The Book of Common Prayer | |||||||
|
|
SEHEMU ZA SALA ZINAZOBADILIKA
|
Prayers for the Christian Year |
MAJILIO ZABURI na Antifona za kawaida. Sala ya Adhuhuri SOMO. Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia, basi, na tuyavue matendo ya giza, na kuzi vaa silaha za nuru. ¶ Siku za kazi wote wapige magoti, na Mhudumu aseme, Bwana, uturehemu. Baba yetu (kimoyomoyo). ¶ Ndipo Mhudumu asimame, aimalize sala kama kawaida. Sala ya Ukumbusho wa Majilio Ant. Njoo, Ee Bwana, utujie kwa amani, Ili tufurahi mbele zako kwa moyo mkamilifu. Sala ya S. B. ya Majilio iliyotangulia |
Advent Translations of some common words: Zab., Zaburi: Psalm(s) |
S. B. I Majilio Ee Bwana, katika maisha haya yasiyodumu ulikuja kwa unyenyekevu mkuu utuangalie: Tunakusihi uuamshe uweza wako, uje, uyaepushie mbali nasi matendo ya giza, na kutuvika silaha za nuru; ili, siku ya mwisho, utakaporudi kwa utukufu wa enzi yako kuwahukumu wahai na wafu, tufufukie maisha yasiyo na mwisho. Uishiye na kumiliki pamoja na Mungu Baba, katika umoja wa Roho Mtakatifu, Mungu daima milele na milele. Amin. |
1 Advent |
S. B. II Majilio Ee Bwana, tunakusihi: Uiamshe mioyo yetu tumfanyizie njia Mwana wako pekee; ili nia zetu zisafishwe kwa kuja kwake, nasi tustahili kukutumikia. Kwa Yeye. |
2 Advent |
S. B. III Majilio Ee Bwana, tunakusihi: Uyatege masikio yako kwa sala zetu; uje, utuangalie, ili nuru yako iziangaze nia zetu za giza. Uishiye na kumiliki pamoja na Mungu Baba, katika umoja wa Roho Mtakatifu, Mungu daima milele na milele. Amin. |
3 Advent |
Robo Mwaka Jumatano Mwenyezi Mungu, tunakusihi: Utujalie tuitazamie kwa furaha Sikukuu ya ukombozi wetu; ili kwa msaada wako tuokoke katika maisha haya, na kwa ukarimu wako tupewe thawabu ya furaha za milele. Kwa. Ijumaa Ee Bwana, tunakuomba: Uje na uweza wako; utujalie tuzidi kulitumainia pendo lako, na kuwekwa huru katika mabaya yote. Uishiye na kumiliki pamoja na Mungu Baba, katika umoja wa Roho Mtakatifu, Mungu daima milele na milele. Amin. Jumamosi Ee Mungu, unaona ya kuwa tunateswa sana kwa sababu ya upotofu wetu: Utujalie, tunakusihi; tufarijiwe kwa kuja kwako. Uishiye na kumiliki pamoja na Mungu Baba, katika umoja wa Roho Mtakatifu, Mungu daima milele na milele. Amin. |
Ember Days |
S. B. IV Majilio Ee Bwana, tunakusihi: Uuamshe uweza wako, uje, utusaidie kwa nguvu nyingi; utupe msaada wa neema yako, ili rehema zako zitusafishie njia yetu tuliyoiziba kwa dhambi zetu. Uishiye na kumiliki pamoja na Mungu Baba, katika umoja wa Roho Mtakatifu, Mungu daima milele na milele. Amin. |
4 Advent |
Des. 24. Mkesha wa Kuzaliwa. |
Christmas Vigil |
KUZALIWA KWA BWANA Sala ya Jioni (ya 1 na ya 2) ANT. ZAB. Mfalme wa amani ametukuzwa Kuliko wafalme wote wa dunia. Haleluya. Sala Mwenyezi Mungu, ulitupa Mwana wako pekee autwae utu wetu, na, kama majira haya, kuzaliwa na Bikira safi: Utuialie sisi tuliozaliwa mara ya pili na kufanyika watoto wako kwa kuchaguliwa na kwa neema; tufanywe upya kila siku kwa Roho wako Mtakatifu. Kwa Yeye, Bwana wetu Yesu Kristo Mwana wako; Aishiye na kumiliki pamoja nawe, katika umoja wake Yeye huyo Roho Mtakatifu, Mungu daima milele na milele. Amin. Sala ya Asubuhi ANT. ZAB. Mara walikuwapo pamoja na huyo Malaika wingi wa jeshi la mbinguni, Wakimsifu Mungu. Haleluya. Sala ya Adhuhuri Ubeti wa mwisho wa Wimbo. Ee Yesu, Mwana wa Bikira, SOMO. Wewe, BWANA, hapo mwanzo uliitia misingi ya nchi, na mbingu ni kazi za mikono yako. Sala ya Ukumbusho wa Kuzaliwa Ant. Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia. Haleluya. |
Christmas Day |
Des. 26. Stefano, Sh. wa Kwanza. 2. (na Jan. 2) Sala Mwenyezi Mungu, wa milele, ulitabaruku malimbuko ya Mashahidi wako katika damu ya Stefano Mbarikiwa: Utujalie, tunakusihi; atuwie mwombezi wetu, kama vile alivyowaombea adui zake. Kwa. |
St. Stephen |
Des. 27. Yohana, Mtume, Mtunga Injili. 2. (na Jan. 3) Sala Ee Bwana, mwenye rehema, tunakusihi, uliangaze Kanisa lako kwa fadhili zako: Ili litiwe nuru kwa mafundisho ya Yohana Mbarikiwa, Mtume wako na Mtunga Injili; na kuzidi kwenda katika nuru ya kweli yako, hatimaye likapate kuifikia nuru ya maisha ya milele. Kwa. |
St. John the Evangelist |
Des. 28. Wasio na Hatia. 2. (na Jan. 4) Sala Mwenyezi Mungu, ulikamilisha sifa kwa vinywa vya watoto nao wanyonyao, ukapenda watoto wadogo wakutukuze kwa kufa wala si kwa kunena: Uyafishe ndani yetu mabaya yote, na kutufanya imara kwa neema yako; ili tulitukuze Jina lako takatifu sikuzote kwa maisha safi, na kwa imani iliyo thabiti hata kufa. Kwa. |
Holy Innocents |
Des.29. Tomaso wa Canterbury, A. Sh. 3 Sala Ee Mungu, kwa ajili ya Kanisa lako Tomasa wa Canterbury, Askofu Mtukufu, aliuawa kwa panga za watu wakorofi: Tunakusihi; wote wajitakiao msaada kwake wapate kuombewa naye, na kwa rehema zako uwajalie wokovu. Kwa. |
Thomas of Canterbury |
S. B. Baada ya Kuzaliwa Mwenyezi Mungu, wa milele, tunakuomba: Utuongoze siku zote kwa mapenzi yako mema; ili tustahili kulichukua Jina la Mwana wako Mpendwa, na kumtendea yaliyo mazuri. Aishiye na kumiliki pamoja nawe, katika umoja wa Roho Mtakatifu, Mungu daima milele na milele. Amin. |
Sunday after Christmas |
Des. 31. Silvesta, A. Mu. 3 Sala Ee Mungu wa wokovu wetu, ulimweka Silvesta Mtakatifu awe Askofu na Kuhani Mkuu katika Kanisa lako, ukampa amani mbele ya adui zake: Utujalie, tunakusihi, amani yako siku zetu zote; ili tuzidi kuendelea katika njia ya wokovu, na kuifurahia maisha ya utulivu. Kwa. |
Sylvester |
Jan. 1. Kutahiriwa kwa Bwana. 2 Mwenyezi Mungu, ulipenda Mwana wako Mtukufu atahiriwe, aifuate torati kwa ajili ya wanadamu: Utujalie kutahiriwa kwa kweli, kwa rohoni; ili, tamaa za dunia na za mwili zikifishwa ndani yetu, tuyatii mapenzi yako katika mambo yote. Kwa Yeye. ¶ Baada ya Jan. 1 zitumike Zaburi na Antifona za kawaida. ¶ Ikiwa Jan. 2, 3, 4, au 5 ni S.B. ibada yake ndiyo ya Jina Takatifu, Yesu. (taz. Aug. 7.) |
Circumcision |
Jan. 5. Mkesha wa Ufunuo Kama S. B. baada ya Kuzaliwa |
Vigil of Epiphany |
UFUNUO WA BWANA Sala ya Jioni (ya 1 na ya 2) ANT. ZAB. Nuru utokaye Nuru, umeonekana, Ee Kristo; Kwako Mamajusi walileta tunu. Haleluya. Sala Ee Mungu, uliwafunulia mataifa Mwana wako pekee kwa kutokea nyota: Kwa rehema zako utubariki sisi tunaokujua sasa kwa imani; ili baada ya maisha haya tuufurahie Uungu wako Mtukufu. Kwa Yeye. Sala ya Asubuhi ANT. ZAB. Mamajusi walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno; Wakaingia nyumbani wakamwona mtoto. Haleluya. Sala ya Adhuhuri Ubeti wa mwisho wa Wimbo. Kwa Ufunuo wako, Bwana, SOMO. Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, na utukufu wa BWANA umekuzukia. Sala ya Ukumbusho wa Ufunuo Ant. Twafanya Sikukuu yenye kupambwa miujiza mitatu; Leo nyota iliwaongoza Mamajusi kwenve zizi, leo maji yaligeuka kuwa divai arusini, leo Kristo alikubali kubatizwa na Yohana katika Yordani, ili atuokoe. Haleluya. |
Epiphany |
S. B. I Ufunuo Ee Bwana, tunakusihi: Ufikilize kwa wema wako wa mbinguni haja za watu wakuombao; ili wajue yawapasayo kuyatenda, na kupewa nguvu ya kuyatimiza wayajuayo. Kwa. |
1 Epiphany |
S. 8. Ufunuo Ee Mungu, ulipenda Mwana wako wa azali aonekane amejitwalia ubinadamu wetu: Utujalie; kama vile alivyo-kubali kufanana nasi kwa mambo yote ya mwilini, sisi nasi tufananishwe naye kwa mambo yote ya moyoni. Aishiye na kumiliki pamoja nawe, katika umoja wa Roho Mtakatifu, Mungu daima milele na milele. Amin. ¶ Baada ya Siku ya Nane ya Ufunuo hata Kwaresima Ibada ndiyo ya kawaida, isipokuwa ni Sikukuu. |
Octave of Epiphany (?) |
S. B. II Ufunuo Mwenyezi Mungu wa milele, unayatawala yaliyo mbinguni na yaliyo duniani: Uzisikie kwa rehema dua za watu wako; na kutujalia amani siku zetu zote. Kwa. |
2 Epiphany |
S. B. III Ufunuo Mwenyezi Mungu wa milele, uutazame kwa huruma udhaifu wetu: Uunyoshe mkono wako wa kuume; na kutuhifadhi katika hatari na shida zetu zote. Kwa. |
3 Epiphany |
S. B. IV Ufunuo Ee Mungu, unajua ya kuwa sisi tumo hatarini sana, wala hatuwezi kusimama kwa sababu ya udhaifu wa ubinadamu: Utujalie uzima wa roho na wa mwili; ili, kwa' msaada wako, tusishindwe na mambo yatupatayo kwa ajili ya dhambi zetu. Kwa. |
4 Epiphany |
S. B. V Ufunuo Ee Bwana, tunakusihi: Uwalinde watu wako kwa pendo lisilokwisha; ili tukilitegemea tumaini la neema yako ya mbinguni, tuhifadhiwe kwa himaya yako ya daima. Kwa. |
5 Epiphany |
S. B. VI Ufunuo Ee Mungu, Mwana wako Mtakatifu alitokea makusudi azivunje kazi za Shetani, na kutufanya wana wa Mungu: Tunakusihi, utujalie sisi tulio nalo tumaini hili, tuwe watakatifu kama Yeye alivyo mtakatifu; ili, atakapotokea tena, tufananishwe naye katika ufalme wako mtukufu wa milele. Kwa Yeye. |
6 Epiphany |
SEPTUAJESIMA Yote kama kawaida isipokuwa haya, ¶ Katika Sala ya Jioni ya kwanza ya Septuajesima V na R ya mwisho huimbwa, au kusemwa, hivi. V. Tumhimidi BWANA. Haleluya. Haleluya. S. B. Septuajesima Ee Bwana, tunakusihi: Uzisikilize kwa upole sala za watu wako; ili sisi, tunaoteswa kwa haki kwa sababu ya dhambi zetu, tupate kwa rehema zako kuachiliwa, kwa ajili ya utukufu wa Jina lako. Kwa. |
Septuagesima |
S. B. Seksajesima Ee Mungu, unaona ya kuwa sisi hatutumainii tendo letu liwalo lote: Kwa neema yako, ukubali kutulinda; ili tuhifadhiwe na mabaya yote. Kwa. |
Sexagesima |
S. B. Kwinkwajesima Ee Bwana, umetufundisha ya kuwa matendo yetu yote pasipo upendo hayafai: Tunakusihi; utumiminie mioyoni mwetu upendo huo, na kwa rehema zako utujalie kuzidi kuzitubia dhambi zetu. Kwa. |
Quinquagesima |
Jumatano ya Majivu Mwenyezi Mungu wa milele, huchukii kitu cho chote ulichokifanya, bali waziondoa dhambi za wote waliotubu: Utuumbie moyo mpya na uliopondeka; ili tujililie dhambi zetu kama itupasavyo, na kusamehewa nawe kabisa, Ee Mungu mwenye rehema nyingi. Kwa. Alhamisi Ee Mungu, wachukizwa kwa kosa na kuridhishwa kwa toba: Uzikubali kwa rehema sala za watu wako wakuombao; uiepushie mbali nasi hasira yako tunayoistahili kwa dhambi zetu. Kwa. Ijumaa Ee Bwana, tunakusihi: Utusaidie kwa hisani yako katika mfungo wetu tuliouanza ; ili tupate kufanya bidii katika mioyo yetu, kama vile tunavyoionyesha miilini mwetu. Kwa. Jumamosi Ee Bwana, uyafanikishe maombi yetu: Utujalie tuufululize vema mfungo huu; ulio amriwa kwa afya yetu ya mwili na ya roho. Kwa. |
Ash Wednesday |
KWARESIMA (Tokea S. B. ya 1 Kwaresima) ZABURI na Antifona za kawaida. Sala ya Aduhuri SOMO. Tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa. Tusiwe kwazo la namna yo yote katika jambo lo lote, ili utumishi wetu usilaumiwe. ¶ Siku za kazi wote wapige magoti, na Mhudumu aseme, Bwana, uturehemu. Baba yetu (kimoyomoyo). ¶ Ndipo Mhudumu asimame, aimalize sala kama kawaida. Sala ya Ukumbusho wa Kwaresima Ant. Ee Mungu, unirehemu sawasawa - na fadhili zako; Kiasi cha wingi wa rehema zako uyafute makosa yangu. Sala ya siku ya kazi ya Kwaresima. |
Lent (Until the first Sunday in Lent) |
S. B. I Kwaresima Ee Bwana, ulifunga kwa ajili yetu siku arobaini mchana na usiku: Utujalie tufunge chakula hata mwili utiishwe kwa roho; ili tufuate sikuzote maelekezo yako katika haki na utakatifu halisi, kwa heshima na utukufu wako. Uishiye na kumiliki pamoja na Mungu Baba, katika umoja wa Roho Mtakatifu, Mungu daima milele na milele. Amin. Jumatatu Ururudishe, Ee Mungu wa wokovu wetu: Uielemishe mioyo yetu kwa malezi yako ya mbinguni; ili tufaidiwe kwa kufunga kwetu wakati huu wa Kwaresima. Kwa. Jumanne Ee Bwana, uiangalie jamaa hii ya watu wako: Utujalie sisi tujirudi kwa kuzifisha tamaa za mwili; ili mbele zako mioyo yetu iangazwe kwa kukuonea shauku. Kwa. Jumatano, Robo Mwaka Ee Bwana, tunakusihi: Kwa huruma zako uzisikilize dua zetu; uunyoshe mkono wako wa kuume, na kutuondolea mambo yote yanayotupinga, Kwa. Alhamisi Ee Bwana, tunakuomba, uikubali nia njema ya watu wako: Ili tupate kujiweza mwili kwa kufunga; na kuburudika moyoni kwa mazao ya matendo mema. Kwa. Ijumaa, Robo Mwaka Ee Bwana, utuonee huruma sisi watumishi wako: Tuzidi kujiweka kwako kwa neema yako; ili turehemiwe na kufarijiwa kwa ukarimu wako. Kwa. Jumamosi, Robo Mwaka Ee Bwana, tunakusihi: Uwaangalie watu wako kwa upendo wako; na kwa rehema zako uyageuzie mbali nasi mapigo ya hasira yako. Kwa. |
1 Lent (Robo Mwaka = Ember Days) |
S. B. II Kwaresima Mwenyezi Mungu, unaona ya kuwa sisi hatuna wema wo wote: Utulinde ndani na nje; ili tuhifadhiwe na madhara yote yawezayo kuupata mwili, na kusafishwa na mawazo mabaya ya moyoni. Kwa. Jumatatu Mwenyezi Mungu, tunakusihi: Uwajalie watoto wako wafunge chakula kwa kujinyima mwilini; na kujiepusha na dhambi kwa kuifuata haki. Kwa. Jumanne Ee Bwana, tunakuomba, uikamilishe ndani yetu kazi hii ya kufunga: Ili kwa maagizo yako tuyajue yatupasayo; na kwa uweza wako tuyatimize. Kwa. Jumatano Ee Bwana, tunakusihi, uwatazame kwa rehema watu wako: Utujalie tuyaepuke mabaya yote; kama vile ulivyotuagiza kujihinisha chakula. Kwa. Alhamisi Ee Bwana, tunakusihi, utupe msaada wa neema yako: Ili tujitahidi katika kufunga na kusali; na kuokolewa na adui zetu zote za mwili na za roho. Kwa. Ijumaa Mwenyezi Mungu, tunakuomba, utujalie neema yako: Ili tutakaswe kwa kufunga kwetu; na kwa mioyo safi tuikaribie Sikukuu inayokuja. Kwa. Jumamosi Ee Bwana, tunakusihi, utujalie tufunge kwa faida ya roho zetu: Ili tuongezewe nguvu za rohoni; kwa ajili ya kujirudi miilini mwetu. Kwa. |
2 Lent |
S. B. III Kwaresima Mwenyezi Mungu, tunakusihi: Uzitafakari haja za watu wako wanyenyekevu; uunyoshe mkono wako wa kuume ili utuhifadhi na adui zetu zote. Kwa. Jumatatu Ee Bwana, tunakuomba: Kwa rehema zako utumiminie mioyoni mwetu neema yako; Ili tunavyopunguza chakula chetu, vivyo hivyo tujiepushe na upotovu wote unaotudhuru. Kwa. Jumanne Mwenyezi Mungu, mwenye rehema: Utusikie kwa kibali; na kwa wema wako utupe kipawa chako cha uzuilifu wa tamaa. Kwa. Jumatano Ee Bwana, tunakusihi: Utujalie kuelimishwa kwa kufunga na kwa kuepuka mabaya; ili tuzidi kupata kwa wingi fadhili zako. Kwa. Alhamisi Mwenyezi Mungu, tunakusihi: Utujalie tusafishwe kwa kufunga kwetu; na kupata kibali machoni pako. Kwa. Ijumaa Ee Bwana, tunakuomba, kwa wema wako uukubali mfungo wetu: Ili kama tunavyojinyima chakula cha mwilini; vivyo hivyo tujihadhari na maovu ya moyoni. Kwa. Jumamosi Mwenyezi Mungu, tunakusihi: Uwajalie wao wautiishao mwili kwa kufunga chakula; wajitenge na dhambi kwa kuifuatisha haki. Kwa. |
3 Lent |
S. B. IV Kwaresima Mwenyezi Mungu, tunakusihi: Utujalie neema yako; ili tusizidi kuteswa kwa ubaya wa matendo yetu, bali tuburudishwe kwa faraja ya neema yako. Kwa. Jumatatu Mwenyezi Mungu, tunakusihi: Utujalie sisi tunaozishika nyakati hizi za kufunga kila mwaka; tukupendeze kwa mwili na roho. Kwa. Jumanne Ee Bwana, tunakuomba: Kwa kufunga kwetu tuzidi kuutengeneza mwenendo wetu; na kujipatia daima msaada wa fadhili zako. Kwa. Jumatano Ee Mungu, unawapa wenye haki thawabu na wenye dhambi masamaha kwa njia ya kufunga: Uturehemu sisi tukuombao; ili kwa kuungama dhambi tujiweke tayari kupokea ghofira. Kwa. Alhamisi Mwenyezi Mungu, tunakuomba: Utujalie sisi tunao-adhibiwa kwa kufunga tufurahishwe kwa ibada yetu; ili tupunguziwe tamaa za duniani, na kuzidi kuambatana na mambo ya mbinguni. Kwa. Ijumaa Ee Mungu, unafanya upya ulimwengu kwa Sakramenti za ajabu: Utujalie, tunakusihi; Kanisa lako lifaidiwe kwa ibada za milele, wala lisikose msaada wako hapa duniani. Kwa. Jumamosi Ee Bwana, tunakusihi: Ibada yetu ya upendo iwe na mazao tele kwa neema yako; kwa maana kufunga kwetu kwafaa tupatapo kibali kwa rehema zako. Kwa. |
4 Lent |
WAKATI WA MATESO ZABURI na Antifona za kawaida. Sala ya Adhuhuri SOMO. Damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai. ¶ Siku za kazi wote wapige magoti, na Mhudumu aseme, Bwana, uturehemu. Baba yetu (kimoyomoyo). ¶ Ndipo Mhudumu asimame, aimalize sala kama kawaida. |
Season of the Passion |
S. B. ya Mateso Mwenyezi Mungu, tunakusihi: Uiangalie kwa neema jamaa ya watu wako; ili kwa ukarimu wako miili yao itawaliwe, na roho zao zitunzwe. Kwa. Jumatatu Ee Bwana, tunakusihi: Uutakase mfungo wetu; na kwa rehema zako utusamehe makosa yetu. Kwa. Jumanne Ee Bwana, tunakuomba, utukubali tufungapo: Ili tuistahili neema yako kwa fidia hii ya dhambi zetu; hata na tuletewe dawa ya milele. Kwa. Jumatano Ee Mungu, uiangaze mioyo yao wenye imani kwa kuutakasa mfungo huu: Uwajalie moyo wa ibada; ili uwasikilize kwa kibali wakuombapo. Kwa. Alhamisi Mwenyezi Mungu, tunakuomba: Utujalie kurudishiwa heshima ya ubinadamu kwa kujinyima kwetu; kwa maana imeharibika kwa kujipendeza kwetu. Kwa. Ijumaa Ee Bwana, tunakusihi, utupe kwa ukarimu neema yako: Ili tukomeshe dhambi kwa kuhiari maadili; na kwa kurudiwa sasa tuiepuke adhabu ya milele. Kwa. Jumamosi Ee Bwana, tunakuomba, watu wako wazidi kukuabudu: Ili wafundishwe kwa ibada takatifu; na kama vile walivyo-pokea kibali kwako, wazidi kukutolea sadaka. Kwa. |
Passion Sunday |
S. B. ya Mitende Mwenyezi Mungu wa milele, ulimtuma Mwokozi wetu autwae mwili wetu na kuu vumilia msalaba, ili tuufuatishe unyenyekevu wake: Utujalie tuyakumbuke mateso yake itupasavyo; ili, kwa njia ya saburi yake, tuufikie utukufu wa kufufuka kwake. Kwa Yeye. |
Palm Sunday |
Jumatatu katika Juma Takatifu Mwenyezi Mungu, upende kutusikiliza: Utuburudishe kwa ajili ya Mateso ya Mwana wako pekee; kwa maana tumedhoofika kwa mabaya mengi yaliyotupata. Kwa Yeye. Jumanne katika Juma Takatifu Mwenyezi Mungu, wa milele, tunakuomba, uzikubali dua zetu: Utujalie tuufululize ukumbusho wa Mateso ya Bwana wetu; ili tustahili kupewa masamaha aliyotupatia. Kwa Yeye. Jumatano katika Juma Takatifu Ee Mungu, ulipenda Mwana wako auvumilie msalaba, ili aziepushie mbali nasi nguvu za Shetani: Utujalie, tunakuomba; sisi watumishi wako tuipate neema ya kufufuliwa. Kwa Yeye. |
Monday in Holy Week |
ALHAMISI YA AMRI ¶ Atukuzwe isisemwe kamwe po pote. Sala ya Asubuhi ¶ Inaanzia Zaburi (zikiisha sala za siri). Ant. Mungu hakumwachilia Mwana wake mwenyewe, Bali alimtoa kwa ajili yetu. ZAB. 40 1. Nalimngoja BWANA kwa saburi, * 5. Wengi wataona na kuogopa, * 10. Ndipo niliposema, Tazama nimekuja, katika gombo la chuo nimeandikiwa, * 15. Nawe, BWANA, usinizuilie rehema zako, * 19. Ee BWANA, uwe radhi kuniokoa, * Ant. Mungu hakumwachilia Mwana wake mwenyewe; Bali alimtoa kwa ajili yetu. ZAB. 54 1. Ee Mungu, kwa Jina lako uniokoe, * Ant. Kama mwana-kondoo BWANA alipelekwa machinjoni; Naam, hakufumbua kinywa chake. ZAB. 88 1. Ee BWANA, Mungu wa wokovu wangu, * 7. Mimi umenilaza katika shimo la chini, * 11. Ee BWANA, nimekuita kila siku; * 15. Lakini mimi nimekulilia Wewe, BWANA, * Ant. Enyi nyote mpitao, angalieni, Mtazame kama kuna majonzi yo yote mfano wa majonzi yangu. WIMBO, V. na R. hapana. ¶ Ikiisha BENEDICTUS na Antifona yake mara husemwa na wote, wamepiga magoti, Kristo alikuwa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. ZAB. 51 (Isemwe na wote pamoja kwa sauti ndogo.) ¶ Ndipo hufuata pasipo BWANA akae nanyi wala Tuombe, Mwenyezi Mungu, tunakusihi: Uiangalie jamaa hii ya ¶ Wala wasiongeze neno. Sala ya Adhuhuri ¶ Inaanzia Zaburi (zikiisha sala za siri). ANT. ZAB. hapana. ¶ Zikiisha Zaburi wapige magoti, waseme yote tangu Kristo alikuwa mtii hata mwisho wa sala, kama sala ya asubuhi. Sala ya Jioni ¶ Imekatazwa isiimbwe. Ant. Nitakipokea kikombe cha wokovu; Na kulitangaza Jina la BWANA. ZAB. 69 1 Ee, Mungu, uniokoe, * 9. Wewe, Mungu, unajua upumbavu wangu, * 17. Waketio langoni hunisema, * 23. Ee BWANA, unijibu maana fadhili zako ni njema, * 29. Wakanipa uchungu kuwa chakula changu; * 37. Nami niliye maskini na mtu wa huzuni, * Ant. Nitakipokea kikombe cha wokovu; Na kulitangaza Jina la BWANA. ZAB. 90 1. Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, * 5. Wawagharikisha, huwa kama usingizi, * 10. Siku za miaka yetu ni miaka sabini, * 15. Utushibishe asubuhi kwa fadhili zako, * Ant. Nalitazama mkono wangu wa kuume, nikaona, Ya kuwa hakuna mtu anijuaye. WIMBO, V. na R. hapana. ANT. MAGNIFICAT. Walipokuwa wakila, Yesu alitwaa mkate, akabariki, Akaumega, akawapa wanafunzi wake. ¶ Ikiisha DEUS MISEREATUR na Antifona yake, wapige magoti, waseme, Kristo, etc., kama sala ya asubuhi. Sala ya Usiku Naungama, etc. ¶ Ikiisha, wapige magoti, waseme, Kristo, etc., kama sala ya asubuhi. |
Maundy Thursday |
IJUMAA KUU ¶ Leo mwisho wa Masomo, Msomaji asikibusu kitabu wala isisemwe, V. Nawe, BWANA, uturehemu. Yote kama Alhamisi ya Amri isipokuwa haya, Sala ya Asubuhi ANT. BENEDICTUS. Waliweka juu ya kichwa chake mashitaka yake, yaliyoandikwa, Huyu ni Yesu, Mfalme wa Wayahudi. Sala ya Jioni ANT. MAGNIFICAT. Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema, Imekwisha; Akainama kichwa, akaisalimu roho yake. |
Good Friday |
MKESHA WA PASAKA Sala ya Asubuhi Yote kama Alhamisi ya Amri isipokuwa, Sala ya Adhuhuri Yote kama Alhamisi ya Amri. Sala ya Jioni (Ndiyo ya kwanza ya Pasaka) ¶ Ikiimbwa pamoja na Missa tafuta amri zake katika Missale. ¶ Ikiimbwa kama kawaida ya Sala ya Jioni, inaanzia (zikiisha sala za siri), V. Ee Mungu, uwe radhi kutuokoa. Kama kawaida. ¶ Ndipo hufuata, V. BWANA akae nanyi. Tuombe Ee Bwana, utumiminie mioyoni mwetu Roho wa upendo wako: Ili sisi sote tuwe na moyo mmoja; kwa kuwa umetushibisha siri zako za Pasaka. Kwa Bwana wetu Yesu Kristo Mwana wako; Aishiye na kumiliki pamoja nawe, katika umoja wake Yeye huyo Roho Mtakatifu, Mungu daima milele na milele. Amin. Sala ya Usiku ¶ Isemwe kama kawaida ya sikuzote, isipokuwa, ANT. ZAB. Haleluya, Haleluya, Haleluya. ¶ Tangu mwanzo hata mwisho hakuna kupiga magoti Wakati wa Pasaka. |
Easter Vigil |
PASAKA Sala ya Asubuhi BADALA ya VENITE ¶ (Sikukuu tu; siyo katika siku nyinginezo saba za Oktavo.) 1. Pasaka yetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo; * Basi na tuifanye karamu. Tuombe Sala V. BWANA akae nanyi. Sala ya Adhuhuri WIMBO hapana. ¶ Zikiisha Zaburi na Antifona yake, Siku hii ndiyo aliyoifanya BWANA; * Tutashangilia na kuifurahia. Tuombe Sala V. BWANA akae nanyi. Sala ya Jioni ANT. ZAB. Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu. Haleluya. Tuombe Sala V. BWANA akae nanyi. Sala ya Usiku ANT. ZAB. Haleluya, Haleluya, Haleluya. ¶ Ikiisha Nunc Dimittis na Antifona yake, Siku hii ndiyo aliyoifanya BWANA; * Tutashangilia na kuifurahia. Tuombe Sala V. BWANA akae nanyi. |
|
Sikukuu ya Pasaka 1 Mwenyezi Mungu, ulishinda mauti na kutufungulia mlango wa uzima wa milele kwa Mwana wako pekee, Yesu Kristo: Utujalie tuzitimize nadhiri zetu kwa msaada wako; kwa kuwa umezitia mioyoni mwetu kwa neema yako. Kwa Yeye. |
Easter Day |
Jumatatu ya Pasaka 1 Ee Mungu, umeuponya ulimwengu kwa kufufuka kwake Mwana wako Yesu Kristo: Tunakuomba, watu wako wakae na karama zako za mbinguni; ili waustahili uhuru wa uana, na kuufikia uzima wa milele. Kwa Yeye. Jumanne ya Pasaka 1 Ee Mungu, wapenda sikuzote kuliongeza Kanisa lako kwa kulitilia watu wapya: Uwajalie watumishi wako waambatane na siri ya kufufuka kwake Mwana wako; ili waiitikie siri hiyo kwa matendo kama walivyoikubali kwa imani. Kwa Yeye. Jumatano ya Pasaka Ee Mungu, watufurahisha kila mwaka kwa ukumbusho wa kufufuka kwake Bwana wetu: Utujalie, tunakusihi; tustahili kuzifikia furaha za milele kwa Sikukuu hizi tunazozishika hapa duniani. Kwa Yeye. Alhamisi ya Pasaka Ee Mungu, umeunganisha kabila za watu mbalimbali kwa kulikiri Jina lako: Uwajalie wote waliozaliwa mara ya pili katika Ubatizo; wawe na umoja wa imani mioyoni mwao, na umoja wa utii katika mwenendo wao. Kwa. Ijumaa ya Pasaka Mwenyezi Mungu wa milele, umetupa siri hii ya Pasaka iwe agano la kupatanishwa kwetu nawe: Utujalie, tunakusihi; tuyaige kwa mwenendo wetu mambo hayo tunayoyakiri kwa midomo yetu. Kwa. Jumamosi ya Pasaka Mwenyezi Mungu, tunakuomba: Utujalie sisi tulioishika Sikukuu hii ya Pasaka kwa heshima nyingi; tustahili kuzifikia furaha zilizo za milele kwa Sikukuu hiyo. Kwa. |
Monday in Easter Week |
WAKATI WA PASAKA (Tokea Oktavo ya Pasaka) Sala ya Jioni (ya 1 na ya 2) ANT. ZAB. Haleluya, Haleluya, Haleluya. Sala ya Asubuhi ANT. ZAB. Haleluya, Haleluya, Haleluya. Sala ya Adhuhuri Ubeti wa mwisho wa Wimbo. Ahimidiwe Mungu Baba, ANT. ZAB. Haleluya, Haleluya, Haleluya. ¶ Ibada isemwe hivyo Wakati wa Pasaka hata Mkesha wa Kupaa, kila siku, isipokuwa ni Sikukuu. Sala ya Ukumbusho wa Msalaba (M) Ant. Aliyesulibiwa amefufuka katika wafu; Na kutukomboa sisi. Haleluya. Tuombe Ee Mungu, ulikubali Mwana wako auvumilie Msalaba kwa ajili yetu, azifukuzie mbali nasi nguvu zote za adui: Utukirimie sisi, watumishi wako; tuwe na neema ya kufufuliwa katika wafu. Kwa Yeye. |
Easter Season (actually the Octave of Easter) |
S. B. I Pasaka Baba Mwenyezi, ulimtoa Mwana wako pekee afe kwa ajili ya dhambi zetu, na kufufuka tupate kufanyizwa wema: Utujalie tuitupie mbali chachu ya uovu na ubaya; ili tupate kukutumikia sikuzote kwa usafi wa imani na mwenendo. Kwa Yeye. |
1st Sunday after Easter |
S. B. II Pasaka Mwenyezi Mungu, ulimtoa Mwana wako awe kwetu dhabihu kwa dhambi na mfano wa wema: Utujalie neema tuifahamu sikuzote kwa shukrani fadhili yake iliyo bora; tujitahidi kila siku kuzifuata nyayo zake takatifu. Kwa Yeye. |
2 Easter |
J5 Yusufu, Mfadhili wa Kanisa Katholiko, 1. |
St. Joseph |
S. B. III Pasaka Mwenyezi Mungu, umewaonyesha wanaopotea nuru ya kweli yako, wapate kuirudia njia ya haki: Uwajalie wote walioingizwa katika ushirika wa dini ya Kristo; wayakatae yasiyopatana na jina hilo, na kuyafuata yanayopatana nalo. Kwa Yeye. |
3 Easter |
S. B. IV Pasaka Mwenyezi Mungu, Wewe peke yako waweza kuzitawala nia kaidi za wenye dhambi: Uwajalie watu wako wayapende uliyoyaamuru, na kuyataka uliyoyaahidi; ili, katika dunia hii isiyo starehe, mioyo yetu istarehe huko kunako furaha za kweli. Kwa. |
4 Easter |
S. B. V Pasaka Ee Mungu, uliye asili ya mema yote: Utujalie tuyaombayo; uziangaze nia zetu, ili tuyawaze yaliyo ya haki, na kutuelekeza mioyo hata tuyatimize. Kwa. |
5 Easter |
KUPAA KWA BWANA Sala ya Jioni (ya 1 na ya 2) ANT. ZAB. Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni Atakuja jinsi iyo hiyo. Haleluya. Sala Mwenyezi Mungu, tunasadiki ya kwamba Bwana wetu Yesu Kristo, Mwana wako pekee, amepaa mbinguni: Utujalie na sisi tupae huko kwa moyo na akili; na kukaa pamoja naye sikuzote katika mambo ya mbinguni. Kwa Yeye. Sala ya Asubuhi ANT. ZAB. Bwana, baada ya kusema nao, alichukuliwa juu mbinguni; Akaketi mkono wa kuume wa Mungu. Haleluya. Sala ya Adhuhuri Ubeti wa mwisho wa Wimbo. Uliyeshinda, ukapaa, ANT. ZAB. Haleluya, Haleluya, Haleluya. Sala ya Ukumbusho wa Kupaa Ant. Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu; Kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu. Haleluya. |
Ascension Day |
S. B. ya Kupaa Ee Mungu, Mfalme wa utukufu, ulimpandisha kwa shangwe Mwana wako pekee Yesu Kristo katika ufalme wako wa mbinguni: Usituache yatima; bali utupelekee Roho wako Mtakatifu, atufariji, na kutupandisha huko alikotangulia Mwokozi wetu Kristo. Aishiye na kumiliki pamoja nawe, katika umoja wake Yeye huyo Roho Mtakatifu, Mungu daima milele na milele. Amin. |
Sunday after the Ascension |
Ijumaa na Mkesha wa Pentekote |
Friday & Vigil of Pentecost |
PENTEKOTE Sala ya Jioni (ya 1 na ya 2) ANT. ZAB. Nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine; Roho wa kweli. Haleluya. Sala ya Asubuhi ANT. ZAB. Mitume wakasema kwa lugha nyingine Matendo makuu ya Mungu. Haleluya. Sala ya Adhuhuri Ubeti wa mwisho wa Wimbo. Ahimidiwe Mungu Baba, ANT. ZAB Haleluya, Haleluya, Haleluya |
Pentecost (Whitsunday) |
Sikukuu ya Pentekote I Ee Mungu, kama majira haya, uliwafundisha mioyo yao wenye imani kwa nuru ya Roho Mtakatifu: Utujalie kwa Roho huyo tuyajue mambo yote kwa akili; na kuifurahia sikuzote faraja yake takatifu. Kwa Bwana wetu Yesu Kristo Mwana wako; Aishiye na kumiliki pamoja nawe, katika umoja wake Yeye huyo Roho Mtakatifu, Mungu daima milele na milele. Amin. |
Day of Pentecost |
Jumatatu ya Pentekote I Ee Mungu, uliwapa Mitume wako Roho Mtakatifu: Uwajalie watu wako mazao ya maombi yao yenye ibada; ili wale uliowapa imani wakirimiwe nawe amani pia. Kwa Bwana wetu Yesu Kristo Mwana wako; Aishiye na kumiliki pamoja nawe, katika umoja wake Yeye huyo Roho Mtakatifu, Mungu daima milele na milele. Amin. Jumanne ya Pentekote I Ee Mungu, tunakuomba: Nguvu za Roho Mtakatifu ziwe pamoja nasi; zitusafishe mioyo yetu kwa neema yake, na kutulinda na mambo yote yanayotupinga. Kwa Bwana wetu Yesu Kristo Mwana wako; Aishiye na kumiliki pamoja nawe, katika umoja wake Yeye huyo Roho Mtakatifu, Mungu daima milele na milele. Amin. |
Monday of the Week of Pentecost |
Jumatano, Robo Mwaka Ee Bwana, tunakusihi: Mfariji atokaye kwako atuangaze nia zetu; na kutuongoza katika kweli yote, kama vile Mwana wako alivyoahidi. Aishiye na kumiliki pamoja nawe, katika umoja wake Yeye huyo Roho Mtakatifu, Mungu daima milele na milele. Amin. ¶ Siku ya Alhamisi itumike sala ya Sikukuu ya Pentekote. Ijumaa, Robo Mwaka Ee Mungu, mwenye rehema, uzisikilize dua za Kanisa lako: Uliweke salama katika umoja wa Roho Mtakatifu; lisisumbuliwe kwa mapigano ya adui ye yote. Kwa Bwana wetu Yesu Kristo Mwana wako; Aishiye na kumiliki pamoja nawe, katika umoja wake Yeye huyo Roho Mtakatifu, Mungu daima milele na milele. Amin. Jumamosi, Robo Mwaka Ee Bwana, tunakusihi: Utumiminie mioyoni mwetu Roho wako Mtakatifu; ili tulivyoumbwa kwa hekima yake, vivyo hivyo tutawaliwe kwa maongozi yake. Kwa Bwana wetu Yesu Kristo Mwana wako; Aishiye na kumiliki pamoja nawe, katika umoja wake Yeye huyo Roho Mtakatifu, Mungu daima milele na milele. Amin. ¶ Sala ya Adhuhuri, Jumamosi, ndiyo mwisho wa Wakati wa Pasaka. |
Wednesday, Ember Days |
UTATU MTUKUFU Sala ya Jioni (ya 1 na ya 2) ANT. ZAB. Utukufu una Wewe, Utatu uliye Uungu mmoja; Tangu milele, na sasa, na hata milele. Sala Mwenyezi Mungu wa milele, umetupa sisi watumishi wako neema, katika imani ya kweli, kuutambua utukufu wa Utatu wa milele, na katika uweza wa Enzi ya Uungu kuuabudu Umoja: Utujalie, tunakusihi; tulindwe daima na adui zetu, kwa uthabiti wa imani hiyo. Kwa. Sala ya Asubuhi ANT. ZAB. Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, Hata milele na milele. Sala ya Adhuhuri SOMO. Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nasi sote sasa na milele. |
Trinity |
S. B. I Pentekote Ee Mungu, uliye uwezo wao wakutumainio, pasipo Wewe udhaifu wetu wa kibinadamu haufai kitu: Uzikubali kwa rehema dua zetu; utujalie tukupendeze kwa kuzikubali amri zako, na kuzitimiza kwa moyo wote. Kwa. ¶ Baada ya Sikukuu ya Utatu Mt. hata Majilio Ibada ndiyo ya kawaida, isipokuwa ni Sikukuu. |
1 Pentecost (Trinity Sunday) |
MWILI MTUKUFU WA KRISTO Sala ya Jioni (ya 1 na ya 2) ANT. ZAB. Kuhani wa milele kwa mfano wa Melkizedeki, Kristo aliye BWANA, Alileta mkate na divai. Haleluya. Sala Ee Mungu, umetuachia ukumbusho wa Mateso yako katika Sakramenti iliyo ya ajabu: Utujalie, tunakusihi, tuziheshimu siri takatifu za Mwili na Damu yako; ili tuyaone daima ndani yetu mazao ya ukombozi wako. Uishiye na kumiliki pamoja na Mungu Baba, katika umoja wa Roho Mtakatifu, Mungu daima milele na milele. Amin. Sala ya Asubuhi ANT. ZAB. Uliwalisha watu wako chakula cha mashujaa; Ukawaandalia mkate utokao mbinguni. Haleluya. Sala ya Adhuhuri Ubeti wa mwisho wa Wimbo. Ee Yesu, Mwana wa Bikira, SOMO. Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate, na akiisha kushukuru akaumega, akasema: Huu. ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Sala ya Ukumbusho wa Mwili wa Kristo Ant. Ee ajabu ya wema wa Roho wako, BWANA! unawapa watoto wako chakula bora cha mbinguni, ili uwaonyeshe wema wako; Wenye njaa unawashibisha mema; na wenye mali walioshiba unawaondoa mikono mitupu. Haleluya. |
Corpus Christi |
S. B. II Pentekote Ee Bwana, hukosi kuwatawala watu unaowalea daima kwa pendo lako: Utulinde, tunakusihi, chini ya himaya ya tunza lako jema; ututie hofu na pendo lisilokoma la Jina lako takatifu. Kwa. |
2 Pentecost |
MOYO MTAKATIFU WA YESU Sala ya Jioni (ya 1 na ya 2) ANT. ZAB. Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, Nami nitawapumzisha. Sala Ee Mungu, umetupa kwa rehema zako upendo usiopimika katika Moyo wake Mwana wako uliojeruhi kwa dhambi zetu: Utujalie, tunakusihi; tumtolee ibada yetu ya utauwa, na kumwonyesha shukrani itupasavyo. Kwa Yeye. Sala ya Asubuhi ANT. ZAB. Yesu alisimama, akapaza sauti yake, akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe. Sala ya Adhuhuri SOMO. Nampigia Baba magoti, ambaye kwa Jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa, awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa. kazi ya Roho wake, katika mtu wa ndani; Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani. Sala ya Ukumbusho wa Moyo Mt. Ant. Walipomjia Yesu, na kuona ya kuwa amekwisha kufa, hawakumvunja miguu; Lakini askari mmojawapo alimchoma ubavu kwa mkuki, na mara ikatoka damu na maji. |
Sacred Heart of Jesus |
S. B. III Pentekote Ee Mungu, Mlinzi wao wote wakuaminio, pasipo Wewe hakuna nguvu, hakuna utakatifu: Utuzidishie rehema zako; ili sisi, tulio nawe kuwa Mtawala na Kiongozi wetu, tuyapitie mambo yenye mwisho, yasije yakatupotea mambo yasiyo na mwisho. Kwa. |
3 Pentecost |
S. B. IV Pentekote Ee Bwana, tunakusihi: Uyaongoze mambo ya ulimwengu huu; ili sisi tuwe na amani, na Kanisa lako lipate furaha kwa kukuabudu katika utulivu. Kwa. |
4 Pentecost |
S. B. V Pentekote Ee Mungu, umewawekea wakupendao mema yapitayo akili za wanadamu: Utumiminie mioyoni mwetu pendo lako; ili sisi tukupende Wewe katika yote na kuliko yote, na kuzipata ahadi zako zipitazo haja zetu zote. Kwa. |
5 Pentecost |
S. B. VI Pentekote Ee Mungu, Mwenye uweza wote, kwako Wewe hutoka yote yaliyo bora: Utumiminie mioyoni mwetu pendo lako, tulipende Jina lako na kuongezewa roho ya ibada; uyazidishe yaliyo mema ndani yetu, na kuyahifadhi kwa tunza lako la Ubaba. Kwa. |
6 Pentecost |
S. B. VII Pentekote Ee Mungu, tunza lako halikosi kuuongoza ulimwengu mzima: Tunakusihi kwa unyenyekevu; utuondolee madhara yote, na kutuletea mambo yote ya kutufaa. Kwa. |
7 Pentecost |
S. B. VIII Pentekote Ee Bwana, pasipo Wewe hatuwezi neno lo lote lililo jema: Tunakusihi; utukirimie sikuzote moyo wa kuyafikiri yaliyo mema, na kuyatenda, ili tuwe na nguvu ya kuenenda kama upendavyo. Kwa. |
8 Pentecost |
S. B. IX Pentekote Ee Bwana, tunakusihi: Uyatege masikio yako ya rehema kwa sala zao wakuombao; uwape moyo wa kuyataka uyapendayo, ili uwajalie haja zao wakuombapo. Kwa. |
9 Pentecost |
S. B. X Pentekote Ee Mungu, wazionyesha nguvu zako zisizo na kiasi hasa kwa kuachilia na kurehemu: Utuzidishie rehema zako; ili, tukizikimbilia ahadi zako, tuyashiriki mema ya mbinguni. Kwa. |
10 Pentecost |
S. B. XI Pentekote Mwenyezi Mungu, wa milele, kwa wema wako mwingi wa Ubaba watupa karama za kupita stahili zetu na dua zetu: Utumiminie rehema zako; ili tusamehewe makosa yaitishayo mioyo yetu, na kupewa baraka zako sala zetu zisizozistahili. Kwa. |
11 Pentecost |
S. B. XII Pentekote Mwenyezi Mungu, mwenye rehema, watu wako wakuaminio hukutumikia vema na amini kwa karama yako tu: Utujalie, tunakusihi; tusijikwae po pote, bali tuzifikie ahadi zako za mbinguni. Kwa. |
12 Pentecost |
S. B. XIII Pentekote Mwenyezi Mungu, wa milele: Utuzidishie imani, tumaini, na upendo; utupe moyo wa kuyapenda uliyoyaamuru, ili tuyapate uliyoyaahidi. Kwa. |
13 Pentecost |
S. B. XIV Pentekote Ee Bwana, pasipo Wewe udhaifu wetu wa kibinadamu huteleza: Tunakusihi, ulilinde Kanisa lako kwa neema yako ya daima; ukalisaidie liokolewe na madhara, na kuongozwa kwenye mambo ya wokovu. Kwa. |
14 Pentecost |
S. B. XV Pentekote Ee Bwana, tunakusihi: Huruma yako ya daima ilitakase Kanisa lako na kulilinda; na kwa kuwa pasipo Wewe haliwezi kukaa salama, liongozwe sikuzote kwa msaada wa wema wako. Kwa. |
15 Pentecost |
S. B. XVI Pentekote Ee Bwana, tunakusihi: Utujalie neema yako; itutangulie sikuzote na kutufuata, ili kututia moyo wa bidii wa kutenda kazi zilizo njema. Kwa. |
16 Pentecost |
S. B. XVII Pentekote Ee Bwana, hakuna Mungu ila Wewe: Tunakusihi; uwajalie watu wako wayaepuke mambo yote ya kishetani, ili wakufuate Wewe kwa mioyo safi. Kwa. |
17 Pentecost |
Robo Mwaka Jumatano Ee Bwana, tunakusihi, uzisikie dua zetu: Huruma zako zituwie dawa ya udhaifu wetu; ili tulivyojiharibu kwa dhambi zetu, tutengenezwe kwa rehema zako. Kwa. Ijumaa Mwenyezi Mungu, tunakusihi: Uisikie dua yetu; ili tuifulize ibada ya siku hii ya leo, na kukupendeza kwa mwili na kwa roho. Kwa. Jumamosi Mwenyezi Mungu, wa milele, unatuletea afya ya mwili na roho kwa njia ya kujinyima kwetu: Tunakusihi kwa unyenyekevu; utukubali katika kufunga kwetu na kusali kwetu, na kutujalia msaada wako sasa na siku zijazo. Kwa. |
Ember Days |
S. B. XVIII Pentekote Ee Bwana, pasipo msaada wako hatuwezi kukupendeza: Tunakusihi; utuonyeshe uweza wa huruma zako, ili Roho wako Mtakatifu aiongoze mioyo yetu. Kwa Bwana wetu Yesu Kristo Mwana wako; Aishiye na kumiliki pamoja nawe, katika umoja wake Yeye huyo Roho Mtakatifu, Mungu daima milele na milele. Amin. |
18 Pentecost |
S. B. XIX Pentekote Mwenyezi Mungu, mwenye rehema: Utuondolee kwa neema yako mambo yote yanayatupinga; ili tuwe tayari, miili na roho, kuzitimiza kazi zako kwa mioyo iliyotulia. Kwa. |
19 Pentecost |
S. B. XX Pentekote Ee Bwana, tunakusihi: Uwakirimie watu wako wakuaminio samaha na amani; ili watakaswe na machukizo yote, na kukutumikia kwa mioyo isiyoshughulika. Kwa. |
20 Pentecost |
S. B. XXI Pentekote Ee Bwana, tunakusihi: Uulinde ujamaa wako kwa pendo lako la daima; ili uponywe kwa himaya yako katika shida zote, na kulitumikia Jina lako kwa matendo mema. Kwa. |
21 Pentecost |
S. B. XXII Pentekote Ee Mungu, Wewe ndiwe kimbilio letu na nguvu zetu, asili ya utakatifu wote: Uzikubali sala takatifu za Kanisa lako; utujalie tuyapate yote tunayoyaomba kwa imani. Kwa. |
22 Pentecost |
S. B. XXIII Pentekote Ee Bwana, unatuona tumejifungia dhambi kwa udhaifu wetu: Tunakusihi; uyasamehe makosa ya watu wako, ili kwa wema wako tufunguliwe katika vifungo vyetu. Kwa. ¶ Ikiwa S. B. baada ya Pentekote zimezidi, zitumike sala za S. B. baada ya Ufunuo zilizoachwa. Tafuta habari yake katika Kalendari ya Mwaka. Na sala hii ifuatayo itumike sikuzote S. B. Kabla ya Majilio. |
23 Pentecost |
S. B. Kabla ya Majilio Ee Bwana, tunakusihi: Uiamshe mioyo ya watu wako wakuaminio; ili wayatamani mazao ya neema yako, na kuzidi kuuona msaada wako wa Ubaba. Kwa. |
Sunday before Advent |
KUTABARUKU KANISA Sala ya Jioni (ya 1 na ya 2) ANT. ZAB. Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala, Kwa mataifa yote. Sala Ee Mungu, wapenda kila mwaka kutuleta salama kwa Sikukuu ya ukumbusho wa kulitabaruku Kanisa letu [Kuu], ili tuzihudhurie siri zako: Utusikie sisi tulio watu wako; kila mtu atakayeomba baraka katika Kanisa hilo, apate ayatakayo na kuyafurahia. Kwa. Sala ya Asubuhi ANT. ZAB. Bila shaka hapa ni nyumba ya Mungu, Na hili ni lango la mbinguni. Sala ya Adhuhuri SOMO. Nilisikia sauti kubwa kutoka mbinguni ikisema, Tazama, maskani ya Mungu i pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake; naye mwenyewe, Mungu pamoja nao, atakuwa Mungu wao. Sala ya Ukumbusho Ant. Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka hapa ni nyumba ya Mungu, na hili ni lango la mbinguni. |
Dedication of a Church |
Return to the Zanzibar Prayer Book
Web author: Charles Wohlers | U. S. England Scotland Ireland Wales Canada World |