The Book of Common Prayer
United States England Scotland Ireland Wales Canada World

    Kitabu cha Sala za Kanuni (1918)
The Zanzibar Book of Common Prayer in Swahili

 

AMRI ZA SALA

Antifona za Zaburi

    1. Katika Sala ya Asubuhi na Sala ya Jioni kila Zaburi ina antifona yake, zimepigwa chapa pamoja na Zaburi.
    2. Sikukuu za 1 na 2, na Wakati wa Pasaka, antifona ya Zaburi ni moja tu; Zaburi zote za siku ile husemwa chini ya antifona hiyo moja, iliyopigwa chapa pamoja na sehemu za sala zinazobadilika; zile za kawaida na ziachwe siku ile.
    3. Antifona za Sikukuu husemwa nzima na wote, mwanzo na mwisho wa Zaburi.
    4. Siku za Bwana na siku nyinginezo zote antifona husemwa hata mwisho wa italics tu kabla ya Zaburi; ikasemwa nzima baada ya Zaburi.
    5. Kabla ya Zaburi Mhudumu au Kantori husema peke yake mwanzo wa antifona; baada ya Zaburi watu wote huisema pamoja.
    6. Katika Sala ya Adhuhuri na Sala ya Usiku antifona ya Zaburi ni moja tu kama ilivyoandikwa, wala haisemwi nzima kabla ya Zaburi siku yo yote.
    7. Pengine katika antifona za Zaburi na antifona nyingine huja mwisho neno hili, Haleluya; basi, tokea Septuajesima hata Pasaka ni lazima kuacha neno hili lisisemwe; siku nyinginezo lisemwe.
    8. Lakini neno hili likipigwa chapa kati ya vifungo, hivi (W. P. Haleluya), maana yake lisemwe Wakati wa Pasaka tu; siku nyinginezo zote lisisemwe.
    9. Zaburi zikiimbwa, watu hawawezi kuiimba antifona kabla ya Zaburi, kwa sababu hawajajua tuni yake bado; kwa hiyo Kantori aiimbe peke yake
 

Rules for Prayers

Antiphons for Psalms

Zaburi

    1. Katika kuimba, au kusema, Zaburi ni lazima tutue penye (*) tupaze pumzi, kadiri mtu atakavyoweza kusema kimoyomoyo, Bwana Yesu. Penye (;) tutue kidogo. Penye (,) hakuna kutua, lakini tusiirukize kwa haraka, tukaiharibu maana ya maneno tuyasemayo.
    2. Kantori au Mhudumu na aianzishe kila Zaburi. Ikiwezekana watu waimbe, au kusema, Zaburi zamu kwa zamu, watu wa upande wa Waraka wakichukua aya za kwanza, za tatu, za tano, n.k.
    3. Mwisho wa kila Zaburi watu waimbe au kusema,
    Atukuzwe Baba, na Mwana, * Na Roho Mtakatifu.
    Kama ilivyokuwa mwanzo na iwe sasa na sikuzote, * Na hata milele na milele. Amin.
    4. Atukuzwe. haisemwi kamwe mahali po pote siku ya Alhamisi ya Amri, wala Ijumaa Kuu, wala Mkesha wa Pasaka hata jioni.
    5. Atukuzwe. haisemwi katika Sala za Kuombea Wafu; badala yake husemwa,

Raha ya milele * Uwajalie, Ee BWANA.
Na nuru ya daima * Iwaangaze.
 

Psalms

Masomo

    1. Msomaji asome Masomo kwa sauti kuu, ya heshima, bila haraka. Maana, wajibu wake ni kuyasoma kwa taratibu na kwa adabu, kwa akili na kwa sauti ya kusikika; kana kwamba ametumwa na Mungu kuwajulisha wamsikiao neno wasilolijua bado.
    2. Mwanzo wa kila Somo Msomaji akitangaze kitabu asomacho, na sura, na aya, mwisho wake akibusu kitabu kwa heshima, na watu wasimame; kisha Msomaji aseme,

V. Nawe, BWANA, uturehemu.
R. Tumshukuru Mungu.
 

Lessons

Antifona za Benedictus na Magnificat

    Antifona hizi zimepigwa chapa pamoja na Nyimbo za Kanuni. Siku isemwapo nzima mara mbili antifona ya Zaburi, na antifona hizi zisemwe nzima mara mbili vile vile; kadhalika na antifona ya Zab. 67 katika Sala ya Jioni.
 

Antiphons for Benedictus & Magnificat

Sala

    Katika kuimba Sala Mhudumu azifuate amri zilizoandikwa katika Amri za Missa.
 

Collects

Antifona za Sala za Ukumbusho

    Katika kuimba, au kusema, antifona za Sala za Ukumbusho Kantori au Mhudumu na aseme peke yake maneno yenye chapa za italics, akiendelea kuyasema yabakiyo watu na wayaseme pamoja naye. Wala yeye asiwaachie kuyasema peke yao.
 

Antiphons for memorial Prayers / Collects

Sala za Ukumbusho

    1. Sala za Ukumbusho zihusuzo kila siku zimeandikwa katika Kalendari ya Mwaka.
    2. Sala ya Ukumbusho wa Watakatifu imeandikwa S katika Kalendari ya Mwaka. Sala hii isisemwe wakati wote wa Majilio na Kuzaliwa, wala wakati wote wa Mateso na Pasaka; wala isisemwe Sikukuu yo yote, wala katika Oktavo, wala Siku ya Bwana yenye Ukumbusho wa Sikukuu. Siku nyinginezo zote isemwe.
    3. Sala ya Ukumbusho wa Msalaba isemwe kila siku Wakati wa Pasaka, tokea Jumatatu baada ya Oktavo hata Mkesha wa Kupaa, isipokuwa ni Sikukuu. Na katika Kalendari ya Mwaka imeandikwa M.
    4. Sala za Ukumbusho wa Wakati zimepigwa chapa pamoja na sehemu za sala zinazobadilika. Na zisemwe zilivyoamriwa katika Kalendari ya Mwaka.
 

Memorial Prayers / Collects

Maombezi

    1. Sala za kuombea zisiimbwe kamwe; zisemwe kwa sauti ya taratibu, ya kusikika.
    2. Antifona zake zisemwe kama antifona za Sala za Ukumbusho.
 

Intercessions

Viitikio

    1. Kantori ana ruhusa ya kuimba kila V. ifuatayo Wimbo au antifona ya Sala ya Ukumbusho; hata na V. ya mwisho, Tumhimidi BWANA, Mhudumu akipenda, iwapo sauti yake mwenyewe ni ngumu. Bali Viitikio vyote vya kwanza, mwanzo wa ibada, ni juu yake Mhudumu mwenyewe; kadhalika na V. BWANA akae nanyi. kila mara.
    2. V. BWANA akae nanyi. isisemwe na mtu asiyepewa daraja la Shemasi. Badala yake aseme,

V. Ee BWANA, usikie kuomba kwetu.
R. Kilio chetu kikufikie.
 

Responses

Mwisho wa Sala

    1. Sala zimepigwa chapa bila mwisho wake. Mwisho wa kawaida ni,
    Kwa Bwana wetu Yesu Kristo Mwana wako; Aishiye na kumiliki pamoja nawe, katika umoja wa Roho Mtakatifu, Mungu daima milele na milele.
   Sala za namna hii zimetiwa mwishoni,
   Kwa.
    2. Ikiwa Bwana wetu ametajwa katika sala, mwisho wake ni,
    Kwa Yeye, Bwana wetu Yesu Kristo Mwana wako; Aishiye na kumiliki pamoja nawe, katika umoja wa Roho Mtakatifu, Mungu daima milele na milele.
    Sala za namna hii zimetiwa mwishoni,
    Kwa Yeye.
    3. Sala nyinginezo zimetiwa mwisho wake bila mkato.
    4. Sala ya Siku ina mwisho wake sikuzote; na hii ndiyo ile inayosemwa kwanza, baada ya V. BWANA akae nanyi.
    5. Ikiwa sala mbili tatu zimeamriwa katika Kalendari ya Mwaka, ya kwanza ndiyo Sala ya Siku; na nyingine ni Sala za Ukumbusho.
    6. Kila Sala ya Ukumbusho isemwe pamoja na Antifona yake na V. na R. vilivyohusika; ikiwa ni Ukumbusho wa Siku ya Bwana, au wa Mtakatifu, au wa Wakati, au vinginevyo. Na habari zote zipo zimepangwa tayari kitabuni humu.
    7. Sala za Ukumbusho zisitiwe mwisho wake, isipokuwa ile inayokuja mwisho wa zote. Sala ya Ukumbusho iliyo ya mwisho ina mwisho wake kila mara.
    8. Katika Sala ya Adhuhuri Sala ni moja tu kila siku, ndiyo Sala ya Siku. Kadhalika Sala ni moja tu katika Sala ya Usiku.
 

Conclusion of Prayers / Collects

Sala ya Bwana

    Wakati maneno haya, Usitutie majaribuni, yasemwa po kwa sauti ya kusikika mwisho wa Sala ya Bwana, maneno mawili, Baba yetu, na yasemwe kwa sauti ya kusikika vile vile. Kadhalika kwa habari za Imani ya Mitume; maneno haya, Kufufuliwa kwa mwili, yakisemwa kwa sauti ya kusikika, maneno mawili, Namwamini Mungu, yasemwe kwa sauti ya kusikika. Kama sivyo, wakati mwingineo wote, maneno yote husemwa kimoyomoyo.
 

Lord's Prayer

Venite na Te Deum

    1. Venite husemwa kila siku mwaka mzima, isipokuwa Alhamisi ya Amri, Ijumaa Kuu, Mkesha wa Pasaka, na Sikukuu ya Pasaka. Siku nyingine za Oktavo ya Pasaka husemwa kama kawaida; Sikukuu yenyewe ya Pasaka upo wimbo mwingine ulioamriwa.
    2. Te Deum husemwa kila siku ulipoamriwa Ut. katika Kalendari ya Mwaka wakati wa Missa. Basi na isemwe siku hizi,
    Kila Siku ya Bwana, isipokuwa S.B. za Majilio na tokea Septuajesima hata Pasaka.
    Kila Sikukuu, kubwa na ndogo, mwaka mzima, isipokuwa Alhamisi ya Amri, Ijumaa Kuu, Mkesha wa Pasaka, na Sikukuu ya Wasio na Hatia ikiangukia siku ya kazi.
    Kila siku ya Wakati wa Pasaka.
    Mikesha ya Ufunuo, Kupaa, na Pentekote.
    Siku nyinginezo haisemwi.

 

Venite & Te Deum

Antifona za Sikukuu

    1. Kila Sikukuu antifona zote zisemwe nzima mwanzo na mwisho kila mahali katika Sala ya Asubuhi na Sala ya Jioni.
    2. Ikiwa Sikukuu ina Oktavo, antifona zisemwe nzima vile vile siku ya nane pia; bali siku zilizo ndani ya Oktavo sivyo, hata Siku ya Bwana katika Oktavo yasemwe mwanzo yale maneno yaliyopigwa chapa ya italics tu.
    3. Aidha, Siku ya Bwana yenye ukumbusho wa Sikukuu yahusika na desturi ya Siku ya Bwana, siyo ya Sikukuu; yaani, ibada ni ya Siku ya Bwana, na Sikukuu ina ukumbusho tu siku ile.
    4. Mikesha ya Kuzaliwa na Pentekote hufuata desturi ya Sikukuu.
 


Antiphons for Holy Days

SALA ZA SIRI

Sala hizi zisemwe kimoyomoyo na kila mtu mmoja mmo 'a amepiga magoti mahali pake,
 

 
Private Prayer

KABLA YA SALA

Mwenyezi Mungu, tunakusihi, utujalie tukuabudu kwa mioyo safi. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.

Bwana Kristo, nataka kukutolea sala hii: Uikubali, ukaipeleke mbele za Baba yetu wa mbinguni pamoja na dua zako ulizoomba duniani; na maombezi ya Watakatifu wako huko mbinguni. Amin.
 

 
Before the Prayer (Service?)

BAADA YA SALA

Ee Bwana, uikubali sala yetu; utusamehe makosa yetu. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.

Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu, ukae nasi sote sasa na milele. Amin.
 


 

After the Prayer
Baba yetu, uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, Hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo riziki yetu. Utusamehe makosa yetu, Kama sisi tunavyowasamehe waliotukosa. Usitutie majaribuni, Lakini utuokoe na yule mwovu. Amin.
 
Lord's Prayer
Salamu, Mariamu, umejaa neema; Bwana yu pamoja nawe; Umebarikiwa kuliko wanawake wote; Na Yesu, uzao wa tumbo lako, amebarikiwa. Mariamu Mtakatifu, Mama wa Mungu, Utuombee sisi wenye dhambi, Sasa na saa ya kufa kwetu. Amin.
 
Hail Mary

Namwamini Mungu, Baba Mwenyezi, Muumba mbingu na nchi.
    Na Yesu Kristo, Mwana wake pekee, Bwana wetu. Aliyechukuliwa mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu, Akazaliwa na Bikira Mariamu; Akateswa zamani za Pontio Pilato; Akasulibiwa, Akafa, Akazikwa, Akashuka mahali pa wafu. Siku ya tatu akafufuka; Akapaa mbinguni; Ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba Mwenyezi; Kutoka huko atakuja kuwahukumu wahai na wafu.
    Namwamini Roho Mtakatifu; Kanisa Takatifu, Katholiko; Ushirika wa Watakatifu; Ondoleo la dhambi; Kufufuliwa kwa mwili, Na uzima wa milele. Amin.
 


 

Apostles' Creed

SALA YA ASUBUHI

Baba yetu. Salamu, Mariamu. Namwamini Mungu.

Mhudumu aseme,

    V. Ee BWANA, uifumbue midomo yetu.
    R. Na vinywa vyetu vitazinena sifa zako.
    V. Ee Mungu, uwe radhi kutuokoa.
    R. Ee BWANA, utusaidie hima.
    Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.
    Kama ilivyokuwa mwanzo na iwe sasa na sikuzote, na hata milele na milele. Amin.
    V. Msifuni BWANA.
    R. Jina la BWANA lisifiwe.

Kisha isemwe VENITE, zaburi hii ifuatayo.

VENITE.   Zab. 95

    1. Njoni, tumwimbie BWANA, * Tumfanyie shangwe Mwamba wa wokovu wetu.
    2. Tuje mbele zake kwa shukrani, * Tumfanyie shangwe kwa zaburi.
    3. Kwa kuwa BWANA ni Mungu mkuu, * Na Mfalme mkuu juu ya miungu yote.
    4. Mkononi mwake zimo bonde za dunia, * Hata vilele vya milima ni vyake.
    5. Bahari ni yake, ndiye aliyeifanya, * Na mikono yake iliiumba nchi kavu.
    6. Njoni, tuabudu, tusujudu, * Tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba.
    7. Kwa maana ndiye Mungu wetu; * Na sisi tu watu wa malisho yake, na kondoo za mkono wake.
    8. Ingekuwa heri leo msikie sauti yake! * Msifanye migumu mioyo yenu;
    9. Kama vile huko Meriba, * Kama siku ya Masa jangwani.
    10. Hapo waliponijaribu baba zenu; * Wakanipima, wakayaona matendo yangu.
    11. Miaka arobaini na1ihuzunika na kizazi kile; * Nikasema, Hao ni watu waliopotoka mioyo, hawakuzijua njia zangu.
    12. Nikaapa kwa hasira yangu, * Wasiingie rahani mwangu.

    Atukuzwe Baba, na Mwana, * Na Roho Mtakatifu.
    Kama ilivyokuwa mwanzo na iwe sasa na sikuzote, * Na hata milele na milele. Amin.

¶ Ndipo ZABURI husemwa, kama kawaida.
 

Morning Prayer

Lord's Prayer; Hail Mary; Apostles' Creed

¶ Kisha lisomwe SOMO LA KWANZA lililoamriwa.

¶ Kisha hufuata TE DEUM, au mmojawapo wa Nyimbo zifuatazo.

TE DEUM

    1. Wewe, Mungu, twakusifu; * Wewe, BWANA, twakukiri.
    2. Wewe, Baba wa milele, * Ulimwengu wote unakuabudu.
    3. Wewe Malaika zote, * Nazo Mbingu na Nguvu zote,
    4. Nao Makerubi na Maserafi, * Wakuimbia hawakomi;
    5. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, * BWANA, Mungu wa majeshi.
    6. Mbingu na nchi zimejaa * Enzi ya Utukufu wako.
    7. Wakusifu Wewe * Jamii tukufu ya Mitume.
    8. Wakusifu Wewe * Shirika lenye sifa la Manabii.
    9. Wakusifu Wewe * Jeshi la Mashahidi waliovaa mavazi meupe.
    10. Kanisa takatifu katika nchi zote * Lakukiri Wewe.
    11. Baba mwenye enzi * Isiyo na kiasi.
    12. Mwana wako pekee, * Wa kweli, wa kuabudiwa.
    13. Na Mfariji, * Roho Mtakatifu.
    14. Wewe, Kristo, * Ndiwe Mfalme wa Utukufu;
    15. Wewe Mwana wa milele * Wa Baba.
    16. Wewe ulipotadariki kuokoa binadamu, * Huku-chukizwa na tumbo la Bikira.
    17. Wewe ulipoushinda uchungu wa mauti, * Uliwafungulia waaminio Ufalme wa Mbinguni.
    18. Wewe unakaa mkono wa kuume wa Mungu, * Katika utukufu wake Baba.
    19. Tunasadiki utakuja * Kuwa Mwamuzi.
    20. Kwa hiyo twakuomba, uwasaidie watumishi wako; * Uliowakomboa kwa damu yako ya thamani.
    21. Uwajalie pamoja na Watakatifu wako * Thawabu ya utukufu wa milele.
    22. Uwaokoe watu wako, BWANA, * Uubariki urithi wako.
    23. Uwachunge, * Uwachukue milele.
    24. Sisi kila siku * Twakuhimidi.
    25. Twalisifu Jina lako * Milele na milele.
    26. Ee BWANA, ukubali kutulinda, * Leo tusitende dhambi.
    27. Uturehemu, Ee BWANA, * Uturehemu sisi.
    28. Ee BWANA, fadhili zako zikae nasi, * Kama vile tulivyokungoja Wewe.
    29. Nimekukimbilia Wewe, Bwana, * Nisiaibike milele.
 

First Lesson

¶ Siku ya Bwana, ikiwa TE DEUM imekatazwa, Wimbo huu, isipokuwa wakati wa Majilio,

    Ant. Tuimbe wimbo.

BENEDICTUS ES.   Dan. iii

    1. Umehimidiwa, Ee BWANA, Mungu wa baba zetu; * Wastahili kusifiwa na kuadhimishwa milele.
    2. Limehimidiwa Jina lako takatifu, tukufu; * Lastahili kusifiwa na kuadhimishwa milele.
    3. Umehimidiwa katika Hekalu la fahari yako takatifu; * Wastahili kusifiwa na kutukuzwa milele.
    4. Umehimidiwa utazamaye vilindi, uketiye juu ya Makerubi; * Wastahili kusifiwa na kuadhimishwa milele.
    5. Umehimidiwa juu ya kiti cha ufalme wako; * Wastahili kusifiwa na kuadhimishwa milele.
    6. Umehimidiwa katika anga la mbinguni; * Wastahili kusifiwa na kutukuzwa milele.
    Atukuzwe.

    Ant. Tuimbe wimbo wa vijana watatu, Waliouimba katika tanuu la moto, wakamhimidi BWANA.

Lakini Wakati wa Majilio isemwe BENEDICITE, (uk. 179) pamoja na Antifona hii,

    Ant. Vijana watatu kwa amri ya mfalme walitupwa katika tanuu la moto; Wasiuogope moto, wakasema, Atukuzwe Mungu. Haleluya.
 

Sunday

¶ Jumatatu.

    Ant. Twalihimidi Jina lako tukufu, Ee Mungu wetu.

BENEDICTUS ES, DOMINE.   1 Mambo xxix

    1. Ee BWANA, Mungu wa Israeli, baba yetu, * Uhimidiwe milele na milele.
    2. Ee BWANA, ukuu ni wako, na uweza na utukufu na kushinda, * Na enzi pia, yaani, vyote vilivyo mbinguni na duniani ni vyako.
    3. Ee BWANA, ufalme ni wako; * Nawe umetukuzwa, ndiwe uliye mkuu juu ya yote.
    4. Utajiri na heshima hutoka kwako; * Wewe unavitawala vitu vyote.
    5. Mkononi mwako mna uweza na nguvu; * Mkononi mwako mna kukuza na kuwaimarisha wote.
    6. Kwa hiyo, Ee Mungu wetu, tunakushukuru, * Na kulihimidi Jina lako tukufu.
    Atukuzwe.

    Ant. Twalihimidi Jina lako tukufu, * Ee Mungu wetu.
 

Monday

¶ Jumanne.

    Ant. Uniponye, Ee BWANA, Na kunihuisha.

EGO DIXI.   Isa. xxxviii

    1. Nalisema, Katika usitawi wa siku zangu * Nitakwenda kuingia malango ya kuzimu.
    2. Nimenyimwa mabaki ya miaka yangu; * Nalisema, Sitamwona BWANA.
    3. Sitamwona BWANA katika nchi ya wahai; * Sitamwona mwanadamu tena pamoja na hao wakaao duniani.
    4. Kao langu limeondolewa kabisa; * Limechuku1iwa kama hema ya mchungaji.
    5. Nimekunja maisha yangu kama mfumaji; * Atanikatilia mbali na kitanda cha mfumi.
    6. Tangu mchana hata usiku wanimaliza; * Nalijituliza hata asubuhi.
    7. Kama simba aivunja mifupa yangu yote; * Tangu mchana hata usiku wanimaliza.
    8. Kama mbayuwayu au korongo ndivyo nilivyolia; * Naliomboleza kama hua.
    9. Macho yangu yamedhoofu kwa kutazama juu; * Ee BWANA, nimeonewa, na uwe mdhamini wangu.
    10. Niseme nini? ndiye Yeye aliyenena; * Na Yeye mwenyewe ameyatenda hayo.
    11. Nitakwenda polepole miaka yangu yote, * Kwa sababu ya uchungu wa nafsi yangu.
    12. Ee BWANA, kwa mambo hayo watu huishi, * Na uhai wa roho yangu u katika hayo yote.
    13. Kwa hiyo uniponye na kunihuisha; * Tazama, nalikuwa na uchungu mwingi kwa ajili ya amani yangu.
    14. Lakini kwa kunipenda umeniokoa na uharibifu; * Kwa maana umezitupa dhambi zangu zote nyuma yako.
    15. Kwa kuwa kuzimu hakuwezi kukusifu; * Mauti haiwezi kukuadhimisha.
    16. Wale washukao shimoni hawawezi kuitarajia kweli yako; * Aliye hai, naam, aliye hai ndiye atakaye-kusifu, kama mimi leo.
    17. Baba atawajulisha watoto kweli yako; * BWANA yu tayari kunipa wokovu.
    18. Basi, kwa vinubi tutaziimba nyimbo zangu, Siku zote za maisha yetu nyumbani mwa BWANA.
    Atukuzwe.

    Ant. Uniponye, Ee BWANA, Na kunihuisha.
 

Tuesday

¶ Jumatano.

    Ant. Bwana ataihukumu * Miisho ya dunia.

EXSULTAVIT.   1 Sam. ii

    1. Moyo wangu wamshangilia BWANA; * Pembe yangu imetukuka katika BWANA.
    2. Kinywa changu kimepanuka juu ya adui zangu; * Kwa kuwa naufurahia wokovu wako.
    3. Hakuna aliye Mtakatifu kama BWANA; * Kwa maana hakuna ye yote ila Wewe.
    4. Wala hakuna mwamba mwingine, * Aliye mfano wa Mungu wetu.
    5. Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo; * Majivuno yasitoke vinywani mwenu.
    6. Kwa kuwa BWANA ni Mungu wa maarifa, * Na matendo hupimwa naye kwa mizani.
    7. Pinde zao mashujaa zimevunjika, * Nao waliojikwaa wamefungiwa nguvu.
    8. Walioshiba wamejikodisha ili kupata chakula; * Nao waliokuwa na njaa wamepata raha.
    9. Naam, aliyekuwa tasa amezaa watoto saba; * Naye aliye na wana wengi amedhoofika.
    10. BWANA huua, naye hufanya kuwa hai; * Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu.
    11. BWANA hufukarisha mtu, naye hutajirisha; * Yeye hushusha chini, tena huinua juu.
    12. Humwinua mnyonge kutoka mavumbini; * Humpandisha mhitaji kutoka jaani.
    13. Ili awaketishe pamoja na wakuu, * Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu.
    14. Kwa maana nguzo za dunia zina BWANA, * Naye ameuweka ulimwengu juu yake.
    15. Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake; * Bali waovu watanyamazishwa gizani.
    16. Maana kwa nguvu hakuna atakayeshinda; * Washindanao na BWANA watapondwa kabisa.
    17. Toka mbinguni Yeye atawapigia radi; * BWANA ataihukumu miisho ya dunia.
    18. Naye atampa mfalme wake nguvu, * Na kuitukuza pembe ya Masihi wake.
    Atukuzwe.

    Ant. BWANA ataihukumu Miisho ya dunia.
 

Wednesday

¶ Alhamisi.

    Ant. Tumwimbie Bwana Kwa maana ametukuka sana.

CANTEMUS.   Kutoka xv

    1. Nitamwimbia BWANA, kwa maana ametukuka sana; * Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini.
    2. BWANA ni nguvu zangu, na wimbo wangu, * Naye amekuwa wokovu wangu.
    3. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu; * Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza.
    4. BWANA ni mtu wa vita; * BWANA ndilo Jina lake.
    5. Magari ya Farao na jeshi lake amewatupa baharini; * Maakida wake wateule wamezama katika bahari ya Shamu.
    6. Vilindi vimewafunikiza, * Walizama vi1indini kama jiwe.
    7. BWANA, mkono wako wa kuume umepata fahari ya uweza; * BWANA, mkono wako wa kuume huwaseta adui.
    8. Kwa wingi wa ukuu wako wawaangusha chini wanaokuondokea; * Wapeleka hasira yako, nayo huwateketeza kama mabua makavu.
    9. Kwa upepo wa mianzi ya pua yako maji yalipandishwa; * Mawimbi yakasimama juu wima mfano wa chungu, vilindi vikagandamana ndani ya moyo wa bahari.
    10. Adui akasema, Nitafuatia, nitapata, nitagawanya nyara, * Nafsi yangu nitashibishwa nao.
    11. Nitaufuta upanga wangu, * Mkono wangu utawaangamiza.
    12. Ulivuma kwa upepo wako, bahari ikawafunikiza; * Wakazama kama risasi ndani ya maji makuu.
    Atukuzwe.

    Ant. Tumwimbie BWANA Kwa maana ametukuka sana.
 

Thursday

 

Exodus 15

¶ Ijumaa.

    Ant. Katika ghadhabu, Ee BWANA, Utakumbuka rehema.

DOMINE, AUDIVI.   Hab. iii

    1. Ee BWANA, nimesikia habari zako, nami naogopa; * Ee BWANA, fufua kazi yako katikati ya miaka.
    2. Katikati ya miaka tangaza habari yake; * Katika ghadhabu kumbuka rehema.
    3. Mungu alikuja kutoka Temani; * Yeye aliye Mtakatifu kutoka mlima Parani.
    4. Utukufu wake ukazifunika mbingu, * Nayo dunia ikajaa sifa yake.
    5. Mwangaza wake ulikuwa kama nuru; * Alikuwa na mishale ya nuru ubavuni pake.
    6. Ndipo ulipofichwa uweza wake; * Mbele zake ilikwenda tauni.
    7. Na makaa ya moto * Yakatoka miguuni pake.
    8. Akasimama, akaitetemesha dunia; * Akatazama, akawasitusha mataifa.
    9. Na milima ya zamani ikatawanyika, vilima vya kale vikainama; * Miendo yake ilikuwa kama siku za kale.
    10. Naliziona hema za Kushani katika taabu; * Mapazia ya nchi ya Midiani yakatetemeka.
    11. Je! BWANA aliikasirikia mito? * Je! hasira yake ilikuwa juu ya mito;
    12. Au ghadhabu yake juu ya bahari; * Hata ukapanda farasi zako katika magari yako ya wokovu ?
    13. Uta wako ukafanywa wazi kabisa; * Viapo walivyopewa kabila vilikuwa neno thabiti.
    14. Ukaipasua nchi kwa mito, milima ikakuona ikaogopa; * Gharika ya maji ikapita.
    15. Vilindi vikatoa sauti yake, vikainua juu mikono yake; * Jua na mwezi vikasimama makaoni mwake.
    16. Mbele ya nuru ya mishale yako ilipotapakaa; * Mbele ya mwangaza wa mkuki wako umeremetao.
    17. Ulikwenda katikati ya nchi kwa ghadhabu; * Ukawapura mataifa kwa hasira.
    18. Ukatokea kwa ajili ya wokovu wa watu wako, * Kwa ajili ya wokovu wa Masihi wako.
    Atukuzwe

    Ant. Katika ghadhabu, Ee BWANA, Utakumbuka rehema.
 

Friday

¶ Jumamosi.

    Ant. Utuonyeshe, Ee BWANA, Nuru ya rehema zako

MISERERE.   Yoshua bin Sira xxxvi

    1. Ee BWANA, Mungu wa watu wote, utuokoe; * Uangalie, uwatishe mataifa yote.
    2. Uuinue mkono wako juu ya watu wageni; * Na kuwaonyesha nguvu zako zilizo kuu.
    3. Kama vile u1ivyojitakasa kati yetu mbele yao, * Vivyo hivyo ujitukuze kati yao mbele yetu.
    4. Nao wakujue Wewe kama sisi tukujuavyo, * Ya kwamba hakuna Mungu ila Wewe peke yako.
    5. Tuonyeshe ishara tena, na kufanya mambo ya ajabu; * Uutukuze mkono wako, naam, mkono wako wa kuume.
    6. Uuamsheukali wako na kumimina hasira; * Umtiishe mtesi, na kumwangamiza adui.
    7. Uuhimize wakati na kuiamuru muhula; * Yu nani atakayekuambia Wewe, Unafanyaje?
    8. Uwaponde kichwa wakuu wa maadui, * Wanaosema, Hakuna ila sisi.
    9. Uwakusanye kabila zote za Yakobo, * Na kuwafanya urithi wako kama siku za kale.
    10. Ee BWANA, uwarehemu watu walioitwa kwa Jina lako, * Na Israeli, uliyemwita mzaliwa wa kwanza wako.
    11. Uuonee huruma mji wa Patakatifu pako, * Yerusalemu, mahali pako pa raha.
    12. Uujaze Sayuni adhama yako, * Na Patakatifu pako utukufu wako.
    Atukuzwe.

    Ant. Utuonyeshe, Ee BWANA, Nuru ya rehema zako.
 

Saturday

 

Sirach 36

Kisha lisomwe SOMO LA PILI lililoamriwa.

Ndipo huimbwa, au kusemwa, WIMBO WA KANUNI ulioamriwa, pamoja na V. na R.

Baada yake huimbwa, au kusemwa, BENEDICTUS na Antifona yake.

    Antifona iliyohusika

BENEDICTUS. Luka Mt. i

    1. Atukuzwe BWANA, Mungu wa Israeli; * Kwa kuwa amewajia watu wake na kuwakomboa.
    2. Ametusimamishia pembe ya wokovu, * Katika mlango wa Daudi mtumishi wake.
    3. Kama alivyosema tangu mwanzo * Kwa kinywa cha manabii wake watakatifu.
    4. Tuokolewe na adui zetu, * Na mikononi mwao wote wanaotuchukia.
    5. Ili kuwatendea rehema baba zetu; * Na kulikumbuka agano lake takatifu.
    6. Uapo aliomwapia Ibrahimu, baba yetu, * Ya kwamba atatujalia sisi,
    7. Tuokoke mikononi mwa adui zetu, * Na kumwabudu pasipo hofu,
    8. Kwa utakatifu na kwa haki, * Mbele zake siku zetu zote.
    9. Nawe, mtoto, utaitwa nabii wake Aliye juu, * Kwa maana utatangulia mbele za uso wa BWANA, ili umtengenezee njia zake.
    10. Uwajulishe watu wake wokovu, * Katika kusamehewa dhambi zao.
    11. Kwa njia ya rehema za Mungu wetu, * Ambazo kwa hizo mwangaza utokao juu umetufikia.
    12. Kuwaangaza wakaao katika giza na uvuli wa mauti; * Na kuiongoza miguu yetu mnamo njia ya amani.
    Atukuzwe.

   Antifona iliyohusika.

Kisha Mhudumu aseme SALA,

V. BWANA akae nanyi.
R. Pia na roho yako.

Tuombe
 

Second Lesson

Sala ya Siku

Ikiwa imeamriwa sala nyingine katika Kalendari ya Mwaka, au mbili, au tatu, kila sala isemwe hapa, pamoja na Antifona yake, na V. na R.

Kila sala ya ukumbusho isemwe bila kutia mwisho wake, isipokuwa sala ya mwisho; hii ndiyo ya kutiwa mwisho wake.

Wakati wa Pasaka Ant. na V. na R. za kila sala ya ukumbusho zitiwe Haleluya mwishoni.
 

Collect of the Day

(1) Ukumbusho wa Siku ya Bwana

    Ant. Ahimidiwe Utatu Mtakatifu aliye Umoja, Muumba, Mtawala vyote; Sasa, na sikuzote, na hata milele na milele.

V. BWANA ametamalaki, amejivika adhama.
R. BWANA amejivika na kujikaza nguvu.

Tuombe
 

Memorial for Sunday

(2) Ukumbusho wa Mariamu Mb.

    Ant. U heri, Mariamu, uliyesadiki; Kwa maana yatatimizwa uliyoambiwa na BWANA.

V. Salamu, Mariamu, umejaa neema.
R. BWANA yu pamoja nawe.

Tuombe
 

Memorial for St. Mary

(3) Ukumbusho wa Mtakatifu

    Ant. Wakusifu Wewe jamii tukufu ya Mitume, shirika lenye sifa la Manabii, jeshi la Mashahidi waliovaa mavazi meupe; Watakatifu na wateule wote kwa sauti moja wakukiri, Utatu Mtukufu, Mungu mmoja.

V. Watakatifu na waushangi1ie utukufu.
R. Waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao.

Tuombe
 

Memorial of a Saint

(4) Ukumbusho wa Robo Mwaka, au wa Siku ya Kuombea

    Ant. Huyu Msaidizi, huyu Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa Jina langu, Atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.

V. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu.
R. Wakaanza kusema.

Tuombe
 

Memorial of Ember Days, or a Day of Prayer

(5) Ukumbusho wa Mkesha

    Ant. Ee Bwana, uwaangaze wakaao katika giza na uvuli wa mauti; Uiongoze miguu yetu mnamo njia ya amani.

V. Utushibishe asubuhi kwa fadhili zako.
R. Nasi tutashangilia na kufurahi.

Tuombe

Kadhalika na sala ya Ukumbusho wa Wakati, kama ipo, na sala ya UKUMBUSHO WA WATAKATIFU siku iliyoamriwa.
 

Memorial of a Vigil

Ukumbusho wa Watakatifu (S)

    Ant. Bikira Mariamu, Mama mbarikiwa wa Mungu, Na Watakatifu wote, watuombee kwa Mungu.

V. Mungu amewatukuza Watakatifu wake.
R. Walipomwita akawasikia.

Tuombe

Ee Bwana, tunakusihi, utuokoe na hatari zote za mwili na za roho: Na kwa ajili ya sala za Mariamu, Bikira Mtukufu wa daima, Mama Mbarikiwa wa Mungu, pamoja na sala za fulani Mtakatifu, na Watakatifu wote, utujalie salama na amani; ili tuondolewe taabu zote na makosa, na Kanisa lako likutumikie pasipo hofu. Kwa.

Mahali pa fulani Mhudumu ataje jina la Mtakatifu wa Mtaani.

Zikiisha sala zote zilizoamriwa, Mhudumu aseme,

    V. BWANA akae nanyi.
    R. Pia na roho yako.
    V. Tumhimidi BWANA.
    R. Tumshukuru Mungu.
    Roho zao waaminifu kwa rehema ya Mungu wastarehe katika amani.
    R. Amin.

Kisha hufuata MAOMBEZI, wote wakiwa wamepiga magoti. Mwisho kila mtu aseme peke yake kimoyomoyo,
 

Memorial of Saints

Baba yetu.
Msaada wa Mungu ukae nasi daima. Amin.

Kwenye Sikukuu za 1 na za 2 hakuna Maombezi. Mhudumu ana ruhusa kusema sala hii kwa hiari yake.

    Ant. Utushibishe asubuhi kwa fadhili zako; Nasi tutashangilia na kufurahi siku zetu zote.
    V. Uzuri wa BWANA Mungu wetu uwe juu yetu.
    R. Na kazi ya mikono yetu uithibitishe.

Tuombe

Bwana Mtakatifu, Baba Mwenyezi, Mungu wa milele, umetujalia tuione na siku hii: Utulinde leo kwa nguvu zako; ili tusitelemke dhambini, wala tusijihatarishe nafsi zetu; bali kila siku uyaelekeze matendo yetu yote katika njia ya haki. Kwa Kristo Bwana wetu. Amin.

au sala nyingine.

Lord's Prayer

 

Return to the Zanzibar Prayer Book

Web author: Charles Wohlers U. S. EnglandScotlandIrelandWalesCanadaWorld