The Book of Common Prayer
United States England Scotland Ireland Wales Canada World

    Kitabu cha Sala za Kanuni (1918)
The Zanzibar Book of Common Prayer in Swahili

 

MAOMBEZI YA SIKU ZA JUMA

Siku zisizo Sikukuu za 1 au za 2, watu wapige magoti; Mhudumu ayaseme maombezi yaliyoamriwa, kila siku na maombezi yake.
 

Intercessions fo the Days of the Week

SIKU YA BWANA

Sala ya Asubuhi

(1) Tuwaombee Walio batizwa wadumu kuwa imara

    Ant. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.
    V. Ee Mungu, utuumbie mioyo safi.
    R. Wala Roho wako Mtakatifu usituondolee.

Tuombe

Ee Mungu, Roho wako hulitawala Kanisa lako lote na kulitakasa: Uwaimarishe wote waliobatizwa, wawe viungo hai vya mwili wa siri wa Mwana wako; ili wote waliopewa neema ya kuwa safi wapate nguvu ya kukutumikia amini. Kwa Yeye, Kristo Bwana wetu. Amin.
 

Sunday

Morning Prayer

We pray for those baptized, that they will continue to persevere

(2) Tuwaombee Watu waongoke kwa Bwana Kristo

    Ant. Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, na miisho ya dunia kuwa milki yako.
    V. Enendeni ulimwenguni mwote.
    R. Mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.

Tuombe

Ee Mungu wa mataifa yote ya ulimwengu: Ukumbuke watu walivyo wengi, ambao .wameumbwa kwa mfano wako, lakini hawajui upendo wako; uwajalie, kwa upatanisho wa Mwana wako Yesu Kristo, waondolewe uovu wo wote uliomo mioyoni mwao, kwa sala na kazi za Kanisa lako takatifu, wakaletwe kwako na kukuabudu. Kwa Yeye, Kristo Bwana wetu. Amin.
 

We pray for people, that they may be converted to Christ the Lord

Sala ya Jioni

(1) Tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa fadhili zake

    Ant. Tunakushukuru, Ee BWANA Mungu wetu; tunalihimidi Jina lako milele na milele.
    V. Kazi zako zote zitakushukuru, Ee BWANA.
    R. Na Watakatifu wako watakuhimidi.

Tuombe

Ee Baba, mwenye fadhili zote, sisi watumishi wako tulio wanyonge tunakushukuru kwa unyenyekevu na kwa moyo, kwa wema wako wote na kwa pendo lako lote, kwetu sisi, na kwa watu wote; [na hasa kwa watu hawa wanaotaka kukushukuru kwa fadhili zako ulizowaletea wakati huu.] Tunakutukuza kwa ajili ya kuumbwa kwetu, na kuhifadhika kwetu, na kwa baraka zote za maisha haya; lakini zaidi ya yote, kwa pendo lako lisilopimika, tulilofunuliwa hapo Bwana wetu Yesu Kristo alipoukomboa ulimwengu; kwa njia ya neema, na tumaini la utukufu. Utujalie, tunakusihi, mioyo. yetu ikushukuru pasipo hila, nasi tuzionyeshe sifa zako, si kwa midomo yetu tu, ila na kwa maisha yetu; tukijitia kabisa katika utumishi wako, tukienenda kwa utakatifu na kwa haki mbele zako siku zetu zote. Kwa Yeye, Kristo Bwana wetu. Amin.
 

Evening Prayer

We thank Almighty God for his favor

(2) Tumwombee Askofu wetu

    Ant. Watoto wako utawafanya kuwa wakuu katika nchi zote.
    V. Ee Mungu, Ngao yetu, uangalie.
    R. Umtazame uso Masihi wako.

Tuombe

Ee Mungu, mchunga waaminifu wako wote na kuwatawala: Umtazame kwa rehema mtumishi wako fulani, Askofu wetu; umlinde, umfariji, umtakase, na kumwokoa; umjalie neema yako azidi kutufalia kwa neno na mwenendo safi; hata pamoja na wateule wako aliokabidhiwa, aufikie uzima wa milele. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

We pray for our bishops

JUMATATU

Sala ya Asubuhi

(1) Tuiombee Jumuiya ya Madola

    Ant: Njia yako ijulike duniani. wokovu wako kati ya mataifa yote.
    V. Ee Bwana. uwaokoe watu wako.
    R. Uubariki urithi wako.

Tuombe

Ee Bwana mtakatifu. Baba wa mbinguni. Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana. kutoka kiti chako cha enzi unawaanqalia wote wakaao duniani; tunakuomba uibariki Jumuiya ya Madola: nasi tunakusihi uwajalie watu wote wa Jumuiya hiyo udugu wa kweli; ili, huku wakichukuliana mizigo na kusaidiana kwa upendano. wayatimize mapenzi yako na kuueneza ufalme wako. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

Monday

Morning Prayer

We pray for the Commonwealth

(This section was pasted in; it replaces a prayer for the King)

(2) Tuwaombee wote wenye mamlaka

    Ant. Li heri taifa ambalo BWANA ni Mungu wao, watu aliowachagua kuwa urithi wake.
    V. BWANA wa majeshi yu pamoja nasi.
    R. Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.

Tuombe

Mwenyezi Mungu, mtawala watu wote: Uwabariki Wakuu wote wa Serikali yetu, na hasa fulani, uwakirimie hekima yako, uwape neema ya kutenda haki, na kuhukumu kwa kweli; ili sisi, watumishi wako, tukiyatenda yaliyo mema, tukae salama chini ya ulinzi wako, tukutumikie sikuzote katika utulivu na amani. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

We pray for those in authority

Sala ya Jioni

(1) Tumshukuru Mungu kwa ulinzi wa Malaika Watakatifu

    Ant. Tazama, Mimi namtuma Malaika mbele yako akulinde njiani.
    V. Atakuagizia Malaika zake.
    R. Wakulinde katika njia zako zote.

Tuombe

Ee Mungu, tunakushukuru kwa mioyo yetu yote kwa jinsi unavyowatuma Malaika zako Watakatifu ili watulinde hapa duniani: Utujalie tujiepushe na dhambi zote; na kuhifadhika daima chini ya himaya yako. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

Eveninig Prayer

We thank God for the protection of his holy angels

(2) Tuwaombee Wahudumu wa Kanisa

    Ant. Yapasa midomo ya kuhani ihifadhi maarifa, tena yawapasa watu kuitafuta sheria kinywani mwake; kwa kuwa yeye ni mjumbe wa BWANA wa majeshi.
    V. Makuhani wako na wavikwe haki.
    R. Watauwa wako na washangilie.

Tuombe

Ee Bwana, wapenda kwa neema yako kutuwezesha sisi tulio dhaifu: Uzisikilize kwa rehema sala zetu; uwazidishie utauwa Maaskofu na Wahudumu wote wa Kanisa lako; ili wakikuhudumu katika utakatifu, neno lako litoke kwao kama moto, ili kuteketeza maovu, kuyeyusha mioyo iliyo migumu, kusafisha wasio safi, kutia nguvu waaminifu, kuangaza wajinga, na kuhuisha waliokufa roho. Kwa Kristo wana Bwetu, Amin.
 

We pray for the ministers of the Church.

JUMANNE

Sala ya Asubuhi

(1) Tuwaombee Watoto wa Shule

    Ant. Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
    V. Kumcha BWANA ndiyo hekima.
    R. Na kujitenga na uovu ndiyo fahamu.

Tuombe

Ee Bwana Yesu Kristo, Mungu wa milele, ulifanyika mtoto kwa ajili yetu: Uwabariki watoto wote wanao-fundishwa kwetu; uwajalie utauwa, usafi, na utii, waipende haki na kweli, wakayatimize mapenzi yako katika hali yo yote utakayowaitia. Uishiye na kumiliki, Mungu, milele na milele. Amin.
 

Tuesday

Morning Prayer

We pray for children in school

(2) Tuwaombee Wagonjwa wote

    Ant. Bwana ameyaotesha madawa katika nchi, naye amewapa wanadamu maarifa, ili atukuzwe mwenyewe kwa ajili ya miujiza yake.
    V. Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu.
    R. Na kuyachukua magonjwa yetu.

Tuombe

Mwenyezi Mungu, mwenye rehema, waweza peke yako kuwasaidia wagonjwa wanaotujia ili wapate dawa na kupona: Tunakusihi uzibariki kazi zote za uganga zifanywazo kwetu; waganga na wasaidizi wao uwape akili na imani; wagonjwa uwaponye na kuwajazi heri, ili kila mmoja azidi kukutumaini na kukutii. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

We pray for all sick people

Sala ya Jioni

(1) Tumshukuru Mungu kwa Ubatizo wetu

    Ant. Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.
    V. Alituokoa kwa rehema yake.
    R. Kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili, na kufanywa upya na Roho Mtakatifu.

Tuombe

Mwenyezi Mungu wa milele, tunalitukuza Jina lako kwa kuwa umetuita tuijue neema yako na kukuamini: Na hasa tunakushukuru sana kwa Ubatizo wetu, kwa kuondolewa dhambi zetu, kukaribishwa katika Kanisa lako, na kufanywa viungo hai vya Kristo; utujalie tuzidi kila siku kukuamini na kukutii, ili tuendelee vema katika njia ya wokovu wa milele. Kwa Yeye, Kristo Bwana wetu. Amin.
 

Evening Prayer

We thank God for our Baptism

(2) Tuwaombee Waalimu wote

    Ant. Matendo yako na yaonekane kwa watumishi wako, na adhama yako kwa watoto wao.
    V. Uzuri wa BWANA Mungu wetu uwe juu yetu.
    R. Na kazi ya mikono yetu uithibitishe.

Tuombe

Ee Bwana Mungu wetu, tunajifunza elimu kwa kuyatafakari maagizo yako: Uwakirimie Waalimu wako wote hekima na akili, na kuwazidishia saburi na bidii; ili wazidi kuchunga vizuri roho za watu, na kuwalea watoto wako, hata hao wakue katika pendo lako, na kujifunza kutumia vema neema yako. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

We pray for all ?

JUMATANO

Sala ya Asubuhi

(1) Tuliombee Kanisa la Mungu, lipate amani

    Ant. Bwana atawapa watu wake nguvu, BWANA atawabariki watu wake kwa amani.
    V. Ee BWANA, utupe amani siku zetu.
    R. Kwa maana hakuna mwingine wa kutu pigania, ila Wewe, Mungu wetu.

Tuombe

Ee Bwana Yesu Kristo, uliwaambia Mitume wako, Amani nawaachieni, amani yangu nawapeni: Usitazame dhambi zetu, bali uitazame imani ya Kanisa lako; ulijalie amani na umoja kama vile utakavyo mwenyewe. Uishiye na kumiliki, Mungu, milele na milele. Amin.
 

Wednesday

Morning Prayer

We pray for the Church of God; may it find peace

(2) Tuwaombee Wakaao mbali na kanisa

    Ant. Yu heri mtu yule umchaguaye, na kumkaribisha, akae nyuani mwako.
    V. Wewe usikiaye kuomba.
    R. Wote wenye mwili watakujia.

Tuombe

Mwenyezi Mungu, mpenda roho za watu: Uwatazame kwa jicho la rehema ndugu zetu wakaao mbali na nyumba yako; Uwavute mioyo waambatane nawe; uwape nia ya kukukumbuka na kulitukuza Jina lako katikati ya watu. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

We pray for your continued concern with the Church (?)

Sala ya Jioni

(1) Tumshukuru Mungu kwa kutupa Sakramenti Mbarikiwa

    Ant. Ee karamu takatifu! Twampokea Kristo; twafanya ukumbusho wa mateso yake; mioyo yetu hujazwa neema; twapewa arabuni ya utukufu ujao.
    V. Uliwapa chakula cha mbinguni.
    R. Ndicho kilicho kitamu.

Tuombe

Ee Mungu, umetuachia ukumbusho wa Mateso yako, katika Sakramenti iliyo ya ajabu: Utujalie, tunakusihi, tuziheshimu siri takatifu za Mwili na Damu yako; ili tuyaone daima ndani yetu mazao ya ukombozi wako. Uishiye na kumiliki, Mungu, milele na milele. Amin.
 

Evening Prayer

We thank God for giving us the blessed Sacrament

(2) Tuwaombee Wajiwekao tayari kupokea [Sakramenti za Kanisa. *]

    Ant. Utufumbue macho yetu tuyatazame maajabu yatokayo katika sheria yako.
    V. Wewe ndiwe Mungu ufanyaye maajabu.
    R. Uliudhihirisha uweza wako kati ya mataifa.

Tuombe

Mwenyezi Mungu, mpenda watu wote: Uwaangalie kwa rehema wote wajiwekao tayari kupokea [Sakramenti za Kanisa]*; uwape afya ya mwili na roho; uwahifadhi daima; uwafumbue mioyo walipokee kwa furaha Neno lako; uwatie nguvu wadumu kukupenda, hata wakazae matunda ya Roho kwa utukufu wako. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.

    * Au Mhudumu ataje Sakramenti fulani, ambayo wakati ule wengine wanajiweka tayari kuipokea.
 

We pray for we may be prepared to receive [the Sacraments of the Church] (?)

ALHAMISI

Sala ya Asubuhi

(1) Tuwaombee Wajiwekao tayari kupokea Daraja Takatifu

    Ant. Ee Bwana, utufundishe njia yako, nasi tutakwenda katika kweli yako; mioyo yetu na ifurahi kulicha Jina lako.
    V. Ee BWANA, uwaokoe watumishi wako.
    R. Wanaokutumaini Wewe.

Tuombe

Mwenyezi Mungu wa milele, unaabudiwa daima na Malaika Watakatifu, bali unachagua watu kuwa mawakili wa siri zako: Uwabariki, tunakusihi, wote wajiwekao tayari kupokea Daraja Takatifu, (na hasa . . . ); ili wale wasioweza kutenda neno pasipo Wewe wajazwe nawe usafi na upendo, na kuangazwa elimu ya kweli ya Neno lako na Sakramenti zako; hata wafanywe Wahudumu wa kufaa, na kuueneza utukufu wako na wokovu wa wateule wako. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

Thursday

Morning Prayer

We pray that we may be prepared to receive a holy rank (?)

2) Tuwaombee Wenye kitubio cha Kanisa

    Ant. Bwana, kama Wewe ungehesabu maovu; Ee Bwana, nani angesimama?
    V. Lakini kwako kuna msamaha.
    R. Ili Wewe uogopwe.

Tuombe

Ee Bwana, mwenye rehema nyingi, uwasamehe wote wenye kitubio: Na kwa ajili ya msalaba wa Mwokozi wetu, Yesu Kristo, na mateso yake, ulikubali toba lao. Uyasikie maombi yao, uzifute dhambi zao, uwavute mioyo na kuwaongezea upendo. Kwa Yeye, Kristo Bwana wetu. Amin.
 

We pray that ? repentance of the Church

Sala ya Jioni

(1) Tumshukuru Mungu kwa kuieneza Injili

    Ant. Neno langu, litokalo katika kinywa changu, halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu.
    V. Sauti yao imeenea duniani mwote.
    R. Na maneno yao hata miisho ya ulimwengu.

Tuombe

Ee Bwana, uliwatuma Mitume wako ili waende kuihubiri Injili kwa kila kiumbe, ukaahidi ya kuwa neno lako halitakurudia bure: Tunalihimidi Jina lako kwa kuwa kila mahali Imani ya Kikristo imeenea; tunakutukuza kwa ajili ya nuru ya Injili ya milele ilivyohubiriwa kwa kila taifa na kabila na jamaa na lugha, hata na kutufikia kwetu sisi katika nchi hii; nasi tunakuomba uitimize hesabu ya wateule wako na kuuhimiza ufalme wako. Uishiye na kumiliki, Mungu, milele na milele. Amin.
 

Evening Prayer

We give thanks to God for spreading the Gospel.

(2) Tuwaombee Wanafunzi wa Dini

    Ant. Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.
    V. Alituokoa kwa rehema yake.
    R. Kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili, na kufanywa upya na Roho Mtakatifu.

Tuombe

Ee Bwana, uwakumbuke wote wanaofundishwa ili wapate Ubatizo Mtakatifu: Uwarehemu, uwatie nguvu katika kuamini, na kuwaondolea uovu wo wote uliomo mioyoni mwao; hata wazidi kuwa imara katika kulishika Neno lako takatifu, wakaonekane wamestahili kubatizwa katika Kanisa lako takatifu, kwa kuondolewa dhambi zao. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin
 

We pray for students of religion

IJUMAA

Sala ya Asubuhi

(1) Tuwaombee Waislamu, wamkubali Bwana Kristo

    Ant. Bwana Mungu wetu ni BWANA mmoja; nawe mpende BWANA Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.
    V. BWANA, Mungu wako, atakuondokeshea nabii.
   R. Msikilizeni Yeye.

Tuombe

Mwenyezi Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Muumba watu wote na Baba yao: Usitazame dhambi zetu, bali uzikumbuke roho za watu uliowaumba uwajulishe Waislamu pendo lako la ubaba; ili waukubali ufunuo wa Mwana wako pekee, Yesu Kristo Bwana wetu. Aishiye na kumiliki, Mungu, milele na milele. Amin.
 

Friday

Morning Prayer

We pray that Moslems will accept the Lord Christ

(2) Tuwaombee Wasio Wakristo, waongozwe katika njia ya kweli

    Ant. Naliisikia sauti ya BWANA, akisema, Nimtume nani? Ndipo niliposema, Mimi hapa, nitume mimi.
    V. Mataifa wataliogopa Jina lako, BWANA.
    R. Na wafalme wote wa dunia utukufu wako.

Tuombe

Ee Mungu, kwa damu moja ulifanya kila taifa Ia watu wakaao juu ya nchi yote, ukamtuma Mwana wako pekee aihubiri amani kwao; Uwajalie watu wote wa nchi hii wakutafute na kukuona; ukaitimize hima ahadi yako ya kummimina Roho wako juu ya wote wenye mwili. Kwa Yeye, Kristo Bwana wetu. Amin.
 

We pray that all who are not Christians will be led into the way of truth

Sala ya Jioni

(1) Tumshukuru Mungu kwa sala za Watakatifu wake

    Ant. Mwimbieni. BWANA wimbo mpya, sifa zake katika kusanyiko la Watakatifu.
    V. Waupendao wokovu wako.
    R. Waseme daima, Atukuzwe BWANA.

Tuombe

Ee Mungu wa majeshi, katika maajabu uliyoyafanya katikati ya wanadamu umewawezesha Watakatifu wako ili waishi maisha ya utauwa : Tunakushukuru sana kwa msaada wa sala zao; na kuomba neema yako ili tuwafuate. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

Evening Prayer

We thank God for the prayers of his Saints

(2) Tuwaombee Walisikiao neno la Mungu

    Ant. Bwana, dunia imejaa fadhili zako, utufundishe amri zako.
    V. Ee BWANA, utuonyeshe rehema zako.
    R. Utupe wokovu wako.

Tuombe

Ee Mungu, mwenye rehema, katika ulinzi wako hukaa wanadamu wote: Uwajalie wote walisikiao neno lako walipende Jina lako; uwageuze mioyo wawe tayari kuacha dhambi na kuzitii amri zako; uwavute kwa pendo lako wasidanganywe na Shetani, bali wakufuate Wewe na kuushiriki wokovu wako. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

We pray that God will listen to our word

JUMAMOSI

Sala ya Asubuhi

(1) Tumwombe Mungu awaite watu ili waiingie maisha ya utauwa

    Ant. Jueni ya kuwa BWANA amejiteulia watauwa, naye atasikia wamwitapo.
    V. Ee Bwana, utuinulie nuru ya uso wako.
    R. Umewatia furaha mioyoni mwao.

Tuombe

Ee Bwana, una waongoza upendavyo waaminifu wako kwa Roho wako Mtakatifu: Tunakusihi, uwaite wengi katika Kanisa lako; ili waache mali, wazazi, hata na mapenzi yao wenyewe, waiingie maisha ya utauwa, na kujitwika msalaba, na kukufuata Wewe katika umaskini, na usafi, na utii. Na wale uliowaita, wanaume kwa wanawake, uwajalie neema yako tele, ili wachocheane katika upendo na kazi njema, na kwa mwenendo wao safi waieneze sifa yako. Uishiye na kumiliki, Mungu, milele na milele. Amin.
 

Saturday

Morning Prayer

We pray that God will call everyone so that they may enter into his life (?)

(2) Tuwaombee Wanadamu wote

    Ant. Fadhili na masamaha ni kwa BWANA, Mungu wetu, ingawa tumemwasi, wala hatukuitii sauti yake.
    V. Ee BWANA, fadhili zako zikae nasi.
    R. Kama vile tulivyokungoja Wewe.

Tuombe

Ee Mungu, Muumba wanadamu wote na kuwahifadhi, tunawaombea kwa unyenyekevu watu wote, upende kuwaonyesha njia zako na wokovu wako. Hasa tunaliombea Kanisa Katholiko, hali yake iwe njema. Tena, Ee Baba, tunawaombea walio na shida na huzuni iwayo yote, ya mwili au ya roho; [na hasa wao wanaotaka tuwaombee leo;] upende kuwafariji na kuwasaidia kwa kadiri ya mahitaji yao; uwajalie kuvumilia kwa saburi, na kutoka kwa furaha katika shida zao. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

We pray for all people

Sala ya Jioni

(1) Tumshukuru Mungu kwa ajili ya wote wanao-saidia kazi ya Kanisa

    Ant. Umehimidiwa, Ee BWANA, Mungu wa baba zetu; wastahili kusifiwa na kuadhimishwa milele.
    V. Tumhimidi Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.
    R. Tumsifu na kumwadhimisha milele.

Tuombe

Ee Mungu wa wokovu wetu, tunakushukuru sana kwa ajili ya watumishi wako, walioishika kweli yako na kufanya kazi katika Kanisa lako: Na hasa tunaliadhimisha Jina lako kuu kwa ajili ya wote, wenyeji kwa wageni, waliojitahidi kuieneza nuru ya Injili katika nchi hii yetu; uwasamehe makosa yao, uwakumbatie kwa rehema zako, uwajazi heri na kuwaonyesha utukufu wako. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

Evening Prayer

We thank God as a result of all ? work of the Church

(2) Tuwaombee Wakaao katika mitaa yetu

    Ant. Nitammimina Roho wangu juu ya wazao wako na baraka yangu juu yao utakaowazaa.
    V. Uwaokoe watu wako, BWANA.
    R. Uubariki urithi wako.

Tuombe

Mwenyezi Mungu wa milele, mtawala yote yaliyo mbinguni na yaliyo duniani: Utusikie sisi watumishi wako tukuombapo; Utujalie yote tunayoyahitaji kwa kazi ya Kanisa mitaani mwetu. Uwaimarishe waaminio; uwaongoze watoto; uwatie nuru wanafunzi; uwalinde wasikiaji; uwafariji wenye huzuni; uwatunze wagonjwa; uwatubishe wakaidi; uwafufue waliokufa roho; uwasimamishe walioanguka; uwarudishe watubuo; uyaondoe makwazo yote, ili kweli yako izidi kuenea; uwape wote umoja na amani katika Kanisa lako takatifu; kwa utukufu wa Jina lako. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

We pray for the continuation of our neighborhoods (?)

KWA WAFU

Sala hii na isemwe jioni panapo Missa ya Wafu ipo asubuhi ifuatayo.

(3) Tuwaombee Waliofariki katika imani

    Ant. Wa heri wafu wafao katika BWANA. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao.
    V. Raha ya milele uwajalie, Ee BWANA.
    R. Na nuru ya daima iwaangaze.

Tuombe

Mwenyezi Mungu, kwako waishi wote: Tunakusihi uzikumbuke roho zao wote walioifariki dunia katika imani ya kweli na kicho chako, [na hasa* N.]; Uwakumbuke na wazee wetu, ndugu zetu, rafiki zetu, na wote wanaotuhusu. Uwape, Ee Bwana, raha, nuru, na amani, panapo kuburudika na kufurahi. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.

* Ikiwa ni Missa ya mtu fulani, na atajwe katika sala hiyo.
 

For the Dead

 

We pray for all who have died in the faith

SIKU ZA ROBO MWAKA

Sala hizi na zisemwe siku za Robo mwaka.

JUMATANO YA ROBO MWAKA

(3) Tuwaombee Maaskofu

    Ant. Watoto wako utawafanya kuwa wakuu katika nchi zote.
    V. Ee Mungu, Ngao yetu, uangalie.
    R. Umtazame uso Masihi wako.

Tuombe

Mwenyezi Mungu, kwa Mwana wako Yesu Kristo uliwapa Mitume wako watakatifu karama bora nyingi, ukawaamuru kuwalisha kundi lako: Uwajalie, tunakusihi, Maaskofu wote, walichungao Kanisa lako, walihubiri Neno lako, na kuzifuata amri zako; uwajalie watu wako kuwatii; ili wote waipokee taji ya utukufu wa milele. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

Ember Days

 

Wednesday

We pray for Bishops

IJUMAA YA ROBO MWAKA

(3) Tuwaombee Makasisi

    Ant. Kwa Jina lako hufurahi mchana kutwa, na kwa haki yako hutukuzwa.
    V. Umewapa ngao ya wokovu wako.
    R. Na unyenyekevu wako umewakuza.

Tuombe

Ee Bwana Mtakatifu, Baba Mwenyezi, Mungu wa milele, uwazidishie Makasisi wako wote karama za neema yako: Ili wahudumuo mbele ya madhabahu zako takatifu waimarishwe katika imani; wawafalie watu wako kwa kuwa nyeupe roho zao. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

Friday

We pray for Priests

JUMAMOSI YA ROBO MWAKA

(3) Tuwaombee Watakaoamriwa Huduma yo yote katika Kanisa

    Ant. Ee Bwana, utufundishe njia yako, nasi tutakwenda katika kweli yako; mioyo yetu na ifurahi kulicha Jina lako.
    V. Ee BWANA, uwaokoe watumishi wako.
    R. Wanaokutumaini Wewe.

Tuombe

Mwenyezi Mungu, mtoa mambo yote yaliyo mema, uliamuru kwa hekima yako ya Uungu Daraja mbalimbali katika Kanisa lako: Tunakusihi kwa unyenyekevu, uwape neema yako watu wote watakaoitwa kwa kazi yo yote na huduma katika Kanisa; uwajaze kweli ya elimu yako, uwa pambe maisha safi, wapate kutumika amini mbele zako, Jina lako kuu litukuzwe, na Kanisa lako takatifu likafaidiwe. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

Saturday

We pray that what we ask for may give help in all of your Church

KILA SIKU

Mhudumu akiisha sema sala zote za kuombea, watu wote waseme sala hizi za mwisho, kila mtu peke yake kimoyomoyo.

Baba yetu.

Msaada wa Mungu ukae nasi daima. Amin.
 

Every Day

 

 
Lord's Prayer

MAOMBEZI MENGINE

Tumshukuru Mungu kwa karama za Roho Mtakatifu.

    Ant. Katika hili tunafahamu ya kuwa tunakaa ndani yake, naye ndani yetu, kwa kuwa ametushirikisha Roho wake.
    V. Wampeleka Roho wako, wanaumbwa.
    R. Nawe waufanya upya uso wa nchi.

Tuombe

Mwenyezi Mungu, mtoa mambo yote yaliyo mema: Tunakushukuru sana kwa vipawa vyako vyote vya uzima na afya; na hasa kwa karama yako kuu ya kutupa Roho wako Mtakatifu awe Rafiki yetu na Kiongozi wetu. Tunakusihi utuvute mioyo yetu ili tuitii sauti yake katika dhamiri zetu; tuitumie vema neema atupayo, na karama zake saba za ajabu; tumpokee sikuzote kwa heshima; na kuelimishwa njia ya haki kwa mafundisho yake ya upole. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

Intecessions at other times

We give thanks to God for the honor of the Holy Spirit

Tumshukuru Mungu kwa ajili ya ndugu zetu waliopokea Sakramenti ya . . . .

    Ant. Bwana ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana, wala ukuu wake hautambulikani,
    V. BWANA huwaridhia wao wamchao.
    R. Na kuzitarajia fadhili zake.

Tuombe

Ee Mungu, tunakushukuru sana, na kulitukuza Jina lako, kwa fadhili zako zote, za leo na za kila siku: Na hasa kwa ukombozi aliotuletea Bwana wetu Yesu Kristo, na neema ya utakaso tupewayo katika Sakramenti za Kanisa; tunakuadhimisha kwa ajili ya ndugu zetu waliopokea Sakramenti ya...; uwaimarishe kwa Roho wako Mtakatifu, uwazidishie matendo mema, uwahifadhi majaribuni, uwajalie kumshinda adui wetu, na hatimaye uwalete kunako ufalme wako wa milele. Kwa Yeye, Kristo Bwana wetu. Amin.
 

We give thanks to God for the sake of our brothers / sisters who were welcomed in the Sacrament of . . .

Tumshukuru Mungu kwa kutuondolea tauni (au ugonjwa).

    Ant. Sauti ya furaha na wokovu imo hemani mwao wenye haki; mkono wa kuume wa BWANA hutenda makuu.
    V. Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji.
    R. Na katika tauni iharibuyo.

Tuombe

Ee Bwana Mungu wetu, una haki kutupiga kwa makosa yetu na kutuadhibisha kwa maovu yetu, bali wakati wa hukumu unakumbuka rehema: Tunakuhimidi na kukushukuru kwa jinsi ulivyotuopoa katika hatari ya kuambukizwa; utujalie, tunakusihi, tujitoe nafsi zetu ziwe sadaka kwako, na kukusifu daima katika Kanisa lako Takatifu. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

We give thanks to God for relief from the plague (or sickmess)

Tumshukuru Mungu kwa kutuletea mvua.

    Ant. Ee Mungu, ulinyesha mvua ya neema; urithi wako ulipochoka uliutia nguvu.
    V. Huzifunika mbingu kwa mawingu.
    R. Huitengenezea nchi mvua.

Tuombe

Mwenyezi Mungu, Baba yetu wa mbinguni, kwa wema wako watupa mvua kutoka mbinguni na nyakati za mavuno, ukitujaza mioyo yetu chakula na furaha: Tunakushukuru kwa unyenyekevu kwa sababu umependa kutuletea mvua siku hizi, na kutufariji wakati wa uhitaji wetu; utujalie neema yako, ili tuzitumie vema fadhili zako zote kwa utukufu wa Jina lako. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

We give thanks to God for bringing us rain

Tumshukuru Mungu kwa baraka za mavuno.

    Ant. Mshukuruni Bwana kwa kuwa yu mwema, kwa maana fadhili zake ni za milele.
    V. Na ahimidiwe BWANA, tangu milele hata milele.
    R. Watu wote na waseme, Amin. Msifuni BWANA.

Tuombe

Ee Baba, mwenye fadhili zote, tunakushukuru sana kwa kuwa umezibariki kazi za wakulima, ukatupa tena mwaka huu mazao ya nchi yetu: Tunakusihi utukirimie neema yako, mioyo yetu ikuzalie mazao ya matendo mema; ili tuone kibali machoni pako. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

We give thanks to God for blessing our harvest

Kushukuru baada ya Safari

    Ant. Tumshukuru BWANA kwa fadhili zake, na maajabu yake kwa wanadamu.
    V. Aliwaongoza kwa njia ya kunyoka.
    R. Wapate kwenda mpaka mji wa kukaa.

Tuombe

Baba Mwenyezi, tunakushukuru sana kwa kuwa umetufanikisha safari yetu, ukatulinda, na kutufikisha salama: Nasi tunakuomba utuongoze katika safari yetu ya maisha haya; ukatulete kwenye kiti chako cha enzi mbinguni, tukae nawe milele. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

Thanksgiving after a journey

Tuwaombee wote wafanyao kazi ya dawa.

    Ant. Wenye afya hawana haja na tabibu, bali wale walio hawawezi.
    V. Yu heri kila mtu amchaye BWANA.
    R. Aendaye katika njia yake.

Tuombe

Ee Bwana Yesu Kristo, ndiwe peke yako uliye Mponya wote: Tunakuomba uwabariki wote wafanyao kazi ya dawa katika Hospitali zetu na kila mahali; ili wafuatane nawe kila saa, na kuzitumia akili zao kama ipasavyo; uzibariki na dawa ili ziwafalie wenye kuugua, hata wakapone kwa rehema zako na kama ikupendezavyo. Uishiye na kumiliki, Mungu, milele na milele. Amin.
 

We pray for all those working in medicine

Tumwombe Mungu aibariki kazi ya Hospitali na Dawani.

    Ant. Walimletea wote waliokuwa hawawezi, walio-shikwa na maradhi mbalimbali na mateso; akawaponya.
    V. Huwaponya waliopondeka moyo.
    R. Na kuziganga jeraha zao.

Tuombe

Mwenyezi Mungu, mwenye rehema, tunakukimbilia Wewe kwa sababu tunajua hakika ya kwamba una nguvu, na uweza wote wa kuponya. Tunakusihi uwatazame wagonjwa wote na kuwahurumia. Uwabariki wote wanaouguza wagonjwa katika Hospitali zetu na Dawani; uwajalie huruma na upendo ili wawatunze vema, na akili ya kuyakinisha ugonjwa. Uzibariki dawa zinazotumika ili zifae kwa kuleta afya na uzima. Uwajalie wagonjwa saburi na tumaini ili wayavumilie maumivu yao; uwape neema ya kukutumaini Wewe katika shida yao; uwavute mioyo ili watamani kufundishwa, hata wakujue Wewe uliye Mungu wa kweli, wawe wako katika ulimwengu huu na katika ulimwengu ujao. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

We pray to God to bless the work of the Hospital and councilor (?)

Tuombe msaada wa Mungu wakati huu wa tauni (au ugonjwa).

    Ant. Ee Mungu, mbona umetutupa milele? Kwa nini hasira yako inatoka moshi?
    V. Ndiwe msaada wetu na Mwokozi wetu.
    R. Ee Mungu wetu, usikawie.

Tuombe

Ee Mungu, hupendi mwenye dhambi afe, bali atubu na kuishi: Uwatazame kwa huruma watu wako wanapokurudia; ili tuondolewe mapigo yako, na kukutumikia kwa uaminifu. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

We pray for God's help in this time of plague (or sickmess)

Tuombe msaada wa Mungu wakati huu wa machafuko ya dunia.

    Ant. Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya BWANA, dunia na wote wakaao ndani yake.
    V. Mungu awamiliki mataifa.
    R. Mungu ndiye Mfalme wa dunia yote.

Tuombe

Ee Bwana, tunakusihi, uyaongoze mambo ya ulimwengu huu: Ili machafuko yote yaondolewe; na mataifa yote wakae kwa amani na usitawi kama ikupendezavyo. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

We pray for God's help in this time of disorders in the world

Tuombe msaada wa Mungu wakati huu wa vita.

    Ant. Ee Bwana, uondoke, uwe msaada wetu, utukomboe kwa ajili ya fadhili zako.
    V. Utuletee msaada juu ya mtesi.
    R. Maana wokovu wa binadamu haufai.

Tuombe

Mwenyezi Mungu, Wewe peke yako waweza kuzitawala nia kaidi za watu wakosao : Tunakuomba utusamehe dhambi zetu zilizo nyingi sana; uvikomeshe vita vilivyopo leo; uwajalie mataifa yote wakae katika umoja na amani. Uwahurumie wale waliotekwa vitani; uwafariji wateswao mwili na roho; nao waliokufa uwarehemu na kuwasafisha katika dhambi zao. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

We pray for God's help in this time of war

Tumwombe Mungu awahurumie wafungwa (na waliotekwa vitani).

    Ant. Enyi mmtafutao Mungu, mioyo yenu ihuishwe, kwa kuwa BWANA hawadharau wafungwa wake.
    V. Kuugua kwake aliyefungwa.
    R. Kuingie mbele zako, BWANA.

Tuombe

Ee Bwana, waweza kuondoa taabu na mateso yo yote ya mwili au ya roho: Tunakuomba uwasaidie wote wanao-kukimbilia, na hasa uwafariji wafungwa wote (nao waliotekwa vitani); ili wakipata kutoka katika shida zao wa1ihimidi Jina lako, na kukutumikia vema katika maisha ya utakatifu. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

We pray that God will take pity on captives (those taken hostage)

Tumwombe Mungu alete amani duniani.

    Ant. Ee Bwana, utatuamuria amani; maana ndiwe uliyetutendea kazi zetu zote.
    V. BWANA atawapa watu wake nguvu.
    R. Atawabariki watu wake kwa amani.

Tuombe

Mwenyezi Mungu, kwako Wewe hutoka mawazo yote ya kweli na amani: Tunakuomba, uwashe katika mioyo ya watu wote pendo la amani, na kuwaongoza kwa hekima yako wote watawalao mataifa wa dunia; ili ufalme wako uzidi kusitawi katika utulivu, hata dunia ijae habari za upendo wako. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

We pray that God will resolve to bring peace. (?)

Tumwombe Mungu atuzidishie upendano.

    Ant. Hivi watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.
    V. Jinsi ilivyo vema na kupendeza kama nini.
    R. Ndugu wakae pamoja, pia kwa umoja.

Tuombe

Ee Mungu, Baba wa wanadamu wote, unampenda kila mtoto wako ukitaka sisi sote tupendane: Utuzidishie, tunakusihi, udugu na upendano wa kweli kati ya Wakristo wote; ili tupendane sisi kwa sisi, na kusaidiana, na kuungamana katika Imani moja iliyo kweli; hata kwa moyo mmoja na kwa kinywa kimoja tukutukuze Wewe uliye Mungu mmoja. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

We pray that God will increase our mutual affection.

Tuwaombee wote wenye dhambi ili wapate kutubu.

    Ant. Uturudishe, Ee Mungu wa wokovu wetu; uikomeshe hasira uliyo nayo juu yetu.
    V. Ubaya wao wasio haki na ukome.
    R. Lakini umthibitishe mwenye haki.

Tuombe

Mwenyezi Mungu, tunakusihi: Uyasikie maombi yetu kwa ajili ya wote watendao dhambi, na waliorudi nyuma wakaacha kukutumikia ; uwajalie toba la kweli, na moyo wa kutii, na bidii ya kujitengeneza roho, ili wakurudie. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

We pray that all those suffering from sin will repent

Tumwombe Mungu ayabariki mashamba yetu.

    Ant. Wamtafutao BWANA hawatahitaji kitu cho chote kilicho chema.
    V. Ombeni nanyi mtapewa.
    R. Tafuteni nanyi mtaona.

Tuombe

Mwenyezi Mungu, kwako Wewe twapata chakula chetu kila mwaka: Uyabariki mashamba yetu ili tupate mazao yake; utuletee jua na mvua kadiri itakavyotufaa; wala usituache kupoteza roho zetu kwa ajili ya riziki za duniani. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

We pray to God for success for our farms

Tumwombe Mungu atuletee mvua.

    Ant. Ikiwa mbingu zimefungwa, wala hakuna mvua kwa sababu tumekukosa, tuombapo unyeshe mvua juu ya nchi yako.
    V. Huinywesha milima toka orofa zake.
    R. Nchi imeshiba mazao ya kazi zake.

Tuombe

Ee Mungu, ndani yako Wewe tunaishi, tunakwenda, tuna uhai wetu: Utujalie mvua ya kadiri utakavyoona vema; ili sisi tupokee baraka zako za maisha haya, na kuzidi kutafuta kwa bidii baraka za milele. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

We pray that God will bring us rain.

Tumwombe Mungu atuhifadhi na nzige.

    Ant. Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.
    V. Uziamshe nguvu zako.
    R. Ee BWANA, uje utuokoe.

Tuombe

Mwenyezi Mungu, uliibariki ardhi itoe mazao yake kwa matumizi ya wanadamu: Tunakusihi kwa unyenyekevu uzifanikishe kazi za wakulima, na wakati huu utuponye na nzige; ili tupate mavuno yetu na kuushangilia wema wako. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

We pray that God will save us from locusts

Tumwombe Mungu atuepushe na njaa.

    Ant. Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
    V. Huyameesha majani kwa makundi.
    R. Na mboga kwa matumizi ya mwanadamu.

Tuombe

Ee Bwana, uzisikilize haja zetu tunazokuomba kwa unyenyekevu: Na kwa rehema zako utuepushe na njaa; ili sisi tuliojipatia adhabu kwa makosa yetu tuponywe kwa huruma zako. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
 

We pray that God will spare us from hunger

Kabla ya Safari

    Ant. Bwana ndiye mchungaji wangu; sitapungukiwa na kitu
    V. Walimlilia BWANA katika dhiki zao.
    R. Akawaponya na shida zao.

Tuombe

Ee Mungu, ulimwita Ibrahimu atoke kwao, aende utakakomleta, ukamlinda sana katika safari zake zote: Uwaangalie sasa hawa N. na N. wanaosafiri; uwajalie safari njema, amani njiani, na kufika salama; uwatie kivuli kunako jua, uwaokoe katika dhoruba, uwalinde na taabu zote; nasi tukiisha safari yetu ya maisha haya hapa duniani, utuongoze kwetu mbinguni. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.

Before a journey

 

Return to the Zanzibar Prayer Book

Web author: Charles Wohlers U. S. EnglandScotlandIrelandWalesCanadaWorld