The Book of Common Prayer | |||||||
|
|
KAWAIDA YA MARIAMU MB. ZABURI Sehemu B, na Antifona zake. ¶ Hizi zitumike Sikukuu tu; siku nyingine zitumike Zaburi na Antifona za kawaida. Asubuhi: WIMBO 43. Sala Ee Bwana, utujalie, sisi watumishi wako neema yako ya mbinguni: Ibada za Sikukuu hii ya . . . Mariamu, Bikira Mbarikiwa, zitupatie amani nyingi; kwa maana kuzaa kwake kulituletea Mwokozi wetu. Kwa Yeye. au sala iliyohusika. Sala ya Adhuhuri Ubeti wa mwisho wa Wimbo. Ee Yesu, Mwana wa Bikira, SOMO. Tazama, bikira atachukua mimba, naye atazaa mwana, nao watamwita Jina lake Imanueli. |
Common of St. Mary
Translations of some common words: Zab., Zaburi: Psalm(s) |
WAKATI WA PASAKA ANT. ZAB. Haleluya, Haleluya, Haleluya Sala ya Adhuhuri VIITIKIO hivi, |
Easter Season |
KAWAIDA YA MTUME Sala ya Jioni (ya 1 na ya 2) ANT. ZAB. Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, Kama nilivyowapenda ninyi. Sala ya Asubuhi ANT. ZAB. Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, Wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. Sala ya Adhuhuri SOMO. Kwa mikono ya mitume zilifanyika ishara na maajabu mengi katika watu. |
Common of a Prophet |
WAKATI WA PASAKA ANT. ZAB. Haleluya, Haleluya, Haleluya. Sala ya Adhuhuri Ubeti wa mwisho wa Wimbo. Ahimidiwe Mungu Baba, SOMO. Twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao, katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. |
Easter Season |
KAWAIDA YA MTAKATIFU ZABURI na Antifona za kawaida. Sala ya Adhuhuri SOMO. Baraka na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uweza na nguvu zina Mungu wetu hata milele na milele. Amin. |
Common of a Saint |
WAKATI WA PASAKA ANT. ZAB. Haleluya, Haleluya, Haleluya. Sala ya Adhuhuri Ubeti wa mwisho wa Wimbo. Ahimidiwe Mungu Baba, VIITIKIO hivi, |
Easter Season |
SALA ZA KAWAIDA (1) Mkesha wa Mtume Mwenyezi Mungu, tunakuomba, utujalie rehema zako: Tuifurahie Sikukuu ya N. Mtume wako Mbarikiwa; ili tusaidiwe kwa sala zake, na kuokoka na hatari zote. Kwa. |
Collects Vigil of a Prophet |
(2) Shahidi aliye Askofu Mwenyezi Mungu, uuangalie udhaifu wetu: Utujalie tusaidiwe kwa sala tukufu za N. Mbarikiwa, Shahidi wako na Askofu; kwa kuwa tunalemewa na mzigo wa dhambi zetu. Kwa. |
Martyred Bishop |
(3) Shahidi asiye Askofu Mwenyezi Mungu, tunakuomba, utujalie baraka zako: Tuiadhimishe vema Sikukuu hii ya N. Shahidi wako Mbarikiwa; ili tusaidiwe kwa sala zake, na kuzidi kulipenda Jina lako. Kwa. |
Marty who was not a Bishop |
(4) Mashahidi wengi Mwenyezi Mungu, umetujalia kuiadhimisha Sikukuu ya N. na N., Mashahidi wako Wabarikiwa: Tunakusihi utuonyeshe rehema zako; ili tufurahi pamoja nao katika utukufu wako wa milele. Kwa. (5) (Wakati wa Pasaka) |
Many Martyrs |
(7) Mwungamaji aliye Askofu Mwenyezi Mungu, tunakuomba, Sikukuu hii ituletee baraka zako: Tumwadhimishe N. Mbarikiwa, Mwungamaji wako na Askofu; ili tuzidi kukupenda, tukajaliwe wokovu wa milele. Kwa. |
A penitent Bishop |
(8) Mwalimu wa Dini. I Ee Bwana, tunakusihi, uzisikie sala zetu: Tunazo-kutolea katika Sikukuu hii ya N. Mbarikiwa, Askofu wako na Mwalimu wa Dini; na kwa kuwa astahili kukuhudumia, kwa kuombea kwake utusamehe dhambi zetu zote. Kwa. (9) Mwalimu wa Dini. II Mwenyezi Mungu, umemweka N. Mwalimu wako Mbarikiwa awahudumie watu wako uzima wa milele: Utusikie tunakusihi; sisi tulioelimishwa naye hapa duniani, tuzidi kuombewa naye huko mbinguni. Kwa. |
A Teacher of the Faith |
(10) Mwungamaji asiye Askofu Ee Mungu, watufurahisha kila mwaka kwa sifa njema za N. Mwungamaji wako Mbarikiwa: Utujalie tunakuomba; ili tuiadhimishe vema Sikukuu yake, na kumfuatisha mwenendo wake. Kwa. |
A Penitent who was not a Bishop |
(11) Mtauwa Ee Bwana, tunakusihi: Tuombewe na N. Mtauwa mkuu Mbarikiwa; ili kwa sala zake tuone kibali kwako, kwa maana stahili zetu hazifai neno. Kwa. |
A Monastic |
(12) Bikira aliye Shahidi Mwenyezi Mungu, Mfanya miujiza yote, ulipenda wanawake wamshinde adui wetu kwa kufa kishahidi: Utujalie tuiadhimishe vema Sikukuu ya N. Bikira na Shahidi wako Mbarikiwa; ili tumfuatishe mwenendo wake, na kukufikia Wewe salama. Kwa. |
A virgin Martyr |
(13) Bikira asiye Shahidi Utusikie, Ee Mungu wa wokovu wetu: Tuifurahie Sikukuu hii ya N. Bikira wako Mbarikiwa; na kuelimishwa hali ya utauwa lia upendo. Kwa. |
A Virgin not a Martyr |
(14) Mwanamke aliye Shahidi Mwenyezi Mungu, Mfanya miujiza yote, ulipenda wanawake wamshinde adui wetu kwa kufa kishahidi: Utujalie tuiadhimishe vema Sikukuu ya N. Shahidi wako Mbarikiwa; ili tumfuatishe mwenendo wake, na kukufikia Wewe salama. Kwa. |
A female Martyr |
(15) Mwanamke asiye Shahidi Utusikie, Ee Mungu wa wokovu wetu: Tuifurahie Sikukuu hii ya N. Mtakatifu wako; na kuelimishwa hali ya utauwa na upendo. Kwa. |
A Woman not a Martyr |
MTAKATIFU WA MTAANI (ambaye kwamba Sikukuu yake imeamriwa Kawaida ya Mtakatifu) ¶ Sikukuu iliyo kubwa, ina Oktavo. (Masomo 314J, 322A, 315J, yaweza kufaa.) Sala ya Jioni (ya 1 na ya 2) ANT. ZAB. Msifuni Bwana, enyi wateule wake; Ziadhimisheni Sikukuu zake zenye furaha. Sala ya Asubuhi ANT. ZAB. Nikaona mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, Watu wa kila taifa, wamesimama mbele ya kiti. Sala ya Adhuhuri Kama kawaida ya Mtakatifu. |
A Saint of this country (?) |
KAWAIDA YA MALAIKA ZABURI na Antifona za kawaida. Sala ya Adhuhuri SOMO. Nalisikia sauti ya Malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi, na elfu mara elfu, wakisema kwa sauti kuu, Wokovu una Mungu wetu. Sala ya Ukumbusho Ant. Hawa wote ni roho waabuduo, Wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu. |
Common of an Angel |
Return to the Zanzibar Prayer Book
Web author: Charles Wohlers | U. S. England Scotland Ireland Wales Canada World |