The Book of Common Prayer
United States England Scotland Ireland Wales Canada World

    Chuo cha Sala ya Umoja (1662)
The 1662 Book of Common Prayer in Swahili

 

TARATIBU YA KUSONGEZA KARAMU YA BWANA; AU, USHIRIKA MTAKATIFU

Kadiri ya walio na azima ya kushirikiana Ushirika Mtakatifu na wampe majina yule Padre kabla ya jambo hilo, uchache ni usiku wa kuamkia siku ya kushirikiana.

Na watu hao akionekana kwao mtu mwenye makosa yaliyo wazi, au aliyedhilimu mwenziwe kwa maneno au kwa vitendo, ikawa ni sababu ya kulichukiza Kanisa; yule Padre akiisha kupata hakika ya neno lile, humwita yule mtu akamwonya asisubutu kabisa kukaribia Meza ya Bwana, hata aishe kutoa dalili zilizo dhahiri za kutubia kwake kweli, na za ule mwendo wake mbaya kugeuka ukawa mwema; ili kwamba wapate kuridhika tena wale ambao mbele walichukiwa katika Kanisa, kisha na wale aliowadhilimu nao awape haki zao ; au uchache ni kutoa ahadi ya kuwapa haki zao, atakapokwisha kupata nafasi.

Ni vivyo hivyo, na watu atakaowaona wa hali ya kukaliana kwa mfundo wa moyo na kuchukizana wenyewe kwa wenyewe, yule Padre huwatwaa kwa jinsi iyo hiyo; asiwakubalie Ushirika wa Meza ya Bwana, hata awaone wansha kupatana. Na wale waliofanya tofauti akikubali yule mmoja kumsamehe mwenziwe kwa moyo ulio safi kadiri ya aliyomkosa, na kufanya malipo, kwa kuwa naye alimchukiza mwenziwe, akawa yule wa pili hataki kuridhia umoja wa uchaji-zoa-Mungu, yuadumu hali ile ile ya upotofu na uchuhisi; hapo imempasa Padre kumpa ruhusa yule mwenye kutubia ya kuuingia Ushirika Mtakatifu, akamkataza yule mshupavu. Isipokuwa kila awapo Padre kumsukumiza mtu kama ilivyoelezwa katika maagizo haya katika upambanuzi huu, au huo uliotangulia, yamlazimu kumwarifu habari yake yule Mwenye Amri kabla ya siku kumi na nne wala asizidi siku kumi na nne. Na yule Mwenye Amri humtenda yule aliye na makosa kama yaliyoagizwa katika Kanuni.

Ile Meza ili hali imetandikwa nguo njema nyeupe ya katani, kwa kila zamani ya kushirikiana Ushirika, hukaa katikati ya Msikiti au katika Mwimbwamo, pale palipoagizwa kusaliwa Sala za Asubuhi na Jioni. Na yule Kasisi ali hali amesimama pale penye Meza ya Bwana upande wa Kaskazini wa Meza, husema Sala ya Bwana, pamoja na Sala hiyo ifuatanayo baadaye, wale watu wakiisha kupiga magoti.
 

The Order of the Administration of the Lord's Supper, or
Holy Communion

BABAETU uliye mbinguni, Jina lako litakaswe, Ufalme wako na uje. Mapenzi yako yatendeke juu ya nchi, Kama yatendekavyo mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kututosha. Nawe utusamehe makosa yetu, Kama nasi tulivyowasamehe watukosao. Nawe usitupeleke katika kujaribiwa, Utuokoe maovuni. Amina.

Sala.
 

Lord's Prayer

EWE Mwenyezi Mungu, kwako wewe mioyo ya watu wote i wazi, na kila haja imejulikana, wala hakuna neno lililofichamana kwako; uyasafi mawazo ya mioyo yetu kwa kutuvuvilia Roho wako Mtakatifu, ili tukupende wewe kwa ukamilifu, tulitukuze na jina lako takatifu kama ipasavyo; kwa Kristo Bwana wetu. Amina.

Ndipo hapo yule Kasisi huwalekea wale watu, na kuwatajia Amri kumi zote kwa sauti ya kusikilikana ; na mwisho wa kila Amri wale watu, wali hali ile ile ya kupiga magoti, humtaka Mwenyezi Mungu msamaha wa hizo walizozivunja katika zamani zilizopita, wakaomba na neema wapate kuzishika mbeleni, wasije wakazivunja tena kama vile; waseme namna hii:
 

Collect for Purity

Kasisi.

MWENYEZI Mungu alinena maneno haya, huku akisema, Mimi ni Yehova Mwenyezi Mungu wako. Usiwe na miungu mingine mbele zangu yoyote.
    Watu. Bwana, uturehemu, nawe utulekeze mioyo yetu iishike amri hii.
    Kasisi. Usifanye sanamu wa kuchonga, umbo lolote lililo juu mbinguni, au lililo chini duniani, au lililo chini ya dunia katika maji: usivisujudie, wala kuvitumikia: kwa kuwa mimi Yehova Mungu wako ni Mungu mwenye wivu, niwapatilizaye wana kwa uovu wa baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao; na kuwapa rehema watu elfu elfu wanipendao, wayashikao maagizo yangu.
    Watu. Bwana, uturehemu, nawe utulekeze mioyo yetu iishike amri hii.
    Kasisi. Usitaje jina la Yehova Mungu wako kwa upuzi, kwani Yehova hatamfanya kuwa hana makosa mtu atajaye jina lake kwa upuzi.
    Watu. Bwana, uturehemu, nawe utulekeze mioyo yetu iishike amri hii.
    Kasisi. Ikumbuke siku ya sabatu kuitakasa. Siku sita tumika, ufanye kazi zako zote; ila siku ya saba ndiyo sabatu ya Yehova Mungu wako; siku hiyo usifanye kazi, wewe, wala mwanayo mume na mke; wala mtumwayo mume na mke; wala nyama zako za mji; wala mgeni wako aliye ndani ya malango yako; maana, kwa siku sita Yehova alifanya mbingu na nchi, na bahari, na vyote vilivyo humo, akapumzika kwa siku ya saba; ndipo akaibarikia Yehova ile siku ya sabatu, akaitakasa.
    Watu. Bwana, uturehemu, nawe utulekeze mioyo yetu iishike amri hii.
    Kasisi. Mheshimu babaako na mamaako, siku zako zifanyike ndefu juu ya nchi upewayo na Yehova Mungu wako.
    Watu. Bwana, uturehemu, nawe utulekeze mioyo yetu iishike amri hii.
    Kasisi. Usiue.
    Watu. Bwana, uturehemu, nawe utulekeze mioyo yetu iishike amri hii.
    Kasisi. Usizini.
    Watu. Bwana, uturehemu, nawe utulekeze mioyo yetu iishike amri hii.
    Kasisi. Usiibe.
    Watu. Bwana, uturehemu, nawe utulekeze mioyo yetu iishike amri hii.
    Kasisi. Usimshuhudie mwenzio kwa uwongo.
    Watu. Bwana, uturehemu, nawe utulekeze mioyo yetu iishike amri hii.
    Kasisi. Usitamani nyumba ya mwenzio, usimtamani mke wa mwenzio; wala mtumwawe mume au mke; wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala kiwacho chote alicho nacho mwenzio.
    Watu. Bwana, uturehemu, nawe uziandike mioyoni mwetu amri zako hizi pia zote, sisi twakuomba sana.
 

Ten Commandments

Iko ruhusa kutosoma Amri kumi, isipokuwa zisomwe (kwa uchache) mara moja kila mwezi siku ya Jumapili; kisha wakati wa kutozisoma, mafupizo ya sheria yaliyotolewa na Bwana wetu yasomwe badala yake:

    Kasisi. Bwana wetu Yesu Kristo alisema: Sikiza, Isiraeli; Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; nawe mpende Bwana Mungu wako katika moyo wako wote, na nafsi yako yote, na nia yako yote, na nguvu zako zote. Hilo ni agizo la kwanza. La pili ni mfano wake, nalo ni hili: Mpende mwenzio kama nafsi yako. Hakuna jingine tena katika maagizo lililo kubwa zaidi ya haya. Katika maagizo mawili hayo imetundamana torati yote na manabii wote.
    Watu. Bwana, uturehemu, nawe utulekeze mioyo yetu iishike amri hii.

Optional section in place of the Ten Commandments

 
Hapa hufuata moja ya Sala mbili hizi za kumwombea Mfalme, yule Kasisi ali amesimama kama vile, husema:

Na tuombe.

EWE Mwenyezi Mungu, ufalme wako hauna mwisho, uwezo wako hauna upungufu; ulirehemu kanisa lako pia lote; nawe uutawale sana sana moyo wa mtumishi wako mteule wako GEORGE, Mfalme wetu, Mtawala wetu, hata yeye (kwa kumjua ni nani huyo amtumikiaye), mbele ya yote atafute kwanza mambo ya heshima yako wewe na utukufu wako wewe: na sisi na raia zake wote (kwa kule kufikiri kwetu ni nani aliyempa amri hiyo aliyo nayo), tuwe wenye kumtumikia kwa uaminifu, na kumheshimu na kumtii kwa unyenyekevu, katika wewe na kwa ajili yako, sawasawa na Neno lako na Maagizo yako mema ; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu, aishiye na kutawala daima pamoja na wewe na Roho Mtakatifu, Mungu mmoja, milele. Amina.

Au hii,

EWE Mwenyezi Mungu, Mkazi wa milele, sisi hujifunza katika Neno lako takatifu ya kuwa mioyo ya wafalme i mkononi mwako, nawe huigeuza na kuiongoza kama uonavyo vyema kwa hekima yako ya Uungu; sisi hapa tulipo miguuni pako, twakuomba kwa ajili ya Mfalme wetu, Mtawala wetu, GEORGE, mtumishi wako, ya kwamba wewe uugeuze na kuuongoza moyo wake sana, katika mawazo yake, na maneno yake, na vitendo vyake pia vyote, hata awe katika kuitafuta daima heshima yako wewe na utukufu wako; afanye bidii kuwatunza hao watu wako uliowatia mkononi mwake, apate kuwaweka hali ya nafuu na amani na uchaji-wa-Mungu: na haya twakuomba, ewe Baba mwenye huruma, kwa ajili ya Mwanayo, Mpenzi wako, Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Ndipo hapo husomwa Sala ya siku hiyo. Nayo ikiisha kusomwa hiyo Sala, yule Padre husoma Waraka, akisema, Waraka (au, Fungu la Maandikoni lililoagizwa badala ya Waraka) umeandikwa katika Mlango kadhawakadha wa Waraka kadha, mwanzo Kifungo kadha. Nao ukiisha kusomwa ule Waraka, husema, Waraka umekoma hapa. Ndipo hapo huisoma Injili (watu huinuka na kusimama wote) akisema, Injili takatifu imeandikwa katika Mlango kadhawakadha wa Injili kadha, mwanzo Kifungo kadha. Nayo ikiisha kusomwa ile Injili huimbwa au husomwa Imani hii ifuatanayo, watu wakali wamesimama kama vile.
 

 

 

Prayer for the King

NAAMINI kwa Mwenyezi Mungu mmoja, Baba Mweza wa yote, Muumba mbingu na nchi, Na vitu vyote, vionekanavyo na visivyoonekana:
    Tena kwa Bwana mmoja Yesu Kristo, Mwana wa Mungu Mzaliwa pekee, Mwenye kuzaliwa na Babaye kabla ya zamani zote, Mungu katika Mungu, Nuru katika Nuru, Mungu kweli katika Mungu kweli, Mwenye kuzaliwa wala si mwenye kuumbwa, Tabia yake ya asili na hiyo ya Baba ni mamoja, Tena kwa yeye vitu vyote viliumbwa: Naye kwa ajili yetu wanadamu na wokofu wetu alishuka kutoka mbinguni, Akafanyizwa mwili na Roho Mtakatifu kwa Mwanamwali Mariamu, Akafanywa binadamu, Naye akasalibiwa kwa ajili yetu katika enzi ya Pontio Pilato. Akateswa, akazikwa, Hata siku ya tatu akasimama tena, kama alivyoandikiwa katika Maandiko, Kisha akapaa akaingia mbinguni, Naye ameketi upande wa kuumeni wa Baba. Kisha atarudi na utukufu awaamue walio hai hata waliokufa: Na ufalme wake hauna mwisho.
    Tena naamini kwa Roho Mtakatifu, Bwana, Mpaji wa uzima, Atokaye mwa Baba na Mwana, Naye pamoja na Baba na Mwana ni mwenye kuabudiwa na kutukuzwa kama vile, Naye ndiye aliyesema kwa vinywa vya manabii. Tena naamini kanisa moja lililo ulimwenguni mote, kama lilivyowekwa na mitume. Ninakiri ubatizo mmoja wa kusamehewa madhambi, Nami nangojea wafu kufufuka, na maisha ya ulimwengu ujao. Amina.

Kisha yule Padre huwaeleza wale watu mna Siku kuu gani au Siku za kufunga gani katika juma hilo lijalo, ambazo zataka kushikwa. Kisha pawapo na sababu huwapa habari ya siku ya Ushirika; tena husomwa hati za maana, na notisi, na za kuzuiliwa waliokosa. Wala lisitangazwe neno wala kuhubiriwa humo msikitini katika muda wa Ibada ya Mungu, isipokuwa kwa kinywa cha yule Padre: wala yeye naye asitangaze wala kuhubiri neno ila ambalo limeamriwa katika Kanuni za Chuo hiki, au lililoagizwa na Mfalme, au na Mwenye Amri ya Ibada aliye na pahali hapo.

Hapa hufuata Hotuba, au Mauidha yoyote katika hayo yaliyokwisha kuandaliwa, au yatakayoandaliwa huko mbeleni, kwa amri ya wakubwa.

Kisha yule Kasisi hurudi pale penye Meza ya Bwana, na kuyaanziliza Matoleo ya Sadaka, kwa kutamka Aya hizi, moja au zaidi, zifuatanazo hapa, kama aonavyo kufaa sana moyoni mwake.
 

Nicene Creed

NA mwanga wenu ung'are vivyo mbele ya watu, hata wazione kazi zenu nzuri, wamtukuze na Babaenu aliye mbinguni.   Mathayo 5.16.
    Msiweke hazina zenu za akiba juu ya nchi, napo ndipo nondo na kutu viharibupo, na wevi hutoboa na kuiba; ila hazina zenu za akiba ziwekeni mbinguni, pasipoharibika kitu kwa nondo wala kutu, na wevi hawatoboi wala hawaibi.   Mathayo 6. 19-20.
    Basi na mambo yote kadiri myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni kadhalika. Kwani hiyo ndiyo torati na manabii.   Mathayo 7. 12.
    Si kila mmoja aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia ndani ya ufalme wa mbingu: lakini ni afanyaye mapenzi ya Babaangu aliye mbinguni.   Mathayo 7. 21.
    Akasimama Zakayo akamwambia Bwana, Hivi ndivyo, Bwana, nusu ya vitu vyangu nawapa maskini, nami kwamba nimemnyang'anya mtu kwa njia ya hila katika neno lolote, namrudishia mara nne.   Luka 19. 8.
    Ni askari yupi atumikaye majira yoyote kwa gharama zake mwenyewe? ni nani atuliaye kiunga cha mizabibu, naye asile matunda yake? au ni nani alishaye kundi la nyama, naye asinywe maziwa ya kundi?   1 Wakorintho 9. 7.
    Ikiwa sisi tuliwapandia ninyi vitu vya rohoni, je, ni neno kubwa kwamba tutavuna vitu vyenu vya mwilini?   1 Wakorintho 9. 11.
    Je, hamjui ya kwamba hao watumikao katika mambo ya hekalu, hula vitu vya hekaluni, na hao watumikiao madhabahu wana sehemu yao pamoja na hayo madhabahu? Ni vivyo hivyo, Bwana aliagiza kwamba hao waitangazao ile habari njema watapata kuishi katika hiyo habari njema.   1 Wakorintho 9. 13-14.
    Apandaye kwa choyo naye huvuna vya choyo. Apandaye kwa ukarimu, naye huvuna vya ukarimu. Kila mtu na afanye kama alivyoazimia moyoni mwake, si kwa kinyongo wala kwa lazima, kwani Mwenyezi Mungu yuampenda mtu apaye kwa kufurahi.   2 Wakorintho 9. 6-7.
    Ila yeye afunzwaye lile neno, na afanye ushirika na huyo afunzaye katika vitu vyema vyote. Msidanganyike, Mungu hafanyiwi dhihaka: kwani binadamu hicho apandacho, atakuja kuvuna hicho.   Wagalatia 6. 6-7.
    Basi hivi, kama tutakavyokuwa na nafasi, na tuwafanyie vyema watu wote, hasa hao jamaa wenye kuamini.   Wagalatia 6. 10.
    Ila uchaji-wa-Mungu pamoja na moyo uliokinai ni pato kuu: kwani hatukuingia na kitu ndani ya ulimwengu, kwa kuwa hata kutoka na kitu hatuwezi.   1 Timotheo 6. 6-7.
    Uwaagize hao walio matajiri katika zamani hizi za sasa, kwamba watende mema, wawe matajiri kwa kazi nzuri, wawe wapaji-wa-vitu, na wenye kufanya ushirika na wengine kwa moyo; huku wakiziwekea akiba nafsi zao msingi mzuri hata wakati ujao, ili kwamba waushike uhai huo ambao ndio uhai halisi.   1 Timotheo 6. 17-19.
    Kwani Mwenyezi Mungu hana batili hata akaisahau. kazi yenu, na mapenzi yenu mliyoyaonya ya jina lake, kwa kuwatumikia kwenu watakatifu, nanyi mwawatumikia.   Wahibirania 6. 10.
    Ila msisahau kutenda mema na kushirikiana, kwani dhabihu namna hizi Mwenyezi Mungu huzifurahia.   Wahibirania 13. 16.
    Ila yeye aliye na vitu-vipasavyo-maisha ya dunia hii, kisha akamwona nduguye ni mwenye kuhitaji, naye akazifunga huruma zake zisimfikilie, hayo mapenzi ya Mwenyezi Mungu yakaaje ndani yake huyo?   1 Yohana 3.17.
    Wewe toa katika ulivyo navyo, usimgeuzie uso wako maskini awaye yote. Kwani ufanyapo hivyo utauona uso wa Bwana haugeuzwi kwako wewe.   Tobiti 4. 7.
    Uwe mwenye huruma kwa jinsi upatavyo. Utakapokuwa na kingi, toa kwa wingi; utakapokuwa na kidogo, katika hicho kidogo wewe fanya bidii kumpasha mwenzio kwa ukarimu. Kwani kwa haya utaweka akiba njema; utakuwa nayo kwa siku ya uhitaji.   Tobiti 4. 8.
    Mwenye kumhurumia maskini yuamkopesha Yehova, naye atamlipa hicho kitendo chake chema tena.   Mifano ya Maneno 19. 17.
    Yu heri amkumbukaye maskini; Yehova atamwokoa siku ya taabu.   Zaburi 41. 1.

Muda zisomwapo aya hizi, wale mashemasi, au wale walinzi wa msikiti, au mtu mwingine afaaye mwenye kuweka kwa ajili ya hayo, huzipokea katika kile kitasa kiwekwacho kwa haja hiyo na waabuduo mle msikitini sadaka za kupewa maskini, na vingine vitakavyotolewa na wale watu kwa ajili ya Ibada: wakiisha kumpelekea yule Kasisi kwa namna ya ibada, naye hukisongeza kile kitasa kwa unyenyekevu na kukiweka juu ya Meza takatifu.

Na pawapo na Ushirika, yule Kasisi huweka juu ya Meza Mkate na Divai kadiri ya aonavyo kutosha kwa haja ile. Hata yakiisha kufanywa hayo, yule Kasisi hunena,

    Na tuiombee hali yake Kanisa la Kristo lililo katika vita hapa duniani.
 
Offertory sentences

EWE Mwenyezi Mungu uishiye milele, wewe umetufunza kwa mtume wako mtakatifu kuwafanyia sala na maombi na shukrani watu wote; sisi tu miguuni pako twataka kwako kwa ajili ya rehema zako nyingi (*uzipokee sadaka zetu na matoleo yetu, nawe hizi) sala zetu tunazotoa kwako, ewe Mungu Mfalme wetu, uzikubali; huku tukikuomba wewe kulivuvia daima kanisa lako lililo ulimwenguni mote roho ya kweli na umoja na kupatana: nawe utupe ya kwamba wote walikubalio jina lako takatifu wapatane katika kweli ya Neno lako takatifu, na kuishi kwa umoja na mapendano ya uchaji-wa-Mungu. Tena, twataka kwako uwaokoe na kuwalinda wafalme wa Kikristo na maseyidi na wenyeenzi pia wote; na sana twamwombea mtumishi wako GEORGE Mfalme wetu; tupate kutawaliwa chini yake kwa haki na utulivu; nawe uwape washauri wake wote, na waliopewa amri chini yake, kila mmoja, ya wao kuamua kwa kweli pasipo kufanya upendeleo, huku kwa kuadhibu uovu na shari, na huku kwa kuitunza dini yako ya kweli na mambo yaliyo mema. Uwape neema, ewe Baba wa mbinguni, mabishopu wote na watunzao roho za wenziwao, ili kwamba wao, kwa maisha yao na mafunzo yao walifunue wazi Neno lako la kweli na uhai, na Sakramenti zako takatifu wazisongeze kama taratibu yake kwa haki. Na watu wako wote uwape neema yako ya mbinguni; na sana mkutano huu uliopo hapa; ili kwamba, kwa mioyo ya kunyenyekea na ibada iliyo sawa, walisikize Neno lako takatifu, na kulipokea wakikutumikia wewe kwa utakatifu na haki siku zote waishizo duniani. Na sana twataka kwako, kwa kunyenyekea sana, kwa ajili ya wema wako, ewe Bwana, uwatulize na kuwasaidia wote ambao kwamba katika maisha haya yasiyo dumu wamepatikana na mashaka, huzuni, uhitaji, ugonjwa, au baa nyingine iwayo yote. Kisha na jina lako takatifu twalishukuru kwa asante, kwa ajili ya watumishi wako wote waliofariki dunia katika imani yako na kicho chako: huku tukitaka kwako utupe nasi neema, tupate kufuata sana vie1elezo vyao vizuri, hata iwe sisi pamoja na wao kuurithi ufalme wako wa mbinguni: utupe haya, ewe Baba, kwa ajili ya Yesu Kristo, aliyekaa pweke Mwombezi wetu kati yetu sisi na wewe. Amina.

Wakati aitangazapo habari yule Padre, ni siku gani utakaosongezwa Ushirika Mtakatifu (naye hufanya hivi siku zote kwa siku ya Jumapili au siku mojawapo katika Siku kuu za ibada iliyo mbele ya siku hiyo, kwa karibu), baada ya kwisha kuhubiri, husoma Masisitizo haya yafuatanayo hapa.
 

Prayer for the whole state of Christ's Chruch

* Na pasipotozwa sadaka wala matoleo ndipo maneno haya (uzipokee sadaka zetu na matoleo yetu) yatarukizwa.

ENYI wapenzi, kwa siku ya . . . ijayo mimi nakusudia kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, kuwasongezea hao wote watakaokuwa na nia ya uchaji-wa-Mungu na ibada, Sakramenti hiyo yenye kutuliza itiayo nguvu sana ya Mwili na Damu ya Kristo; ipate kupokewa na wao kwa kuukumbuka Msalaba wake na Mateso yake yaliyo na mafaa mengi; ambayo kwa hayo peke yake sisi twapata msamaha wa madhambi yetu, na kufanywa kuwa washirika wa Ufalme wa mbingu. Basi kwa ajili ya hayo imetupasa kumpa Mwenyezi Mungu Babaetu wa mbinguni shukrani zilizo nyenyekevu sana, za ndani sana, kwa alivyotupa Mwanawe Mwokozi wetu Yesu Kristo, naye si kwamba apate kufa tu kwa ajili yetu, ila na apate kuwa ni chakula cha roho zetu cha kututia nguvu kwa hiyo Sakramenti takatifu. Nalo neno hilo la Mwenyezi Mungu likiwa lawatia nguvu na utulivu hao walipokeao kama ifaavyo kulipokea, lina na hatari mno kwa wasubutuo kulipokea ili hali hawafai kulipokea; mimi lililonipasa sana ni kuwaonya ninyi na' mapema, muwe katika kuifikiri siri hii takatifu jinsi ilivyotukuka, na ilivyo na hatari itakapopokewa na watu ambao hawafai; na jinsi mtakavyoyapeleleza na kuyapima yaliyo katika mioyo yenu (si juujuu kama wanafiki kwa Mungu); mpate kuijilia karamu ya ki-mbinguni namna hiyo kwa hali takatifu na usafi, mli hali mmeyavaa mavao ya arusi hayo ambayo yalilazimishwa na Mwenyezi Mungu katika Maandiko matakatifu, ili mpate kukaribishwa kama wenye kufaa kushirikiana katika Meza hiyo takatifu.
    Njia yake basi, jinsi yake, itupayo kuyapata mambo hayo, ni hivi: Kwanza, mpeleleze katika maisha yenu na mazungumzo yenu kwa kuyalinganisha na Maagizo ya Mwenyezi Mungu; na katika hayo mjionayo wenyewe mmekosa mumo, kwa kupenda, au kunena, au kutenda, mlilie mambo yenu yalivyo na dhambi, na kuungama kwa Mwenyezi Mungu, kama wenye kukusudia sana kuyarejeza maisha yenu hali mpya. Nanyi mtakapoyaona makosa yenu kuwa hamkumkosa Mwenyezi Mungu tu, mmewakosa na wenzenu, ndipo hapo mtajipatanisha nao; mridhie kurejeza na kulipa, kwa hali na mali, kadiri ya mtakavyoweza, katika kila mlilomtenda mwenzenu awaye yote la madhara au batili; mridhie na kuwasamehe wenzenu nao waliowakosa ninyi, kama vile wenyewe mpendavyo mpate kwa Mwenyezi Mungu naye msamaha wa makosa yenu; kwani msipokaa hali hiyo, kule kushirikiana Ushirika Mtakatifu hakutawafaa neno, mtazidi kuwa hali ya kupasa mapigo. Basi pakiwa pana mtu kwenu atukanaye Mungu, au aliye mzuizi au mwenye kupinga Neno lake; ni mzinifu, au yuna mfundo, au husuda, au aliyetenda neno jingine la hatari lolote, ninyi mlio hivi tubieni kwa madhambi yenu, au msiikaribie Meza ile takatifu; msije mkaingiwa na Ibilisi ndani yenu baada ya kwisha kuitwaa ile Sakramenti takatifu, kama alivyoingiwa Yudasi, akawajaza ninyi Ibilisi maovu kila jinsi, akawatia katika uangamivu wa roho pamoja na wa mwili.
    Na kwa kuwa haifai mtu kuingia katika Ushirika Mtakatifu ila awapo anazitumaini kabisa rehema za Mwenyezi Mungu, yuna na moyo uliotulia; ni hivyo, akipatikana mtu kwenu, moyo wake hakupata kuutuliza kwa jinsi hiyo, ajijua ni mhitaji wa kupewa faraja, au yuataka shauri, mtu huyo na aje kwangu au kwa mwingine mtumishi wa Neno lake Mwenyezi Mungu aliye na busara na elimu ya utakatifu, akayaseme yaliyomtia majonzi; ili kwamba kwa kusongezewa Neno takatifu la Mwenyezi Mungu ayapokee mtu huyo manufaa ya ondoleo la dhambi, apewe na mashauri ya ki-rohoni, aambiwe na maneno ya kumwonya njia, atulie moyo wake, na kuondoa kila shida na tashwishi.

Au, awaonapo kwamba hawana bidii ya kuja kwa Ushirika Mtakatifu, badala ya yale hutumia masisitizo haya:

NDUGU zangu niwapendao mno, kwa siku ya . . . ijayo mimi kwa fadhili za Mwenyezi Mungu nakusudia kuifanya Karamu ya Bwana: basi ninyi nyote mliopo hapa nawaalika mje katika karamu hiyo; kisha kwa ajili ya Bwana Yesu Kristo nawaomba mwito huu msiukatae, nanyi awaalikaye na kuwaita ni Mwenyezi Mungu mwenyewe, kwa kule kuwapenda kwake sana. Au wenyewe hamwoni jinsi lilivyo neno ovu na ubaya, aandaapo binadamu karamu ya vyakula vyema kwa gharama nyingi, akaandika na meza ya vinono, asisaze lolote ila la kuwakaribisha awaitao, nao wakakataa pasipokuwa na sababu, wasimtolee hata asante! Hata ninyi mkitokewa na neno kama hili, asiyekasirika ni nani? Ni nani asiyefikiri, Mimi nimeonewa, mimi nimedhilimiwa? Basi ninyi nanyi, wapenzi sana sana katika Kristo, jilindeni wenyewe msije mkamtia hasira Mwenyezi Mungu juu yenu mtakapo kujitenga na hii karamu yake iliyo takatifu sana. Ni upesi kusema mtu, Neno hili la Ushirika mimi siingii, maana nimeshikwa na udhuru mimi, nimezuiwa na mambo ya ulimwengu. Lakini je! kwa Mwenyezi Mungu udhuru kama huo nao utakubaliwa kuwa ni neno la maana? Au mtu akisema, Mimi nina dhambi sana; jinsi nilivyo mwenye dhambi mimi, basi nacha: ndipo nami nisije. Ninyi mbona hamtaki kutubia? Wala hamzingatii? Hivyo mlivyoalikwa na Mungu, je, hamwoni haya kusema, Hatuji? Hivyo ilivyowapasa kurejea kwa Mwenyezi Mungu, mtatoa udhuru wa nafsi zenu mseme, Hatu tayari? Fikirini basi wenyewe kwa wenyewe, jinsi usivyofaa udhuru wa uwongo kama huo mbele za Mwenyezi Mungu! Wale waliokataa ile karamu ya Injili, wakasema, Tumenunua mashamba; au, Twataka kwenda kuangalia jozi zetu za ng'ombe; au, Tumeoa wake; hawakuachiliwa kuwa wana udhuru hivyo, walihesabiwa hawafai kamwe kuila karamu ile ya ki-mbinguni. Basi mimi langu sitawacha ; Mwenyezi Mungu akipenda, nitakuwapo tayari; nami kwa hayo niliyowekewa juu yangu ya utumishi huu nilio nao, nawaalika ninyi hivi sasa kwa jina lake Mwenyezi Mungu, nawaita kwa ajili ya Kristo, nawaonya kwa hivyo wenyewe mpendavyo kuokoka, mje mkashirikiane Ushirika Mtakatifu huu niwaalikao. Basi, kama vile Mwana wa Mungu alivyokubali kuutoa uhai wake kuutia katika kufa, alipoangikwa juu ya msalaba kwa kuutuma wokofu wenu, nanyi ni vivyo inawapasa kuupokea Ushirika huu nao kwa kuikumbuka sadaka ya mauti yake yule, huku mkiyafuata mwenyewe aliyowausia. Msipofanya hivi, fikirini wenyewe, jinsi mtakavyomtenda Mwenyezi Mungu ya jeuri, fikirini na adhabu yake ilivyo kali, itakayokuja ilewe-lewe juu ya vichwa vyenu, mkijiepua kusudi na hii Meza ya Bwana, na kujitenga na hawa ndugu zenu wajao kula Karamu hiyo ya Chakula, ambacho ni cha mbinguni halisi. Mambo haya mkiyawaza mioyoni kwa bidii, kwa neema ya Mwenyezi Mungu mtatubu na kurejea akili njema, nalo ni neno ambalo kwamba hatutawacha kuwaombea kwa kumnyenyekea Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye Babaetu wa mbinguni, m1ipate.

Wakati wa kusongezwa ule Ushirika, wale watu watakaoshirikiana wakiisha kukaa kama watakavyopata kusongezewa taratibu Sakramenti takatifu, yule Kasisi husoma maonyo haya:

ENYI wapenzi sana katika Bwana, ninyi mlio na nia ya kuja kuingia Ushirika Mtakatifu wa Mwili na Damu vyake Mwokozi wetu Kristo, inawapasa kufikiri jinsi mtakatifu Paulo awasisitizavyo watu wote kufanya bidii ya kuijaribu mioyo yao na kuipima, kwanza wasijasubutu kula katika Mkate ule na kunywa katika Kikombe kile. Kwani kama vile yalivyo mengi sana yale manufaa yake, iwapo tuna kweli ya moyo uliotubu, na imani iliyo hai, katika kuipokea Sakramenti hiyo takatifu, (kwani hapo ndipo tuulapo kwa jinsi ya rohoni ule Mwili wake Kristo, na kuinywa ile Damu yake; tukawa kukaa katika Kristo, Kristo akakaa ndani yetu; tukawa kitu kimoja na Kristo, na Kristo nasi:) basi na ile hatari nayo huwa nyingi vivyo, iwapo twaipokea siri hiyo kwa jinsi isivyofaa. Kwani hivyo itakuwa sisi kuwa wakosa katika Mwili na Damu vyake Kristo Mwokozi wetu: twaila na kuinywa hesabu ya hukumu yetu, kwa kule kutouona Mwili wake Bwana; twamkasirisha Mwenyezi Mungu; twamsongeza katika kutupiga kwa maradhi mengine mengine, na mauti namna namna. Basi, ndugu zangu, jihukumuni wenyewe msije" mkahukumiwa na yeye Bwana; tubieni sana wenyewe kwa madhambi yenu yaliyokwisha kupita; iweni na imani iliyo hai kwa Kristo Mwokozi wetu, isiyoweza kutukusika; tengezeni maisha yenu, muwe wenye kupendana na watu wote; ni hivyo mtakuwa watu mfaao kuwamo katika siri hizi zilizo takatifu. Na zaidi ya yote, juu ya yote, ninyi mmekuwa watu wa kumshukuru kwa kunyenyekea mno Mwenyezi Mungu, kwa mioyo yenu yote, Mungu Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, kwa vile alivyoukomboa ulimwengu kwa kufa kwake na kuteswa kwake yeye Mwokozi wetu Kristo, ambaye mwenyewe ni Mungu kisha ni Binadamu, aliyejifanya mdogo, hata ikawa yeye kuyakubali mauti ya Msalabani, kwa ajili yetu wenye dhambi wanyonge, tuliokuwa tumelala gizani katika uvuli wa mauti; ili kwamba apate kutufanya kuwa wana wa Mwenyezi Mungu, na kututukuza hata maisha yasiyokuwa na ukomo. Naye kwa vile alivyotaka tuyakumbuke daima yale mapenzi makuu ya Bwana wetu, Mwokozi wetu pekee, Yesu Kristo, alipokufa kwa ajili yetu, tusije tukayasahau popote manufaa yasiyohesabika aliyotupa kwa kutoa damu yake ya thamani; ameweka na kuanziza siri ambazo ni takatifu, ili ziwe dalili za mapenzi yake, na ukumbusho wa daima wa kufa kwake, kwa kutuvutia faraja na utulivu mkuu visivyokoma. Basi na tumpe yeye, pamoja na Baba na Roho Mtakatifu, kama ilivyotupasa sana, shukrani ya daima, kwa kujiweka wenyewe kabisa chini ya radhi yake na mapenzi yake matakatifu, tufanye na bidii kumtumikia kwa utakatifu na haki ya kweli siku zote za maisha yetu.

Ndipo hapo Kasisi huwaambia hao wausongeao Ushirika Mtakatifu maneno haya:
 

Exhortations

NINYI mtubiao kwa dhambi zenu kwa kweli, mlio na toba ya mioyoni, mu katika kupendana na kusameheana na wenzenu, mna na nia ya kuyafanya upya maisha yenu, kwa kuyafuata .maagizo ya Mwenyezi Mungu, kutaka kwenenda tokea sasa katika njia zake takatifu: songeeni hapa kwa imani mje mkaitwae Sakramenti takatifu hii, mpate kuituliza mioyo yenu; tena ungameni kwa Mwenyezi Mungu kwa kumnyenyekea, mpige magoti kwa upole.

Hapo wakaungamishwa na mmoja katika wale mapadre waliopo maungamo haya ya waliopo wote, kwa jina lao wote walio na nia ya kushirikiana katika Ushirika Mtakatifu; yule Padre husoma akipiga magoti, na waliopo wote nao hupiga magoti kwa kujitweza, waseme:
 

Invitation

EWE Mwenyezi Mungu uwezaye mambo yote, Wewe ndiwe Babaye Bwana wetu Yesu Kristo, nawe ndiwe Mtenzi mambo yote, Kisha ndiwe Mwamuzi wa watu wote: Sisi madhambi yetu na maovu yetu namna namna, Tu katika kuyaungama na kuyalilia, Tuliyokuwa tukiyatenda mara kwa mara, kwa njia ya mawazo, na maneno, na vitendo, kwa kukuchukiza mno mno, kwako wewe Mwenye Enzi ya Uungu, Huku tukikutia kasirani, na machungu ya haki. Sisi twatubia sana, Tumeona vibaya kwa kweli, Kwa ajili ya ukengeufu wetu huu; Mambo haya tuyakumbukapo yatuchukiza wenyewe; Mzigo wake hauchukuliki kamwe. Uturehemu, uturehemu, ewe Baba mwenye rehema nyingi; Kwa ajili ya Mwanayo Bwana wetu Yesu Kristo, utusamehe yote hayo yaliyopita; Utupe ya kwamba mwanzo wa sasa tuendelee siku zote, Katika kukutumikia na kukupendeza, Kwa upya wa maisha, Kwa kuliheshimu na kulitukuza jina lako; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Ndipo hapo asimamapo yule Kasisi, au husimama yule Bishopu akiwa yupo, hata akiisha kuwalekea wale watu akanena Ondoleo hili la madhambi.

MWENYEZI Mungu, Babaetu wa mbinguni, ambaye kwa wingi wa huruma zake amewapa ahadi ya msamaha wa madhambi wote hao wageukao kulekea kwake yeye kwa toba ya moyoni na imani ya kweli: awarehemu ninyi; awasamehe na madhambi yenu yote na kuwaokoa nayo; awakaze na kuwatia imara hata muutimize wema wote: awatie katika uzima wa milele; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Hapo yule Kasisi husema,
 

Confession & Absolution

SIKIZENI maneno yalivyo mazuri ya kumtuza mtu moyo Mwokozi wetu Kristo awaambiayo wote hao warejeao kweli kumlekea yeye.

    Njoni kwangu ninyi nyote mtaabikao kwa kazi nzito, mliolemelewa na mizigo, nami nitawapumzisha.   Mathayo 11. 28.
    Mwenyezi Mungu jinsi alivyoupenda ulimwengu, amewapa watu Mwanawe mzaliwa pekee, kila mwenye kuamini kwake asipotee, awe na uzima wa milele.   Yohana 3. 16.

    Sikizeni na aliyoyanena mtakatifu Paulo.
    Ni la kuaminiwa lilo neno, tena lapasa kila kukubaliwa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni kuwaokoa wenye dhambi.   1 Timotheo 1. 15.

    Sikizeni tena yaliyonenwa na mtakatifu Yohana.
    Na atakapofanya dhambi mmojawapo, tuna mwenye kutuombea kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki: naye ndiye dhabihu wa dhambi zetu.   1 Yohana 2.1-2.

Hata baadaye yule Kasisi huendelea kunena,

Ikuzeni mioyo yenu.

    Huitika. Twaikuza hata kwa Yehova.
    Kasisi. Na tumshukuru Bwana wetu, Mwenyezi Mungu.
    Huitika. Ndio wajibu wetu; ndiyo yanayopasa kama haya.

Ndipo hapo yule Kasisi huilekea Meza ya Bwana, na kunena,

NDIO wajibu wetu wa haki, ndiyo yanayotupasa sana, na kutulazimu; ya sisi kila wakati na kila pahali kusema asante kwako wewe Bwana, Baba Mtakatifu, Mwenye nguvu zote, Mwenyezi Mungu, usiye mwanzo wala mwisho.
 

Comfortable words

 

Maneno yale (Baba Mtakatifu) hurukizwa kwa Jumapili ya Utatu.
 

Hapo hufuata dibaji zilizohusika kwa zamani zake; ila siku nyingine zote huendelea na kusema,

KWA ajili ya hayo sisi nasi pamoja na malaika na malaika wakuu, na jeshi lote la mbinguni, tu katika kulisifu na kulikuza jina lako tukufu, huku tukikutukuza milele, twanena, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Yehova Mungu wa majeshi, mbingu na nchi zimejaa utukufu wako: utukufu uwe kwako, ewe Mwenyezi Mungu uliye juu. Amina.
 

 
 

DIBAJI ZILIZOHUSIKA

Kwa Siku ya Christmas, na siku saba ziandamazo baadaye

KWA vile ulivyo tupa Mwanayo Mzaliwa pekee Yesu Kristo akazaliwe kwa ajili yetu kama majira haya ya sasa; ambaye kwa ule utendaji wake Roho wako Mtakatifu, alifanyika binadamu halisi katika mwili wake yule mwanamwali Mariamu mamaye; asipatikane na kipaku cha dhambi kiwa cho chote, ili atusafi na dhambi zote: Kwa ajili ya hayo, sisi nasi, wa kadhalika.

Kwa Siku ya Ufufuo, na siku saba ziandamazo baadaye

ILA litupalo kukusifu sana, ni ile habari tukufu ya kufufuka kwake Mwanayo Bwana wetu Yesu Kristo; kwani ndiye Mwana-wa-kondoo wa Pasaka halisi, aliyetolewa kwa ajili yetu, akayaondoa makosa ya ulimwengu; ambaye kwa kufa kwake aliyaangamiza mauti, na kwa kufufuka kwake kurejea uhai aliturejezea uzima wa milele; Kwa ajili ya hayo, sisi nasi, w. k.

Kwa Siku ya Kupaa, na siku saba ziandamazo baadaye

KWA ajili ya Mwanayo umpendaye sana, naye ndiye Bwana wetu Yesu Kristo; ambaye baada ya ile habari tukufu ya kufufuka kwake, aliwatokea waziwazi mitume yake wote, akaonekana kwao ali hali yuapaa juu kwenda mbinguni, akaenda kutufanyia pahali pa kukaa ili kwamba huko akaako yeye na sisi tupae kwenda kuko, tuwe watu wa kukaa na kutawala pamoja naye katika utukufu; Kwa ajili ya hayo, sisi nasi, w. k.

Kwa Siku ya Pentecost, na siku sita ziandamazo baadaye

KWA ajili ya Yesu Kristo, Bwana wetu; ambaye Ilikuwa ni kwa ahadi yake ya kweli sana Roho Mtakatifu alivyotushukia kama wakati huu kutoka mbinguni, pamoja na kivumi kikuu kilichokuja ghafula, kama cha dharuba kuu ya upepo, yuna na mfano wa ndimi za miali ya moto, zilizotenga juu ya vichwa vyao wale wanafunzi, kwa kuwafunza na kuwaongoza katika kweli yote: akawapa vipawa vya lugha mbali-mbali, na vya ushujaa na bidii, ili wapate kwendelea kuwafunza mataifa wote, wafulize wasichoke; ikawa ndiyo sababu ya kututoa sisi nasi katika giza, kututia mwangani; kututoa katika upotevu, kututia katika kuijua njia; maana, aliye mwanga wako na njia yako ni yeye Mwanayo Yesu Kristo: Kwa ajili ya hayo, sisi nasi, w. k.

Kwa Idi ya Utatu; hiyo tu

AMBAYE u Mungu mmoja, Bwana mmoja; si kwamba u Nafsi moja iliyo pweke, ila u nafsi tatu nawe uli katika Tabia ya Asili moja. Kwani hayo tuliyoshika kuyaamini katika habari ya Utukufu wake Baba, ndiyo tuyaaminiyo katika Mwana naye, na katika Roho Mtakatifu, hatuyatilii tofauti wala upungufu: Kwa ajili ya hayo, sisi nasi, w. k.
 

Proper Prefaces

Dibaji hizi nyingine zifuatanazo hutumika kwa siku kadhawakadha akiona vyema yule Kasisi.

Kwa Idi ya Mafunuo, na siku saba ziandamazo baadaye

KWA Yesu Kristo, Bwana wetu: aliyefunua utukufu wake katika hali ya mwili wetu upatwao na mauti: apate kuwatoa watu wote katika giza na kuwaleta katika nuru yake ya ajabu. Kwa ajili ya hayo, sisi nasi, w. k.

Kwa Alhamisi iliyo kabla ya Ufufuo

KWA Yesu Kristo, Bwana wetu, aliyewapenda wao walio wake ulimwenguni, aliwapenda hata mwisho: naye usiku wa kuamkia kuteswa kwake, alipoketi kula chakula pamoja na wanafunzi wake, aliweka siri hizi takatifu: ili sisi tuliokombolewa kwa kufa kwake na kuhuishwa kwa kufufuka kwake, tuwe washirika wa tabia ya Uungu iliyo yake. Kwa ajili ya hayo, sisi nasi, w. k.

Kwa Siku za Kutakata kwake na Kupewa habari kwake mtakatifu Mariamu mwanamwali

KWA kuwa ulitupa Yesu Kristo Mwanayo wa pekee azaliwe kwa ajili ya wokofu wetu: naye alifanywa binadamu kweli katika mwili wa mwanamwali Mariamu mamaye, pasipo mawaa ya dhambi, atusafishe katika dhambi zote. Kwa ajili ya hayo, sisi nasi, w. k.

Kwa Siku ya Kugeuka Sura

KWA kuwa utukufu wako uliokuwa katika Neno lililofanyizwa mwili ulimulika katika mlima mtakatifu mbele ya mashahidi wa ukuu wake: na sauti yako mwenyewe kutoka mbinguni ilimtaja Mwanayo mpendwa. Kwa ajili ya hayo, sisi nasi, w. k.

Kwa Siku ya Watakatifu wote, na Siku za mitume, na Siku za wahubiri wa Injili, na Siku ya Kuzaliwa kwake mtakatifu Yohana mbatizaji, isipokuwa imeagizwa dibaji ya Siku nyingine

ULIYETUPA katika haki ya watakatifu wako mfano wa maisha mema, na katika hali yao iliyobarikiwa umetupa ahadi yenye utukufu ya tumaini la mwito wetu: ili sisi kwa kuwa tumezingirwa na wingu kubwa la mashahidi jinsi hii, tupige mbio kwa uvumilivu kwa yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu; nasi pamoja nao tupokee taji ya utukufu, isiyonyauka. Kwa ajili ya hayo, sisi nasi, w. k.

Dibaji iwezayo kutumiwa katika siku ya kuweka wakf msikiti

NAWE, ijapokuwa mbingu za mbingu hazikutoshi, na utukufu wako u katika ulimwengu wote: wakubali kumtakasa mwahali muwe mwa ibada yako, namo wawamiminia waaminifu wako vipawa vya neema. Kwa ajili ya hayo, sisi nasi, w. k.

Dibaji iwezayo kutumiwa Jumapili yoyote katika mwaka isiyo na dibaji yake

KWA Yesu Kristo, Bwana wetu; kwa kuwa yeye ndiye Kuhani mkuu wa kweli, aliyetuosha dhambi zetu kwa damu yake, na kutufanya kuwa ufalme na makuhani kwako wewe, Mungu wetu, Babaetu. Kwa ajili ya hayo, sisi nasi, w. k.

Na ikiisha dibaji hiyo, mara huimbwa au husomwa maneno yale,

KWA ajili ya hayo, sisi nasi pamoja na malaika na malaika wakuu, na jeshi lote la mbinguni, tu katika kulisifu na kulikuza jina lako tukufu; huku tukikutukuza milele, twanena, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Yehova Mungu wa majeshi, mbingu na nchi zimejaa utukufu wako; utukufu uwe kwako, ewe Mwenyezi Mungu uliye juu. Amina.

Ndipo hapo yule Kasisi hupiga magoti penye Meza ya Bwana, na kusema kwa jina la wote hao watakaoshirikiana Ushirika Mtakatifu maneno ya sala hii:
 

Addiotional, optional Proper Prefaces

HATUSUBUTU kuijilia Meza yako, ewe Bwana mwenye rehema, kwa kutumai haki yetu wenyewe, ila kwa kutumai rehema zako zilizozidi sana kwa wingi na ukuu. Hamstahili hata kuyazoa makombo yaliyo chini ya Meza yako. Lakini wewe ndiwe yeyule Bwana, nayo ndiyo sifa yako kuwa na rehema daima: basi utupe, ewe Bwana mwenye neema, jinsi tutakavyokula nyama ya Mwili wake Mwanayo Mpenzi wako Yesu Kristo, na kuinywa Damu yake, hata miili yetu iliyo na dhambi ipate kusafiwa kwa Mwili wake, na roho zetu kuoshwa kwa Damu yake iliyo ya thamani sana, tupate kukaa hivi sasa na mbeleni ndani yake yeye, naye akae ndani yetu. Amina.

Hata yule Kasisi akiisha kuvitengeza Mkate na Divai, hali amesimama mbele ya Meza takatifu, kwa jinsi atakavyozidi kuwa na wepesi na makini katika kuuvunja Mkate mbele ya wale watu, na kukitwaa Kikombe kukishika mikononi mwake, huisoma Sala hii, ya kuviweka kwa Mungu:
 

Prayer of Humble Access

EWE Mwenyezi Mungu, Babaetu wa mbinguni, ni kwa huruma za wema wako wewe ulivyotupa Mwanayo wa pekee Yesu Kristo hata akafa juu ya Msalaba kuwa ni ukombozi wetu; ndipo hapo naye kwa kuyatoa matoleo mamoja nayo ni nafsi yake iliyotolewa mara moja tu, akafanya dhabihu na matoleo na kafara, vilivyokamilika na kutimia na kutosha, kwa ajili ya makosa ya ulimwengu wote: naye akaweka, akatuusia sisi katika Injili yake takatifu kudumisha ukumbusho wa hayo mauti yake ya thamani, hata aje tena. Utusikize sisi tulio miguuni pako, ewe Baba mwenye huruma; nawe utukirimu ya kwamba, tuingiapo kuvipokea hivi ulivyoviumba, navyo ni Mkate huu na Divai hii, kama vile alivyoviweka Mwanayo Mwokozi wetu Yesu Kristo, kwa kukumbuka kuteswa kwake na kufa kwake; tuwe wenye kushirikiana Mwili wake na Damu yake vilivyobarikiwa sana; ambaye kwa usiku huo wa kusalitiwa kwake, *alitwaa Mkate; hata alipokwisha kushukuru †akauvunja, akawapa wanafunzi wake, akawaambia, Twaeni mle, ‡ni Mwili wangu huu utolewao kwa ajili yenu: fanyeni hivi kwa kunikumbuka· mimi. Ni kama vile na baada ya chakula §akakitwaa Kikombe; hata alipokwisha kushukuru, akawapa yuanena, Katika hiki nyweni nyote: ||kwani ni Damu yangu hii ya Agano Jipya, imwagwayo kwa ajili yenu ninyi na kwa watu wengi, kwa msamaha wa madhambi; fanyeni hivi, kila mnywapo, kwa kunikumbuka mimi. Amina.

Ndipo hapo yule Kasisi kwanza huutwaa Ushirika yeye mwenyewe namna zote mbili, akiisha huendelea kuwapa mabishopu nao, na makasisi, na mashemasi, kwa namna iyo hiyo, kila wakiwapo watu hao, na baadaye huwapa hao watu kwa taratibu ambayo ni njema, akiwatilia mikononi mwao hali wamepiga magoti kwa unyenyekevu. Na kila akimpa mtu ule Mkate, Padre husema,
 

Eucharistic Prayer

  * Hapo yule Kasisi huitwaa sahani na kuishika mkononi mwake.
  † Hapo huuvunja Mkate.
  ‡ Hapo huuweka mkono Mkate huo wote.
  § Hapo hutwaa na kile kikombe na kukishika mkononi mwake.
  || Hapo hukiweka mkono kila chombo (ama kikombe ama dumu), kilicho na Divai yoyote itakayowekwa kwa mambo ya ibada.

 

 

 

MWILI wa Bwana wetu Yesu Kristo, uliotolewa kwa ajili yako, na ukuweke salama mwili wako na roho yako hata uzima wa milele. Huu twaa uule, kwa kukumbuka alivyokufa Kristo kwa ajili yako; nawe lisha moyo wako kwake, uamini ukishukuru.

Na Padre awapaye watu kile Kikombe husema,

DAMU ya Bwana wetu Yesu Kristo, iliyomwagwa kwa ajili yako, na ikuweke salama mwili wako na roho yako hata uzima wa milele. Nywaa hii kwa kukumbuka Damu yake Kristo ilivyomwagwa kwa ajili yako, uwe na shukrani.

Na utakapokwisha Mkate au Divai katika vilivyowekwa kwa Mungu kabla wale waliopo hawajashirikiana wote, yule Kasisi huweka kwa Mungu Mkate zaidi na Divai zaidi kwa kufuata kawaida iliyoandikwa juu katika hayo: ukiwa uliokwisha ni ule Mkate huanza katika: Mwokozi wetu Kristo kwa usiku huo wa kusalitiwa kwake, w.k.: ama ikiwa ni Divai huanza kwa: Ni kama vile na baada ya chakula w.k. : kwa kwibarikisha vitu hivyo.

Wakiisha kushirikiana pia wote, hurudi yule Kasisi hata pale penye Meza ya Bwana, na kuviweka juu yake kwa unyenyekevu vile vilivyosalia katika zile asili za vitu zilizowekwa kwa Mungu, na kuvifinika kwa kitambaa chema cha katani.

Kisha ndipo hapo yule Kasisi huisoma Sala ya Bwana, wale watu nao wakinena nyuma yake.
 

Words of administration

BABAETU uliye mbinguni, Jina lako litakaswe, Ufalme wako na uje, Mapenzi. yako yatendeke juu ya nchi, Kama yatendekavyo mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kututosha, Nawe utusamehe makosa yetu, Kama nasi tulivyowasamehe watukosao, Nawe usitupeleke katika kujaribiwa, Utuokoe maovuni. Kwa kuwa ufalme, na nguvu, na utukufu, ni vyako milele. Amina.

Kisha baadaye husoma haya :

EWE Bwana, nawe ndiwe Babaetu wa mbinguni, sisi watumishi wako wanyenyekevu twatamani sana kwa wema wako wa Ubaba, uturehemu, nawe uipokee hii sadaka yetu ya sifa na shukrani; twakuomba hivi tulivyo miguuni pako utukirimu kwa ajili ya kustahili kwake na mauti yake Mwanayo Yesu Kristo, na kwa tulivyo na imani kwa Damu yake, sisi na kanisa lako lote tupate msamaha wa madhambi yetu, na manufaa mengine yote ya Kuteswa kwake. Nasi hapa twatoa nafsi zetu, twajisongeza wenyewe mbele zako, ewe Bwana, miili yetu pamoja na roho zetu, tupate kuwa sadaka iliyo na maana na utakatifu na uhai kwako wewe; nasi twakunyenyekea sana huku tukitaka kwako ya kwamba sisi sote tulioshirikiana Ushirika Mtakatifu huu tujawe na neema yako na baraka yako ya mbinguni. Basi na tungawa hatufai, kwa ajili ya madhambi yetu namna namna, kuku tolea sadaka iwayo yote, lakini hii sadaka yetu ya sasa twakuomba uipokee; maana, ndilo lililotupasa neno hilo, ndio utumishi wetu tulioagizwa ; nawe usihesabu kustahili kwetu, ila utusamehe kila ukengeufu wetu, kwa Yesu Kristo, Bwana wetu; ambaye wewe, pamoja naye, katika umoja wa Roho Mtakatifu, u katika kuheshimiwa na kutukuzwa milele kwake yeye, kwa utukufu wote na heshima yote, ewe Baba Mweza-wa-yote. Amina.

Au hii.

EWE Mwenyezi Mungu uishiye milele, twakushukuru kwa mioyo yetu yote, kwa hivyo ulivyotuneemesha sisi tuliokuja kupokea siri hizi takatifu kama ipasavyo, hata ukatulisha chakula cha roho cha Mwili na Damu yake M wanayo Mwokozi wetu Yesu Kristo vilivyo na thamani mno; ukatuthubutishia sisi kwa ajili ya hayo neema yako na wema wako; na kuwa tu viungo vya mwili wake halisi yeye Mwanayo, maana Mwili wake wa sirini, nacho ndicho kikao kilichobarikiwa cha wenye imani wote; tena ya kuwa tu warithi sisi wa ufalme wako wa milele, kwa njia ya kutumaini, kwa kustahili kwa kuteswa kwake na mauti yenye thamani ya Mwanayo Mpenzi wako. Basi twakuomba sana, ewe Baba wa mbinguni, hapa miguuni pako tulipo, utusaidie kwa neema yako, tupate kwendelea katika umoja huo mtakatifu, tutimize na kazi njema zote, kadiri ya ulizotutengezea tangu hapo, za kwendelea mbele ndani yake; kwa ajili ya Yesu Kristo, Bwana wetu, ambaye milele, pamoja na wewe na Roho Mtakatifu, yuna heshima na utukufu uliotimia. Amina.

Hapo husomwa au huimbwa,
 

Lord's Prayer

UTUKUFU una Mwenyezi Mungu aliye juu, duniani nako ni salama, na kwa binadamu ni ihisani.
    Twakusifu wewe, Twakuhimidi wewe, Twakuabudu wewe, Twakutukuza wewe, Twakushukuru wewe kwa ajili ya huo utukufu wako, Ewe Bwana Mwenyezi Mungu, Mfalme wa mbinguni, Mungu Baba Mweza-wa-yote.
    Ewe Bwana, Yesu Kristo Mwana mzaliwa pekeo; Bwana Mwenyezi Mungu, Mwana-wa-kondoo wa Mungu, Mwana wa Baba, Wewe uondoaye makosa ya ulimwengu, Uturehemu sisi. Wewe uondoaye makosa ya ulimwengu, Uturehemu sisi. Wewe uondoaye makosa ya ulimwengu, Upokee hii sala yetu. Wewe uliyekaa upande wa mkono wa kuume wa Mwenyezi Mungu Baba, Uturehemu sisi.
    Kwani ni wewe pekeo uliye mtakatifu; Ni wewe pekeo uliye Bwana; Ni wewe pekeo Kristo, pamoja na Roho Mtakatifu, uliyetukuka sana katika utukufu wa Mungu Baba. Amina.

Hapo yule Kasisi, ama yule Bishopu akiwa yupo, huwafumua wale watu kwa Baraka hii.

AMANI ya Mungu, ipitayo fahamu zilizo zote, na iwalinde mioyo yenu na nia zenu katika kumjua na kumpenda Mungu, na Bwana wetu, Yesu Kristo Mwanawe. Na baraka .ya Mungu Mweza-wa-yote, Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, iwe mwenu ikae kwenu daima. Amina.

Sala hizi zifuatazo husomwa baada ya kule kukusanya sadaka, kwa kila siku isiyokuwa na Ushirika huo, hutumiwa moja tu au zaidi; nazo hizo husomwa baada ya Sala za Sala ya Asubuhi au ya Jioni, kila pakiwa na haja, au baada ya Sala za Ushirika Mtakatifu au za Litania, kila atakapoona yafaa yule Kasisi.
 

Gloria

EWE Bwana, uturehemu, utusaidie humu katika kunyenyekea kwetu na kusali kwetu, nawe uilekeze njia yetu sisi watumishi wako, tupate kufikilia katika wokofu wa milele; ili kwamba na ungawa huu ulimwengu tuliomo ndani yake wawazungukia wenyewe na kuwapiga mno, lakini iwe sisi watu wako kulindwa humo daima, kwa msaada wa neema yako ufikiliao kwa upesi; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

EWE Bwana Mweza, Mungu usiye mwanzo wala mwisho, twakuomba utuneemeshe mioyo yetu pamoja na miili yetu, vipate kuongozwa hivyo na kutakaswa na kutawaliwa na wewe katika njia za sheria zako na vitendo vya mausio yako, ili kwa vile wewe utakavyotulinda duniani na milele, tuhifadhike miili yetu na roho zetu , kwa Bwana wetu, Mwokozi Yesu Kristo. Amina.

UTUTAKABALIE, twakuomba, ewe Mungu Mweza-wa-yote, ya kwamba maneno haya tuliyoyasikia leo kwa masikio yetu ya nje, yashikamanishwe sana kwa neema yako katika mioyo yetu ndani, hata yazae ndani yetu matunda ya maisha safi, kwa kuliletea jina lako heshima na utukufu; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

UTUONGOZE, ewe Bwana, Katika vitendo vyetu vyote kwa fadhili ya neema yako, utupeleke mbele mumo kwa msaada wako daima; ili kwa kazi zetu kuanzilizwa na kufulizwa na kutimilizwa ndani yako wewe, tulitukuze jina lako takatifu, na mwishowe tuyapate kwa rehema yako maisha ya milele; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

EWE, Mwenyezi Mungu, Mwanzo wa hekima zote ni wewe, huu uhitaji wetu wewe waufahamu mbele hatujaingia kukuomba, na ujinga wa kukuomba kwetu pia waujua; twakuomba uurehemu udhaifu wetu, nawe hayo tusiyosubutu kuyaomba kwako kwa kuwa hatustahili pamoja na tusiyoyajua kuyaomba kwa ajili ya utofu wetu wa macho, pia uwe radhi kutupa; kwa kustahili kwake Mwanayo Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

EWE Mungu Mweza-wa-yote, wewe umetupa ahadi ya kusikiza haja zao wote wakuombao kwa jina la Mwanayo ; twakuomba uyatege kwetu masikio yako, uturehemu sisi tuliokuja kukusongezea hivi sasa sala zetu na haja zetu; utupe ya kwamba tuyapate pasipo shaka hayo tuliyoyataka kwako kwa uaminifu kama mapenzi yako, ili hali ya uhitaji wetu isaidiwe, na utukufu wako utangae; kwa ajili ya Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Kwa kila siku ya Jumapili au ya Idi iwayo yote, usiposongezwa ule Ushirika, husomwa yote hayo yaliyoagizwa kusomwa kwa zamani za Ushirika, hata iishe Sala ya Kuwaombea Watu Wote (Na tuiombee hali yake Kanisa la Kristo lililo katika vita hapa duniani), pamoja na Sala hizi za sasa zinazotangulizwa hapa, moja tu au zaidi : na mwisho atie ile Baraka.

Wala haisongezwi Karamu ya Bwana ila hapo wapatikanapo watu ambao watosha hesabu yao kushirikiana katika Ushirika pamoja na yule Kasisi, kama mwenyewe aonavyo.

Na watu wangawa hawakuzidi ishirini hesabu yao katika mipaka ya msikiti, ambao wafaa kushirikiana Ushirika, na haya yote usifanyike Ushirika, ila wapatikanapo wanne, au uchache ni watatu wasipungue, watakaoshirikiana Ushirika huo pamoja na yule Kasisi.

Na katika misikiti mikuu iliyo na viti vya Ubishopu, na misikiti ya jamaa : namo ni mwahali mwenye makasisi wengi na mashemasi wengi: hupokea Ushirika pia wote kila Jumapili wasipungue, pamoja na yule Kasisi, ila washikwapo na uhuru wa kuwaachisha.

Na kwa kuepua kila huja iwezayo kuleta mashindano au ibada isiyopasa, kwa mtu awaye yote, katika habari ya ule Mkate au ya ile Divai, hutosha kwa huja yake ukiwa Mkate namna yake ni kama huo uliwao siku zote: lakini na uwe katika wema wa mikate ya nganu, utakaopatikana kwa wepesi.

Na kikisalia chochote katika Mkate na Divai, nacho hakikuwekwa kwa Mungu, yule Padre hukichukua na kukitumia yeye: lakini kitakaposalia chochote katika hicho kilichowekwa kwa Mungu, na kisichukuliwe hata nje ya msikiti, ila mara baada ya kuisema Baraka, yule Kasisi na wengine katika wale walioshirikiana Ushirika, ambao kwamba atawaita waje kwake, watakuwa wao kula na kunywa kwa ustahivu vile vilivyosalia.

Mkate na Divai vya Ushirika hulazimishwa Padre na Walinzi wa msikiti, kwa gharama za watu wa mipaka ya msikiti.

Kisha tunza! kila mtu wa humo mipakani, huingia Ushirika Mtakatifu mwaka kwa mara tatu asipungue na katika Ushirika huo mara tatu hizo, ya Idi ya Ufufuo asikosekane. Na mwaka hata mwaka katika zamani za Idi ya Ufufuo, kila mmoja wale waketio humfanyia hesabu Padre, au mtu mmoja (au zaidi) awa,ye yote, aliye badala yake yule (au badala yao wale): amlipe yule (au awalipe wale) maada yote ya kanisani, ambayo hulipwa majira hayo na zamani hizo.

Baada ya kwisha Ibada ya Mwenyezi Mungu, ile fedha iliyotolewa kupewa Mwenyezi Mungu hapo katika kukusanya sadaka, huitumia yule Padre na wale Walinzi kwa gharama za haja za uchaji-wa-Mungu na kuwafaa maskini, kama watakavyoona vyema wao wenyewe: ila wakiwa hawapatani wao kwa wao, katika jambo hili, na itumiwe kama atakavyoagiza Mwenye Amri kuu.
 

Collects
KWA ajili ya vile ilivyoamriwa katika kawaida hii ya kuisongeza Ibada ya Karamu ya Bwana, ya kila mwenye kuwamo katika Ushirika huo kuupokea kwa kupiga magoti yake (nayo ni amri iliyo na maana mazuri, kwa kuwa yaonyesha jinsi tulivyoyakiri sisi, kwa unyenyekevu na asante nyingi, yale manufaa yake Kristo wapewayo humo wote washirikianao kama ilivyopasa, na kwa ajili ya kujitenga na mambo ya maasia na fujo katika kushirikiana kwetu Ushirika, ambayo yamkini kuingia kwamba si amri kama hii); lakini pamoja na haya, asije mtu akavidhania mengine, akavitusha hivyo tupigavyo magoti sisi, ama ni mtu aliye mjinga au mnyonge, ama ni fitina au pingamizi; basi, na ijulikane ya kuwa katika neno hili la kupiga magoti, hamna ibada, wala haifai kuwamo ibada, iwayo yote, ya Mkate wake ile Sakramenti au Divai yake, vipokewavyo humo kwa kitu chake hivyo: wala ibada ya Mwili na Damu vyake Kristo vya asili, vitakavyodhaniwa na mtu kupatikana humo kwa jinsi ya mwili. Kwani ule Mkate na ile Divai vya Sakramenti hiyo, vikali vinakaa mumo kila kimoja kina tabia yake ya asili, hiyo tu: basi hivyo imekuwa ibada yake haijuzu (kwani ingekuwa ni kuabudu sanamu, nayo ni machukizo kwa Wakristo wote walio waaminifu): nasi twavijua Mwili wake na Damu yake Mwokozi wetu Kristo vi mbinguni, havipo tena hapa chini: kwani imepingamana na kweli ya hali yake Mwili wake Kristo wa asili, utakapoambiwa ni wa kupatikana, wakati huo mmoja, katika mwahali mwingi.
"Black" Rubric

 

Return to the 1662 Book of Common Prayer in Swahili

Web author: Charles Wohlers U. S. EnglandScotlandIrelandWalesCanadaWorld