SALA YA ADHUHURI
Baba yetu. Salamu, Mariamu.
¶ Mhudumu aseme,
V. Ee Mungu, uwe radhi kutuokoa.
R. Ee BWANA, utusaidie hima.
Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.
Kama ilivyokuwa mwanzo na iwe sasa na sikuzote, na hata milele na milele. Amin.
V. Msifuni BWANA.
R. Jina la BWANA lisifiwe.
¶ Ndipo huimbwa WIMBO.
Tuni, 2,9
Ee Mungu, mwenye nguvu zote,
Wayaamuru mambo yote;
Mapambazuko asubuhi,
Na jua kali adhuhuri.
Uzime moto wa ugomvi,
Tamaa mbaya ziondoe;
Amani tupe mioyoni,
Na afya miilini mwetu
Tuangazie nuru yako,
Tusije tukaona giza;
Kwa kufa kwema tujalie
Kupata raha ya milele.
Ee Baba, hayo ruombayo
Kwa Mwana wako tujalie ;
Ami1ikiye sikuzote
Pamoja nawe, naye Roho. Amin.
(Ubeti huu wa mwisho hubadiliwa.)
¶ Ndipo ZABURI husemwa, kama kawaida.
|
Lord's Prayer; Hail Mary |
Siku ya Bwana
Ant. Kwa moyo wangu. Ant. Pasaka. Haleluya.
ZAB. 119
1. Wa heri walio kamili njia zao, * Waendao katika sheria ya BWANA.
2. Wa heri wazitiio shuhuda zake, * Wamtafutao kwa moyo wote.
3. Naam, hawakutenda ubatili; * Wamekwenda katika njia zake.
4. Wewe umetuamuru mausia yako, * Ili sisi tuyatii sana.
5. Ningependa njia zangu ziwe thabiti, * Nizitii amri zako.
6. Ndipo mimi sitaaibika, * Nikiyaangalia maagizo yako yote.
7. Nitakushukuru kwa unyofu wa moyo, * Nikiisha kujifunza hukumu zako za haki.
8. Nitazitii amri zako; * Usiniache kabisa.
Atukuzwe.
9. Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? * Kwa kutii akilifuata neno lako.
10. Kwa moyo wangu wote nimekutafuta; * Usiniache nipotee mbali na maagizo yako.
11. Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, * Nisije nikakutenda dhambi.
12. Wewe, BWANA, umehimidiwa; * Unifundishe amri zako.
13. Kwa midomo yangu nimezisimulia * Hukumu zote za kinywa chako.
14. Nimeifurahia njia ya shuhuda zako, * Kana kwamba ni mali nyingi.
15. Nitayatafakari mausia yako, * Nami nitaziangalia njia zako.
16. Nitajifurahisha sana kwa amri zako; * Sitalisahau neno lako.
Atukuzwe.
17. Umtendee mtumishi wako ukarimu, * Nipate kuishi nami nitalitii neno lako.
18. Unifumbue macho yangu niyatazame * Maajabu yatokayo katika sheria yako.
19. Mimi ni mgeni katika nchi; * Usinifiche maagizo yako.
20. Roho yangu imepondeka kwa kutamani * Hukumu zako kila wakati.
21. Umewakemea wenye kiburi; * Wamelaaniwa waendao mbali na maagizo yako.
22. Uniondolee laumu na dharau, * Kwa maana nimezishika shuhuda zako.
23. Wakuu nao waliketi wakaninena, * Lakini mtumishi wako atazitafakari amri zako.
24. Shuhuda zako nazo ndizo furaha yangu, * Na washauri wangu.
Atukuzwe.
25. Nafsi yangu imeambatana na mavumbi; * Unihuishe sawasawa na neno lako.
26. Nalizisimulia njia zangu ukanijibu; * Unifundishe amri zako.
27. Unifahamishe njia ya mausia yako, * Nami nitayatafakari maajabu yako.
28. Nafsi yangu imeyeyuka kwa uzito; * Unitie nguvu sawasawa na neno lako.
29. Uniondolee njia ya uongo; * Unineemeshe kwa sheria yako.
30. Nimeichagua njia ya uaminifu, * Na kuziweka hukumu zako mbele yangu.
31. Nimeambatana na shuhuda zako; * Ee BWANA, usiniaibishe.
32. Nitakwenda mbio katika njia ya maagizo yako, * Utakaponikunjua moyo wangu.
Atukuzwe.
Ant. Kwa moyo wangu wote nimekutafuta; Ee BWANA, unifundishe amri zako.
Ant. Pasaka. Haleluya, Haleluya, Haleluya.
|
Sunday
Psalm 119 |
Jumatatu
Ant. Uniendeshe. Ant. Pasaka. Haleluya.
33. Ee BWANA, unifundishe njia ya amri zako, * Nami nitaishika hata mwisho.
34. Unifahamishe nami nitaishika sheria yako, * Na kuitii kwa moyo wangu wote.
35. Uniendeshe katika mapito ya maagizo yako, * Kwa maana nimependezwa nayo.
36. Unielekeze moyo wangu na shuhuda zako, * Wala usiielekee tamaa.
37. Unigeuze macho yangu nisitazame visivyofaa; * Unihuishe katika njia yako.
38. Umthibitishie mtumishi wako ahadi yako, * Inayohusu kicho chako.
39. Uniondolee laumu niiogopayo, * Maana hukumu zako ni njema.
40. Tazama nimeyatamani mausia yako; * Unihuishe kwa haki yako.
Atukuzwe.
41. Ee BWANA, fadhili zako zinifikie na mimi; * Naam, wokovu wako sawasawa na ahadi yako.
42. Nami nitamjibu neno anilaumuye, * Kwa maana nalitumainia neno lako.
43. Usiliondoe neno la kweli kinywani mwangu kamwe, * Maana nimezingojea hukumu zako.
44. Nami nitaitii sheria yako daima; * Naam, milele na mlele.
45. Nami nitakwenda panapo nafasi, * Kwa kuwa nimejifunza mausia yako.
46. Nitazinena shuhuda zako mbele ya wafalme, * Wala sitaona aibu.
47. Nami nitajifurahisha sana kwa maagizo yako, * Ambayo nimeyapenda.
48. Na mikono yangu nitayainulia maagizo yako, * Nami nitazitafakari amri zako.
Atukuzwe.
49. Likumbuke neno ulilomwambia mtumishi wako, * Kwa sababu umenitumainisha.
50. Hii ndiyo faraja yangu katika taabu yangu, * Ya kwamba ahadi yako imenihuisha.
51. Wenye kiburi wamenidharau mno; * Sikujiepusha na sheria yako.
52. Nimezikumbuka hukumu zako za kale, * Ee BWANA, nikajifariji.
53. Ghadhabu imenishika kwa sababu ya wasio haki, * Waiachao sheria yako.
54. Amri zako zimekuwa nyimbo zangu * Katika nyumba ya ugeni wangu.
55. Wakati wa usiku nimelikumbuka Jina lako, * Ee BWANA, nikaitii sheria yako.
56. Hayo ndiyo niliyokuwa nayo * Kwa sababu nimeyashika mausia yako.
Atukuzwe.
Ant. Uniendeshe, Ee BWANA, Katika mapito ya maagizo yako.
Ant. Pasaka. Haleluya, Haleluya, Haleluya.
|
Monday |
Jumanne
Ant. Rehema zako. Ant. Pasaka. Haleluya.
57. BWANA ndiye aliye fungu langu; * Nimesema kwamba nitayatii maneno yako.
58. Nimekuomba radhi kwa moyo wangu wote; * Unifadhili sawasawa na ahadi yako.
59. Nalizitafakari njia zangu, * Na miguu yangu nikazielekezea shuhuda zako
60. Nalifanya haraka wala sikukawia * Kuyatii maagizo yako.
61. Kamba za wasio haki zimenifunga; * Sikuisahau sheria yako.
62. Katikati ya usiku nitaamka nikushukuru, * Kwa sababu ya hukumu zako za haki.
63. Mimi ni mwenzao watu wote wakuchao, * Na wale wayatiio mausia yako.
64. BWANA, dunia imejaa fadhili zako; * Unifundishe amri zako.
Atukuzwe.
65. Umemtendea mema mtumishi wako, * Ee BWANA, sawasawa na neno lako.
66. Unifundishe akili na maarifa, * Maana nimeyaamini maagizo yako.
67. Kabla sijateswa mimi nalipotea, * Lakini sasa nimelitii neno lako.
68. Wewe U mwema na mtenda mema; * Unifundishe amri zako.
69. Wenye kiburi wamenizulia uongo; * Kwa moyo wangu wote nitayashika mausia yako.
70. Mioyo yao imenenepa kama shahamu; * Mimi nimeifurahia sana sheria yako.
71. Ilikuwa vema kwangu kuwa na1iteswa, * Nipate kujifunza amri zako.
72. Sheria ya kinywa chako ni njema kwangu, * Kuliko maelfu ya dhahabu na fedha.
Atukuzwe.
73. Mikono yako ilinifanya ikanitengeneza; * Unifahamishe nikajifunze maagizo yako.
74. Wakuchao na wanione na kufurahi, * Kwa sababu nimelingojea neno lako.
75. Najua ya kuwa hukumu zako ni za haki, * Ee BWANA, na kwa uaminifu umenitesa.
76. Nakuomba fadhili zako ziwe faraja kwangu, * Sawasawa na ahadi yako kwa mtumishi wako.
77. Rehema zako zinijie nipate kuishi, * Maana sheria yako ni furaha yangu.
78. Waaibike wenye kiburi walionidhulumu kwa uongo; * Mimi nitayatafakari mausia yako.
79. Wakuchao na wanirudie,
* Nao watazijua shuhuda zako.
80. Moyo wangu na uwe mkamilifu katika amri zako, * Nisije mimi nikaaibika.
Atukuzwe.
Ant. Rehema zako, Ee BWANA, Zinijie nipate kuishi.
Ant. Pasaka. Haleluya, Haleluya, Haleluya.
|
Tuesday |
Jumatano
Ant. Mimi ni wako. Ant. Pasaka. Haleluya.
81. Nafsi yangu imefifia kwa kuutamani wokovu wako; * Nimelingojea neno lako.
82. Macho yangu yamefifia yakiitazamia ahadi yako, * Nisemapo, Lini utakaponifariji ?
83. Maana nimekuwa kama kiriba katika moshi; * Sikuzisahau amri zako.
84. Siku za mtumishi wako zi ngapi? * Lini utakapowahukumu wale wanaonifuatia ?
85. Wenye kiburi wamenichimbia mashimo, * Ambao hawaifuati sheria yako.
86. Maagizo yako yote ni amini; * Wananifuatia bure, unisaidie.
87. Walikuwa karibu na kunikomesha katika nchi, * Lakini sikuyaacha mausia yako.
88. Unihuishe kwa fadhili zako, * Nami nitazishika shuhuda za kinywa chako.
Atukuzwe.
89. Ee BWANA, neno lako lasimama * Imara mbinguni hata milele.
90. Uaminifu wako upo kizazi baada ya kizazi; * Umeiweka nchi nayo inakaa.
91. Kwa hukumu zako vimesimama imara hata leo, * Maana vitu vyote ni watumishi wako.
92. Kama sheria yako isingalikuwa furaha yangu, * Hapo ningalipotea katika taabu zangu.
93. Hata milele sitayasahau maagizo yako, * Maana kwa hayo umenihuisha.
94. Mimi ni wako, uniokoe, * Kwa maana nimejifunza mausia yako.
95. Wasio haki wameniotea ili kunipoteza; * Nitazitafakari shuhuda zako.
96. Nimeona ukamilifu wote kuwa na mwisho, * Bali agizo lako ni pana mno.
Atukuzwe.
97. Sheria yako naipenda mno ajabu; * Ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa.
98. Maagizo yako hunitia hekima kuliko adui zangu, * Kwa maana ninayo sikuzote.
99. Ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote, * Maana shuhuda zako ndizo nizifikirizo.
100. Ninao ufahamu kuliko wazee, * Kwa kuwa nimeyashika mausia yako.
101. Nimeiepusha miguu yangu na kila njia mbaya, * Ili mimi nilitii neno lako.
102. Sikujiepusha na hukumu zako, * Maana Wewe mwenyewe umenifundisha.
103. Mausia yako ni matamu sana kwangu, * Kupita asali kinywani mwangu.
104. Kwa mausia yako najipatia ufahamu; * Ndiyo maana naichukia kila njia ya uongo.
Atukuzwe.
Ant. Mimi ni wako; Uniokoe, Ee BWANA.
Ant. Pasaka. Haleluya, Haleluya, Haleluya.
|
Wednesday |
Alhamisi
Ant. Usiniache. Ant. Pasaka. Haleluya.
105. Neno lako ni taa ya miguu yangu, * Na mwanga wa njia yangu.
106. Nimeapa nami nitaifikiliza * Kuzishika hukumu za haki yako.
107. Ee BWANA, nimeteswa mno; * Unihuishe sawasawa na neno lako.
108. Ee BWANA, uziridhie sadaka za kinywa changu, * Na kunifundisha hukumu zako.
109. Nafsi yangu imo mkononi mwangu daima, * Lakini sheria yako sikuisahau.
110. Watendao uovu wamenitegea mtego, * Lakini sikuikosa njia ya mausia yako.
111. Shuhuda zako nimezifanya urithi wa milele, * Maana ndizo changamko la moyo wangu.
112. Nimeuelekeza moyo wangu nizitende amri zako, * Daima, naam, hata milele.
Atukuzwe.
113. Watu wa kusita-sita nawachukia; * Lakini sheria yako naipenda.
114. Ndiwe sitara yangu na ngao yangu; * Neno lako nimelingojea.
115. Enyi watenda mabaya, ondokeni kwangu, * Niyashike maagizo ya Mungu wangu.
116. Unitegemeze sawasawa na ahadi yako nikaishi, * Wala usiniache niyaaibikie matumaini yangu.
117. Unisaidie nami nitakuwa salama, * Nami nitaziangalia amri zako daima.
118. Umewakataa wote wazikosao amri zako; * Kwa maana hila zao ni uongo.
119. Wabaya wa nchi pia umewaondoa kama takataka; * Ndiyo maana nimezipenda shuhuda zako.
120. Mwili wangu unatetemeka kwa kukucha Wewe, * Nami ninaziogopa hukumu zako.
Atukuzwe.
121. Nimefanya hukumu na haki; * Usiniache mikononi mwao wanaonionea.
122. Uwe mdhamini wa mtumishi wako nipate mema; * Wenye kiburi wasinionee.
123. Macho yangu yamefifia kwa kutamani wokovu, * Na ahadi ya haki yako.
124. Zilivyo rehema zako umtendee mtumishi wako, * Na amri zako unifundishe.
125. Mimi ni mtumishi wako, unifahamishe, * Nipate kuzijua shuhuda zako.
126. Wakati umewadia BWANA atende kazi, * Kwa kuwa wameitangua sheria yako.
127. Ndiyo maana nimeyapenda maagizo yako, * Kuliko dhahabu, naam, dhahabu iliyo safi.
128. Mradi nayaona mausia yako yote kuwa ya adili; * Kila njia ya uongo naichukia.
Atukuzwe.
Ant. Usiniache, Ee BWANA, Niyaaibikie matumaini yangu.
Ant. Pasaka. Haleluya, Haleluya, Haleluya.
|
Thursday |
Ijumaa
Ant. Umwangazie. Ant. Pasaka. Haleluya.
129. Shuhuda zako ni za ajabu; * Ndiyo maana roho yangu imezishika.
130. Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, * Na kumfahamisha mjinga.
131. Na1ikifumbua kinywa changu nikatweta, * Maana na1iyatamani maagizo yako.
132. Unigeukie unirehemu mimi, * Kama iwahusuvyo wa1ipendao Jina lako.
133. Uzielekeze hatua zangu kwa neno lako, * Uovu usije ukanimiliki.
134. Unikomboe na dhuluma ya mwanadamu, * Nipate kuyashika mausia yako.
135. Umwangazie mtumishi wako uso wako, * Na kunifundisha amri zako.
136. Macho yangu yachuruzika mito ya maji, * Kwa sababu hawaitii sheria yako.
Atukuzwe.
137. BWANA, Wewe ndiwe mwenye haki, * Na hukumu zako ndizo za adili.
138. Umeziagiza shuhuda zako kwa haki, * Na kwa uaminifu mwingi.
139. Juhudi yangu imeniangamiza, * Mradi watesi wangu wameyasahau maneno yako.
140. Neno lako limesafika sana; * Kwa hiyo mtumishi wako amelipenda.
141. Mimi ni mdogo, nadharauliwa, * Lakini siyasahau mausia yako.
142. Haki yako ni haki ya milele, * Na sheria yako ni kweli.
143. Taabu na dhiki zimenipata; * Maagizo yako ni furaha yangu.
144. Haki ya shuhuda zako ni ya milele; * Unifahamishe nami nitaishi.
Atukuzwe.
145. Nimeita kwa moyo wangu wote, uitike, * Ee BWANA, nitazishika amri zako.
146. Nimekuita Wewe, uniokoe, * Nami nitazishika shuhuda zako.
147. Kutangulia mapambazuko naliomba msaada; * Naliyangojea maneno yako kwa tumaini.
148. Macho yangu yalitangulia makesha ya usiku, * Ili kuitafakari ahadi yako.
149. Uisikie sauti yangu sawasawa na fadhili zako; * Ee BWANA, unihuishe sawasawa na hukumu zako.
150. Wanakaribia wanaonifuatia kwa chuki; * Wamekwenda mbali na sheria yako.
151. BWANA, Wewe U karibu, * Na maagizo yako yote ni kweli.
152. Tokea zamani nimejua kwa shuhuda zako * Ya kuwa umeziweka zikae milele.
Atukuzwe.
Ant. Umwangazie mtumishi wako Uso wako, Ee BWANA.
Ant. Pasaka. Haleluya, Haleluya, Haleluya.
|
Friday |
Jumamosi
Ant. Unifahamishe. Ant. Pasaka. Haleluya.
153. Uyaangalie mateso yangu uniokoe, * Maana sikuisahau sheria yako.
154. Unitetee na kunikomboa; * Unihuishe sawasawa na ahadi yako.
155. Wokovu u mbali na wasio haki, * Kwa maana hawajifunzi amri zako.
156. Ee BWANA, rehema zako zi nyingi, * Unihuishe sawasawa na hukumu zako.
157. Wanaonifuatia na watesi wangu ni wengi, * Lakini sikujiepusha na shuhuda zako.
158. Nimewaona watendao uhaini nikachukizwa, * Kwa sababu hawakulitii neno lako.
159. Uangalie niyapendavyo mausia yako; * Ee BWANA, unihuishe sawasawa na fadhili zako.
160. Jumla ya neno lako ni kweli, * Na kila hukumu yako ya haki ni ya milele.
Atukuzwe.
161. Wakuu wameniudhi bure, * Ila moyo wangu unayahofia maneno yako.
162. Naifurahia ahadi yako * Kama apataye mateka mengi.
163. Nimeuchukia uongo, umenikirihi; * Sheria yako nimeipenda.
164. Mara saba kila siku nakusifu, * Kwa sababu ya hukumu zako za haki.
165. Wana amani nyingi waipendao sheria yako, * Wala hawana la kuwakwaza.
166. BWANA, nimeungojea wokovu wako, * Na maagizo yako nimeyatenda.
167. Nafsi yangu nimezishika shuhuda zako, * Nami nazipenda mno.
168. Nimeyashika mausia yako na shuhuda zako, * Maana njia zangu zote zi mbele zako.
Atukuzwe.
169. Ee BWANA, kilio changu na kikukaribie; * Unifahamishe sawasawa na neno lako .
170. Dua yangu na ifike mbele zako; *' Uniponye sawasawa na ahadi yako.
171. Midomo yangu na itoe sifa, * Kwa kuwa unanifundisha mausia yako.
172. Ulimi wangu na uiimbe ahadi yako, * Maana maagizo yako yote ni ya haki.
173. Mkono wako na uwe tayari kunisaidia, * Maana nimeyachagua mausia yako.
174. Bwana, nimeutamani wokovu wako, * Na sheria yako ndiyo furaha yangu.
175. Nafsi yangu na iishi nipate kukusifu, * Na hukumu zako zinisaidie.
176. Nimetanga-tanga kama kondoo aliyepotea, umtafute mtumishi wako, * Kwa maana sikuyasahau maagizo yako.
Atukuzwe.
Ant. Unifahamishe, Ee BWANA; Sawasawa na neno, lako.
Ant. Pasaka. Haleluya, Haleluya, Haleluya.
|
Saturday |
¶ Kisha huja SOMO FUPI na VIITIKIO.
Siku ya Bwana
SOMO. Mchukuliane mizigo mkaitimize hivyo sheria ya Kristo.
R. Tumshukuru Mungu.
V. Ee BWANA, neno lako lasimama imara mbinguni hata milele.
R. Ee BWANA, neno lako lasimama imara mbinguni hata milele.
V. Uaminifu wako upo kizazi baada ya kizazi.
R. Imara mbinguni hata milele.
V. Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.
R. Ee BWANA, neno lako lasimama imara mbinguni hata milele.
V. BWANA ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.
R. Katika malisho ya majani mabichi hunilaza.
V. BWANA akae nanyi.
R. Pia na roho yako.
Tuombe
|
Brief lesson & Responses
Sunday |
Sala ya Siku
V. BWANA akae nanyi.
R. Pia na roho yako.
V. Tumhimidi BWANA.
R. Tumshukuru Mungu.
Roho zao waaminifu kwa rehema ya Mungu wastarehe katika amani.
R. Amin.
|
Collect of the Day |
Siku za Kazi
SOMO. Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria.
R. Tumshukuru Mungu.
V. Nitamhimidi BWANA kila wakati.
R. Nitamhimidi BWANA kila wakati.
V. Sifa zake zi kinywani mwangu daima.
R. Kila wakati.
V. Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.
R. Nitamhimidi BWANA kila wakati.
V. BWANA ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.
R. Katika malisho ya majani mabichi hunilaza.
V. BWANA akae nanyi.
R. Pia na roho yako.
Tuombe
|
Workdays |
Sala ya Siku
V. BWANA akae nanyi.
R. Pia na roho yako.
V. Tumhimidi BWANA.
R. Tumshukuru Mungu.
Roho zao waaminifu kwa rehema ya Mungu wastarehe katika amani.
R. Amin.
¶ Mwisho wote wapige magoti na husema kimoyomoyo,
|
Collect of the Day |
Baba yetu.
Msaada wa Mungu ukae nasi daima. Amin.
|
Lord's Prayer |
SALA YA JIONI
Baba yetu. Salamu, Mariamu.
¶ Mhudumu aseme, au aimbe,
V. Ee Mungu, uwe radhi kutuokoa.
R. Ee BWANA, utusaidie hima.
Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.
Kama ilivyokuwa mwanzo na iwe sasa na sikuzote, na hata milele na milele. Amin.
V. Msifuni BWANA.
R. Jina la BWANA lisifiwe.
¶ Ndipo ZABURI husemwa, au kuimbwa, kama kawaida.
|
Lord's Prayer; Hail Mary |
¶ Kisha lisomwe SOMO LA KWANZA lililoamriwa.
¶ Ndipo huimbwa, au kusemwa, WIMBO WA KANUNI ulioamriwa, pamoja na V. na R.
¶ Baada yake huimbwa, au. kusemwa, MAGNIFICAT na Antifona yake.
Antifona iliyohusika.
MAGNIFICAT. Luka Mt. i
1. Moyo wangu wamwadhimisha BWANA; * Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu.
2. Kwa kuwa ameutazama * Unyonge wa mjakazi wake;
3. Kwa maana tazama, tokea sasa, * Vizazi vyote wataniita Mbarikiwa.
4. Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu; * Na Jina lake ni takatifu.
5. Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi * Kwa hao wanaomcha.
6. Amefanya nguvu kwa mkono wake; * Amewatawanya walio na kiburi katika mawazo ya mioyo yao;
7. Amewaangusha wakuu katika viti vyao vya enzi; * Na wanyonge amewakweza.
8. Wenye njaa amewashibisha mema; * Na wenye mali amewaondoa mikono mitupu.
9. Amemsaidia Israeli, mtumishi wake; * Ili kukumbuka rehema zake.
10. Kama alivyowaambia baba zetu, * Ibrahimu na uzao wake, hata milele.
Atukuzwe.
Antifona iliyohusika.
|
First Lesson |
¶ Kisha lisomwe SOMO LA PILI lililoamriwa.
¶ Kisha hufuata DEUS MISEREATUR na Antifona yake.
Ant. Njia yako ijulike duniani, Wokovu wako katikati ya mataifa yote. (W. P. Haleluya.)
DEUS MISEREATUR, Zab. 67
1. Mungu atufadhili na kutubariki, * Na kutuangazia uso wake.
2. Njia yake ijulike duniani, * Wokovu wake katikati ya mataifa yote.
3. Watu na wakushukuru, Ee Mungu; * Watu wote na wakushukuru.
4. Mataifa na washangilie; * Naam, waimbe kwa furaha.
5. Maana kwa haki utawahukumu watu, * na kuwaongoza mataifa walioko duniani.
6. Watu na wakushukuru, Ee Mungu; * Watu wote na wakushukuru.
7. Nchi imetoa mazao yake; * MUNGU, Mungu wetu, ametubariki.
8. Mungu atatubariki sisi; * Miisho yote ya dunia itamcha Yeye.
Atukuzwe.
Ant. Njia yako ijulike duniani, Wokovu wako katikati ya mataifa yote. (W. P. Haleluya.)
¶ Kisha Mhudumu aseme, au aimbe, SALA.
V. BWANA akae nanyi.
R. Pia na roho yako.
Tuombe
|
Second Lesson |
Sala ya Siku
¶ Ikiwa imeamriwa sala nyingine katika Kalendari ya Mwaka, au mbili, au tatu, kila sala isemwe, au iimbwe, hapa, pamoja na Antifona yake, na V. na R.
¶ Kila sala ya ukumbusho isemwe bila kutia mwisho wake, isipokuwa sala ya mwisho; hii ndiyo ya kutiwa mwisho wake.
¶ Wakati wa Pasaka Ant. na V. na R. za kila sala ya ukumbusho zitiwe Haleluya mwishoni.
|
Collect of the Day |
(1) Ukumbusho wa Siku ya Bwana
Ant. Twakushukuru, Ee Mungu, twakushukuru; Utatu uliye Umoja halisi, Uungu mmoja usio na mfano, Umoja uliye mmoja, Mtakatifu.
V. Sala zetu zipae, Ee BWANA.
R. Mbele zako kama uvumba.
Tuombe
|
Memorial for Sunday |
(2) Ukumbusho wa Mariamu Mb.
Ant. Vizazi vyote wataniita Mbarikiwa; Kwa kuwa Mungu ameutazama unyonge wa mjakazi wake.
V. Salamu, Mariamu, umejaa neema.
R. BWANA yu pamoja nawe.
Tuombe
|
Memorial for St. Mary |
(3) Ukumbusho wa Mtakatifu
(Sala ya Jioni ya 1 yake)
Ant. Wamevikwa mavazi meupe, wakilia kwa sauti kuu, wakisema, Wokovu una Mungu wetu, aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-kondoo.
V. Shangilieni, enyi wenye haki.
R. Pigeni vigelegele vya furaha.
Tuombe
(4) Ukumbusho wa Mtakatifu
(Sala ya Jioni ya 2 yake)
Ant. Ee ajabu ya utukufu wa ufalme ule! Ndipo wanapofurahi Watakatifu wote pamoja na Kristo; Wamevikwa nguo nyeupe, wanamfuata Mwana-kondoo kila aendako.
V. Watakatifu na waushangilie utukufu.
R. Waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao.
Tuombe
¶ Kadhalika na sala ya Ukumbusho wa Wakati, kama ipo, na sala ya UKUMBUSHO WA WATAKATIFU siku iliyoamriwa.
|
Memorial of a Saint |
Ukumbusho wa Watakatifu (S)
Ant. Bikira Mariamu, Mama mbarikiwa wa Mungu, Na Watakatifu wote, watuombee kwa Mungu.
V. Mungu amewatukuza Watakatifu wake.
R. Walipomwita akawasikia.
Tuombe
Ee Bwana, tunakusihi, utuokoe na hatari zote za mwili na za roho: Na kwa ajili ya sala za Mariamu, Bikira Mtukufu wa daima, Mama Mbarikiwa wa Mungu, pamoja na sala za fulani Mtakatifu, na Watakatifu wote, utujalie salama na amani; ili tuondolewe taabu zote na makosa, na Kanisa lako likutumikie pasipo hofu. Kwa.
¶ Mahali pa fulani Mhudumu ataje jina la Mtakatifu wa Mwani.
¶ Zikiisha sala zote zilizoamriwa, Mhudumu aseme,
V. BWANA akae nanyi.
R. Pia na roho yako.
V. Tumhimidi BWANA.
R. Tumshukuru Mungu.
Roho zao waaminifu kwa rehema ya Mungu wastarehe katika amani.
R. Amin.
¶ Kisha hufuata MAOMBEZI, wote wakiwa wamepiga magoti. Mwisho kila mtu aseme peke yake kimoyomoyo,
|
Memorial of Saints |
Baba yetu.
Msaada wa Mungu ukae nasi daima. Amin.
¶ Kwenye. Sikukuu za 1 na za 2 hakuna Maombezi. Mhudumu ana ruhusa kusema sala hii kwa hiari yake.
Ant. Utuokoe, Ee BWANA, tulipo macho, tulalapo utulinde; Tukeshe na Kristo, tukastarehe kwa amani.
V. Ee BWANA, utulinde kama mboni ya jicho.
R. Utufiche chini ya uvuli wa mbawa zako.
Tuombe
Ee Bwana, tunakuomba: Utuangaze sisi tulio gizani; na kwa rehema zako uwafukuzie mbali nasi adui zote wanaotuotea usiku huu. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
au sala nyingine.
|
Lord's Prayer |
SALA YA USIKU
¶ Mhudumu aseme,
BWANA Mwenyezi atupe usiku wa raha na mwisho mkamilifu. Amin.
Ndugu, mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa. mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze. Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani.
V. Nawe, BWANA, uturehemu.
R. Tumshukuru Mungu.
V. Msaada wetu u katika Jina la BWANA.
R. Aliyezifanya mbingu na nchi.
|
Baba yetu (kimoyomoyo).
¶ Akiwapa Kasisi, aseme,
Naungama kwa Mwenyezi Mungu, na kwa Watakatifu wote, na kwenu, ndugu, ya kwamba nimekosa sana, kwa mawazo, na maneno, na matendo; kwa kosa langu, kosa langu, kosa langu baya sana. Kwa hiyo nawasihi Watakatifu wote waniombee; nanyi, ndugu, mniombee kwa Bwana Mungu wetu.
¶ Watu wamjibu,
Mwenyezi Mungu akurehemu, akusamehe makosa yako, akufikishe kwenye uzima wa milele. Amin.
¶ Ndipo watu waseme,
Naungama kwa Mwenyezi Mungu, na kwa Watakatifu wote, na kwako, baba, ya kwamba nimekosa sana, kwa mawazo, na maneno, na matendo; kwa kosa langu, kosa langu, kosa langu baya sana, Kwa hiyo nawasihi Watakatifu wote waniombee; nawe, baba, uniombee kwa Bwana Mungu wetu.
¶ Kasisi awa jibu,
Mwenyezi Mungu akurehemuni, akusameheni makosa yenu, akufikisheni kwenye uzima wa milele. Amin.
Bwana Mwenyezi na mwenye rehema atujalie masamaha, ghofira, na ondoleo la dhambi zetu. Amin.
|
Lord's Prayer (silently) |
¶ Ikiwa Kasisi hayupo, watu waseme hivi,
Naungama kwa Mwenyezi Mungu, na kwa Watakatifu wote, [na kwenu, ndugu,] ya kwamba nimekosa sana, kwa mawazo, na maneno, na matendo; kwa kosa langu, kosa langu, kosa langu baya sana. Kwa hiyo nawasihi Watakatifu wote waniombee; [nanyi, ndugu, mniombee] kwa Bwana Mungu wetu.
Mwenyezi Mungu aturehemu, atusamehe makosa yetu, atufikishe kwenye uzima wa milele. Amin.
Bwana Mwenyezi na mwenye rehema atujalie masamaha, ghofira, na ondoleo la dhambi zetu. Amin.
¶ Ikiwa unasali peke yako, acha maneno haya, na kwenu, ndugu, na, nanyi, ndugu, mniombee.
¶ Kisha Mhudumu aseme,
V. Uturudishe, Ee Mungu wa wokovu wetu.
R. Uikomeshe hasira uliyo nayo juu yetu.
V. Ee Mungu, uwe radhi kutuokoa.
R. Ee BWANA, utusaidie hima.
Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.
Kama ilivyokuwa mwanzo na iwe sasa na sikuzote, na hata milele na milele. Amin.
V. Msifuni BWANA.
R. Jina la BWANA lisifiwe.
¶ Ndipo ZABURI husemwa kama kawaida.
Ant. Unifadhili. Ant. Pasaka. Haleluya.
|
If a Priest is not present |
ZAB. 4
1. Ee Mungu wa haki yangu, uniitikie niitapo; * Umenifanyizia nafasi wakati wa shida, unifadhili na kuisikia sala yangu.
2. Enyi wanadamu, hata lini utukufu wangu uta-fedheheka? * Je! mtapenda ubatili na kutafuta uongo?
3. Bali jueni ya kuwa BWANA amejiteulia mtauwa; * BWANA atasikia nimwitapo.
4. Mwe na hofu wala msitende dhambi, * Tafakarini vitandani mwenu na kutulia.
5. Toeni dhabihu za haki, * Na kumtumaini BWANA.
6. Wengi husema, Nani atakayetuonyesha mema? * Ee BWANA, utuinulie nuru ya uso wako.
7. Umenitia furaha moyoni mwangu, * Kupita yao wanapozidishiwa nafaka na divai.
8. Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara, * Maana Wewe, BWANA, peke yako ndiwe unijaliaye kukaa salama.
Atukuzwe.
|
Psalm 4 |
ZAB. 91
1. Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu * Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
2. Asemaye, BWANA ndiye kimbilio na ngome yangu, * Mungu wangu nitakayemtumaini,
3. Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, * Na katika tauni iharibuyo.
4. Kwa manyoya yake atakufunika; * Chini ya mbawa zake utapata kimbilio.
5. Uaminifu wake ni ngao na kigao; * Usiogope hofu ya usiku;
6. Wala mshale urukao mchana; * Wala tauni ipitayo gizani;
7. Wala uele uharibuo adhuhuri; * Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako.
8. Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume! * Hata hivyo hautakukaribia wewe.
9. Ila kwa macho yako utatazama, * Na kuyaona malipo ya wasio haki.
10. Mradi umesema, BWANA ndiye kimbilio langu; * Umemfanya Aliye juu kuwa makao yako.
11. Mabaya hayatakupata wewe, * Wala tauni haitaikaribia hema yako.
12. Kwa kuwa atakuagizia malaika zake * Wakulinde katika njia zako zote;
13. Na mikononi mwao watakuchukua, * Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
14. Utawakanyaga simba na nyoka, * Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu.
15. Kwa kuwa amekaza kunipenda * Nitamwokoa na kumweka palipo juu.
16. Kwa kuwa amenijua Jina langu * Ataniita nami nitamwitikia.
17. Nitakuwa pamoja naye taabuni; * Nitamwokoa na kumtukuza;
18. Kwa siku nyingi nitamshibisha; * Nami nitamwonyesha wokovu wangu.
Atukuzwe.
|
Psalm 91 |
ZAB. 134
1. Enyi watumishi wa BWANA, * Mhimidini BWANA nyote pia.
2. Ninyi mnaosimama usiku * Katika nyumba ya BWANA.
3. Painulieni patakatifu mikono yenu, * Na kumhimidi BWANA.
4. BWANA akubariki toka Sayuni, * Aliyezifanya mbingu na nchi.
Atukuzwe.
Ant. Unifadhili, Ee BWANA; * Uisikie sala yangu.
Ant. Pasaka. Haleluya, Haleluya, * Haleluya.
¶ Ndipo huimbwa WIMBO.
Usiku twakuomba,
Muumba ulimwengu;
Utuhifadhi sasa,
Gizani utulinde.
Fukuza ndoto mbaya,
Na njozi za kutisha;
Adui umzuie,
Uchafu tusitiwe.
Ee Baba, tuombayo,
Kwa Yesu tujalie;
Amilikiye nawe,
Na Roho Mtakatifu. Amin
|
Psalm 134 |
¶ Kisha huja SOMO FUPI na VIITIKIO.
SOMO. Wewe, BWANA, u katikati yetu nasi tunaitwa kwa Jina lako; usituache, Ee BWANA Mungu wetu.
R. Tumshukuru Mungu.
V. Ee BWANA, mikononi mwako naiweka roho yangu. (W. P. Haleluya, Haleluya.)
R. Ee BWANA, mikononi mwako naiweka roho yangu. (W. P. Haleluya, Haleluya.)
V. Umetukomboa, Ee BWANA, Mungu wa kweli.
R. Naiweka roho yangu. (au W. P. Haleluya, Haleluya.)
V. Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.
R. Ee BWANA, mikononi mwako naiweka roho yangu. (W. P. Haleluya, Haleluya.)
V. Ee BWANA, utulinde kama mboni ya jicho. (W. P. Haleluya.)
R. Utufiche chini ya uvuli wa mbawa zako. (W. P. Haleluya.)
¶ Baada yake huimbwa, au kusemwa, NUNC DIMITTIS na Antifona yake.
Ant. Utuokoe.
NUNC DIMITTIS. Luka Mt. ii
1. Sasa, BWANA, wamruhusu mtumishi wako; * Kwa amani, kama ulivyosema.
2. Kwa kuwa macho yangu * Yameuona wokovu wako.
3. Uliouweka tayari * Machoni pa watu wote.
4. Nuru ya kuwa mwangaza wa mataifa, * Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli.
Atukuzwe.
Ant. Utuokoe, Ee BWANA, tulipo macho, tulalapo utulinde; Tukeshe na Kristo, tukastarehe kwa amani. (W. P. Haleluya.)
|
Brief lesson & Responses |
¶ Sala zifuatazo zisemwe kila siku, Siku za Bwana na Siku za kazi, watu wamesimama, isipokuwa ni Sikukuu, au ni siku yenye ukumbusho wake, au katika Oktavo yake: ndipo zisisemwe.
¶ Piga magoti, lakini, siku za kazi, wakati wa Majilio, Kwaresima, na Robo Mwaka.
Bwana, uturehemu.
Kristo, uturehemu.
Bwana, uturehemu.
|
On Holy Days, memorial days, & during the Octave |
Baba yetu (kimoyomoyo).
V. Usitutie majaribuni.
R. Lakini utuokoe na yule mwovu.
|
Lord's Praywer (silently) |
Namwamini Mungu (kimoyomoyo)
V. Kufufuliwa kwa mwili.
R. Na uzima wa milele. Amin.
V. Umehimidiwa, Ee BWANA, Mungu wa baba zetu.
R. Wastahili kusifiwa na kuadhimishwa milele.
V. Tumhimidi Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.
R. Tumsifu na kumwadhimisha milele.
V. Ee BWANA, umehimidiwa katika anga la mbinguni.
R. Wastahili kusifiwa na kutukuzwa milele.
V. BWANA Mwenyezi na mwenye rehema atubariki, atulinde.
R. Amin.
V. Ee BWANA, ukubali kutulinda.
R. Usiku huu tusitende dhambi.
V. Uturehemu, Ee BWANA.
R. Uturehemu sisi.
V. Ee BWANA, fadhili zako zikae nasi.
R. Kama vile tulivyokungoja Wewe.
V. Ee BWANA, usikie kuomba kwetu.
R. Kilio chetu kikufikie.
¶ Watu wakiwa wamepiga magoti, Mhudumu asimame hapa.
|
Apostles' Creed (silently) |
V. BWANA akae nanyi.
R. Pia na roho yako.
Tuombe
Ee Bwana, tunakusihi, uingie nyumbani humu: Uzifukuzie mbali nasi hila zote za adui; Malaika zako watakatifu wakae humu ili watulinde katika amani, na baraka yako ikae nasi daima. Kwa Bwana wetu Yesu Kristo Mwana wako; Aishiye na kumiliki pamoja nawe, katika umoja wa Roho Mtakatifu, Mungu daima milele na milele. Amin.
V. BWANA akae nanyi.
R. Pia na roho yako.
V. Tumhimidi BWANA.
R. Tumshukuru Mungu.
BWANA Mwenyezi na mwenye rehema, Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, atubariki, atulinde.
R. Amin.
¶ Mwisho wote wapige magoti na kusema kimoyomoyo,
Msaada wa Mungu ukae nasi daima. Amin. |
|
Baba yetu. Salamu, Mariamu. Namwamini Mungu.
¶ Ikiwa Sala ya Asubuhi hufuata mara baada ya Sala ya Usiku, watu wasipige magoti. Aidha, Baba yetu, Salamu Mariamu, na Namwamini Mungu zisemwe mara mbili; yaani, mwisho wa Sala ya Usiku na mwanzo wa Sala ya Asubuhi pia.
¶ Kadhalika ikiwa Sala ya Jioni hufuata mara baada ya Sala ya Adhuhuri, watu wasipige magoti; bali Sala ya Jioni huanzia Baba yetu mara baada ya Roho zao waaminifu. |
Lord's Prayer; Hail Mary; Apostles' Creed |