LITANIA
¶ Hapa yaletwa LITANIA, au Matangamano ya Sala, hutumiwa katika mwisho wa Sala ya Asubuhi, kwa siku za Jumapili na Jumatano na Ijumaa, na nyakati nyingine atakazoona vyema yule Mwenye amri; nayo huimbwa au husomwa.
EWE Mungu Baba, wa mbinguni: uturehemu maskini wenye dhambi.
Ewe Mungu Baba, wa mbinguni: uturehemu maskini wenye dhambi.
Ewe Mungu Mwana, Mkombozi wa ulimwengu: uturehemu maskini wenye dhambi.
Ewe Mungu Mwana, Mkombozi wa ulimwengu: uturehemu maskini wenye dhambi.
Ewe Mungu Roho Mtakatifu, utokaye kwa Baba na kwa Mwana: uturehemu maskini wenye dhambi.
Ewe Mungu Roho Mtakatifu, utokaye kwa Baba na kwa Mwana: uturehemu maskini wenye dhambi.
Ewe Utatu, Mtakatifu, Mwenye-baraka, Mtukufu, Nafsi tatu, Mungu mmoja: uturehemu maskini wenye dhambi.
Ewe Utatu, Mtakatifu, Mzonye-baraka, Mtukufu, Nafsi tatu, Mungu mmoja: uturehemu maskini wenye dhambi.
Usikumbuke makosa yetu, Bwana, wala makosa ya baba zetu; wala usitwae kisasi cha dhambi zetu: utusamehe, Bwana mwema, utusamehe watu wako, uliowakomboa kwa damu yako ya thamani, wala usitukasirikie milele.
Utusamehe, Bwana mwema.
Uovu wote na madhara yote; dhambi, na hila, na majaribu ya Shetani; hasira zako, na kuhukumiwa adhabu ya milele,
Bwana mwema, utuokoe nayo.
Upofu wa moyo kila aina: kunyeta, na kujiona, na unafiki; uhasidi, na uchukivu, na mfundo wa moyo, na upungufu wa mapenzi kila aina,
Bwana mwema, utuokoe nayo.
Uzinifu, na dhambi za mauti nyingine kila aina; na hila zote za dunia, na mwili, na Shetani,
Bwana mwema, utuokoe nayo.
Radi na tufani; baa, na tauni, na njaa; vita na uuaji, na mauti ya ghafula,
Bwana mwema, utuokoe nayo.
Fitina, na shauri la uasi, na uhalifu kila aina; elimu ya uwongo, na uzuzi, na matengano kila aina; uzito wa moyo, na kudharau Neno lako na Maagizo yako,
Bwana mwema, utuokoe nayo.
Nawe kwa siri ya Ulivyo twaa mwili; na kwa Kuzaliwa kwako kutakatifu na Kutahiriwa kwako; kwa huo Ubatizo wako, na hivyo Ulivyofunga, Ukajaribiwa,
Bwana mwema, utuokoe.
Kwa hiyo Dhiki iliyokupata na hizo Hari zako za damu; kwa Msalaba wako na Mateso yako; kwa Mauti yako ya thamani na Kuzikwa kwako; kwa Kufufuka kwako kutukufu na Kupaa kwako; na kwa Roho Mtakatifu kutujia,
Bwana mwema, utuokoe.
Kila tusumbuliwapo, na kila tufanikiwapo; saa ya kufa, na siku ya hukumu,
Bwana mwema, utuokoe.
Sisi wenye dhambi twakuomba sana utusikize, Ewe Bwana Mungu wetu; kisha uone vyema kuliamuru na kulitawala kanisa lako takatifu lililo ulimwenguni mote liishike njia iliyolekea;
Twakuomba utusikize, Bwana mwema.
Uwe radhi kumweka na kumtia imara katika ibada yako iliyo kweli, na katika maisha yaliyolekea na kutakata, Mtumishi wako GEORGE, Mfalme wetu mwenye fadhili nyingi, Mtawala wetu ;
Twakuomba utusikize, Bwana mwema.
Uwe radhi kumtawala moyo wake kwa imani yako, na kicho chako, na mapenzi yako, naye siku zote aendelee kukutumaini wewe, atafute na heshima yako na utukufu wako kwa mambo yote;
Twakuomba utusikize, Bwana mwema.
Uwe radhi wewe kuwa Mteteaji wake, na ulinzi wake, kwa kumpa kushinda adui zake wote;
Twakuomba utusikize, Bwana mwema.
Uwe radhi kuwabarikia na kuwahifadhi mkewe Mfalme wetu, Bibi Elizabeth mwenye fadhili, na Bibi Mary mamaake Mfalme, na Princess Elizabeth, na jamaa wote wa Ufalme;
Twakuomba utusikize, Bwana mwema.
Uwe radhi, kuwafikiliza neema yako Wakubwa wa nchi hii, na walio na amri wote, ili waupate ufalme wako wa mbinguni;
Twakuomba utusikize, Bwana mwema.
Uwe radhi, hao mabishopu wote, na makasisi wote, na mashemasi wote; kuwapa mwanga wa kweli ulio na maarifa na fahamu ya Neno lako, walifunue na kuliweka wazi, huku kwa kuhubiri na huku kwa kuishi ;
Twakuomba utusikize, Bwana mwema.
|
|
(Uwe radhi kuwabarikia watumishi wako watakaokubaliwa sasa kuwa Nyakati nne za mashemasi na makasisi, uwamiminie neema yako, ili watimize kazi yao kwa kujenga kamsa lako, na kwa kutukuza jina lako takatifu;
Twakuomba utusikize,Bwana mwema.)
Uwe radhi, hao wazee wa Baraza ya Mfalme na jamii ya Makabaila, kuwavika fadhili, na hekima, na fahamu;
Twakuomba utusikize, Bwana mwema.
Uwe radhi, hao Wenye-amri kuwabarikia na kuwalinda, kwa kuwapa neema ya kupisha hukumu kwa haki na kuitetea ile kweli;
Twakuomba utusikize, Bwana mwema.
Uwe radhi, watu wako wote, kuwabarikia na kuwalinda; Twakuomba utusikize, Bwana mwema.
Uwe radhi mataifa yote, kuwapa umoja, na amani, na masikizano;
Twakuomba utusikize, Bwana mwema.
Uwe radhi, kutupa sisi mioyo ya kukupenda na kukucha, na kufanya bidii kuyanyosha maisha yetu kama maagizo yako;
Twakuomba utusikize, Bwana mwema.
Uwe radhi, watu wako pia wote, kuwapa maongeo ya neema, ili wawe wenye kulisikiza Neno lako kwa unyenyekevu, na kulipokea kwa mapenzi yaliyo safi, na kuzaa matunda ya Roho;
Twakuomba utusikize, Bwana mwema.
Uwe radhi, kadiri ya waliokosa, wenye kudanganyika, kuwatia katika njia ya kweli;
Twakuomba utusikize, Bwana mwema.
Uwe radhi, hao waliosimama kuwapa nguvu; na wenye mioyo dhaifu kuwatia imara na kuwasaidia; na walioanguka kuwainua ; hata mwishowe kumpomosha Shetani chini ya miguu yetu ;
Twakuomba utusikize, Bwana mwema.
Uwe radhi, walio katika hatari, na uhitaji, na masumbuko, kuwatunza na kuwasaidia na kuwatuza mioyo, pia wote;
Twakuomba utusikize, Bwana mwema.
Uwe radhi, watu wote wasafiri o bara na bahari, na wanawake wenye uchungu, na watu wauguao, na watoto wakuao, kuwalinda wote; na wafungwa wote na mateka wote kuwafikiliza huruma zako;
Twakuomba utusikize, Bwana mwema.
Uwe radhi, watoto mayatima na wanawake wa1iofiliwa na waume, na wote walio hali ya ukiwa na kuonewa, watu hao kuwahifadhi na kuwaruzuku;
Twakuomba utusikize, Bwana mwema.
Uwe radhi kuwarehemu watu wote;
Twakuomba utusikize, Bwana mwema.
Uwe radhi, adui zetu, na watesi wetu, na watu watuambao kwa uovu, kuwasamehe, na kuwalekeza mioyo yao katika njia;
Twakuomba utusikize, Bwana mwema.
Uwe radhi, kutupa matunda ya nchi kwa aina zake na kutuhifadhia, tupate kuyatumia na kuyafurahia kwa zamani zake;
Twakuomba utusikize, Bwana mwema.
Uwe radhi, kutupa sisi toba ya kweli; nawe utusamehe madhambi yetu yote, na ulegevu wetu wote, na ujinga wetu wote; nawe utuvike neema ya Roho wako Mtakatifu, tuyafanyize maisha yetu kama Neno lako takatifu;
Twakuomba utusikize, Bwana mwema.
Mwana wa Mungu; twakuomba utusikize.
Mwana wa Mungu; twakuomba utusikize.
Ewe Mwana-wa-kondoo wa Mwenyezi Mungu, mwenye kuziondoa dhambi za ulimwengu;
Utupe amani yako.
Ewe Mwana-wa-kondoo wa Mwenyezi Mungu, mwenye kuziondoa dhambi za ulimwengu;
Uturehemu.
|
Kutumiwa katika majuma ya Nyakati nne za mwaka; na siku ya watu kupewa daraja la kanisa kwa kuwekewa mikono. |
BABAETU uliye mbinguni, Jina lako litakaswe, Ufalme wako na uje. Mapenzi yako yatendeke juu ya nchi, Kama yatendekavyo mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kututosha. Nawe utusamehe makosa yetu, Kama nasi tulivyowasamehe watukosao. Nawe usitupeleke katika kujaribiwa; Utuokoe maovuni. Amina.
Padre. Ewe Bwana, usitutwae kama makosa yetu.
Huitika. Wala usitupatilize kwa viovu vyetu.
Na tuombe.
EWE Mwenyezi Mungu, Baba mwingi wa rehema, huyadharau mauguzi ya moyo uliovunjika, wala kutamani kwao walio na majonzi; uzikubali kwa rehema sala zetu tukuleteazo mbele zako kwa mashaka yetu yote na ukiwa wetu wote, kila yatulemeapo; utusikize kwa neema, ili hivyo viovu, tutengezewavyo na hila na werevu wa Shetani au binadamu, vitanguke, viondolewe; navyo kwa uangalizi wa wema wako vitawanyike; ili kwamba sisi watumishi wako tusidhurike kwa masumbuko yawayo yote, twendelee katika kukushukuru wewe daima katika kanisa lako takatifu, kwa Yesu Kristo, Bwana wetu.
Ewe Bwana, inuka, utusaidie; utuponye kwa ajili ya jina lako.
Ewe Mwenyezi Mungu, sisi tumesikia kwa masikio yetu, baba zetu wametuwekea wazi mambo makuu uliyofanya kwa siku zao, na zamani za kale mbele yao.
Ewe Bwana, inuka, utusaidie, utuponye kwa ajili ya heshima yako.
Utukufu uwe kwa Baba, na kwa Mwana: na kwa Roho Mtakatifu;
Huitika. Kama vile mwanzo, na sasa: hata milele ni vivyo. Amina.
Utukinge na adui zetu, Ewe Kristo.
Uyaangalie kwa fadhili' yako mateso yetu.
Uyatazame majonzi ya mioyo yetu kwa huruma.
Uya samehe makosa ya watu wako kwa rehema.
Uzisikize sala zetu, uzikubali pamoja na kuturehemu.
Ewe Mwana wa Daudi, uturehemu.
Hivi sasa na zamani zote ukubali kutusikiza, Ewe Kristo.
Utusikize kwa fadhili yako, Ewe Kristo ; utusikize kwa fadhili yako, Ewe Bwana Kristo.
Padre. Ewe Bwana, rehema zako na zionekane kwetu;
Huitika. Kwa vile tunavyokutumaini wewe.
Na tuombe.
EWE Baba, tu miguuni pako, twakuomba sana uurehemu udhaifu wetu; nawe kwa ajili ya utukufu wa jina lako, utupishie mbali maovu hayo yote tuliyo stahili kwa haki mno; tena utukirimu ya kwamba, kila tukipatikana na mashaka tulitie tumaini letu lote na mategemeo yetu yote katika rehema zako, na kwendelea daima katika kukutumikia kwa maisha safi na utakatifu, kwa kukuletea heshima na utukufu: kwa Mwombezi wetu, Msaada wetu, Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
|
Lord's Prayer |