TARATIBU YA SALA YA JIONI YA KILA SIKU MWAKA MZIMA
¶ Mwanzo wa Sala ya Jioni yule Padre husoma kwa sauti kuu aya moja au zaidi ya Maandiko Matakatifu katika hizo zilizowekwa : kisha hunena yafuatanayo na aya hizo.
MTU mbaya atakapotubu na kuuacha huo ubaya wake alioufanya, akayafanya yaliyo halali na haki, ataiponya nafsi yake awe hai. Ezekieli 18. 27
Ninakiri mimi makosa yangu, na dhambi yangu i mbele yangu daima. Zaburi 51. 3
Ufiche uso wako, usitazame dhambi zangu, uzifute hatia zangu zote. Zaburi 51. 9
Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika : moyo uliovunjika na kupondeka, ewe Mungu, hutaudharau. Zaburi 51. 17
Rarueni mioyo yenu, msirarue mavao yenu, nanyi rejeeni kwa Yehova Mungu wenu : kwa kuwa yeye ni mwenye neema na huruma : si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema: naye hujutia lile shari. Yoeli 2. 13
Ni ya Yehova Mungu wetu huruma na msamaha, kwani mmemwasi, wala hatukusikiza sauti ya Yehova Mungu wetu kwa kwenenda katika sheria yake aliyotuwekea mbele yetu. Danieli 9. 9-10
Ewe Yehova, nirudi, ila kwa haki, si kwa hasira, usije ukanidhili. Yeremia 10.24
Tubuni, kwani ufalme wa mbingu umekwisha kukaribia. Mathayo 3. 2
Nitaondoka, niende kwa baba, nikamwambie, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele zako; sistahili tena kuitwa mwanayo. Luka 15. 18-19
Ewe Yehova, usimhukumu mtumishi wako; kwani mbele zako hakuna aliye hai atakayehesabiwa kuwa ni mwenye haki. Zaburi 143. 2
Ikiwa twanena ya kwamba hatuna dhambi, twapoteza nafsi zetu, na hiyo kweli haimo ndani yetu. Ila ikiwa twaziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu kisha yuna haki akatusamehe dhambi zetu na kutusafi na uovu wote. 1 Yohana 1. 8-9
|
Ni roho Mwenyezi Mungu; nao wenye kumwabudu imewapasa kuabudu katika roho na kweli. Yohana 4. 24
Mwabuduni Yehova kwa uzuri wa utakatifu; tetemekeni mbele zake, nchi yote. Zaburi 96. 9
Usiku umekwendelea sana, mchana umekaribia: basi na tuzivulie mbali zile kazi za giza, na kujivisha silaha za mwanga. Warumi 13.12
Uzazi wa Bwana wetu, au Christmas
Ninawahubirini habari nzuri za furaha nyingi zitakazokuwa ni za wenyeji wote; kwani leo amezaliwa kwa ajili yenu katika mji wa Daudi, Mwokozi, naye ni Kristo Bwana. Luka 2. 10-11
Katika neno hili hayo mapenzi ya Mwenyezi Mungu yamefanywa wazi ndani yetu sisi, ya kwamba Mwenyezi Mungu amemtuma Mwanawe mzaliwa pekee aingie duniani, ili kwamba tupate kuwa hai kwa yeye. 1 Yohana 4. 9
Mafunuo
Tokea kucha kwake jua hata kutua kwake lilo, jina langu ni kuu katika watu wa hao mataifa; tena kila pahali uvumba wasongezwa katika jina langu, na dhabihu iliyo safi: kwa kuwa jina langu ni kuu katika watu wa hao mataifa, asema Yehova wa majeshi. Malaki 1. 11
Yehova ameujulisha wokofu wake; machoni pa mataifa amedhihirisha haki yake. Zaburi 98.2
Mateso
Angalieni, mwone kwamba pana majonzi mengine yawayo yote yaliyo mfano wa majonzi niliyo nayo mimi, hayo niliyotendewa. Maomboleo 1. 12
Ijumaa Njema
Mwenyezi Mungu ayadhihirisha kwetu mapenzi yake mwenyewe aliyotupenda, kwa maana, tulipokuwa tukali wenye dhambi, Kristo akafa kwa ajili yetu. Warumi 5.8
Siku iliyo kabla ya Ufufuo
Ukae kimya mbele za Yehova, ukamngojee wala usikasirike; naye atakupa haja za moyo wako. Zaburi 37. 7, 4
Ufufuo
Na ashukuriwe Mwenyezi Mungu Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye katika rehema zake kuu, ametuzaa sisi mara ya pili kwa njia ya kufufuliwa kwake Yesu Kristo. 1 Petero 1. 3
Siku ya Kupaa
Kwa kuwa tuna kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu Mwana wa Mwenyezi Mungu, na tukiendee hicho kiti-cha-neema kwa uthubutifu, ili kwamba tupate rehema na kuona neema ya kutusaidia wakati wa haja. Wahibirania 4. 14, 16
Pentecost
Mapenzi ya Mwenyezi Mungu yamekwisha kumiminwa na kutiwa ndani ya mioyo yetu na Roho Mtakatifu ambaye tumepewa sisi. Warumi 5. 5
Utatu
Mwenyezi Mungu ni mapenzi; na yeye akaaye katika mapenzi yuakaa ndani ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu yuakaa ndani yake yeye. 1 Yohana 4. 16
Watakatifu Wote
Kwa kuwa tumezingirwa na wingu kubwa la mashahidi jansi hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na hiyo dhambi iliyotuzunguka sisi kwa wepesi, na tupige mbio kwa uvumilivu kwa yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu, tukimtazama Yesu, mwenye kuanziliza na mwenye kutimiliza imani yetu. Wahibirania 12. 1-2
Siku za Watakatifu
Mwenye haki atakumbukwa milele. Kuwakumbuka hao wenye haki huwa na baraka. Zaburi 112. 6; Mifano 10. 7
Mwaka Mpya
Hao wamngojeao Yehova watarejeza upya nguvu zao; watakwea juu kwa mabawa mfano wa kipungu; watapiga mbio, wasichoke; watakwenda kwa miguu, nao hawatazima roho. Isaya 40.31
Mavuno
Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Yehova. Zaburi 24. 1
Wakati wa Mashaka
Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu: msaada uonekanao wakati wa mateso. Zaburi 46. 1
Mambo ya Ufalme
Mataifa wafurahi na kuimba kwa furaha: kwani wewe utawahukumu watu kwa haki, utawaongoza watu walioko duniani. Zaburi 67. 4
|
The following introductory sentences are additions, and are optional. |
ENYI ndugu zangu mpendwao sana, twaonyeshwa katika Maandiko mwahali kadhawakadha, ya kukiri na kuyaungama madhambi yetu na viovu vyetu Kila namna; pasipo kuvificha wala kuvifinika mbele ya uso wa Mwenyezi Mungu Babaetu wa mbinguni: twaonyeshwa ya kuviungama kwa moyo wa unyonge na unyenyekevu, wenye kutubia na kufuata; ili kwamba kwa wema wake na rehema zake zisizo ukomo, tupate kusamehewa. Nasi ingawa kule kumwekea wazi Mwenyezi Mungu madhambi yetu kwa unyenyekevu ni neno litupasalo sana kila wakati; ni zaidi sana wakati tukutanapo wenyewe kwa wenyewe, kuja kumshukuru kwa rehema kuu tulizopokea mikononi mwake, na kumsifu kama ilivyopasa sana, na kusikiza Neno lake lililo takatifu, na kumtaka kadiri ya tulivyo na haja navyo, rohoni hata mwilini. Basi, kwa ajili ya hayo, mimi nawasihi ninyi nyote mliopo, mfuatane nami kwa mioyo myeupe, na sauti nyenyekevu, tuje tukaribie katika kiti cha neema ya mbinguni, mseme nyuma yangu ;
|
Invitation to Confession |
¶ Hapa Padre aweza kusema maneno kama haya, akiona ni vizuri ;
TUKIWA tumepiga magoti, na tukae kimya kwa dakika chache, tukikumbuka ya kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi hapa.
|
A shorter, optional invitation to Confession |
¶ Haya ni maneno ya watu pia wote, ya kuungama makosa, nayo husemwa na watu wote nyuma yake yule Padre, hali wamepiga magoti pia wote.
EWE Baba, Mwenyezi, Mwingi wa rehema; Sisi nimekosa, Tumepotea njia zako, kama kondoo waliopotea. Tumefuata mno mashauri na tamaa za mioyo yetu wenyewe. Tumekosa sheria zako takatifu. Yaliyopasa kuyafanya hatukuyafanya, Tumefanya yasiyotupasa kuyafanya: Wala hatuna salama ndani yetu wenyewe. Ila wewe, Bwana, uturehemu, sisi wakosaji dhaifu: Ewe Mungu, uwasamehe wenye kuyaungama makosa yao. Uwakubali waliotubia : Kama ahadi zako walizofunuliwa wanadamu katika Kristo Yesu, Bwana wetu. Kisha, Baba mwingi wa rehema, Utupe kwa ajili yake yeye; Ya sisi kuishi tangu leo maisha ya uchaji-wa-Mungu na haki na mambo ya kiasi, Kwa kulitukuza jina lako lililo safi. Amina.
¶ Ghofira, au Ondoleo la madhambi: nalo hutamkwa na Kasisi pekee, hali amesimama, watu wakali wamepiga magoti.
MWENYEZI Mungu, Babaye Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye hataki mauti ya mwenye dhambi, afadhali ataka auache uovu wake awe hai: naye amewapa amri watumishi wake, amewaagiza, ya kuwaeleza na kuwaambia watu wake walio tubia, ya wao kusamehewa na kuondolewa madhambi yao: yeye huwasamehe na kuwaondolea madhambi wote waliotubu kweli, walioamini Injili yake takatifu pasipo kuitilia shaka. Kwa ajili ya hayo na tumwombe atupe toba ya kweli, atupe na Roho wake Mtakatifu, ili tuyafanyayo hivi sasa yampendeze ; na maisha yetu ya tangu sasa yawe safi na utakatifu, ili mwisho tufikilie katika furaha zake za milele; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu.
¶ Hapa na kila pahomapo Sala watu huitika, Amina.
¶ Kisha Padre hupiga magoti na kuisoma Sala ya Bwana kwa sauti ya kusikilikana : na watu nao hali wamepiga magoti, husoma pamoja naye: kwa wakati huo, na kila itumiwapo katika Ibada ya Mwenyezi Mungu.
|
Confession & Absolution |
BABAETU uliye mbinguni, Jina lako litakaswe, Ufalme wako na uje. Mapenzi yako yatendeke juu ya nchi, Kama yatendekavyo mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kututosha. Nawe utusamehe makosa yetu, Kama nasi tulivyowasamehe watukosao. Nawe usitupeleke katika kujaribiwa; Utuokoe maovuni: Kwa kuwa ufalme, na nguvu, na utukufu, ni vyako milele. Amina.
¶ Kisha husoma,
Ewe Bwana, ufunue midomo yetu.
Huitika. Na vinywa vyetu vitatangaza utukufu wako.
Padre. Ewe Mungu, utuokoe upesi.
Huitika. Ewe Bwana, utusaidie haraka.
¶ Wakati huo watu wakiisha kusimama wote, Padre husoma,
Utukufu uwe kwa Baba, na kwa Mwana: na kwa Roho Mtakatifu ;
Huitika. Kama vile mwanzo, na sasa: hata milele ni vivyo. Amina.
Padre. Msifuni Bwana.
Huitika. Jina la Bwana lisifiwe.
¶ Hapa husomwa au kuimbwa Zaburi, kwa taratibu yake kama ilivyoagizwa. Kisha husomwa Somo la Agano la Kale kama ilivyoagizwa. Na baada ya hayo, huwa Magnificat (au Wimbo wa Mwanamwali Mariamu Mbarikiwa), kama ulivyoletwa hapa.
MAGNIFICAT
Luka 1. 46-55
MOYO wangu wamtukuza Bwana : na roho yangu imemfurahia Mungu Mwokozi wangu.
Kwa kuwa ameuangalia : unyonge wa kijakazi chake.
Kwani tazama, mwanzo wa sasa : watanitaja kwa wema vizazi vyote.
Kwa kuwa Mwenye-nguvu amenifanyia mambo makuu : na Jina lake ni takatifu.
Tena rehema zake hufikilia vizazi na vizazi : kwa hao wenye kumcha.
Amefanya ubora kwa mkono wake : amewatawanya wenye unyeti katika mawazo ya mioyo yao.
Wenye kutawala amewashusha katika viti vyao vya enzi : tena amewatukuza wanyonge.
Wenye njaa amewajazia tele vitu vyema : na matajiri amewaondoa utupu.
Amemsaidia Isiraeli mtumishi wake, apate kuwakumbukia rehema : kama alivyosema na baba zetu, Iburahimu na uzao wake, milele.
Utukufu uwe kwa Baba, na kwa Mwana, na kwa Roho Mtakatifu ;
Kama vile mwanzo, na sasa : hata milele ni vivyo. Amina.
¶ Au, badala yake ni Zaburi hii: isipokuwa Mwezi Kumi na Kenda, husomwa hii katika Zaburi, kama zifuatanauyo daima.
|
Lord's Prayer |
CANTATE DOMINO
Zaburi 98
MWIMBIENI Yehova wimbo mpya : kwani amefanya mambo ya ajabu.
Mkono wa kuume wake yeye : mkono wake mtakatifu umemtendea wokofu.
Yehova ametamburisha wokofu wake : machoni mwa hao mataifa ameifanya wazi haki yake.
Amekumbuka ihisani yake na uaminifu wake : kwa nyumba ya Isiraeli.
Ncha zote za nchi zimeuona : wokofu wa Mungu wetu.
Mshangilieni Yehova, nchi nzima yote : inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi.
Mwimbieni Yehova za kinanda : kwa kinanda na sauti ya zaburi.
Kwa tarumbeta na baragumu : shangilieni mbele za Mfalme Yehova,
Bahari na ititime na vilivyojaa humo : ulimwengu na wauketio.
Mito na ipige kofi : vilima na viimbe kwa furaha pamoja,
Mbele za Yehova : kwa kuwa yuaja ili kuihukumu nchi.
Ulimwengu atauhukumu haki : na hao mataifa kwa ulekevu.
Utukufu uwe kwa Baba, na kwa Mwana : na kwa Roho Mtakatifu;
Kama vile mwanzo, na sasa : hata milele ni vivyo. Amina.
¶ Kisha husomwa Somo katika Agano Jipya, kama ilivyoamriwa. Na baadaye, Nunc Dimittis (au Wimbo wa Simeon), kama ulivyoletwa hapa.
NUNC DIMITTIS
Luka 2. 29-32
SASA wamruhusu mtumwa wako, Bwana : mfano wa neno lako, kwa amani.
Kwa kuwa macho yangu : yameuona wokofu wako,
Uliouweka tayari : mbele ya watu wote;
Mwanga wa kuwafunulia mambo mataifa : tena utukufu wa watu wako Isiraeli.
Utukufu uwe kwa Baba, na kwa Mwana : na kwa Roho Mtakatifu ;
Kama vile mwanzo, na sasa : hata milele ni vivyo. Amina.
¶ Au, badala yake huwa Wimbo huu katika Zaburi, isipokuwa kwa siku ya Mwezi Kumi na Mbili.
|
Psalm 98 |
DEUS MISEREATUR
Zaburi 67
MUNGU na atufanyie fadhili, atubarikie : na atufikizie nuru za uso wake kwetu:
Ili njia yako itamburikane juu ya nchi : wokofu wako ujulikane katika mataifa wote.
Watu na wakushukuru wewe, Mungu : watu wote pia na wakushukuru wewe.
Mataifa na wafurahi, waimbe kwa furaha : kwa kuwa wewe utawahukumu watu haki, utawaongoza mataifa walio duniani.
Watu na wakushukuru wewe, Mungu : watu wote pia na wakushukuru wewe.
Nchi na itoe mazao yake : Mungu, Mungu wetu, na atubarikie.
Mungu atatubarikia : ncha zote za dunia na zimche yeye.
Utukufu uwe kwa Baba, na kwa Mwana : na kwa Roho Mtakatifu;
Kama vile mwanzo, na sasa : hata milele ni vivyo. Amina.
¶ Hapo huimbwa au husomwa Imani ya Mitume na yule Padre; a wale watu, hali wamesimama.
|
Psalm 67 |
NAAMINI kwa Mungu Baba, Mwenyezi, Muumba-mbingu na nchi:
Na kwa Yesu Kristo, Mwanawe pekee, Bwana wetu, ambaye alitungishwa mimba na Roho Mtakatifu, Akazaliwa na Mwanamwali Mariamu, Akateswa katika enzi ya Pontio Pilato, Akasalibiwa, akafa, akazikwa, Akashuka na kuingia kuzimu; Hata siku ya tatu akasimama tena, ametoka kwa wafu, Akapaa na kuingia mbinguni, Naye ameketi upande wa mkono wa kuume wa Mwenyezi Mungu, Baba; Ndiko atakakotoka, kuja kuwaamua walio hai hata waliokufa.
Naamini kwa Roho Mtakatifu; na Kanisa Takatifu lililo ulimwenguni mote; na Ushirika wa Watakatifu; na Madhambi kusamehewa; na Mwili kufufuka; na Maisha ya milele. Amina.
¶ Kisha husaliwa Sala hizo zifuatazo hapa, watu hali wamepiga magoti kwa makini ; yule Padre hutangulia kutamka kwa sauti kuu,
Bwana na awe pamoja nanyi.
Huitika. Na awe pamoja na roho yako.
Padre. Na tuombe.
Bwana, uturehemu.
Kristo, uturehemu.
Bwana, uturehemu.
¶ Hapo yule Padre na waimbaji na wale watu husoma Sala ya Bwana kwa sauti kuu.
|
Apostles' Creed |
BABAETU uliye mbinguni, Jina lako litakaswe, Ufalme wako na uje. Mapenzi yako yatendeke juu ya nchi, Kama yatendekavyo mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kututosha. Nawe utusamehe makosa yetu, Kama nasi tulivyowasamehe watukosao. Nawe usitupeleke katika kujaribiwa; Utuokoe maovuni. Amina.
¶ Hapo Padre husimama akasema,
Ewe Bwana, utuonyeshe rehema yako juu yetu ;
Huitika. Utupe na wokofu wako.
Padre. Ewe Bwana, umweke salama Mfalme.
Huitika. Nawe utusikize kwa rehema, wakati tukulinganapo.
Padre. Uwavike haki watumishi wako.
Huitika. Uwaweke na furaha wateule wako.
Padre. Ewe Bwana, uwaokoe watu wako.
Huitika. Ubarikie na urithi wako.
Padre. Ewe Bwana, utupe amani kwa hizi zamani zetu;
Huitika. Kwa maana, hakuna mwenye kumtetea, asiyekuwa wewe, Mwenyezi Mungu.
Padre. Ewe Mwenyezi Mungu, utufanye safi mioyo yetu ndani.
Huitika. Wala usituondolee Roho wako Mtakatifu.
¶ Hapo hufuata Sala tatu ; ya Kwanza ni ya Siku ile ; ya Pili ni ya kuombea Amani; ya Tatu ni ya kuombea Msaada wa kukingia hatari zote, kama iletwavyo humu baadaye ; na Sala hizi mbili za mwisho husomwa siku zote wakati wa Sala ya Jioni mwaka mzima, hazibadiliki.
|
Lord's Prayer |
SALA YA PILI KATIKA SALA YA JIONI
EWE Mwenyezi Mungu, ambaye kwako wewe huanza tamaa takatifu zote, na mashauri-mema yote, na kazi za haki zote; utupe watumishi wako hiyo amani ambayo ulimwengu hauwezi kutupa; ili mioyo yetu ikazane katika kuyashika maagizo yako, kisha na kwa vile tunavyolindwa na wewe na hofu ya adui zetu, iwe sisi kwendesha siku zetu kwa starehe na utulivu; kwa ajili ya kustahili kwake Yesu Kristo, Mwokozi wetu. Amina.
|
2nd Collect at Evening Prayer |
SALA YA TATU, YA KUOMBEA MSAADA KILA WAKATI WA HATARI
UTUTILIE nuru katika giza yetu, twakuomba Bwana; nawe kwa rehema zako kubwa utuhifadhi na hatari zote na zani zote za usiku huu; kwa ajili ya mapenzi ya Mwanayo pekee, Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Amina.
¶ Katika maimbio na penye waimbaji, hapa huletwa Wimbo.
|
3rd Collect, For Aid against all Perils |
SALA YA KUMWOMBEA MTUKUFU MFALME
EWE Bwana, Babaetu wa mbinguni, mtukufu, mweza, Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana, Mtawalamaseyidi pekeo, nawe huko uliko kitini mwako unawaangalia watu wote pia wakaao duniani; sisi twakuomba sana umwangalie kwa neema yako Bwana wetu Sultani mwenye ihisani, Mfalme GEORGE; umwongeze sana neema hiyo ipatikanayo kwa Roho wako Mtakatifu, hata awe siku zote kuyashika uyapendayo wewe, na kwenenda umlekezako: umvike vipawa vyako vya mbinguni kwa wingi; umkirimu kuishi sana kwa afya na uwezo; umtie nguvu apate kuwashinda na kuwapita adui zake wote; na baada ya haya, kisha, afikilie furaha na baraka zisizokoma ; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
|
Prayer for the King's Majesty |
SALA YA KUWAOMBEA WATU WA JAMAA YA UFALME
EWE Mwenyezi Mungu, shina la wema wote, sisi twakuomba sana kwa unyenyekevu umbarikie mkewe mfalme wetu, Bibi Elizabeth mwenye fadhili, na Bibi Mary mamaake mfalme, na Princess Elizabeth, na jamaa wote wa Ufalme: uwavike Roho wako Mtakatifu; uwaneemeshe neema yako ya mbinguni; uwafanishe kwa raha yote; uwafikishe na katika ufalme wako wa milele; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
|
Prayer for the Royal Family |
SALA YA KUWAOMBEA MAPADRE WA KANISANI NA WATU WAO
EWE Mwenyezi Mungu, Mkazi wa milele, kila miujiza bora hakuna mwenye kuifanya isipokuwa wewe; twawaombea mabishopu wetu na watunzao roho za watu, na vikao vyote vya watu walivyopewa hao kuvitunza, ya kwamba uwashushie Roho wako, ambaye ni Mpaji wa neema. yako; kisha, ili kwamba watu hao wakupendeze kweli, uwamiminie umande usiokoma wa baraka yako. Utupe haya, twakuomba, Bwana, kwa ajili ya heshima ya Msaada wetu, Mwombezi wetu, Yesu Kristo. Amina.
|
Prayer for Clergy & People |
SALA YA MTAKATIFU CHRYSOSTOM
EWE Mwenyezi Mungu, uliyetupa neema sisi kwa wakati huu kukuletea wewe maombi yetu sote pia kwa nia moja; nawe ndiwe mwenye kutoa ahadi ya kwamba, watu wawili watatu watakapokutanika pamoja kwa jina lako, utawapa wakutakayo: ututimizie sasa, Bwana, haja zetu na sala zetu watumishi wako, kwa jinsi yatakavyotufaa; kwa kutupa kuijua kweli yako katika ulimwengu huu, na maisha ya milele katika ulimwengu ujao. Amina.
2 Wakorintho 13. 14
NEEMA ya Bwana wetu Yesu Kristo, na mapenzi ya Mwenyezi Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu, viwe pamoja nasi sote milele. Amina.
Taratibu ya Sala ya Jioni ya kila siku mwaka mzima imekoma, hapa
|
Prayer of St. Chrysostom |
WAKATI WA SALA YA ASUBUHI
¶ Katika Idi hizi; Idi ya Uzazi wa Kristo (au, Christmas), na ya Mafunuo, na ya Mtakatifu Mathia, na ya Ufufuo, na ya Kupaa juu, na ya Pentecost, na ya Mtakatifu Yohana Mbatizaji, na ya Mtakatifu Yakobo, na ya Mtakatifu Baritolomayo, na ya Mtakatifu Mathayo, na ya Mtakatifu Simoni pamoja na Mtakatifu Yuda, na ya Mtakatifu Andarea, na ya Jumapili ya Utatu, katika wakati wa Sala ya Asubuhi, badala ya Imani ya Mitume, huimbwa au husomwa huku kukiri kwa Imani yetu ya Ukristo, ambako huitwa Imani ya Mtakatifu Athanasio, na huyo Padre na wale watu, hali wamesimama.
QUICUNQUE VULT
APENDAYE aokoke, awaye yote, linalomlazimu kwanza: ni, kuishika Imani iliyo ya Kanisa la Kristo lililo ulimwenguni mote.
Nayo Imani hiyo mtu asipoishika kwa utimilifu wake na kuisafi: hana shaka atapotea milele.
Nayo hii ndiyo Imani iliyo ya Kanisa la Kristo lililo ulimwenguni mote: ya sisi kumwabudu Mungu mmoja katika Utatu, na ule Utatu katika Umoja.
Pasipo kuzichanganya kwa fujo Nafsi zake : wala kuigawanya ile tabia yake ya asili.
Kwani mna Nafsi moja ya Baba, na Nafsi ya pili ya Mwana : na Nafsi moja tena ya Roho Mtakatifu.
Lakini ule Uungu, katika Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, ni Uungu Mmoja tu : ule Utukufu wake ni sawa, ile enzi yake ni ya milele katika Umoja.
Kama alivyo Baba, na Mwana yu vivyo: yu vivyo na Roho Mtakatifu.
Baba asiyeumbwa, na Mwana asiyeumbwa : na Roho Mtakatifu asiyeumbwa.
Baba asiyefahamika, na Mwana asiyefahamika : na Roho Mtakatifu asiyefahamika.
Baba yuko milele, na Mwana yuko milele : na Roho Mtakatifu yuko milele.
Pamoja na haya, hakuna watatu wa milele : wa milele ni mmoja.
Kisha ni vivyo hivyo hakuna watatu wasiofahamika, wala hakuna watatu wasioumbwa : bali aliyeko ni mmoja asiyeumbwa, ni mmoja asiyefahamika.
Ni kama vile, Baba ni Mwenyezi, na Mwana ni Mwenyezi : na Roho Mtakatifu ni Mwenyezi.
Kisha, hakuna watatu walio Wenyezi : aliye Mwenyezi ni Mmoja.
Ni vivyo, Baba ni Mungu, na Mwana ni Mungu : na Roho Mtakatifu ni Mungu.
Kisha hakuna Waungu watatu : lakini aliyeko ni Mungu Mmoja.
Ni vivyo Baba ni Bwana, na Mwana ni Bwana : na Roho Mtakatifu ni Bwana.
Kisha hakuna Mabwana watatu : lakini aliyeko ni Bwana Moja.
Kwani kama ilivyotulazimisha Kweli ya Ukristo kumkiri kila Nafsi moja kuwa Mungu : naye kuwa Bwana:
Ndivyo tulivyokatazwa na Dini iliyo ya Kanisa Ia Kristo lililo ulimwenguni mote kusema kwamba kuna Waungu watatu: au kwamba kuna Mabwana watatu.
Baba alivyo hakufanywa na awaye yote : hakuumbwa, hakuzawa.
Mwana alivyo ni katika Baba pekee : hakufanywa, hakuumbwa, ila amezawa.
Roho Mtakatifu alivyo ni katika Baba na katika Mwana : hakufanywa, hakuumbwa, ila yuatoka.
Ni hivyo, aliyeko ni Baba mmoja, hakuna Mababa watatu, ni Mwana mmoja, hakuna Wana watatu : ni Roho Mtakatifu mmoja, hakuna Maroho Watakatifu watatu.
Na katika Utatu huo, hakuna aliye mbele, wala aliye nyuma : hakuna mkubwa kuliko mwenziwe, hakuna mdogo kuliko mwenziwe.
Ila Nafsi zote tatu ziko milele katika umoja : kisha ni sawa katika umoja.
Hata lililo pasa katika mambo yote, kama ilivyotangulia kutajwa : ni la kuabudiwa ule Umoja katika Utatu, na ule Utatu katika Umoja.
Basi na apendaye aokoke : inampasa kuuona hivyo ule Utatu.
Na zaidi ya hayo, yamlazimu kwa wokofu wa milele : kuamini sawasawa na katika habari ya Bwana wetu Yesu Kristo kufanywa mwili.
Kwani imani iliyonyoka ni hiyo, ya sisi kuamini mioyoni na kukiri : kwamba Bwana wetu Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, ni Mungu, naye ni Binadamu;
Ni Mungu, kwa Yeye kutokana na Tabia ya Asili ya Baba, amezawa kabla ya dahari : ni Binadamu, kutokana na Tabia ya Asili ya Mamaye, amezaliwa katika ulimwengu huu;
Ni Mungu mtimilifu, ni Binadamu mtimilifu : mwenye kuwa na nafsi yenye akili na mwili wa Binadamu.
Yu sawa na Baba kwa hesabu ya Uungu : apitwa na Baba kwa hesabu ya u-Binadamu.
Kisha na angawa ni Mungu pamoja na kuwa Binadamu : lakini yeye si wawili, ila Kristo ni mmoja.
Na alivyo mmoja, si kwa ule Uungu kugeuka kuwa mwili : ila ni kwa ule u-Binadamu kutwawa kuwa katika Mungu;
Ni mmoja halisi: si kwa ile Tabia ya Asili kuchanganyika kwa fujo : ni kwa umoja wa Nafsi.
Kwani kama ambavyo moyo wenye akili na mwili wa ki-Binadamu ni Binadamu mmoja : ndivyo ilivyokuwa Mungu na Binadamu kuwa ni Kristo mmoja;
Aliyeteseka kwa ajili ya wokofu wetu : akashuka chini kuzimu, akasimama tena kwa siku ya tatu, hali ametoka kwa wafu.
Akapaa akaingia mbinguni, naye ameketi upande wa mkono wa kuume wa Baba, Mungu Mwenyezi : nako ndiko atakakotoka, kuja kuwahukumu walio hai hata waliokufa.
Naye wakati wa kurudi kwake inapasa watu wote kufufuka kusimama na miili yao : na kutoa hesabu ya vitendo vyao, kila mmoja.
Kisha waliofanya mema wataingia katika maisha ya milele : waliofanya maovu wataingia katika moto wa milele.
Hiyo ndiyo Imani ya Kanisa la Kristo lililo ulimwenguni mote : nayo mtu asipoiamini sawa kwa uaminifu, hapati kuokoka.
Utukufu uwe kwa Baba, na kwa Mwana : na kwa Roho Mtakatifu ;
Kama vile mwanzo, na sasa : hata milele ni vivyo. Amina.
|