2)

    ANT. ZAB. Wewe ndiwe Petro; Na juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu.
    ZABURI. Sehemu C. (Sikukuu tu).
    WIMBO 62.

Sala

Mwenyezi Mungu, umeitukuza siku hii ya kuuawa Petro na Paulo, Mitume wako Wabarikiwa: Utujalie tuzifuatishe amri zao takatifu; kwa kuwa ndio hao waliotufunulia kawaida za asili za dini yetu. Kwa.

Sala ya Asubuhi

    ANT. ZAB. Fedha sina, wala dhahabu; Lakini nilicho nacho ndicho nikupacho.
    WIMBO 62.

Sala ya Adhuhuri

    SOMO. Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile.
    R. Tumshukuru Mungu.
    V. Sauti yao imeenea duniani mwote.
    R. Sauti yao imeenea duniani mwote.
    V. Na maneno yao hata miisho ya ulimwengu.
    R. Duniani mwote.
    V. Atukuzwe, etc.
    R. Sauti yao imeenea duniani mwote.
    V. Utawafanya kuwa wakuu katika nchi zote.
    R. Jina lako watalifanya kuwa kumbukumbu, Ee BWANA.

Sala ya Ukumbusho

    Ant. Wewe ndiwe mchunga kondoo, Mkuu wa Mitume; Wewe ulipewa funguo za ufalme wa mbinguni.
    V. Wewe ndiwe Petro.
    R. Na juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu.
 

St. Peter & St. Paul

Jun. 30.   Kutiwa taji Paulo, Mtume. 3

ZABURI na Antifona za kawaida.
WIMBO 62.

Sala

Ee Mungu, ulipenda watu wengi wa mataifa wafundishwe kwa mahubiri ya Paulo, Mtume wako Mbarikiwa: Utujalie tuifurahie Sikukuu yake; na kusaidiwa kwa sala zake. Kwa.

    Asubuhi kuna Ukumbusho wa Petro Mt. na wa Oktavo ya Yohana Mbatizaji pia.
    Ukumbusho wa Petro Mt.

Sala

Ee Mungu, ulimpa Petro, Mtume wako Mbarikiwa, funguo za ufalme wa mbinguni, ukamkabidhi kazi ya kufunga na kufungua: Utujalie kwa rehema; tupate msaada wa kuombewa naye, na kufunguliwa minyororo ya dhambi zetu.

Sala ya Adhuhuri

Kama jana, isipokuwa SALA
 

Commemoration of St. Paul

Kulitabaruku Kanisa Kuu la Unguja. 1

(S.B. katika Oktavo ya Mitume)
Yote kama Kutabaruku Kanisa
 

Dedication of the Cathedral of Zanzibar

Ju1. 1.   Damu ya Thamani ya Bwana. 2

Sala ya Jioni (ya 1 tu)

    ANT. ZAB. Amevikwa vazi lililochovywa katika damu, Na Jina lake aitwa Neno la Mungu.
    ZABURI Sehemu A. (Sikukuu tu).
    WIMBO 63.

Sala

Mwenyezi Mungu wa milele, umependa kumweka Mwana wako pekee awe Mwokozi wa ulimwengu, na kuikubali Damu yake iwe kafara ya dhambi zetu: Utuialie tuiamini sana Damu hiyo kuwa ni dia kamilifu ya wokovu wetu; ili tulindwe kwa uwezo wake duniani, na kuyafurahia mazao yake mbinguni. Kwa Yeye.

Sala ya Asubuhi

    ANT. ZAB. Wa heri waliofua mavazi yao Katika Damu ya Mwana-kondoo.
    WIMBO 63.

Sala ya Adhuhuri

    SOMO. Damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisheni dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai.
    R. Tumshukuru Mungu.
    V. Ee Bwana, umetukomboa kwa Damu yako.
    R. Ee Bwana, umetukomboa kwa Damu yako.
    V. Watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa.
    R. Kwa Damu yako.
    V. Atukuzwe, etc.
    R. Ee Bwana, umetukomboa kwa Damu yako.
    V. Damu yake Yesu, Mwana wa Mungu
    R. Yatusafisha dhambi zote.

Sala ya Ukumbusho

    Ant. Tumeufikilia mlima Sayuni, na Yesu, mjumbe wa agano jipya, Na Damu ya kunyunyizwa inenayo mema kuliko ile ya Habili.
    V. Ee Bwana, umetukomboa kwa Damu yako.
    R. Ukatufanya kuwa ufalme kwa Mungu wetu.
 

Most Precious Blood of the Lord (Jesus Christ)

Jul. 2.   Kusalimiwa Elizabeti na Mariamu B. Mb. 2

Kawaida ya Mariamu Mb. isipokuwa,

Sala

Ee Mungu, ulimwongoza Bikira Mariamu Mbarikiwa aende kumtazama Elizabeti Mtakatifu, ili wafarijiane: Utujalie sisi kuyatafakari hayo; ili tufarijiwe nawe, na kwa nguvu zako tuondolewe mashaka ya dunia hii. Kwa.
 

Greeting of Elizabeth & Mary (The Visitation)

Jul.7.   Ramoni Luli, Sh. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 46.

Sala

Mwenyezi Mungu, wa milele, ulimwita Ramoni Luli Mbarikiwa azitubie dhambi zake, akawahubiri Waislamu wa Afrika, na kuwafia kishahidi: Utujalie, tunakusihi, tuzidi kuifululiza hiyo kazi yake; hata Waislamu wote wakuamini na kukuabudu. Kwa.
 

Ramon Llull (a missionary to Moslems)

Jul. 10.   Mashahidi wa Afrika. 2

Sala ya Jioni (ya 1 na ya 2)

    ANT. ZAB. Miili yao imezikwa katika amani, Na jina lao laishi hata vizazi vyote.
    ZABURI Sehemu C. (Sikukuu tu).
    WIMBO 48.

Sala

Ee Mungu, umetujalia furaha ya kuiadhimisha Sikukuu hii ya Mashahidi wako wote wa Afrika: Tunakusihi utuonyeshe rehema zako; ili tushangilie kushinda kwao, na kuchangamka pamoja nao katika utukufu wa mbinguni. Kwa.

Sala ya Asubuhi

    ANT. ZAB. Enyi ndugu zetu, Mashahidi wa Afrika, Msifuni Bwana kutoka mbinguni.
    WIMBO 49.

Sala ya Adhuhuri

    SOMO. Roho zao wenye haki wamo mkononi mwa Mungu, wala maumivu hayatawagusa. Machoni pa watu walio wajinga walionekana kwamba wamekufa; bali wao wamo katika amani.
    R. Tumshukuru Mungu.
    V. Shangilieni, enyi wenye haki.
    R. Shangilieni, enyi wenye haki.
    V. Pigeni vigelegele vya furaha.
    R. Enyi wenye haki.
    V. Atukuzwe, etc.
    R. Shangilieni, enyi wenye haki.
    V. Wenye haki hufurahi usoni pa Mungu
    R. Naam, hupiga kelele kwa furaha.
 

Martyrs of Africa

Jul. 14.   Bonaventura, A. Mw. 3

Kawaida ya Mtakatifu

Q.   WIMBO 53.   SALA 9.
 

Bonaventure

Jul. 15.   Yusufu wa Arimathaya, Mu. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 54.   SALA 10.
 

Joseph of Arimathea

Jul. 19.   Vinsenti wa Paulo, K. Mu. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 54.

Sala

Ee Mungu, ulimpa Vinsenti wa Paulo karama za utume, ili awahubiri maskini Injili na kuuongeza utauwa wa Wahudumu wako: Urujalie, tunakusihi; tuifuate tabia yake njema, kama vile tunavyomheshimu kwa utauwa wake. Kwa.
 

Vincent de Paul

Jul. 20.   Magarita wa Antiokia, B. Sh. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 56.   SALA 12.
 

Margaret of Antioch

Jul. 22.   Mariamu wa Magdala, Mwenye toba. 3

ZABURI na Antifona za kawaida.
WIMBO 64.

Sala

Ee Baba wa rehema, ulipenda Mariamu wa Magdala asamehewe dhambi zake, na kumpenda Mwana wako pekee kuliko mambo yote: Utujalie ondoleo la dhambi zetu zote; ili tusaidiwe kwa sala zake mwenye toba, na kupewa kustarehe panapo baraka za milele. Kwa Yeye.

Sala ya Adhuhuri

Kama Kawaida ya Mtakatifu
 

Mary Magdalene

Jul. 24.   Mkesha wa Yakobo, Mtume.

Yote ya Siku ya Kazi, isipokuwa, SALA 1
 

Vigil of St. James

Jul. 25.   Yakobo bin Zebedayo, Mtume. 2

Kawaida ya Mtume

Sala

Ee Mungu wa rehema, mtumishi wako Yakobo Mbarikiwa, alipoitwa na Mwana wako pekee, alimwacha baba yake na vyote alivyo navyo: Utujalie na sisi tuziache tamaa zote za dunia na za mwili; ili tupende sikuzote kuzifuata amri zako takatifu. Kwa Yeye.
 

James, son of Zebedee

Jul. 26.   Ana, Mama wa Mariamu Mb. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 57.   SALA 15.
 

Anna, mother of Mary

Jul. 29.   Martha, B. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 56.   SALA 13.
 

Martha (of Bethany)

Ago. 1.   Kufunguliwa kwa Petro, Mtume. 3

ZABURI na Antifona za kawaida.
WIMBO 65.

Sala

Ee Mungu, ulipenda kumfungulia minyororo' Petro, Mtume wako Mbarikiwa, na kumtoa salama gerezani: Tunakuomba; utufungulie minyororo ya dhambi zetu, na kutuepusha na maovu yote. Kwa.

Sala ya Adhuhuri

Kama Kawaida ya Mtume
 

St. Peter in Chains

Ago. 3.   Kulitabaruku Kanisa Kuu la Masasi. 1

Yote kama Kutabaruku Kanisa
 

Dedication of the Cathedral of Masasi

Ago. 4.   Dominiko, K. Mu. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 54.   SALA 10.
 

Dominic

Ago. 6.   Kung'aa kwa Bwana.

Sala ya Jioni (ya 1 tu)

    ANT. ZAB. Yesu aliwatwaa Petro na Yakobo na Yohana nduguye, akawaleta juu ya mlima mrefu faraghani; Akageuka sura yake mbele yao.
    ZABURI. Sehemu A. (Sikukuu tu).
    WIMBO 66.

Sala

Ee Mungu, alipoking'aa Mwana wako pekee kwa ajabu, ulipenda kuzithibitisha siri za Imani yetu kwa kauli za Babu wa kale, na kututabiria kufanywa wana kwetu kwa sauti yako ya mbinguni: Utujalie tuushiriki utukufu wa Mfalme wetu; na kutukuzwa pamoja naye. Kwa Yeye.

Sala ya Asubuhi

    ANT. ZAB. Petro akajibu akamwambia Yesu, Bwana, ni vizuri sisi kuwapo hapa.
    WIMBO 66.

Sala ya Adhuhuri

    SOMO. Sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa BWANA, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa BWANA.
    R. Tumshukuru Mungu.
    V. Umemvika taji ya utukufu na heshima. Haleluya. Haleluya.
    R. Umemvika taji ya utukufu na heshima. Haleluya. Haleluya.
    V. Umemtawaza juu ya kazi ya mikono yako.
    R. Haleluya. Haleluya.
    V. Atukuzwe, etc.
    R. Umemvika taji ya utukufu na heshima. Haleluya. Haleluya.
    V. Utukufu wake ni mkuu kwa wokovu wako, Haleluya.
    R. Heshima na adhama waweka juu yake. Haleluya.

Sala ya Ukumbusho

    Ant. Wanafunzi waliposikia, walianguka kifudifudi, wakaogopa sana; Yesu akaja, akawagusa, akasema, Inukeni wala msiogope.
    V. Ulionekana mtukufu machoni pa BWANA.
    R. Kwa sababu BWANA amekuvika uzuri.
 

Transfiguration of our Lord

Ago. 7.   Jina Takatifu, Yesu. 2

Sala ya Jioni (ya 1 na ya 2)

    ANT. ZAB. Kila atakayeliitia Jina la BWANA Ataokolewa. Haleluya.
    ZABURI Sehemu A. (Sikukuu tu).
    WIMBO 67.

Sala

Ee Mungu, umelitukuza Jina lake Yesu Kristo, Mwana wako pekee, liwe tamu sana kwa watu wako waaminifu, bali la kuwatisha sana pepo wabaya: Uwajalie kwa rehema watu wote waliheshimu vema Jina hilo hapa duniani; ili tufarijiwe nalo katika maisha haya, na kulifurahia daima katika ulimwengu ujao. Kwa Yeye.

Sala ya Asubuhi

    ANT. ZAB. Aliitwa Jina lake Yesu, Kama alivyoitwa na Malaika kabla hajachukuliwa mimba. Haleluya.
    WIMBO 67.

Sala ya Adhuhuri

Ubeti wa mwisho wa Wimbo.

Ee Yesu, Mwana wa Bikira,
    Twakutolea sifa zetu;
Pamoja naye Mungu Baba,
    Na Mungu Roho Mtakatifu. Amin.

    SOMO. Kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika Jina Ia Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa Yeye.
    R. Tumshukuru Mungu.
    V. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Haleluya, Haleluya.
    R. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Haleluya, Haleluya.
    V. Naam, vyote vilivyo ndani yangu vilihimidi Jina lake takatifu.
    R. Haleluya, Haleluya.
    V. Atukuzwe, etc.
    R. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Haleluya, Haleluya.
    V. Ee Bwana, kutukuza usitutukuze sisi. Haleluya.
    R. Bali ulitukuze Jina lako. Haleluya.
 

Holy Name

Ago. 9.   Yohana Viane, K. Mu. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 54.   SALA 10.
 

John Vianney

Ago. 10.   Lorenzo, Shem. Sh. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 46.

Sala

Ee Bwana, ulimpa Lorenzo Mtakatifu neema ya kustahimili maumivu ya moto na kushinda: Utujalie, tunakusihi; tuizimishe miali ya tamaa zetu. Kwa.
 

Laurence

Ago. 12.   Klara, B. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 56   SALA 13.
 

Clare (of Assisi)

Ago. 14.   Mkesha wa Mariamu Mb.

Yote ya Siku ya Kazi, isipokuwa,

Sala

Bwana Mungu, tunakuomba: Utuialie tuifurahie afya ya mwili na ya roho; ili, kwa msaada wa sala za Mariamu Mbarikiwa, Bikira Mtukufu wa daima, tuokoke katika huzuni ya dunia hii na kuifikia furaha ya milele. Kwa.
 

Vigil of St. Mary

Ago. 15.   Kustarehe kwa Mariamu B. Mb. 1

Kawaida ya Mariamu Mb. isipokuwa,

Sala

Mwenyezi Mungu, ulimhifadhi Bikira Mariamu Mbarikiwa asikae amefungwa na mauti: Utujalie, tunakusihi, tusishindwe na udhaifu wetu wa kibinadamu; bali tuzidi kuendelea katika njia ya wokovu, hata tukufikie mbinguni. Kwa.
 

Assumption of the BVM

Ago. 16.   Yoakimu, Baba wa Mariamu Mb. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 54.   SALA 10.
 

Joachim, father of St. Mary

Ago. 18.   Helena, Mjane.

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 57.   SALA 15.
 

Helena (of Constantinople)

Ago. 20.   Benado, Mtauwa, Mw. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 53.   SALA 9.
 

Bernard (of Clairvaux)

Ago. 21.   Jeni wa Chantale, Mjane. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 57.   SALA 15.
 

Jane of Chantale

Ago. 23.   Mkesha wa Bartolomayo, Mtume.

Yote ya Siku ya Kazi, isipokuwa, SALA 1
 

Vigil of Bartholomew

Ago. 24.   Bartolomayo, Mtume. 2

Kawaida ya Mtume

Sala

Mwenyezi Mungu wa milele, ulimpa Mtume wako, Bartolomayo, neema ili aliamini kwa moyo Neno lako na kulihubiri: Tunakusihi; u1ijalie Kanisa lako liyapende aliyoyaamini, na kuyakumbatia aliyayafundisha. Kwa.
 

Bartholomew

Ago. 28.   Agostino wa Hipo, A. Mw. 3

Kawaida ya Mtakatifu

Q.   WIMBO 53.

Sala

Mwenyezi Mungu, umetujaza tumaini la kusamehewa kwa upendo wako: Utujalie, tunakusihi; tuombewe na Agostino wa Hipo, Askofu wako na Mwalimu mstadi, ili tuyaone ndani yetu mazao ya huruma zako. Kwa.
 

Augustine of Hippo

Ago. 29.   Kufa kishahidi kwa Yohana Mbatizaji. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 61.

Sala

Ee Bwana, ulipenda kumtuma Yohana Mbatizaji amtangulie Mwana wako pekee na kukutia kishahidi: Utujalie tuifurahie Sikukuu hii ya kushinda kwake; tukajazwe nguvu ya rohoni. Kwa Yeye.
 

Beheading of John the Baptist

Ago. 31.   Aidano, A. Mu. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 51.   SALA 7.
 

Aidan

Sep. 1.   Egidio, Mtauwa. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 55.   SALA 11.
 

Giles

Sep. 8.   Kuzaliwa kwa Mariamu B. Mb. 2

Kawaida ya Mariamu Mb. isipokuwa,

Sala

Ee Bwana, tunakusihi: Utukirimie sisi watumishi wako neema yako ya mbinguni; ili tulivyoletewa wokovu kwa kuzaa kwake Bikira Mariamu Mbarikiwa, tuufurahie ukumbusho wa kuzaliwa kwake. Kwa.
 

Birth of the BVM

Sep, 13.   Sipriani, A. Sh. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 46.   SALA 2.
 

Cyprian

Sep. 14.   Msalaba Mtakatifu. 2

Sala ya Jioni (ya 1 na ya 2)

    ANT. ZAB. Imetupasa kuona fahari Juu ya Msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo.
    ZABURI. Sehemu A. (Sikukuu tu).
    WIMBO 27.

Ee Mungu, watufurahisha kila mwaka kwa Sikukuu ya Msalaba wa Mwana wako, Mwokozi wetu: Utujalie tuzidi kuifahamu siri yake hapa duniani; ili tupewe thawabu ya ukombozi aliotupatia. Kwa Yeye.

Sala ya Asubuhi

    ANT. ZAB Kwa ishara ya Msalaba Utuokoe na adui zetu, Ee Mungu wetu.
    WIMBO 26.

Sala ya Adhuhuri

    SOMO. Lakini mimi, hasha nisione fahari juu ya kitu, ila Msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo; kwa huo ulimwengu umesulibishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu.
    R. Tumshukuru Mungu.
    V. Twakuabudu, Ee Kristo, twakuhimidi.
    R. Twakuabudu, Ee Kristo, twakuhimidi.
    V. Maana kwa Msalaba wako umeukomboa ulimwengu.
    R. Twakuhimidi.
    V. Atukuzwe, etc.
    R. Twakuabudu, Ee Kristo, twakuhimidi.
    V. Nchi yote itakusujudu na kukuimba.
    R. Naam, italiimba Jina lako, Ee BWANA.
 

Holy Cross

Sep. 20.   Mkesha wa Mathayo, Mtume.

Yote ya Siku ya Kazi, isipokuwa, SALA 1
 

Vigil of St. Matthew

Sep, 21.   Mathayo, Mtume, Mtunga Injili. 2

Kawaida ya Mtume

Sala

Mwenyezi Mungu, ulimwita Mathayo Mbarikiwa kwa neno Ia Mwana wako Mtukufu, awe Mtume na Mtunga Injili badala ya kuwa mtoza ushuru: Utupe neema tuache kutamani fedha na kupenda mali ya kupita kiasi; tumfuate Bwana wetu Yesu Kristo Mwana wako; Aishiye na kumiliki pamoja nawe, katika umoja wa Roho Mtakatifu, Mungu daima milele na milele. Amin.
 

St. Matthew

Sep. 23.   Thekla, B. Sh. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 56.   SALA 12.
 

Thecla

Sep. 28.   Wenseslao, Sh. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 46.   SALA 3.
 

Wenceslaus

Sep. 29.   Mikaeli, Malaika Mkuu, na Malaika zote. 1

Sala ya Jioni (ya 1 na ya 2)

    ANT. ZAB. Mhimidini Bwana, Enyi Malaika zake.
    ZABURI. Sehemu C. (Sikukuu tu).
    WIMBO 68.

Sala

Ee Mungu, umeziamuru huduma za Malaika na za wanadamu kwa kawaida za ajabu: Utujalie, tunakusihi; hao wanaokuhudumia mbinguni watusaidie sisi, na kutulinda hapa duniani. Kwa.

Sala ya Asubuhi

    ANT. ZAB. Malaika za Bwana, Mhimidini Bwana milele.
    WIMBO 69.

Sala ya Adhuhuri

Kama Kawaida ya Malaika
 

St. Michael & All Angels

Sep. 30.   Jerome, K. Mw. 3

Kawaida ya Mtakatifu

Q.   WIMBO 53.

Sala

Ee Mungu, ulimwelimisha kwa ajabu Jerome Mtakatifu, Mwungamaji na Mwalimu wa Kanisa lako: Utujalie kuyapenda daima Maandiko Matakatifu; ili tuyashike mafundisho yaliyomo, na kumulikiwa mwanga wake katika njia zetu. Kwa.
 

Jerome

Okt. 1.   Remigio, A. Mu. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 51.   SALA 7.
 

Remigius

Okt. 2.   Malaika Walinzi. 3

Kawaida ya Malaika

WIMBO 70.

Sala

Ee Mungu, umependa kutuweka chini ya himaya yako, na kuwatuma Malaika zako Watakatifu watuhifadhi: Utujalie tulindwe nao sikuzote hapa duniani; na kukaa nao mbinguni katika furaha ya milele. Kwa.
 

The Guardian Angels

Okt. 4.   Fransisi wa Asisi, Mtauwa. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 55.

Sala

Ee Mungu, umeliongezea Kanisa lako mazao mapya kwa kazi za Mtakatifu wako, Fransisi wa Asisi, na kwa mwenendo wake wa ajabu: Utujalie tumfuatishe vema; tuyadharau yaliyo ya dunia hii, na kuyafurahia daima yaliyo ya mbinguni. Kwa.
 

Francis of Assisi

Okt. 6.  Fidea, B. Sh. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 56   SALA 12.
 

St. Faith (?)

Okt. 8.   Brijita, Mjane. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 57.   SALA 15.
 

Bridget (of Sweden)

Okt. 9.   Dionisio na Wenzake, Mash. 3

Kawaida ya Mtakatifu

NYIMBO 48, 49.   SALA 4.
 

Denis & his Companions

Okt. 11.   Filipo, Shem. Mu. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 54.   SALA 10.
 

Philip (the Deacon)

Okt. 13.   Eduado, Mfalme, Mu. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 54.   SALA 10.
 

Edward (the Confessor)

Okt. 15.   Tereza, B. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 56.

Sala

Ee Mungu, Mwokozi wetu, utusikilize kwa rehema: ili tuishangilie Sikukuu hii ya Tereza Mbarikiwa, Mtauwa mkuu wako na Bikira; na kuadilishwa katika hali ya utauwa kwa kushiba mafundisho yake ya mbinguni. Kwa.
 

Teresa (of Avila)

Okt. 18.   Luka, Mtunga Injili. 2

Kawaida ya Mtume

Sala

Mwenyezi Mungu, ulimwita Luka, Tabibu anayesifiwa katika Injili, awe Mtunga Injili na Tabibu wa roho: Utujalie, tunakusihi; tuponywe maradhi zote za roho zetu kwa dawa bora ya elimu yake. Kwa.
 

St. Luke

Okt. 23.   Yakobo wa Yerusalemu, A. Sh. 3

Kawaida ya Mtakatifu

Q.   WIMBO 46.

Sala

Mwenyezi Mungu, ulimwita Yakobo wa Yerusalemu, ndugu wa Bwana wetu Yesu Kristo, awe Askofu katika Kanisa lako: Utujalie, tunakusihi; tuifuatishe maisha yake ya utauwa, na kuionyesha imani kamili kwa matendo yetu mema. Kwa Yeye.
 

St. James of Jerusalem

Okt. 24.   Rafaeli, Malaika Mkuu. 3

Kawaida ya Malaika

WIMBO 69.

Sala

Ee Mungu, umependa kuwafariji wasafiri kwa ukumbusho wa Rafaeli, Malaika Mkuu Mbarikiwa: Utuialie tuhifadhiwe kwa tunza lake; na kuimarishwa kwa msaada wako. Kwa.
 

The Archangel Raphael

Okt. 25.   Krispino na Nduguye, Mash. 3

Kawaida ya Mtakatifu

NYIMBO 48, 49.   SALA 4.
 

Chrysanthus & Daria (?)

Okt. 27.   Mkesha wa Mitume

Yote ya Siku ya Kazi, isipokuwa, SALA 1
 

Vgil of the Apostles (Simon & Jude)

Okt. 28.   Simoni na Yuda, Mitume. 2

Kawaida ya Mtume

Sala

Mwenyezi Mungu, umelijenga Kanisa lako juu ya msingi wa Manabii na Mitume, katika Yesu Kristo, jiwe kuu la pembeni: Utujalie tuungamane kwa elimu yao katika umoja wa roho; kwa jinsi tufanywe hekalu takatifu la kukubaliwa nawe. Kwa Yeye.
 

St. Simon & St. Jude

Bwana wetu Yesu Kristo, Mfalme. 1

(S.B. ya mwisho ya Oktoba)

Sala ya Jioni (ya 1 na ya 2)

    ANT. ZAB. Ufalme wake ni ufalme wa milele, Na watu wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.
    ZABURI Sehemu A. (Sikukuu tu).
    WIMBO 71.

Sala

Mwenyezi Mungu wa milele, umekusudi kuyatengeneza yote katika Mwana wako Mpendwa, aliye Mfalme wa ulimwengu wote: Utujalie, tunakusihi, neema yako; ili jamaa zote za mataifa, waliofarakana kwa sababu ya dhambi, wajiweke chini ya utawala wake wa upole. Aishiye na kumiliki pamoja nawe, katika umoja wa Roho Mtakatifu, Mungu daima milele na milele. Amin.

Sala ya Asubuhi

    ANT. ZAB. Maji yaliyo hai yatatoka katika Yerusalemu; Naye Bwana atakuwa Mfalme juu ya nchi yote.
    WIMBO 71.

Sala ya Adhuhuri

    SOMO. Vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake, naye alikuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika Yeye. Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha Kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili awe mtangulizi katika yote.
    R. Tumshukuru Mungu.
    V. Mpeni BWANA, enyi jamaa za watu.
    R. Mpeni BWANA, enyi jamaa za watu.
    V. Mpeni BWANA utukufu na nguvu.
    R. Enyi jamaa za watu.
    V. Atukuzwe, etc.
    R. Mpeni BWANA, enyi jamaa za watu.
    V. Naam, wafalme wote na wamsujudie.
    R. Na mataifa yote wamtumikie.
 

Christ the King

(last Sunday in October)

Okt. 31.   Mkesha wa Watakatifu Wote

Yote ya Siku ya Kazi, isipokuwa,

Sala

Ee Bwana Mungu wetu, utuongezee neema yako: Utujalie tuzidi kujiweka kwako; ili tuzidi kuifurahia furaha yao tutakaowaadhimisha kwenye Sikukuu ya kesho. Kwa.
 

Vigil of All Saints

Nov. 1.   Watakatifu Wote 1

Sala ya Jioni (ya 1 na ya 2)

    ANT. ZAB. Msifuni Bwana, enyi wateule wake; Ziadhimisheni Sikukuu zake zenye furaha.
    ZABURI. Sehemu C. (Sikukuu tu).
    WIMBO 72.

Sala

Mwenyezi Mungu, umewaunganisha Watakatifu wako katika ujamaa mmoja wa Mwili wa siri wa Mwana wako, Yesu Kristo Bwana wetu: Utujalie tuwafuate Watakatifu wako katika wema wa kila namna, na mwenendo wa ibada; ili tusaidiwe kwa sala zao, na kuifikia furaha uliyowawekea wao wakupendao kwa kweli. Kwa Yeye.

Sala ya Asubuhi

    ANT. ZAB. Nikaona mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, Watu wa kila taifa, wamesimama mbele ya kiti.
    WIMBO 72.

Sala ya Adhuhuri

    SOMO. Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa na kabila na jamaa na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwanakondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao.
    R. Tumshukuru Mungu.
    V. Wenye haki hufurahi usoni pa Mungu.
    R. Wenye haki hufurahi usoni pa Mungu.
    V. Naam, hupiga kelele kwa furaha.
    R. Usoni pa Mungu.
    V. Atukuzwe, etc.
    R. Wenye haki hufurahi usoni pa Mungu.
    V. Wenye haki waishi milele.
    R. Na thawabu yao i katika Bwana.
 

All Saints

Nov. 2.   Ukumbusho wa Roho Zote

    Sala za kuombea Wafu zisemwe leo.
    Mwisho wa Sala ya Jioni ya 2 ya Watakatifu Wote isisemwe,
Roho zao waaminifu, etc., bali mara hufuata Sala ya Jioni ya Wafu.
 

All Souls

Nov. 6.   Leonado, Mtauwa. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 55.   SALA 11.
 

Leonard (of Noblac)

Nov. 11.   Martino, A. Mu. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 51.

Sala

Mwenyezi Mungu, ulimwita Martino Mtakatifu awe Askofu na Askari hodari wa Bwana wetu Yesu Kristo: Utujalie tusaidiwe kwa sala zake; ili tuyaige maisha yake ya huruma, na kupigana kwa ushujaa na adui zetu za rohoni. Kwa Yeye.
 

Martin (of Tours)

Nov. 17.   Hugo, A. Mu. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 51.   SALA 7.
 

Hugh (of Lincoln)

Nov. 18.   Hilda, B. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 56.   SALA 13.
 

Hilda (of Whitby)

Nov. 19.   Elizabeti, Mjane, 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 57.   SALA 15.
 

Elizabeth (of Hungary)

Nov. 22.   Sisilia, B. Sh. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 56.   SALA 12.
 

Cecilia

Nov. 23.   Klementi wa Rumi, A. Sh. 3

Kawaida ya Mtakatifu

Q.   WIMBO 46.   SALA 2.
 

Clement of Rome

Nov. 24.   Yohana wa Msalaba, K. Mw. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 53.   SALA 9.
 

John of the Cross

Nov. 25.   Katharina wa Iskanderia, B. Sh. 3

Kawaida ya Mtakatifu

WIMBO 56.   SALA 12.

Catherine of Alexandria

 

Return to the Zanzibar Prayer Book

Web author: Charles Wohlers U. S. EnglandScotlandIrelandWalesCanadaWorld