The Book of Common Prayer
United States England Scotland Ireland Wales Canada World

    Chuo cha Sala ya Umoja (1662)
The 1662 Book of Common Prayer in Swahili

 

SALA NA SHUKRANI
za nyakati za haja mbalimbali

Hutumiwa kabla ya Sala mbili za mwisho katika Litania, au katika Sala za Asubuhi na Jioni.

Sala

YA KUOMBEA MVUA

EWE Mwenyezi Mungu, Babaetu wa mbinguni, wewe kwa Mwanayo Yesu Kristo umewapa ahadi watu wote ambao wautafuta ufalme wako, na haki yake, ya wewe kuwapa hao vitu vyote vipasavyo kuwa riziki za miili yao; twakuomba sana, utuletee hivi sasa katika wakati wa uhitaji wetu, mvua na manyonyota mema, kadiri ya kutupa kuyapokea mazao ya nchi, kwa utuzo wetu na heshima yako; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

Prayers and Thanksgivings

 

 

Prayers

For Rain

YA KUOMBEA KIANGA

EWE Mwenyezi Mungu, wewe hapo kale kwa ajili ya makosa ya binadamu uliigharikisha dunia nzima, isipokuwa watu wanane, kisha baadaye kwa rehema zako kubwa ukatoa ahadi ya kutoiangamiza tena dunia kama vile ; sisi tu miguuni pako, na tungawa tulistahili kupigwa na wewe kwa hiyo mvua iliyopita kiasi na hayo maji yaliyo mengi mno, lakini twakuomba sana utuonapo tumetubia kweli, utujalie kupokea mazao ya nchi kwa wakati wake: tujifunze huku kuyafanyiza upya maisha yetu kwa ajili ya adhabu yako hii, na huku kukupa sifa na utukufu kwa ajili ya upole wako; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

For Fair Weather

ZAMANI ZA SHIDA NA NJAA

EWE Mwenyezi Mungu, Baba wa mbinguni, ni katika vipawa vyako, la kunya mvua na nchi kubarikiwa, la nyama kuzaa na samaki kuwa wengi; twakuomba uyaangalie mateso ya watu wako; nawe ukubali ya kwamba hii shida na hii njaa, ituadhibuyo hivi sasa kwa haki sana kwa ajili ya viovu vyetu, igeuzwe kwa wema wako na rehema zako iwe neema na urahisi; kwa ajili ya mapenzi ya Yesu Kristo, Bwana wetu, naye ni wa kusifiwa pamoja na wewe na Roho Mtakatifu, kwa heshima yote na utukufu wote, sasa na milele. Amina.

Au hii,

EWE Mungu, Baba wa rehema, wewe uliyeigeuza shida na njaa iliyokuwako Samaria zamani za nabii Elisha, ikageuka mara moja ikawa neema na urahisi; uturehemu sisi tunao pigwa sasa kwa mashaka kama hayo kwa ajili ya dhambi zetu, tusaidiwe kama vile; uyazidishe mazao ya nchi kwa baraka yako ya mbinguni; ukubali ya kwamba sisi tutakaoupokea ukarimu wako mwingi, tuutumie huo kwa kuuzidisha utukufu wako, na kuwasaidia wenye dhiki, na kwa manufaa ya nafsi zetu ; kwa ajili ya Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

In time of Dearth or Famine

ZAMANI ZA VITA NA MISHINDO

EWE Mwenyezi Mungu, Sultani wa masultani wote, Mtawala mambo pia, nguvu zako hakuna kiumbe kimoja awezaye kuzipinga, ni haki yako wewe kuwaadhibu wenye dhambi, na kuwarehemu wanao tubia kwa kweli; utuokoe sisi, twakuomba kwa unyenyekevu, na kutuepusha na mikono ya adui zetu ; uvipunguze viburi vyao, uuondoe na uovu wao, uwabati1ie hila zao; ili tuwekwe salama milele na kila hatari kwa kuvaa silaha za ulinzi wako, tupate kukutukuza wewe uliye pekeo Mpaji wa kushinda kote; kwa ajili ya wema wake Mwanayo pekee, Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

In Time of War or Tumults

ZAMANI ZA TAUNI AU MARADHI, YALIYOWAPATA WATU WOTE

EWE Mwenyezi Mungu, wewe kwa hasira zako uliwashushia watu wako tauni wakati walipomwasi Musa na Haruni kwa ule ushupavu wao, mle barani; nawe katika zamani za mfalme Daudi ukaua watu elfu sabuini kwa tauni, lakini ulipokumbuka rehema zako ukawaokoa waliosalia; utuhurumie sisi tulio dhaifu wenye madhambi, ambao sasa twapatikana na ugonjwa mwingi na kufa kwingi; nawe kama vile ulivyokubali kufanyiwa sadaka wakati ule, ukamwamuru Malaika wako mwangamizi aache, asiadhibu ; na sasa uridhike vivyo kutuondolea hii tauni, na haya maradhi mazito; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

In time of any common Plague or Sickness

Katika MAJUMA ya NYAKATI NNE za MWAKA, zasomwa kila siku, kwa ajili ya watu watakaopewa DARAJA TAKATIFU:

EWE Mwenyezi Mungu, Babaetu wa mbinguni, uliyepata kanisa nchi zote kwa kulinunua kwa damu ya thamani ya Mpenzi wako Mwanayo ; uliangalie kwa rehema hilo kanisa lako, nawe wakati huu wa sasa, uziongoze sana na kuzitawala sana nia za watumishi wako mabishopu, wachungaji wa kundi lako, ili wasije wakawa kumwekea mtu mikono ghafula, awaye yote; lakini na wachague kwa uaminifu na akili watu wanaofaa kutumika katika utumishi mtakatifu wa kanisa lako. Na hao watakaopewa daraja ya utumishi uwao wote, wewe uwape neema yako na radhi yako ya mbinguni; ili kwamba huku kwa maisha yao na huku kwa kufunza kwao wauonyeshe utukufu wako, wauendeleze na wokofu wa watu wote; kwa ajili ya Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Au hii,

EWE Mwenyezi Mungu, Mpaji wa vipawa vyema vyote, ambaye kwa uangalizi wako wa Uungu umeweka madaraja mbali-mbali ya watumishi ndani ya Kanisa lako; sisi miguuni pako twawaombea watu wote watakaoitwa humo kwa utumishi uwao wote na uwakili uwao wote; ya kwamba uwape neema yako, na kuwaongeza sana watu hao kweli ya elimu yako, na kuwapa usafi wa maisha, hata iwe wao kutumika mbele zako kwa uaminifu, kwa kuvutia utukufu jina lako kuu, na kulifaa kanisa lako takatifu; kwa ajili ya Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

In the Ember Weeks, for those who are to be admitted to Holy Orders

Ni Sala ifaayo kusomwa baada ya zilizotangulia mojawapo.

EWE Mungu, ndiyo tabia yako kuwarehemu watu milele, na kuwasamehe, upokee hizi haja zetu nyenyekevu; nasi tujapofungwa na kuzuiwa kwa mikufu ya madhambi yetu, lakini hizo huruma za wingi wa rehema zako na zitufungue ; kwa heshima yake Yesu Kristo, Mwombezi wetu, Msaada wetu. Amina.
 

Prayer that may be said after any of the former

Sala ya kuombea MKUTANO-wa-SHAURI uitwao PARLIAMENT, nayo husomwa muda unapokutana.

EWE Mungu, mwingi wa neema, sisi twakunyenyekea miguuni pako, kisha kama vile tuuombeavyo Ufalme huu pia wote, tuombeacho sana ni Mkutano-wa-shauri wa Parliament, hali umekutanika wakati huu wa sasa chini ya Mfalme wetu mcha-Mungu sana, mwenye fadhili sana; nawe uone vyema kuyaongoza mashauri yao yote, kwa kuuongeza utukufu wako, na kwa kulifaa kanisa lako, na kwa kuleta salama na heshima na manufaa ya yeye Mkuu wetu, na ufalme wake; ili kwamba, mambo yote jinsi yatakavyotengezwa na kuamrishwa kwa bidii zao katika misingi bora ya salama, hata amani na raha, na kweli na haki, na dini na uchaji-wa-Mungu, yawe imara mambo hayo na kwendelezwa mbele kwetu hata vizazi vyote. Sisi, haja hizi na nyingine zote, twawaombea miguuni pako watu hao, na nafsi zetu na kanisa lako zima, kwa jina lake na Uombezi wake Yesu Kristo, Bwana wetu, Mwokozi wetu, abarikishaye kwa wingi. Amina.
 

Prayer for the High Court of Parliament

Sala ya huwaombea watu wa kila daraja, nayo hutumiwa kama wakati usioagizwa Litania.

EWE Mungu, ndiwe Muumba watu wote, na ulinzi wao; sisi tu miguuni pako, twawaombea wanadamu wote, kila aina na kila daraja; uone vyema kuwaonyesha njia zako, salama yako iokoayo uwajuvishe mataifa yote. Na tuombealo sana, ni la kanisa lako lililo ulimwenguni mote hali yake kuwa njema; liongozwe na kutawaliwa sana na Roho wako Mwema, hata wote wapendao kuitwa jina la Kristo, waongozwe katika njia ya kweli, na kuishika imani kwa umoja wa roho, na kifungo cha amani, na maisha yaliyolekea. Baada ya haya, twakusongezea haja zao na kuzitia kwa kusongezea haja zao na kuzitia kwa wema wako wa ubaba, watu wawao wote wasumbukao na kuteseka kwa neno liwalo lote, la moyo, au la mwili, au la hali; * (hasa hao watakiwao sala zetu,) uwe mwenye kuwa tuliza na kuwasaidia, kila mtu kwa kadiri ya haja yake, huku ukiwapa kuvumilia katika mateso yao, na kupona masumbuko yao kwa salama. Na haya twakuomba kwa ajili ya Yesu Kristo. Amina.
 


Prayer for all Conditions of Men

 

* Haya ni ya kusomwa wakati zitakwapo sala za Mkutano.

 

 

 

SHUKRANI

SHUKRANI YA WATU WOTE

EWE Mwenyezi Mungu, Baba mwenye kila rehema, sisi watumishi wako tusiofaa, twakushukuru kwa unyenyekevu sana, kwa mioyo yetu, ya wema wako wote na ihisani yako pia, uliyo nayo kwetu sisi na watu wote; * (hasa hao watakao sasa kukupazia sifa na shukrani kwa neema zako ulizowapa hivi karibu.) Twakushukuru sisi ya tulivyoumbwa na kuhifadhiwa, na baraka zote za maisha haya; ila zaidi sana, twakushukuru kwa mapenzi yako yasiyopimika kwa vile ulivyoukomboa ulimwengu kwa Bwana wetu Yesu Kristo; tena kwa njia za neema, na tumaini la utukufu. Nasi twaomba sana kwako, kuwa na fahamu njema ya rehema zako zote, hata mioyo yetu nayo iwe kukupelekea shukrani isiyo shaka, tupate kuonyesha sifa zako, huku kwa midomo yetu, na kuku kwa maisha yetu; kwa vile tutakavyojivika katika utumishi wako, na kwenenda kwa utakatifu na haki siku zetu zote mbele zako; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu, ambaye ni wa kuheshimiwa na kutukuzwa pamoja na wewe na Roho Mtakatifu, milele na milele. Amina.
 

Thanksgivings

General Thanksgiving

 

 

* Maneno haya ni ya kusomwa wakati walioombewa wawapo kutaka kumrejezea Mwenyezi Mungu sifa.

KWA AJILI YA MVUA

EWE Mungu Babaetu wa mbinguni, wewe kwa uangalizi wako wa neema huinyesha juu ya nchi mvua ya Mwaka na ya Vuli, ili itoe mazao yawe ni matumizi ya wanadamu; sisi tu miguuni pako, twakushukuru kwa vile ulivyoona vyema kutupa msaada wakati wa hiyo shida yetu kuu, ukatuletea mwishowe mvua ya furaha, ukauburudisha urithi wako ulipokuwa mkavu, kwa kututuza mno mioyo yetu sisi watumishi wako tusiofaa, na kulitukuza jina lako takatifu; kwa rehema zako zilizo katika Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

For Rain

KWA AJILI YA KIANGA

EWE Bwana Mungu, wewe una haki hivyo ulivyotupiga kwa mvua isiyo kiasi, na maji mengi, nawe kwa rehema zako umetutuza roho zetu, umetufurahisha, kwa majira yalivyobadilika hivi kwa kufaa na kubariki ; sisi twalisifu na kulitukuza jina lako takatifu, kwa ajili ya rehema zako hizo, nasi hatutaacha kutangaza wema wako kizazi hata kizazi, milele; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

For Fair Weather

KWA AJILI YA WINGI WA VYAKULA

EWE Baba mwingi wa rehema, wewe kwa wema wako na fadhili zako umeyasikia maombi kanisa lako liliyokuomba kwa uchaji-wa-Mungu, nawe huo uhitaji wetu na upungufu wetu umeugeuza umekuwa urahisi na wingi; sisi twakushukuru miguuni pako kwa ajili ya huo upaji wako mkuu; nasi twakuomba sana uudumishe kwetu, ili nchi yetu ituzalie mazao yake ya kuongea kwake, kwa utukufu wako na utuzo wetu; kwa ajili ya Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

For Plenty

KWA AJILI YA AMANI NA KUEPUSHWA NA ADUI ZETU

EWE Mwenyezi Mungu, wewe ndiwe Mnara wa imara wenye ulinzi wa watumishi wako nyusoni mwa adui zao; sisi twakushukuru na kukupa asante kwa ulivyotuepusha na hizo hatari kubwa zilizotuzunguka ; tumekubali ya kuwa ni wema wako wewe, sisi kutotiwa mikononi mwao kuwa mateka yao; nasi twakuomba sana utudumishie rehema zako namna hii, ili ulimwengu wote ukujue wewe kuwa u Mwokozi wetu, Mponyi wetu mwenye nguvu; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

 
For Peace & Deliverance from our Enemies

KWA AJILI YA AMANI KURUDISHWA KATIKA WENYEJI

EWE Mungu, huna mwanzo huna mwisho, nawe ndiwe Babaetu wa mbinguni; ni wewe pekeo unayewafanya jamaa kuwa na nia moja katika nyumba yao, na kunyamazisha jeuri za watu wakaidi na uasi; sisi twalisifu jina lako takatifu, ya kwamba umependa kuituliza mishindo yenye fitina iliyokuwako hivi karibu; nasi twakuomba sana miguuni pako, utupe neema sote pia, ili mwanzo wa sasa tuende katika maagizo yako matakatifu kwa kutii, na kwa tutakavyoishi maisha matulivu na amani katika kicho . cha Mungu na haki kwa wenzetu, tukupe daima sadaka yetu ya sifa na shukrani kwa ajili ya hizo rehema ulizoturehemu; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

 
For Restoring Peace at Home

KWA AJILI YA KUEPUKANA NA MARADHI YA TAUNI, AU MARADHI MENGINE YOYOTE

EWE Bwana Mungu, wewe umetupiga kwa ajili ya madhambi yetu, umetuangamiza kwa ajili ya makosa yetu, kwa mapatilizo mazito ya' utisho uliyotupatiliza hivi karibu; nawe sasa, ulivyokumbuka rehema humo katika hukumu yako, umeziokoa roho zetu katika kinywa cha mauti; twausongezea wema wako wa ubaba nafsi zetu, maana, roho zetu na miili yetu, ulivyo viponya wewe hivi sasa, viwe hivyo ni sadaka iliyo hai kwako wewe, kwa tutakavyozisifu na kuzifahamu daima hizo rehema zako ndani ya Kanisa lako, kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Au hii,

SISI tu miguuni pako, tumekubali mbele zako, ewe Baba mwingi wa rehema, ya kwamba adhabu zote wakamiwazo maasi katika sheria yako yangelitupata sisi kwa haki, kwa ajili ya hayo makosa yetu, na huo uzito wa mioyo yetu: lakini kwa kuwa umependa kwa rehema zako zenye huruma, kwa maana ya huko kujinyenyekeza kwetu sisi wanyonge tusiofaa, kuyakomesha hayo maradhi yenye wito tuliyoadhibiwa kwa uzito hivi karibu, na kwa ulivyorudisha sauti ya furaha na afya nyumbani mwetu; twakusongezea, ewe Mungu mtukufu, hizi dhabihu zetu za sifa na shukrani, kwa kulitukuza na kulisifu jina lako la ubora, kwa hivyo ulivyotuponya na kutuangalia ; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 


 

For Deliverance from the Plague, or common Sickness

SALA NA SHUKRANI KADHAWAKADHA

    Sala na Shukrani hizi zifuatazo hapa hutumiwa kama Padre aonavyo vyema, zaidi baada ya Sala ya Tatu, au mwisho wa Litania, au katika Taratibu ya Ushirika Mtakatifu, baada ya Sala-ya Siku hiyo, au ya Sala ya kuombea Kanisa lililo katika vita hapa duniani, au mbele ya Baraka.

SALA

(Sala hizi zaweza kusemwa pasipo vifungu vyake. Kisha yawezekana watu kutakwa kuomba kimya.)

KUMWOMBEA MFALME NA WOTE WALIO NA AMRI CHINI YAKE

Na tumwombee Mfalme na wote waliopewa amri chini yake.

    Padre. Mfalme atazifurahia nguvu zako, ewe Yehova.
    Huitika. Na wokofu wako ataufanyia shangwe nyingi sana.

EWE Mwenyezi Mungu, shina la wema wote, sisi tu miguuni pako, twakuomba umbariki Bwana wetu Mfalme GEORGE, na mikutano yote ya mashauri iliyo katika ufalme wake wote, na wote waliopewa amri chini yake: zaidi mtumishi wako . . . Governor wetu, na wote walio pamoja naye katika Serkali ya nchi hii; ili wayatengeneze mambo yote kwa hekima na haki na amani, kwa kuliletea jina lako takatifu heshima, na kwa kufaa kanisa lako na watu wako, kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

Various Prayers and Thanksgivings

Most of these are taken from the C of E 1928 BCP and are all optional


 

Prayers

 

For the King, and all in authority under him

KUOMBEA UFALME WETU

Na tuuombee Ufalme wetu

    Padre. Mungu huyu ni Mungu wetu milele na milele:
    Huitika. Yeye ndiye atakayetuongoza hata mauti.

EWE Mwenyezi Mungu, ndiwe utawalaye katika ufalme wa wanadamu, umemweka Bwana wetu Mfalme GEORGE juu ya ufalme mkubwa katika pande zote za ulimwengu: twakuomba uwavute watu wakaao mumo, ambao kwa taifa na lugha na desturi zao wa mbali-mbali, wawe na ushirika wa kweli, ili kwa kuchukuliana mizigo yao, na kufanya kazi pamoja katika mapatano ya ndugu, wapate kutimiza uyatakayo wewe kwa uangalizi wako, na kusongeza mbele ufalme wako wa milele. Twakuomba utusamehe dhambi zetu na upungufu wetu; ututenge mbali na kujipenda wenyewe, na kiburi, kisha utupe neema kuvitumia vipawa vyako- vyema vya utaratibu na ungwana, kwa kukuletea utukufu, na kwa kuwafaa wanadamu, kwa Yesu Kristo Mwanayo, Bwana wetu, naye apewe utukufu na kutawala pamoja na wewe na Roho Mtakatifu, milele na milele. Amina.
 

Prayer for our Commonwealth

KUONGEZEKA UTUMISHI MTAKATIFU

Na tuombe Utumishi Mtakatifu uongezeke

    Padre. Mwombeni Bwana wa mavuno:
    Huitika. Awapeleke watenda-kazi katika mavuno yake.

EWE Mwenyezi Mungu, uuangalie kwa rehema ulimwengu huu ulioukomboa kwa damu ya Mwanayo mpenzi wako, uilekeze mioyo ya watu wengi wajitoe kwa ajili ya utumishi mtakatifu wa kanisa lako; ili kwa kazi zao mwanga wako ung'ae gizani, na kwa wateule wako kukamilishwa, kuja kwake ufalme wako kuhimizwe; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

For the increase of the sacred Ministry

KWA KAZI YA KUENEZA INJILI

(Yafaa sana kwamba kila Jumapili Sala moja katika hizi tatu isomwe.)

    Na tuombe kwamba Ufalme wa Kristo uenee ulimwenguni.

    Padre. Wahubirini mataifa habari za utukufu wake:
    Huitika. Na watu wote habari za maajabu yake.

EWE Mungu wa mataifa yote ya dunia, ukumbuke jamii ya watu wa mataifa, ambao, wajapoumbwa katika sura zako, hawajui mapenzi yako; kisha kwa ajili ya upatanisho wa Mwanayo Yesu Kristo, ujalie kwamba kwa maombi ya kanisa lako takatifu na kazi zake, waokolewe katika dini za uwongo na kutoamini, wavutwe kukuabudu wewe: kwa yeye uliyemleta awe wokofu wetu, na ufufuo na uzima wa wote waaminio, Mwanayo Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Au hii,

    Padre. Jinsi ilivyo mizuri miguu ya wale wahubirio habari njema ya amani:
    Huitika. Watangazao habari za wokofu.

EWE Mwenyezi Mungu, Babaetu wa mbinguni, uliyeonyesha mapenzi yako kwa kumtuma Mwanayo mzaliwa pekee aje ulimwenguni, ili wote wapate uzima kwa yeye: ulimiminie kanisa lako Roho wako, ili litimize amri zake kuhubiri Injili kwa kila kiumbe; twakuomba uwapeleke watenda-kazi katika mavuno yako; uwakinge katika hatari zote na majaribu yote; ulete upesi wakati ambao kujaa kwao mataifa kutatimia, na Isiraeli wote wataokoka; kwa Mwanayo Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Au hii,

    Padre. Uniombe nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako :
    Huitika. Na miisho ya dunia kuwa milki yako.

EWE Mwenyezi Mungu, uliyefanya mataifa yote ya wanadamu kuwa wa damu moja wakae juu ya nchi, ukamtuma Mwanayo, Mwenye-baraka Yesu Kristo, ahubiri amani kwao walio mbali, na walio karibu: uwajalie watu wote wa ulimwengu wakutafute na kukuona, ukatimize haraka ahadi yako, ewe Bwana, ya kwamba utawamiminia watu wote Roho wako; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

For the Spread of the Gospel

KUOMBEA UMOJA

Na tuombe Wakristo wote wakae na umoja wa moyo.

    Padre. Jinsi lilivyo jambo jema, tena la kupendeza.
    Huitika. Ndugu wakikaa pamoja, kwa umoja halisi.

EWE Bwana Yesu Kristo, uliwaambia mitume wako, Nawaachia amani; amani yangu nawapa; usiziangalie dhambi zetu, uiangalie imani ya kanisa lako, na kulijalia amani na umoja kama vile utakavyo wewe: uishiye na kutawala pamoja na Baba na Roho Mtakatifu, Mungu mmoja, milele na milele. Amina.

Au hii,

EWE Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Mwokozi wetu wa pekee, Mkuu wa amani; utujalie kufikiri sana mioyoni mwetu jinsi zilivyo kuu hatari tulizo nazo' kwa mashaka ya kutengana wenyewe kwa wenyewe. Utuondolee machukio yote na kuhukumiana, na kila neno lituzuialo tusiwe na umoja na mapatano katika kukucha wewe: na kwa kuwa Mwili ni mmoja tu, Roho ni mmoja, Tumaini la mwito wetu ni moja, Bwana ni mmoja, Imani ni moja, Ubatizo ni mmoja, Mungu ni mmoja, naye ni Babaetu sisi sote, tangu sasa tuwe vivyo na moyo mmoja, roho moja, tuungamanishwe katika kifungo kimoja kitakatifu cha kweli na amani, cha imani na mapenzi, nasi kwa nia moja na kwa kinywa kimoja tukutukuze wewe; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

Prayer for Unity

WAKATI WA UBISHOPU AU UCHUNGA KUTOKUWA NA MWENYEWE

Na tuombe kwamba Padre mwaminifu aletwe katika Ubishopu huu

(au, Uchunga huu)

    Padre. Uwavike haki watumishi wako:
    Huitika. Uwaweke na furaha wateule wako.

EWE Mwenyezi Mungu, Mpaji wa kila kipawa chema, twakuomba kwa neema yako uliangalie kanisa lako, ukaziongoze kwa hekima yako ya mbinguni nia za wale ambao ni juu yao kumchagua Bishopu wa Ubishopu huu, (au, Padre wa Uchunga huu), ili tupewe mchunga mwaminifu, atakaye1isha kundi lako sawasawa na mapenzi yako, na kukufanyia tayari watu wa kukupendeza; kwa Yesu Kristo, Mwanayo wa pekee, Bwana wetu. Amina.
 

When Bishops or Presbyters resign (i. e., during a vacancy)

KWA KUITUNZA SABATO

Na tuombe kwamba Siku ya Bwana itakaswe.

    Padre. Siku hii ndiyo aliyoifanya Yehova :
    Huitika. Tutashangilia na kuifurahia.

EWE Mwenyezi Mungu, umewapa watu siku ya kupumzika, nawe kwa Roho wako aliye kanisani umetakasa siku ya kwanza ya juma, iwe ukumbusho hata milele wa kufufuka kwa Mwanayo : utujalie kwamba kwa jinsi tutakavyotumia kipawa chako hiki tupate raha na nguvu rohoni hata mwilini, ili tukutumikie kwa uaminifu siku zote za maisha yetu; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

For the honouring of the Sabbath

 

KWA WALE WATAKAOTHUBUTlSHWA

Na tuwaombee wale wanaowekwa tayari kuthubutishwa

    Padre. Roho wako ni mwema:
    Huitika. Uwaongoze katika nchi ya haki.

EWE Mungu, wewe kwa mafundisho ya Mwanayo Yesu Kristo uliwaweka wanafunzi tayari kujiwa na Msaada: twakuomba uwaweke tayari katika mioyo na akili watumishi wako watakao wakati huu kupewa zaidi Roho Mtakatifu kwa kutiwa mikono, ili wakija na mioyo iliyotubu na kuamini, wajazwe nguvu kwa jinsi yeye atakavyokaa ndani yao; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

For those in danger

KWA MKUTANO MKUU WA UBISHOPU, ISOMWE KATIKA JUMAPILI KABLA YA MKUTANO MKUU WA UBISHOPU, AU MKUTANO WA KANISA

Na tuombe baraka ya Mungu iwe juu ya Mkutano Mkuu wa Ubishopu huu (au Mkutano huu wa Kanisa).

    Padre. Akili na uwezo viko pamoja na Mungu:
    Huitika. Yeye ana mashauri na fahamu.

TWAKUOMBA, ewe Mwenyezi Mungu, uwaongoze kwa mwanga wa Roho wako Mtakatifu, mabishopu na mapadre na watu wengine katika Mkutano Mkuu wa Ubishopu, (au Mkutano wa Kanisa), ili washauriane kwa hekima kwa ajili ya kulifaa kanisa lako na kulitukuza jina lako; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

For Meetings of Archbishops, on the Sunday before the Meeting, or Meetings of the Church

KWA SKULI

Na tuziombee skuli zetu

    Padre. Kumcha Yehova ndio mwanzo wa hekima:
    Huitika. Wote wafanyao haya wana akili njema.

EWE Babaetu wa mbinguni, Mwanayo Mwenyebaraka alisema, Waacheni watoto wanijilie: twakuomba uwafanikishe waalimu wote na wanafunzi wao kwa baraka yako; kisha kama akili za watoto wako zitiwavyo mwanga kwa kupewa elimu, na mioyo yao nayo ivutwe daima na Roho wako Mtakatitfu, hata wakupende wewe na Mwanayo, Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Amina.
 

For Schools

KWA SKULI ZA JUMAPILI

Na tuziombee Skuli za Jumapili

    Padre. Maneno haya nikuagizayo leo yatakuwa katika moyo wako :
    Huitika. Nayo wafunze watoto wako kwa bidii.

EWE Mwenyezi Mungu, Babaetu wa mbinguni, uliyewatia watoto wako katika ulinzi wa kanisa lako takatifu, walindwe na kulewa: uwatie nuru ya hekima yako waalimu na wanafunzi; ili wakifurahi katika kujua kweli yako, wakuabudu na kukutumikia siku zote za maisha yao; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

For Sunday Schools

KWA MAKOLEJI NA MADARASA MENGINE YA ELIMU

Na tuombee makoleji na madarasa mengine ya elimu

    Padre. Kumcha Yehova ndiyo akili :
    Huitika. Na kuepukana na uovu ndiyo fahamu.

UWE radhi, ewe Bwana, kuzifanikisha kwa baraka yako kazi za makoleji yote, na skuli, ili wao wakutumikiao mumo, waalimu na wanafunzi pia, waandame siku zote mapenzi yako matakatifu, na kuongozwa waijue kweli yako: hata baraka ije juu ya kanisa na nchi kwa sababu ya kusoma kwao, na wao wenyewe wafanywe kustahili kuwa washiriki wa uzima wa milele; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

For Universities & other places of Learning

KWA AMANI ULIMWENGUNI

Na tuuombee ulimwengu uwe na amani

    Padre. Yehova ameketi ali Mfalme milele:
    Huitika. Yehova atawabariki watu wake kwa amani.

EWE Mwenyezi Mungu, kwako wewe hutoka mawazo yote ya kweli na ya amani: twakuomba, uwajalie watu wote kupenda amani kwa kweli; ukawaongoze wao wafanyao mashauri ya mataifa ya ulimwengu, kwa kuwapa hekima yako takatifu iletayo amani, ili ufalme wako uendelee mbele katika utulivu wote, hata dunia iyajue kabisa mapenzi yako, kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

For the Peace of the World

KWA USHIRIKA-W A-MASHAURI WA MATAIFA
(LEAGUE OF NATIONS)

Na tuuombee Ushirika-wa-Mashauri wa Mataifa

    Padre. Akomesha vita hata mwisho wa dunia:
    Huitika. Auvunja uta, aukata mkuki, ayateketeza magari motoni.

TWAKUOMBA, ewe Bwana, uwajalie watu wa Ushirika-wa-Mashauri wa Mataifa maongozi yako yaliyo na nguvu zote za kuamrisha. Uwape wote walio mumo mwanga na fahamu ili wayajue mapenzi yako, na uthabiti na nguvu kuyatimiza. Na viwe mashauri yao na hukumu zao kutiwa mioyoni mwao na kutengenezwa na wewe, ili adili na amani vithubutishwe katika mataifa ya ulimwengu, na ufalme wako uendelee katika haki na mapendano ya ndugu, kwa utukufu wako na kwa hali njema ya wanadamu, kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

For the League of Nations

KWA WASAFIRI WA BAHARI

Na tuwaombee wote wasafiria baharini

    Padre. Hao wameziona kazi za Yehova :
    Huitika. Na maajabu yake vilindini.

EWE Bwanga Mungu wa milele, ni wewe pekeo utandazaye mbingu, na kutawala kiburi cha bahari: uwe radhi kuwalinda wote washukao baharini katika merikebu, wafanyao kazi katika maji mengi. Uwahifadhi mwilini na rohoni: uzifanikishe kazi zao; wakati wa hatari uwe mlinzi wao, ukawalete hata bandari wanayoitamani ; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

For Those going to Sea

KWA AMANI KWA WATENDAO KAZI KATIKA NCHI YETU

Na tuombe kwamba watenda-kazi wawe na amani wao kwa wao

    Padre. Msiwiwe na mtu kitu kiwacho chote, ila neno hili kupendana ninyi kwa ninyi:
    Huitika. Kwani huyo ampendaye mwenziwe amekwisha kuitimiza sheria.

EWE Mungu, Baba wa wanadamu wote, twakuomba utuvuvie mapenzi, na kweli, na haki, hata katika shughuli zetu zote tulizo nazo wenyewe kwa wenyewe, utuonyeshe tulivyo ndugu ndani yako wewe, kwa ajili ya Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Au hii,

Na tuombe kwamba Mungu alete hekima na haki, ili mashaka yaliyoko sasa kwa watendao kazi yaishe

    Padre. Pisheni hukumu mkatende ya haki:
    Huitika. Kwani wokofu wangu kuja kwake ni karibu, na haki yangu kufunuliwa.

EWE Mwenyezi Mungu, Baba wa wanadamu wote, wewe umeamuru kwamba watu wote waishi na kutenda kazi zao pamoja kama ndugu; sisi tu miguuni pako, twakuomba kwamba wao wasiosikizana sasa uwaondolee mashindano yote na ugomvi, ili watafute yaliyo ya haki na sawasawa tu, waendelee siku zote katika mapatano na masikizano ya ndugu, ili wajipatie wema wenyewe na kufanikisha ufalme wetu; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

For carrying out the Work of Peace in our Homeland

SIKU ZA KUOMBEA MAVUNO

Na tuombe Mungu ayabariki mazao ya nchi na kazi za wanadamu

    Padre. Macho ya wote yakulekea wewe, ewe Yehova:
    Huitika: Nawe huwapa chakula chao kwa wakati wake.

EWE Mwenyezi Mungu, uliyeibariki nchi iwe na matunda mengi, na kuzaa kila kitu cha kuhitajiwa na wanadamu kwa maisha yao: twakuomba uzifanikishe kazi za wakulima, ukatujalie mvua ya kutosha ili tuvune mazao ya nchi, na kufurahiwa siku zote katika wema wako, kwa utukufu wa jina lako takatifu; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Au hii,

EWE Mwenyezi Mungu, uliyefanya bahari na vyote vipitavyo mumo, uyabarikie mavuno ya bahari, yawe mengi kwa wakati wake, uwabarikie wavuvi wetu nao, na mabaharia, wawe salama katika hatari zote za majini; hata sisi sote kwa mioyo ya shukrani tukukiri wewe uliye Bwana wa bahari na wa nchi kavu; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Au hii,

EWE Baba Mwenyezi, kwa Mwanayo Yesu Kristo umetakasa kazi iwe kwa hali njema ya wanadamu; twakuomba uwafanikishe wote walio na amali katika nchi hii, na kazi zao; walindwe katika majaribu yao yote na hatari zote ziwapatazo, nao huku wakipata ijara ipasayo kazi zao, wakusifu kwa kuwa na mwendo ulio sawasawa na mapenzi yako; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

Prayers for Harvest (Rogation) Days

KWA KILIMO KIZURI

Na tuombe tuletewe kilimo kizuri

    Padre. Atawafanyia wamchao yale watakayo:
    Huitika. Naye atasikia kilio chao na kuwaokoa.

EWE Mwenyezi Mungu, Babaetu, kwa maneno ya Mwanayo, Yesu Kristo, uliahidi kwamba wao watafutao kwanza ufalme wako na haki yako watapewa vyote vipasavyo kuiokoa miili yao: twakuomba utuletee kilimo kizuri, ili tupate mavuno ya nchi kwa kutufaa sisi, na kwa heshima ya jina lako; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

For a good Crop

WAKATI WA NJAA

Na tuombe tuletewe msaada wakati huu wa njaa

    Padre. Umtweke Yehova mzigo wako:
    Huitika. Naye atakutegemeza.

EWE Mwenyezi Mungu, Babaetu wa mbinguni, uliyetufundisha kwa maneno ya Mwanayo Mwenye-baraka kukuomba wewe riziki zetu: twakuomba uyaangalie mashaka ya watu wako, utuletee msaada wa kututosha katika uhitaji wetu huu tulio nao. Uongeze mavuno ya nchi kwa baraka yako ya mbinguni, ukatujalie sisi tuvipokee kwa shukrani vipawa vya neema yako, tukavitumie kwa utukufu wako, na kwa kuwasaidia wao walio na uhitaji, na kwa kutufaa sisi wenyewe: kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

In Time of Famine

WAKATI WA TAUNI AU UGONJWA

Na tuombe tuletewe msaada wakati huu wa ugonjwa

    Padre. Anayekusamehe maovu yako yote:
    Huitika. Anayekuponya magonjwa yako yote.

TWAKUOMBA, ewe Bwana wa rehema, utusaidie na kutuokoa sisi tunaopatikana na ugonjwa mwingi na kufa. Utugeuzie mashaka haya yetu makuu, yatuletee baraka, ukawabarikie siku zote wale wafanyao kazi ya kujaribu kukinga wanadamu katika magonjwa na maumivu; kwa yeye aliyepoza na kutakasa maumivu, Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

In time of Plague or Sickness

WAKATI WA VITA

Na tumwombe Mungu atusaidie na kutuongoza wakati huu wa vita

    Padre. Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu:
    Huitika. Msaada uonekanao wakati wa mateso.

EWE Bwana Mwenyezi, ndiwe ngome ya imara kwa wote wakuaminio; utulinde sasa na siku zote; ikiwa mapenzi yako utupe kushinda; uwaangalie kwa rehema waliojeruhiwa na wafungwa, uwatie moyo wanaofadhaika ; uwafariji waliofiwa; uwasaidie walio katika kufariki; uwarehemu wote; uhimize wakati wa vita kukorna katika ulimwengu wote; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

In time of War

KWA WAGONJWA

Na tuwaombee wagonjwa

    Padre. Huwaponya waliopondeka moyo:
    Huitika. Na kuyafunga majeraha yao.

EWE Baba Mwenyezi, Mpaji wa maisha na afya, twakuomba uwaangalie kwa rehema wagonjwa wote, hasa wao wanaotakiwa maombi yetu, ili kwa baraka yako juu yao, na juu ya wao wawatumikiao, ikiwa mapenzi yako warudishiwe afya yao ya -mwili na ya roho, nao wakutolee shukrani katika kanisa lako takatifu; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

For the Sick

KWA HOSPITALI

Na tuombe baraka ya Mungu iwe juu ya Hospitali zote

    Padre. Mwenyewe aliupokea udhaifu wetu:
    Huitika. Akayachukua na magonjwa yetu.

EWE Mwenyezi Mungu, Mwanayo Mwenyebaraka alikuwa akizunguka akitenda kazi njema, akapoza kila namna ya ugonjwa na udhaifu katika watu; twakuomba kwamba kazi yake hii ya neema iendelee kwetu, zaidi katika hospitali za nchi yetu; uwatie moyo wagonjwa, uwapoze na kuwatakasa; uwape madaktari na hao wawasaidiao na wauguzi wote akili na ustadi, na huruma na uvumilivu; uwabarikie wote wanaojitahidi kuzuia maumivu na kuhimiza mashauri yako ya mapenzi; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

For Hospitals

KUWAKUMBUKA WAAMINIFU MAREHEMU

Na tukumbuke mbele za Mungu waaminifu marehemu

    Padre. Wenye haki huishi milele:
    Huitika. Na thawabu yao iko kwa Yehova.

EWE Mungu wa roho za wote wenye mwili, twalisifu na kulitukuza jina lako takatifu kwa ajili ya watumishi wako wote waliotimiza mwendo wao katika imani yako na kicho chako. Twakuomba kwamba tulivyotiwa moyo kwa vielelezo vyao vizuri, na kupewa nguvu kwa kuwa na ushirika nao, tuonekane nasi pamoja nao kuwa tunastahili kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu walio katika nuru; kwa kustahili kwake Mwanayo, Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Watu wakitaka kuomba kwa ajili ya haja nyingine, itatosha kusema, Na tuombee (jinsi kadhawakadha), kisha watu wawe kimya kitambo kidogo. Ndipo husema,

    Padre. Ewe Bwana, utusikize maombi yetu :
    Huitika. Kilio chetu kikufikilie.
 

Commemoration of the faithful Departed

SALA ZIWEZAZO KUTUMIWA BAADA YA HIZO ZA MBELE

EWE Mwenyezi Mungu, ni hali yako wewe siku zote kuwa mwenye rehema na msamaha, utusikie sisi tulio miguuni pako tukuombavyo ; nasi tujapofungwa na kuzuiwa kwa minyororo ya dhambi zetu, huruma zako nyingi na zitufungue; kwa heshima ya Yesu Kristo, Mwombezi wetu, Msaada wetu. Amina.

UIKUMBUKE, ewe Bwana, kazi uliyo tenda ndani yetu, usikumbuke tunavyostahili kupewa; kisha u1ivyotuita kukutumikia, utujalie tuwe wa kustahili mwito wetu, kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

EWE Bwana, utuchukuze mchana wote wa maisha haya ya taabu, hata kutwa, zitakapotulia kelele za ulimwengu huu, ra fadhaa ya maisha itakoma, na kazi yetu itakwisha. Ndipo, ewe Bwana, kwa rehema zako, utupe makao ya salama, na raha takatifu, na amani mwisho wake. Amina.
 


 

Prayers which may be used after any of the previous

SHUKRANI

KWA KILIMO KIZURI

EWE Bwana Mwenyezi Mungu, uliyetusaidia na kututuliza sisi watumishi wako, kwa kutupa kilimo kizuri; twakushukuru sana kwa mioyo yetu kwa wema wako huu kwetu; twakuomba utupe neema tuvitumie vipawa vyako vyote kwa heshima na utukufu wa jina lako takatifu; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

Thanksgivings

For good Crops

KWA BARAKA ZA MAVUNO

EWE Bwana Mwenyezi Mungu, Muumba, Baba wa wote, twakushukuru sana kwa mioyo yetu, kwa vile ulivyowaagizia wanadamu nyakati z~ kupanda na kuvuna, na kwa kutupa sasa mazao ya nchi kwa wakati wake. Jina lako tukufu twalisifu na kulitukuza kwa rehema zako hizi na nyingine zote nazo; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
 

For an abundant Harvest

KWA KUOKOKA WAKATI WA TAUNI AU WA UGONJWA

EWE Bwana Mungu, moyo wako haupendi kuwatesa wanadamu: twakushukuru sana kwa vile ulivyotuokoa kwa rehema zako katika ugonjwa na mashaka, nasi kwa mioyo ya shukrani twataka kukutolea, ewe Baba mwema, nafsi zetu, roho na miili, tuwe kwako sadaka iliyo hai, siku zote tukusifu na kutukuza huruma zako katika Kanisa lako; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Watu wakitaka kutoa shukrani kwa rehema nyingine, itatosha kusema, Na tumshukuru Mwenyezi Mungu (kwa jinsi kadhawakadha), kisha watu wawe kimya kitambo kidogo. Ndipo husema,

    Padre. Mshukuruni Yehova kwa kuwa yu mwema :
    Huitika. Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Zikiisha Sala na Shukrani kisomwe kimoja katika vikomo hivi, navyo vyaweza kutumiwa baada ya Sala ya Tatu katika Sala ya Jioni.

KWA Mungu Baba aliyetupenda na kutukirimu katika huyo Mpenzi:
    Kwa Mungu Mwana, aliyetupenda na kutufungua katika dhambi zetu kwa damu yake:
    Kwa Mungu Roho Mtakatifu, amiminaye mapenzi ya Mungu katika mioyo yetu:
    Mungu wa pekee wa kweli na apewe mapenzi yote na utukufu wote sasa na hata milele. Amina.

Au hiki,

MUNGU aliye Mwenyezi, Mwenye rehema, atubarikie na kutulinda usiku huu na hata milele. Amina.

Tunza kwamba isipokuwa Bishopu kuagiza vingine, baada ya mwisho wa Sala ya Asubuhi, au Sala ya Jioni, au ya Taratibu nyingine ya Ibada, Padre aweza, akiona ni vizuri, kusali kwa maneno yake mwenyewe.

For deliverance from a Time of Plague or Famine

 

Return to the 1662 Book of Common Prayer in Swahili

Web author: Charles Wohlers U. S. EnglandScotlandIrelandWalesCanadaWorld