The Book of Common Prayer
United States England Scotland Ireland Wales Canada World

    Njia ya Ibada
The 1662 Book of Common Prayer in Swahili

 

NJIA YA IBADA

Sehemu za kitabu cha Sala ya Asubuhi na Jioni, Litania na Ushirika Utakatifu, zisemwe au kuimbwa na watu, pamoja na sehemu za Katekisimo na Zaburi nyingine na nyimbo.

BOOK OF WORSHIP

Parts of the Book of Common Prayer, the Litany and Holy Communion, to be said or sung by the people, together with parts of the Catechism and some Psalms and hymns.
 


 

NJIA YA IBADA

 

 

Swahili: Book of Worship

 

  

LONDON:

SOCIETY FOR PROMOTING
CHRISTIAN KNOWLEDGE


 

DIBAJI

Kusudi la kitabu hiki ni kutoa kitabu rahisi kwa kutumia Wenyeji katika Sala zao za kanuni. Wengi hawawezi kununua Kitabu cha Sala kizima, na kwa hiyo hawawezi kuabudu vizuri. Kitabu hiki kitawasaidia sana kuabudu na akili zaidi na kusali vizuri.
    "Anitoleae sifa mimi hunitukuza."

INTRODUCTORY NOTE

The purpose of this book is to provide a book at low cost for the use of African congregations at the ordinary services of the Church. Many cannot afford the complete Book of Common Prayer and a Hymn Book. They are therefore not able to take their proper part in worship. This book should help them to a more sincere and intelligent worship.
    "Whoso offereth me praise, glorifieth me".


 

This Book of Common Prayer, published around 1939, was one of the first in Standardized Swahili, as opposed to previous ones in the Central (Mombasa) and Southern (Zanzibar) dialects.

As can be seen from the introduction, it was intended to be a 'low-cost alternative' which Africans could afford. As such it omits many services and the ones it does include are heavily abridged, omitting many of the parts not spoken by the people. The Common Prayer portion of this book, in fact, occupies only about 1/8 of the pages, with another 1/8 for a selection of Psalms; the remaining 3/4 of the book is devoted to a words-only hymnal of mostly familiar English hymns translated into Swahili.

In addition to the BCP portion of the book as HTML (see Table of Contents below), we also have the entire book as PDF graphics, including uncorrected text.

This book appears as 167:2 in David Griffiths' Bibliography of the Book of Common Prayer. The text has been spell-checked, but, as the author knows no Swahili, there still may be errors. Please let us know if you find any.

title page

YALIYOMO

 
INTRODUCTORY NOTE
NJIA YA IBADA
  Order of Worship
LITANIA.
  Litany
USHIRIKA UTAKATIFU
  Holy Communion
MAFUNDISHO YA KANISA YANAYOWAPASA
  WATU WOTE KUYAJUA

  Church Teachings which all People Should Know
    (i. e., the Catechism)

ZABURI NYINGINE ZA DAUD
  Other Psalms of David
NYIMBO.
  Hymns
INDEX

Download the entire book as PDF graphics.


 

 

PAGE
v
1

9

15

 
21

 
24

51

213

NJIA YA IBADA

Mwanzo wa Sala ya Asubuhi na Jioni Mhudumu asome mojawapo ya Aya za Maandiko Matakatifu. Kisha aseme maonyo ya Ibada. Baada ya maonyo, wote wapige magoti, waseme ungamo lifuatalo.
 

Order of Worship
(i. e., Morning & Evening Prayer)

UNGAMO

BABA Mwenyiezi na mwenye rehema; Tumekosa kwa kutokufuata njia zako takatifu. Tumekuwa kama kondoo waliopotea, Tumefuata mno mawazo na tamaa zetu. Tumezihalifu sharia zako takatifu. Tumeyaacha yaliyotupasa kutenda. Tumeyatenda yasiyotupasa kutenda; Wala uzima hatunao. Uturehemu Wewe Bwana, sisi maskini wenye dhambi. Uwaachilie, Mungu, wanaoungama dhambi zao. Uwarudishe wanaotubu; Kwa ahadi zako ulizowaahidia wana Adamu kwa Kristo Yesu Bwana wetu. Na kwa ajili yake, Baba wa rehema, Utujalie tuyatende tangu leo mambo ya kitawa, ya haki, na ya kiasi. Jina lako takatifu litukuke. Amin.

Kasisi tu ndiye awezaye kusema Ghofira au Ondoleo la Dhambi, lakini kila Mhudumu ana ruhusa kusema sala hii:

BWANA, twakusihi, uwakarimie watu wako wakuaminio samaha na amani, watakaswe na machukizo yote, wakutumikie kwa moyo usioshughulika; kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Amin.
 

Confession

WOTE WASEME SALA YA BWANA

BABA yetu, uliye mbinguni, Jina lako liwe takatifu. Ufalme wako uje. Mapenzi yako yatimizwe duniani, Kama yatimizwavyo mbinguni. Utupe leo riziki zetu. Utusamehe makosa yetu, Kama sisi tunavyowasamehe waliotukosa. Usitutie majaribuni; Lakini utuokoe maovuni; Kwani ufalme, na nguvu na utukufu ni wako milele. Amin.

Kisha Mhudumu aseme:

Bwana, ufunue midomo yetu.
Watu. Na vinywa vyetu vitanena sifa zako.
Mhudumu. Mungu, utuokoe kwa haraka.
Watu. Bwana, utusaidie hima.

Watu wakiwa wamesimama, Mhudumu aseme:

    Utukufu una Baba, na Mwana: na Roho Mtakatifu;
    Watu. Ulivyokuwa mwanzo: ulivyo sasa, utakavyokuwa milele. Amin.
    Mhudumu. Msifuni Bwana.
    Watu. Jina la Bwana lisifiwe.

VENITE

NJONI, tumwimbie Bwana: tufanyie shangwe mwamba wa wokofu wetu.
    Tuje mbele zake kwa shukrani: tumfanyie shangwe kwa zaburi.
    Kwani Bwana ni Mungu mkuu: na Mfalme mkuu juu ya miungu wote.
    Mkononi mwake zimo bonde za dunia: hata vilele vya milima ni vyake.
    Bahari ni yake, ndiye aliyeifanya : na mikono yake iliiumba nchi kavu.
    Njoni, tuabudu, tusujudu: tupige magoti mbele za Bwana aliyetuumba.
    Kwani ndiye Mungu wetu: na sisi watu wa malisho yake, na kondoo za mkono wake.
    Ingekuwa heri leo msikie sauti yake! Msifanye migumu mioyo yenu: kama vile Meribah, kama siku ya Massah jangwani;
    Kama vile walivyonijaribu baba zenu: wakanipima, wakayaona matendo yangu.
    Miaka arubaini nalihuzunika nacho kizazi hiki nikasema: watu waliopotoka mioyo hawa, hawakujua njia zangu.
    Nikaapa kwa hasira yangu: wasiingie rahani mwangu.
    Utukufu una Baba, na Mwana: na Roho Mtakatifu;
    Ulivyokuwa mwanzo: ulivyo sasa, utakavyokuwa milele. Amin.

Kisha zifuate Zaburi: karatasi 24.
    Kisha lisomwe Somo la kwanza (katika Agano la Kale).
    Baadaye watu waseme au kuimba wimbo huu wakati wa Sala ya Asubuhi:

 

All say the Lord's Prayer

TE DEUM LAUDAMUS

WEWE, Mungu, twaskusifu: wewe, Bwana, twakukiri.
Wewe Baba wa milele: ulimwengu wote unakuabudu.
    Wewe Malaika zote: nazo Mbingu na Nguvu zote,
    Nao Makerubi na Maserafi: wakuimbia hawakomi,
    Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu: Mungu Bwana wa majeshi.
    Mbingu na nchi zimejaa: enzi ya utukufu wako.
    Wakusifu wewe; jamii tukufu ya Mitume.
    Wakusifu wewe: shirika lenye sifa la Manabii.
    Wakusifu wewe: jeshi la Mashahidi waliovaa mavazi meupe.
    Kanisa takatifu katika nchi zote: lakukiri wewe.
    Baba mwenye enzi: isiyo na kiasi.
    Mwana wako pekee: wa kweli, wa kuabudiwa.
    Na Mfariji: Roho Mtakatifu.
    Wewe Kristo: ndiwe Mfalme wa utukufu.
    Wewe Mwana wa milele: wa Baba.
    Wewe ulipotaka kujifanya mtu, ili umwokoe Mwana Adamu: hukuchukizwa na tumbo lake Bikira.
    Wewe ulipoushinda uchungu wa mauti: uliwafunulia waaminio Ufalme wa Mbingu.
    Wewe unakaa mkono wa kuume wa Mungu: katika utukufu wake Baba.
    Tunasadiki : utakuja kuwa Mwamuzi.
    Kwa hiyo, twakuomba uwasaidie watumwa wako: uliowakomboa kwa damu yako ya thamani.
    Uwajalie pamoja na Watakatifu wako: utukufu wa milele.
    Uwaokoe watu wako, Bwana: uubarikie urithi wako.
    Uwatawale: uwainue hata makao ya milele.
    Sisi kila siku: twakutukuza.
    Twalisifu Jina lako: zamani hizi na za milele.
    Ukubali, Bwana, kutulinda leo: tusipate dhambi.
    Uturehemu, Bwana: uturehemu sisi.
    Utuonee huruma, Bwana: kwani sisi twakutumaini wewe.
    Nimekutumaini wewe, Bwana: nisipotee milele.

Wakati wa jioni waseme au kuimba Magnificat — Luka i. 46, ukurasa 7.
    Kisha lisomwe Somo la Pili (katika Agano Jipya).
    Baadaye waimbe wimbo huu ufuatao :

JUBILATE. Zab. c.

MFANYIENI shangwe Bwana, dunia yote: mtumikieni Bwana kwa furaha, njoni mbele zake kwa kuimba.
    Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu: ndiye aliyetuumba, na sisi tu watu wake, na kondoo za malisho yake.
    Ingieni milangoni mwake kwa kushukuru, nyuani mwake kwa kusifu: mshukuruni, lihimidini Jina lake.
    Kwani Bwana ndiye mwema, rehema zake za milele: na uaminifu wake vizazi na vizazi.
    Utukufu una Baba, na Mwana: na Roho Mtakatifu;
    Ulivyokuwa mwanzo, ulivyo sasa: utakavyokuwa milele. Amin.

Wakati wa jioni waseme au kuimba Nune Dimittis — Luka ii. 29, ukurasa 8.

Watu waiseme Imani ya Mitume.
 

 

NAMWAMINI Mungu Baba Mwenyiezi, Muumba mbingu na nchi;
    Na Yesu Kristo Mwana wake pekee Bwana wetu, Aliyechukuliwa mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu, Akazaliwa na Bikira Mariamu, Akateswa zamani za Pontio Pilato, Akasulibiwa, Akafa, Akazikwa, Akashuka pahali pa wafu; Siku ya tatu akafufuka, Akapaa mbinguni, Anaketi mkono wa kuume wa Mungu Baba Mwenyiezi ; Kutoka huko atakuja kuwahukumu watu wahai na wafu.
    Namwamini Roho Mtakatifu; Kanisa Takatifu, Katholiko; Ushirika wa Watakatifu; Ondoleo la dhambi; Kiyama ya mwili, Na uzima wa milele. Amin.

Kisha Mhudumu aseme:

Bwana akae nanyi.
Watu. Akae na roho yako.
Mhudumu. Tuombe.

Wote wapige magoti.

Bwana, uturehemu.
Watu. Kristo, uturehemu.
Mhudumu. Bwana, uturehemu.

Wote waseme pamoja:
 

Apostles' Creed

BABA yetu, uliye mbinguni, Jina lako liwe takatifu. Ufalme wako uje. Mapenzi yako yatimizwe duniani, Kama yatimizwavyo mbinguni. Utupe leo riziki zetu. Utusamehe makosa yetu, Kama sisi tunavyowasamehe waliotukosa. Usitutie majaribuni; Lakini utuokoe maovuni. Amin.

Kisha Mhudumu asimame, aseme:

    Bwana, utuonyeshe rehema yako.
    Watu. Utupe wokofu wako.
    Mhudumu. Bwana, umwokoe Mfalme.
    Watu. Utusikie kwa rehema tukuombapo.
    Mhudumu. Wahudumu wako uwavike haki.
    Watu. Uwafurahishe wateule wako.
    Mhudumu. Uwaokoe watu wako, Bwana.
    Watu. Uubariki urithi wako.
    Mhudumu. Utupe amani, Bwana, siku zetu.
    Watu. Kwani hatuna mwingine wa kutupigania, ila wewe Mungu wetu.
    Mhudumu. Mungu, utuumbie ndani mioyo safi.
    Watu. Wala Roho yako Mtakatifu usituondolee.

Kisha zifuate Sala ya Siku, Sala ya Amani na Sala ya neema, na maombi mengine.
    Nyumbani na vijijini msimopatikana kitabu cha sala semeni sala ifuatayo badala ya Sala ya siku:

EE Baba Mweyiezi, ndiwe uliyetuumba na kutukomboa kwa damu ya Mwana wako Mpenzi, ili tutangaze sifa zako. Utusaidie tukushuhudie kwa mawazo na maneno na matendo, ili tukutukuze na kuonyesha imani yetu kwa wengine, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Amin.

Maombi mengine.
    Wakati wa Sala za Jioni badala ya Sala ya Amani na Sala ya Neema, semeni Sala ya kuondoa Hofu na Sala ya Kuomba Msaada, na maombi mengine.

SALA YA MWISHO.   II Wakor. xiii.

NEEMA ya Bwana wetu Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu, ukae nasi sote sasa na milele. Amin.
 


 

Lord's Prayer

KUSHUKURU

Kushukuru kwa watu wengi pamoja.

MWENYJEZI Mungu, Baba wa rehema zote,sisi watumwa wako wanyonge twakushukuru kwa unyenyekevu na kwa moyo kwa wema wako wote na pendo lako kwetu sisi, na kwa watu wote. Twakutukuza kwa ajili ya kuumbwa kwetu, na kuhifadhika kwetu, na kwa baraka zote za maisha haya; lakini zaidi ya yote, kwa pendo lako lisilopitika la kukombolewa ulimwengu na Bwana wetu Yesu Kristo; kwa njia za neema, na tumaini la utukufu. Utupe, twakusihi, fahamu itupasayo ya rehema zako zote, mioyo yetu ikushukuru pasipo hila, nasi tuonyeshe sifa zako, si kwa midomo yetu tu, ila na kwa maisha yetu: tukijitia kabisa katika utumwa wako, tukienda mbele yako katika utakatifu na haki siku zetu zote; kwa Yesu Kristo Bwana wetu, kwa huyo pamoja na wewe na Roho Mtakatifu iwe heshima yote na utukufu, maisha na milele. Amin.

Wakati wa Sala za Jioni watu waimbe uimbo huu baada ya Somo la Kwanza.

MAGNIFICAT. Luka i.

MOYO wangu wamwadhimisha Bwana: roho yangu yamfurahia Mungu, Mwokozi wangu.
    Kwani ameutazama: unyonge wa mjakazi wake.
    Kwani hakika, tokea leo: vizazi vyote wataniita heri.
    Kwani aliye hodari amenitendea makuu: na Jina lake ni takatifu.
    Na rehema zake vizazi hata vizazi: kwao wanaomcha.
    Ametenda nguvu kwa mkono wake: amewatawanya walio na kiburi katika mioyo yao.
    Amewashusha wakuu katika viti: amewakweza wanyonge.
    Wenye njaa amewashibisha mema: wenye mali amewaondoa mikono mitupu.
    Kwa kukumbuka rehema amemsaidia Israeli mtumishi wake: kwa jinsi alivyowaambia baba zetu, Ibrahimu na uzao wake, hata milele.
    Utukufu una Baba, na Mwana: na Roho Mtakatifu;
    Ulivyokuwa mwanzo; ulivyo sasa, utukavyokuwa milele. Amin.

Tena waimbe wimbo huu baada ya Somo la Pili.

NUNC DIMITTIS. Luka ii. 29.

SASA wamruhusu, Bwana, mtumwa wako kwa amani: kama ulivyosema.
    Kwani macho yangu: yameuona wokofu wako.
    Ulioweka tayari: machoni pa watu wote.
    Nuru ya kuwaangaza mataifa; na kuwa utukufu wa watu wako Israeli.
    Utukufu una Baba, na Mwana; na Roho Mtakatifu;
    Ulivyokuwa mwanzo: ulivyo sasa, utakavyokuwa milele. Amin.
 


 

Thanksgiving

LITANIA

MUNGU Baba, wa mbinguni: uturehemu maskini wenye dhambi.
    Mungu Baba, wa mbinguni: uturehemu maskini wenye dhambi.
   
Mungu Mwana, Mkomboa ulimwengu: uturehemu maskini wenye dhambi.
    Mungu Mwana, Mkomboa ulimwengu: uturehemu maskini wenye dhambi.
    Mungu Roho Mtakatifu, utokae katika Baba na Mwana; uturehemu maskini wenye dhambi.
    Mungu Roho Mtakatifu, utokae katika Baba na Mwana: uturehemu maskini wenye dhambi.
    Utatu Mtakatifu, Mhimidiwa, Mtukufu, Nafsi tatu na Mungu mmoja; uturehemu maskini wenye dhambi.
    Utatu Mtakatifu, Mhimidiwa, Mtukufu, Nafsi tatu na Mungu mmoja: uturehemu maskini wenye dhambi.
    Usiyakumbuke, Bwana, makosa yetu; wala makosa ya baba zetu; wala usitupatilize kwa dhambi zetu; utuachilie, Bwana mwema, waachilie watu wako, uliowakomboa kwa damu yako ya thamani, wala usituonee hasira milele,
    Utuachilie, Bwana mwema.
   
Na mabaya yote na madhara; na dhambi, na hila na jeuri za Shetani; na ghadhabu yako na laana la milele,
    Utuokoe, Bwana mwema.
   
Na upofu wote wa moyo; na kiburi, majisifu, na unafiki; na husuda, chuki, na uovu, na kutopendana kwote,
    Utuokoe, Bwana mwema.
    Na uasharati na dhambi zingine zote za kufisha; na madanganya yote ya dunia, ya mwili, na ya Shetani,
    Utuokoe, Bwana mwema.
    Na umeme na tufani; na tauni, maradhi, nzige na njaa; na vita na uaji, na na mauti ya ghafula,
    Utuokoe, Bwana mwema.
    Na maafikano ya fitina ya siri, na kuasi; na elimu ya uwongo, uzushi, na kufarakana kwa dini; na kuwa na moyo mgumu, na kulidharau Neno na amri zako.
    Utuokoe, Bwana mwema.
    Kwa siri ya Kufanyika mwili kwako kutakatifu; kwa Kuzaliwa kwako kutakatifu, na Kutahiriwa; kwa Kubatizwa kwako, Kutunga, na Kujaribiwa,
    Utuokoe, Bwana mwema.
    Kwa huzuni yako, na Hari ya damu; kwa Msalaba wako na Kuteswa; kwa Kufa kwako kwa thamani, na Kuzikwa; kwa Kufufuka kwako kutukufu na Kupaa; na kwa kuja kwake Roho Mtakatifu,
    Utuokoe, Bwana mwema.
    Wakati wote wa kutaabika kwetu; wakati wote wa kufanikiwa; saa ya kufa, na siku ya kuhukumiwa,
    Utuokoe, Bwana mwema.
   
Sisi wenye dhambi twakusihi utusikie, Bwana Mungu: upende kulitawala na kuliongoza Kanisa lako takatifu Katholiko, lishike njia njema;
    Twakusihi utusikie, Bwana mwema.
    [Upende kumbariki mfalme wa inchi hii, na kuuongoa moyo wake aikubali kweli yako;
    Twakusihi utusikie, Bwana mwema.]
    Upende kuwaangaza Maaskofu wote, Makasisi, na Mashemasi, wajue na kufahamu kwa kweli Neno lako; wakalieneze kwa mafundisho na kwa mwenendo wao;
    Twakusihi utusikie, Bwana mwema.
    Upende kuwavika watu wakuu wa Serkali na wazee wote neema, hekima, na akili;
    Twakusihi utusikie, Bwana mwema.
    Upende kuwabariki na kuwalinda makadhi, [maliwali, na maakida,] na watu wote wenye mamlaka; ukiwajalia neema ya kutenda haki, na kuihakikia kweli ;
    Twakusihi utusikie, Bwana mwema.
    Upende kuwabariki na kuwalinda watu wako wote;
    Twakusihi utusikie, Bwana mwema.
    Upende kuwapa mataifa yote umoja, amani, na urafiki;
    Twakusihi utusikie, Bwana mwema.
   
Upende kutujalia moyo wa kukupenda na kukucha, na kufuata kwa bidii amri zako;
    Twakusihi utusikie, Bwana mwema.
   
Upende kuwazidishia neema watu wako wote, illi kwa unyenyekevu walisikie Neno lako, walikubali kwa moyo safi, na kuzaa matunda ya Roho;
    Twakusihi utusikie, Bwana mwema.
   
Upende kuwaleta katika njia ya kweli Washenzi na Waislamu na wote waliopotea na kudanganyika;
    Twakusihi utusikie, Bwana mwema.
   
Upende kuwaimarisha wasimamao; kuwafariji na kuwasaidia walio na moyo dhaifu; kuwainua waangukao ; na hatima kumkanyaga Shetani chini ya miguu yetu;
    Twakusihi utusikie, Bwana mwema.
    Upende kuwatunza, kuwasaidia, na kuwafariji wote walio katika hatari, shidda, na taabu;
    Twakusihi utusikie, Bwana mwema.
    Upende kuwahifadhi wote wanaosafiri katika inchi au baharini, wanawake wote walio na utungu wa kuzaa, wagonjwa wote, na watoto wote wachanga, na kuwahurumia wafungwa wote;
    Twakusihi utusikie, Bwana mwema.
    Upende kuwalinda na kuwaruzuku watoto wote wasio na baba, wanawake waliofiwa na waume zao, na wote wasio na msaada, na wanaoonewa;
    Twakusihi utusikie, Bwana mwema.
   
Upende kuwarehemu watu wote;
    Twakusihi utusikie, Bwana mwema.
    Upende kuwasamehe adui zetu, nao watufukuzao na watusingiziao, uwageuze mioyo;
    Twakusihi utusikie, Bwana mwema.
    Upende kutupa na kutuhifadhia mazao ya inchi kwa jinsi yake, tupate kuyatumia wakati wake;
    Twakusihi utusikie, Bwana mwema.
    Upende kutujalia tutubu kwa kweli; kutusamehe dhambi zetu zote, za ulegevu na ujinga, na utuvike neema ya Roho yako Mtakatifu, tutengeneze mwenendo wetu kwa Neno lako takatifu ;
    Twakusihi utusikie, Bwana mwema.
   
Mwana wa Mungu: twakusihi, utusikie.
    Mwana wa Mungu: twakusihi, utusikie.
   
Mwana Kondoo wa Mungu: uzichukuae dhambi za ulimwengu;
    Utupe amani yako.
    Mwana Kondoo wa Mungu: uzichukuae dhambi za ulimwengu;
    Uturehemu sisi.

Kristo, utusikie.
    Kristo, utusikie.
Bwana, uturehemu.
    Bwana, uturehemu.
Kristo, uturehemu.
    Kristo, uturehemu.
Bwana, uturehemu.
    Bwana, uturehemu.

Kiisha Mhudumu na watu pamoja nae waseme Sala ya Bwana.
 

Litany

BABA yetu, uliye mbinguni, Jina lako liwe takatifu. Ufalme wako uje. Mapenzi yako yatimizwe duniani, Kama yatimizwavyo mbinguni. Utupe leo riziki zetu. Utusamehe makosa yetu, Kama sisi tunavyowasamehe waliotukosa. Usitutie majaribuni; Lakini utuokoe maovuni. Amin.
    Mhudumu. Bwana, usitutendee kwa hesabu ya dhambi zetu.
    Jibu. Wala usitulipe kwa kadiri ya maovu yetu.

Tuombe

MUNGU, Baba wa rehema, usiyedharau kilio chao waliopondeka moyo, wala haja zao walio na huzuni; ukubali kwa rehema sala zetu tukuombazo katika taabu na misiba yetu yote itulemeapo; utusikie kwa neema, ili mabaya hayo, tutendewayo kwa hila na werevu wa Shetani au wa wana Adamu, yakome; na kwa tunza la wema wako yaondolewe; ili sisi watumwa wako, tusipozuiwa na mafukuzo, tukushukuru daima katika Kanisa lako takatifu; kwa Yesu Kristo Bwana wetu.
    Bwana, uondoke, utusaidie, utuokoe kwa ajili ya Jina lako.
    Mungu, tumesikia kwa masikio yetu, na baba zetu wametuambia mambo makuu, uliyoyatenda siku zao, na zamani za kale kabla yao.
    Bwana, uondoke, utusaidie, utuokoe kwa ajili ya heshima yako.
    Utukufu una Baba, na Mwana: na Roho Mtakatifu;
    Jibu. Ulivyokuwa mwanzo: ulivyo sasa, utakavyokuwa milele. Amin.
    Na adui zetu utulinde, Kristo.
        Uyaangalie kwa wema mateso yetu.
    Utazame kwa huruma huzuni ya mioyo yetu.
        Usamehe kwa rehema dhambi za watu wako.
    Kwa upendeleo na rehema usikie sala zetu.
        Mwana wa Daud, uturehemu.
    Sasa na daima upende kutusikia, Kristo.
        Utusikie kwa wema, Kristo; utusikie kwa wema, Bwana Kristo.
    Mhudumu. Bwana, utuonyeshe rehema yako;
        Jibu. Kama sisi tunavyokuamini wewe.

Tuombe

BABA, twakusihi kwa unyenyekevu, uziangalie kwa rehema dhaifu zetu; na kwa ajili ya kutukuka Jina lako, utuepushie mbali mabaya hayo yote, tuliyoyastahili kwa haki; utujalie, katika taabu zote, tuamini na kutumainia kabisa rehema zako, na tukutumikie siku zote katika utakatifu na mwenendo safi, kwa heshima na utukufo wako; kwa Msuluhisha na Mneni wetu mmoja, Yesu Kristo Bwana wetu. Amin.
 

Lord's Prayer

Sala ya Krusostomo Mt.

MWENYIEZI Mungu, uliyetujalia neema wakati huu kushirikiana kutaka haja zetu mbele yako; umeahidi, ya kwamba watu wawili au watatu wakikutanika kwa Jina lako, utawapa haja zao; Fikiliza sasa, Bwana, haja na maombo ya watumwa wako kwa jinsi itakavyotufaa; ukitujalia tuijue kweli yako katika ulimwengu huu, na katika ulimwengu ujao uzima wa milele. Amin.

2 Wakor. xiii.

NEEMA ya Bwana wetu Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu, ukae nasi sote maisha na milele. Amin.
 


 

Prayer of St. Chysostom

USHIRIKA UTAKATIFU

Kasisi na Askofu tu ndio wawezao kufanya Ibada ya Ushirika Utakatifu.
    Kasisi ataanza Ibada ya Ushirika Utakatifu kwa kusema Sala ya Bwana peke yake, pamoja na Sala ya usafi wa roho. Kisha Kasisi atasema Amri Kumi za Mungu. Baada ya kila amri, watu wajibu:
    Bwana, uturehemu, tuelekeze mioyo tuishike amri hii.
 

Holy Communion

AMRI KUMI

    1. Usiwe na miungu wengine ila mimi.
    2. Usijifanyizie sanamu ya kuchora, wala mfano wa kitu cho chote kilichoko juu mbinguni, wala chini duniani, wala majini chini ya nchi. Usivisujudu, usiviabudu : kwani mimi Bwana Mungu wako Mungu mwivu, nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne wanichukiao; nami nawarehemu elfu elfu wanipendao, na kushika amri zangu.
    3. Usilitaje bure Jina la Bwana Mungu wako, kwani Bwana hatamtoa hatiani alitajaye Jina lake bure.
    4. Ikumbuke sikuya Sabato, itakase. Siku sita fanya kazi, tenda mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana Mungu wako; Usitende kazi yo yote, wewe, wala mwanao, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala nyama zako, wala mgeni aliomo nyumbani mwako. Kwani kwa siku sita Bwana alifanya mbingu na nchi, bahari na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba: kwa sababu hii Bwana akaibariki siku ya saba akaitakasa.
    5. Waheshimu baba yako, na mama yako; siku zako zipate kuzidi katika nchi upewayo na Bwana Mungu wako.
    6. Usiue.
    7. Usizini.
    8. Usiibe.
    9. Usimshuhude jirani yako uwongo.
    10. Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako, wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.

Jibu la mwisho:

Bwana, uturehemu, uziandike, twakusihi, amri hizi zote mioyoni mwetu.

Kisha ifuate Sala ya Mfalme na ya siku.
    Ndipo watu wakae wasikilize Waraka.
    Baada ya Waraka hufuata Injili.
    Wakati wa kutangaza Injili, watu wasimame na kusema:

    Utukufu uwe kwako, Ee Mungu.

Ikiisha Injili, watu waseme:

Shukrani iwe kwako, Ee Mungu, kwa Injili yako hii takatifu.

Ndipo wote waseme au kuimba Imani ya Nike.
 

Ten Commandments

IMANI YA NIKE

NAMWAMINI Mungu mmoja Baba Mwenyiezi, Muumba mbingu na nchi, Na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana:
    Na Bwana mmoja Yesu Kristo, Mwana pekee wa Mungu, Amezaliwa na Baba kabla ya zamani zote, Yu Mungu anatoka katika Mungu, Yu Nuru anatoka katika Nuru, Yu Mungu kweli anatoka katika Mungu kweli, Amezaliwa, hakuumbwa, Mwenye asili moja na Baba, Kwa yeye huyu vitu vyote vyaliumbwa: Aliyeshuka kutoka mbinguni kwa ajili yetu wana Adamu, na kwa wokofu wetu, Akatwaa mwili kwa uweza wa Roho Mtakatifu katika Bikira Mariamu, Akawa mwana Adamu, Akasulibiwa kwa ajili yetu, zamani za Pontio Pilato. Aliteswa akazikwa, Siku ya tatu akafufuka kama yanenavyo Maandiko Matakatifu, Akapaa mbinguni, Anaketi mkono wa kuume wa Baba. Naye atakuja tena kwa utukufu kuwahukumu watu wahai na wafu. Na milki yake haina mwisho.
    Namwamini Roho Mtakatifu, Bwana, Mtoa uzima, Atokaye katika Baba na Mwana, Anayeabudiwa na kutukuzwa pamoja na Baba na Mwana, Aliyenena kwa vinywa vya Manabii. Naamini Kanisa moja, Takatifu, Katholiko, na Apostoliko. Nakiri Ubatizo Umoja wa kuondolea dhambi. Natazamia Kiyama ya wafu, na uzima wa ulimwengu ujao. Amin.
 

Nicene Creed

MATANGAZO
HOTUBA
SADAKA

Kasisi aweke Mkate na Divai mezani, kisha aseme:

Tuliombee Kanisa la Kristo pia lifanyalo vita hapa duniani.

Kuwakaribisha Washiriki.

Waalikwe wote walio tayari, wenye toba na upendano na maisha ya kumpendeza Mungu, wakipokee chakula cha Bwana.
 

Announcements
Sermon
Offertory

UNGAMO

MWENYIEZI Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Muumba vitu vyote, Mhukumu watu wote, Twaungama na kujutia dhambi na uovu wetu, Tuliotenda kwa ubaya mno siku hizi zote. Tumewaza, tumenena, tumetenda mambo ya kukuchukiza wewe, Mwenyiezi Mungu. Hata itakuwia haki kutukasirikia na kutughadhabikia. Tumejuta kwa majuto makuu. Tumeyasikitikia sana haya makosa yetu. Kuyakumbuka tu kunatuhuzunisha; Ni kama mzigo usiochukulika. Uturehemu, Uturehemu, Baba wa rehema; Kwa ajili ya Mwana wako Bwana wetu Yesu Kristo, Utusamehe yote yaliyopita; Utujalie tangu leo tukutumikie, Tukupende katika upya wa maisha, Kwa heshima na utukufu wa Jina lako; kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Amin.
 

Confession

Kasisi (au Askofu akiwapa) aseme GHOFIRA.
MANENO YA FARAJA.

Kisha Kasisi aseme:

Inueni mioyo.

Watu. Twaiinua kwa Bwana.
Kasisi. Na tumshukuru Bwana Mungu wetu.
Watu. Ina haki, tena ni wajib.

Kisha Kasisi aikabili Meza ya Bwana, aseme:

NDIO wajib wetu, ina haki, tena ya faradhi kwetu, kila wakati na kila mahali, tukushukuru Bwana, Baba Mtakatifu, Mungu Mwenyiezi wa milele. Kwa hiyo sisi nasi, pamoja na Malaika na Malaika wakuu, na jeshi la mbinguni lote pia, twakutukuza na kuliadhimisha Jina lako tukufu; tukikusifu daima tukisema,

Wote Waseme

MTAKATIFU, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu wa Sabaoth, mbingu na nchi zimejaa utukufu wako: Utukufu u kwako, Bwana uliye juu. Amin.
 

Absolution
Comfortable Words

Kasisi aseme SALA YA UNYONGE

HATUTHUBUTU kuikaribia Meza yako, Bwana mwenye rehema, tukiitumainia haki yetu sisi, ila rehema zako nyingi zilizo kuu. Hatustahili hata kuokota makombo chini ya Meza yako. Wewe ndiwe Bwana yeye yule, sifa zako ni kuwa na rehema siku zote: Basi utujalie, Bwana mwema, tule nyama ya Mwana wako mpendwa Yesu Kristo, na kunywa damu yake, kwa jinsi miili yetu yenye dhambi isafike kwa mwili wake, na roho zetu ziosheke kwa damu yake ya thamani, tukae daima ndani yake, na yeye ndani yetu. Amin.
 

Prayer of Humble Access

SALA YA KUFANYA WAKF MKATE NA DIVAI

Kasisi aseme peke yake.

MWENYIEZI Mungu, Baba yetu wa mbinguni, kwa wema na huruma zako' ulitupa Mwana wako pekee Yesu Kristo afe msalabani kwa ukombozi wetu nae alitoa Msalabani sadaka ya nafsi yake mara moja tu, iwe dhabihu, na sadaka, na kafara, timilifu, kamili, ya kutosha, kwa dhambi za ulimwengu wote: alituamuru, na katika Injili yake takatifu alituusia tufulize daima kumbukumbu la kufa kwake kwa thamani, hata atakaporudi; Utusikie, Baba wa rehema, twakuomba kwa unyenyekevu: na kwa kupokea viumbe hivi vyako, Mkate na Divai, kwa agizo takatifu la Mwana wako Yesu Kristo Mwokozi wetu, tukikumbuka kufa na kuteswa kwake, utujalie tuushiriki Mwili na Damu yake mbarikiwa: * Yeye usiku ule ule aliotolewa alitwaa Mkate; na akiisha kushukuru † akaumega, akawapa wanafunzi wake, akisema, Twaeni, mle, ‡ Huu ndio Mwili wangu uliotolewa kwa ajili yenu: Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Na vivi hivi baada ya kula § akatwaa Kikombe; na akiisha kushukuru, akawapa, akisema, Nyweeni nyote hiki; kwani || hii ndiyo Damu yangu ya Agano Jipya, imwagikayo kwa ajili yenu, na kwa watu wengi, kwa ondoleo la dhambi: Fanyeni hii, kila mtakapokunywa, kwa ukumbusho wangu. Amin.
 

Prayer of Consecration

* Hapa Kasisi atwae sahani mikononi mwake.
† Hapa amege Mkate.
‡ Hapa aweke mkono wake juu ya kila sahani.
§ Hapa atwae kikombe mkononi mwake.
|| Hapa aweke mkono wake juu ya kila chombo chenye Divai ya kufanyika Ukufu.


Kwanza Kasisi apokee Ushirika mwenyewe, kisha Maaskofu na Makasisi na Mashemasi, kisha na watu.

Akimshirikisha mtu Mkate aseme:

MWILI wa Bwana wetu Yesu Kristo, uliotolewa kwa ajili yako, ukulinde mwili na roho hata uzima wa milele. Pokea, ule huu, ukikumbuka kuwa Kristo alikufa kwa ajili yako, na wewe umle yeye moyoni kwa imani na shukrani.

Akimshirikisha mtu Kikombe, aseme :

DAMU ya Bwana wetu Yesu Kristo, iliyomwagika kwa ajili yako, ikulinde mwili na roho hata uzima wa milele. Unywe hii ukikumbuka kuwa Damu yake Kristo ilimwagika kwa ajili yako, ushukuru.
 

 

 

Words of Administration

Wote waseme SALA YA BWANA.
Kasisi aseme Sala ya Kumshukuru Mungu.

Wote waseme au kuimba.
 

All say the Lord's Prayer

UTUKUFU una Mungu juu, katika nchi amani, kwa watu nia njema. Twakusifu, twakuhimidi, twakuabudu, twakutukuza, twakushukuru, kwa ajili ya utukufu wako mkuu, Bwana Mungu, Mfalme wa mbinguni, Mungu Baba Mwenyiezi.
    Bwana, Mwana pekee, Yesu Kristo; Bwana Mungu, Mwana Kondoo wa Mungu, Mwana wa Baba, uchukuae dhambi za ulimwengu, uturehemu. Uchukuae dhambi za ulimwengu, ukubali kuomba kwetu. Uketiye mkono wa kuume wa Mungu Baba, uturehemu.
    Kwani ndiwe uliye peke yako Mtakatifu; ndiwe peke yako Bwana; ndiwe peke yako uliye juu, Yesu Kristo, pamoja na Roho Mtakatifu, katika utukufu wake Mungu Baba. Amin.
 

Gloria

BARAKA


Blessing

MAFUNDISHO YA KANISA YANAYOWAPASA
WATU WOTE KUYAJUA

SEHEMU ZA KATEKISIMO

AHADI TATU ZA UBATIZO

LA kwanza, kwamba nitamkataa Shetani na kazi zake zote, mapendezo na mambo yasiyofaa ya dunia hii mbaya, na tamaa mbaya zote za mwili. La pili, kwamba nitaziamini sharti zote za Imani ya Kikristo. Na la tatu, kwamba nitayashika mapenzi na amri takatifu za Mungu, na kuzifuata siku zote za maisha yangu.
 

Church Teachings Which All People Should Know

 
Part of the Catechism

Three Promises of Baptism

MAFUNDISHO YA IMANI

KWANZA, nafundishwa kumwamini Mungu Baba, aliyeniumba mimi, na ulimwengu wote.
    La pili, kumwamini Mungu Mwana, aliyenikomboa mimi, na wana Adamu wote.
    La tatu, kumwamini Mungu Roho Mtakatifu, anitakasae mimi, na watu wateule wa Mungu wote.
 

Teaching the Faith

MAFUNDISHO YA AMRI KUMI

NAFUNDISHWA mambo mawili: yanipasayo kwa Mungu, na yanipasayo kwa Jirani yangu.

    Swali. Imekupasaje kwa Mungu?
    Jibu. Imenipasa kwa Mungu, kumwamini, kumcha, na kumpenda, kwa moyo wangu wote, kwa akili zangu zote, kwa roho yangu yote, na kwa nguvu zangu zote; kumwabudu, kumshukuru, kumtumainia kabisa, kumwomba, kuliheshimu Jina lake takatifu na Neno lake, na kumtumikia vema siku zote za maisha yangu.

    Swali. Imekupasaje kwa Jirani yako?
    Jibu. Imenipasa kwa Jirani yangu, kumpenda kama nafsi yangu, na kuwatendea watu wote, kama nitakavyo wao wanitendee mimi: Kuwapenda, kuwaheshimu, kuwasaidia baba na mama yangu: Kumheshimu na kumtii Mfalme, na wakuu wote walio chini yake: Kujitiisha kwa wakubwa wangu, waalimu wangu, mapadri na bwana zangu: Kunyenyekea mbele zao wote walio wakubwa kuliko mimi: Kujiangalia nisimdhuru mtu kwa neno wala kwa tendo: Kuwa adili na mwenye haki katika shughuli zangu zote: Kutokuwa na kinyongo wala machukio moyoni mwangu: Kuizuia mikono yangu isiibe kitu cho chote, ulimi wangu usitukane, wala usiseme uwongo, wala usisingizie: Kujiangalia mwili wangu niwe na kiasi, nisiwe mlevi, wala asharati: Nisitamani wala kutaka mali ya watu; lakini kujifunza na kufanya kwa bidii kazi ya kunipa tia riziki zangu, na kutenda yanipasayo katika hali, Mungu atakayopenda kuniitia.
 

Teaching the Ten Commandments

MAFUNDISHO YA SAKRAMENTI

    Swali. Kuna Sakramenti ngapi alizoamuru Kristo katika Kanisa lake?
    Jibu. Mbili tu, zilizo faradhi kwa wokofu wa watu wote, nazo ni Ubatizo, na Chakula cha Bwana.
    Swali. Neno hili Sakramenti maana yake nini?
    Jibu. Sakramenti ni dalili ya nje, na inayoonekana kwa macho, ya neema ya ndani na ya rohoni tunayopewa, imeamriwa na Kristo mwenyewe, kuwa njia ya kupokelea neema hiyo, na kuwa arabuni ya kutuyakinisha.
    Swali. Kuna sehemu ngapi katika Sakramenti?
    Jibu. Mbili; dalili ya nje na inayoonekana, na neema ya ndani na ya rohoni.
    Swali. Dalili ya nje na inayoonekana kwa macho katika Ubatizo ni nini?
    Jibu. Ni maji; mtu abatizwayo kwayo Kwa Jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.
    Swali. Neema ya ndani na ya rohoni ni nini?
    Jibu. Kufa kwa mambo ya dhambi, na kuzaliwa mara ya pili katika haki; Kwani tukiwa kwa asili mmezaliwa dhambini, na watoto wa ghadhabu, kwa Ubatizo tumefanyika watoto wa neema.
    Swali. Watu watakaobatizwa wamepasiwa nini?
    Jibu. Toba, ili waache dhambi; na Imani, ili waziamini sana ahadi za Mungu walizopewa katika Sakramenti hii.
    Swali. Kwani, basi, hubatizwa watoto wachanga, nao wakiwa hawawezi kutenda haya kwa kuwa wadogo?
    Jibu. Kwa sababu wanaahidi mambo haya yote mawili kwa vinywa vya Wadhamini wao; na wakipata kuwa watu wazima imewapasa wenyewe waifikilize ahadi hiyo.
    Swali. Kwa kusudi gani Sakramenti ya Chakula cha Bwana imeamriwa?
    Jibu. Kuwa kumbukumbu la siku zote la dhabihu ya kufa kwake Kristo, na la mambo mema tunayopokea kwa kumbukumbu hilo.
    Swali. Nini sehemu ya nje au dalili ya nje katika Chakula cha Bwana?
    Jibu. Mkate na Divai, alivyoamuru Bwana vipokewe.
    Swali. Nini sehemu ya ndani, au kitu kinachoashiriwa?
    Jibu. Mwili na Damu ya Kristo zinazotwaliwa na kupokewa kwa kweli na pasipo shaka na waamini katika Chakula cha Bwana.
    Swali. Mambo gani mema tupatayo kwa Mwili na Damu ya Kristo?
    Jibu. Kwa Mwili na Damu ya Kristo twapata nguvu ya kuburudishwa roho zetu, kama vile miili yetu inavyopata nguva na kuburudishwa kwa mkate na divai.
    Swali. Wale wajiao Chakula cha Bwana wamepasiwa nini?
    Jibu. Kujihoji, kama kweli wametubia dhambi zao za zamani, na kukusudia sana kuishi maisha mapya; na kama wanaziamini sana rehema za Mungu zilizo katika Kristo, na kukumbuka kwa shukrani kufa kwake; na kama wana upendano na watu wote.

Teaching the Sacraments

 

Web author: Charles Wohlers U. S. EnglandScotlandIrelandWalesCanadaWorld