The Book of Common Prayer
United States England Scotland Ireland Wales Canada World

    Chuo cha Sala ya Umoja (1662)
The 1662 Book of Common Prayer in Swahili

 

SALA NA NYARAKA NA INJILI VYA MWAKA MZIMA

Tunza. Sala iliyoagizwa kutumiwa kila Jumapili au kila Idi. iliyo na Kesha yake au Matengezo yake, husomwa katika Sala ya Jioni ya siku ya kuamkia siku hiyo.

JUMAPILI YA KWANZA KATIKA WAKATI WA KUJA

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, utupe neema tuzitupe kazi za giza, tuvikwe silaha za nuru, hivi tulivyo katika zamani za maisha haya yapatikanayo na mauti, nayo ndiyo aliyoyaingia Mwanayo Yesu Kristo, wakati alipokuja kutuangalia, hali amejifanya mnyenyekevu sana; ili kwamba, katika siku ya mwisho, wakati wa kuja kwake tena kwa enzi yake kubwa, kuwahukumu walio hai na waliokufa pia, tuwe sisi ni watu wa kufufuka kwa maisha yasiyopatikana na mauti, kwa ajili yake yeye, anayeishi pamoja na wewe na Roho Mtakatifu, sasa na milele. Amina.

Sala hii husomwa kila siku pamoja na sala nyingine za Kuja, hata yatakapokuja Matengezo ya Uzazi wa Kristo.

Waraka. Warumi 13. 8-14
Injili. Mathayo 21. 1-13
 

Collects, Epistles & Gospels to be used throughout the Year

Note that in the original the Biblical texts are printed out in full; they are given here only by reference. The New Testament in Swahili may be found at the Bible Gateway.

First Sunday in Advent

JUMAPILI YA PILI KATIKA WAKATI WA KUJA

Sala

EWE Bwana Mwenye-baraka, uliyeamuru yaandikwe Maandiko Matakatifu yote kuwa mafunzo yetu; utupe ya kwamba myasikie, na kuyasoma, na kuyashika, na kujifunza hayo, na kuyafikiri mioyoni mwetu kwa jinsi hiyo ya kwamba tupate, kwa uvumilivu na imara ya Neno lako takatifu, kulishika na kulitunza milele tumaini hilo lenye baraka ya maisha yasiyokoma, tuliyopewa na wewe katika Mwokozi wetu Yesu Kristo. Amina.

Waraka. Warumi 15.4-13
Injili. Luka 21. 25-33
 

2 Advent

JUMAPILI YA TATU KATIKA WAKATI WA KUJA

Sala

EWE Bwana Yesu Kristo, ambaye ulipokuja pale kwanza ulimtoa mjumbe wako, ukamtanguliza mbele zako apate kukutengezea njia; utupe ya kwamba hao walio watumishi wako na mawakili wa siri zako, watengeze na kuiandaa njia yako kama vile yeye, kwa kuigeuza mioyo ya maasi kuilekeza katika hekima ya wenye haki, ili kwamba utakapokuja mara ya pili kwa kuuhukumu ulimwengu, tuonekane kuwa ni watu wa kukubaliwa machoni pako, uishiye na kutawala pamoja na Baba na Roho Mtakatifu siku zote, Mungu mmoja, milele. Amina.

Waraka. 1 Wakorintho 4. 1-5
Injili. Mathayo 11. 2-10
 

3 Advent

JUMAPILI YA NNE KATIKA WAKATI WA KUJA

Sala

ZITANGAMSHE nguvu zako twakuomba, ewe Bwana, nawe uje kwetu sisi, utuletee msaada kwa uwezo mwingi li kwamba, tungawa twazuiwa mno na madhambi yetu na uovu wetu, na kuvutiwa nyuma mno katika mashindano ya mbio tunayoagizwa, pamoja na hayo yote usikawie huo wema wa neema yako na rehema zako kutusaidia na kutuponya; kwa alivyokuridhi Mwanayo . Yesu Kristo, Bwana wetu, naye ndiye wa kuheshimiwa na kutukuzwa pamoja na wewe na Roho Mtakatifu, milele. Amina.

Waraka. Wafilipi 4. 4-7
Injili. Yohana 1. 19-28
 

4 Advent

IDI YA UZAZI WA BWANA WETU, AU SIKU ALIYOZALIWA KRISTO, IITWAYO,

CHRISTMAS

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, wewe umetupa sisi Mwanayo mzaliwa pekee, apate kutwaa tabia yetu kuwa nayo yeye, na kuzaliwa na mwanamwali safi, kama wakati huu wa sasa; utupe sisi ya kwamba, kwa hivyo tunavyozaliwa mara ya pili na kufanywa kuwa wanayo kwa kuchaguliwa na neema, turejezwe upya kila siku na Roho wako Mtakatifu; kwa ajili ya yeye huyo Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye yuaishi na kutawala pamoja na wewe na Roho Mtakatifu, Mungu mmoja daima, hata milele. Amina.

Waraka. Wahibirania 1. 1-12
Injili. Yohana 1. 1-14
 

Christmas Day

IDI YA MTAKATIFU STEFANO

Sala

UKUBALI, ewe Bwana, ya kwamba sisi kadiri ya tutakavyopatikana na mashaka hapa duniani, kwa ajili ya kule kuishuhudia kweli yako, tuzidi kuangaza macho mbinguni tu, ili tuuone kwa imani ule utukufu utakaofunuliwa baadaye; kisha, kwa kule kujawa na Roho Mtakatifu, tujifunze kuwapenda na kuwaombea baraka watesaji wetu wawao wote, kwa kukifuata kielelezo chake yule shahidi wako wa kwanza, mtakatifu Stefano, aliyewaombea wauaji wake kwako wewe, ewe Yesu Mwenye-baraka, unayesimama upande wa mkono wa kuume wa Mwenyezi Mungu, kwa kuwaletea msaada watu wote wanaoudhiwa kwa ajili yako wewe, Mwombezi wetu pekeo, Msaada wetu. Amina.

Hapo hufuata Sala ya Uzazi wa Bwana, nayo isiachwe kusomwa kila siku hata yaje Matengezo ya Idi ya Tohara.

Badala ya Waraka. Vitendo 7. 55-60
Injili. Mathayo 23. 34-39
 

St. Stephen

IDI YA MTAKATIFU YOHANA MHUBIRI-WA-HABARI-NJEMA

Sala

TWAKUOMBA sana, ewe Bwana mwenye ihisani, uliletee hili kanisa lako nuru za mwanga wako, ili kwamba kwa kung'ariziwa na elimu ya mbarikiwa mtume wako, mhubiri wako, mtakatifu Yohana, kwa jinsi litakavyokwenda katika mwanga wa kweli yako, lifikilie mwisho katika mwanga wa maisha ya milele; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. 1 Johana 1. 1-10
Injili. Yohana 21. 19-25
 

St, John the Evangelist

IDI YA WASIO-MAKOSA

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, ni wewe uliyetimiza uwezo kwa vinywa vya watoto wadogo, na wenye kuamwa; akawapa wana wadogo kukutukuza wewe kwa mauti yao; uviue na kuondoa viovu vyote ndani yetu sisi, huku uki tutia nguvu sana kwa neema yako, ili kwamba kwa maisha yetu kutokuwa na aibu na imani yetu kuwa imara hata mauti, iwe sisi kulitukuza daima jina lako takatifu; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Badala ya Waraka. Ufunuo 14. 1-5
Injili. Mathayo 2. 13-18
 

Holy Innocents

JUMAPILI IANDAMAYO BAADA YA UZAZI WA BWANA

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, wewe umetupa sisi Mwanayo mzaliwa pekee, apate kutwaa tabia yetu kuwa nayo yeye, na kuzaliwa na mwanamwali safi, kama wakati huu wa sasa; utupe sisi ya kwamba, kwa hivyo tulivyozaliwa mara ya pili na kufanywa kuwa wanayo kwa kuchaguliwa na neema, turejezwe upya kila siku na Roho wako Mtakatifu: kwa ajili ya yeye huyo Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye yuaishi na kutawala pamoja na wewe na Roho Mtakatifu, Mungu mmoja daima, hata milele. Amina.

Waraka. Wagalatia 4. 1-7
Injili. Mathayo 1. 18-25
 

Sunday after Christmas

IDI YA KUPASHWA TOHARA KRISTO

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, huyo Mwanayo· Mwenyebaraka uliamuru atahiriwe apate kuifuata sheria kwa ajili ya wanadamu: utupe nasi tohara ya kweli ya Roho, ili kwamba kwa kutahiriwa katika mioyo yetu na via vyetu vyote, na kufiliwa na tamaa zote za ulimwengu na za mwili; tuyafuate kwa kila jambo mapenzi yako yaliyobarikiwa; kwa yeye Mwanayo Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. Warumi 4. 8-14
Injili. Luka 2. 15-21

Sala hii na Waraka huu na Injili hii husomwa kila siku hata ifike Idi ya Mafunuo.
 

Circumcision

IDI YA MAFUNUO,
au, ya Kristo kufunuliwa mbele ya hao mataifa

Sala

EWE Mungu, wewe uliwafunulia mataifa Mwanayo mzaliwa pekee kwa uongozi wa nyota; nawe ukubali kwa rehema zako ya kwamba, sisi tunaokujua sasa kwa kuamini, mwishowe, baada ya kwisha maisha haya ya sasa, tuufurahie Uungu wako mtukufu ; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. Waefeso 3. 1-12
Injili. Mathayo 2. 1-12
 

Epiphany

JUMAPILI YA KWANZA BAADA YA MAFUNUO

Sala

TWAKUOMBA sana, ewe Bwana, kwa rehema zako uwakubalie watu wako wanyenyekevu wakuombayo, ukawape kuyatambua na kuyajua yawapasayo kuyafanya, tena uwape na neema yako na msaada wako, ili wayatimize yote kwa uaminifu; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. Warumi 12. 1-5
Injili. Luka 2. 41-52
 

1st Sunday after the Epiphany

JUMAPILI YA PILI BAADA YA MAFUNUO

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, Mkazi wa milele, uanirishaye mambo yote ya mbinguni na ya duniani; utege masikio yako ya rehema kwa maombi yetu watu wako, utupe amani yako, tuwe nayo siku zote tutakazokuwa hai duniani; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. Warumi 12. 6-16
Injili. Yohana 2. 1-11
 

2 Epiphany

JUMAPILI YA TATU BAADA YA MAFUNUO

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, Mkazi Wa milele, twakuomba uuangalie kwa rehema huu udhaifu wetu, na kila tukisongwa na hatari na shida uunyoshe kwetu mkono wako wa kuume, uwe msaada wetu na ulinzi wetu, kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. Warumi 12. 16-21
Injili. Mathayo 8. 1-13
 

 
3 Epiphany

JUMAPILI YA NNE BAADA YA MAFUNUO

Sala

EWE Mungu, watujua hali yetu, ya kwamba kwa tulivyokaa katika mambo ya hatari nyingi yaliyotuzunguka kote-kote, tumekuwa hatuwezi kusimama sawasawa, kwa sababu ya unyonge wa tabia yetu tuliyo nayo: twakuomba utulinde kwa hifadhi yako na uwezo wako, viwe hivyo vyenye kutuweka salama na kila zani, na kutuponya kila tujaribiwapo; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. Warumi 13. 1-7
Injili. Mathayo 8. 23-34
 

 
4 Epiphany

JUMAPILI YA TANO BAADA YA MAFUNUO

Sala

TWAKUOMBA sana, ewe Bwana, hili kanisa lako, nyumba yako, ulilinde daima katika dini yako ya kweli; ili kwamba hao walitegemeao tumaini la neema yako ya mbinguni, hilo tu, walindwe milele na uwezo wako mkuu; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. Wakolosai 3.12-17
Injili. Mathayo 13. 24-30
 

5 Epphany

JUMAPILI YA SITA BAADA YA MAFUNUO

Sala

EWE Mungu, Mwanayo Mwenye-baraka alifunuliwa ili apate kuziangamiza kazi za Shetani, na kutufanya sisi kuwa wana wa Mungu, warithi wa uzima wa milele; twakuomba, utupe ya kwamba kwa kuwa na tumaini hilo sisi, tujisafi wenyewe kama yeye alivyo safi; hata wakati atakapotokea mara ya pili na uwezo mkuu na utukufu mwingi, iwe sisi nasi kufananishwa naye, na kuwamo katika ufalme wa enzi yake ya milele; humo aishimo na kutawala pamoja na wewe Baba na wewe Roho Mtakatifu, Mungu Mmoja, milele. Amina.

Waraka. 1 Yohana 3. 1-8
Injili. Mathayo 24. 23-31
 

6 Epiphany

JUMAPILI YA TATU MBELE YA SAUMU
(iitwayo Septuagesima)

Sala

TWAKUOMBA, ewe Bwana, uzisikize kwa ihisani yako sala za watu wako; ili kwamba sisi, tulio adhibiwa kwa haki, kwa ajili ya makosa yetu, tuokolewe na kurehemewa na wewe kwa upole wako, kwa utukufu wa jina lako; kwa Yesu Kristo, Mponyi wetu, anayeishi na kutawala siku zote pamoja na wewe na Roho Mtakatifu, Mungu mmoja milele. Amina.

Waraka. 1 Wakorintho 9. 24-27
Injili. Mathayo 20. 1-16
 

Septuagesima

JUMAPILI YA PILI MBELE YA SAUMU
(iitwayo Sexagesima)

Sala

EWE Bwana Mungu, wewe watuona ya kwamba hatutumaini kazi yetu tufanyayo wenyewe iwayo yote; ukubali kwa rehema ya kwamba kwa ngu vu . zako wewe tukingwe kwa kila uovu: kwa Yesu Kristo, Bwana wetu Amina.

Waraka. 2 Wakorintho 11. 19-31
Injili. Luka 8. 4-15
 

Sexagesima

JUMAPILI ILIYO MBELE YA SAUMU
(iitwayo Quinquagesima)

Sala

EWE Bwana, wewe umetufunza ya kwamba, kazi zetu zote hazifai tukikosa kule kupendana; umtume kwetu Roho wako Mtakatifu, aje atumwagie ndani ya mioyo yetu hicho kipawa chako kilicho kizuri sana cha kupendana, nacho ndicho kifungo chenyewe cha amani na kila aina ya wema, ambacho mtu akikosa hicho anakuwa ni maiti machoni pako, ajapokuwa yu hai: utupe haya kwa ajili ya Yesu Kristo, Mwanayo pekee. Amina.

Waraka. 1 Wakorintho 13. 1-13
Injili. Luka 18. 31-43
 

Quinquagesima

SIKU YA KWANZA YA SAUMU, IITWAYO JUMATANO YA IVU

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, Mkazi wa milele, wewe huvichukii ulivyovifanya hata kimoja, ndiwe mwenye kumsamehe makosa yake kila mtu anayetubia; utuumbie ndani yetu mioyo mipya. iliyo sagika, ili kwa kuyalilia makosa yetu kama ilivyopasa na kuukiri huu udhaifu wetu, tupate kwako wewe, Mungu mwenye rehema zote, msamaha na maondoleo yaliyotimia ; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Sala hii husomwa kila siku muda wote wa Saumu, baada ya Sala iliyohusika na siku hiyo.

Badala ya Waraka. Yoeli 2. 12-17
Injili. Mathayo 6. 16-21
 

Ash Wednesday

JUMAPILI YA KWANZA KATIKA SAUMU

Sala

EWE Bwana, wewe kwa ajili yetu ulifunga michana arobaini na masiku yake; utupe sisi neema ya rohoni, ili kwamba kadiri tutakayo kujinyima mambo yetu wenyewe miili yetu itawaliwe na Roho wako, tukufuate wewe daima, kwa hivi ututiavyo bidii ya uchaji-wa-Mungu katika haki na utakatifu wa kweli, ili tuwe wenye kukuheshimu na kukutukuza wewe, unayeishi na kutawala pamoja na Baba na Roho Mtakatifu, Mungu mmoja milele. Amina.

Waraka. 2 Wakorintho 6. 1-10
Injili. Mathayo 4. 1-11
 

1st Sunday in Lent

JUMAPILI YA PILI KATIKA SAUMU

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, wewe watuona ya kwamba kwa nafsi zetu hatuna nguvu za kujipa msaada wenyewe; utulinde, nje katika miili yetu, na ndani katika roho zetu; tupate kulindwa na mashaka yote yenye kuukuta mwili, na mawazo maovu yote yenye kupigana na roho na kuidhuru; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. 1 Wathesalonike 4. 1-8
Injili. Mathayo 15. 21-28
 

2 Lent

JUMAPILI YA TATU KATIKA SAUMU

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, twakuomba uyakubali haya maombi yetu watu wako tukuombayo kwa moyo, nawe utunyoshee mkono 'Wa kuume wako wa enzi, ututetee na kutukinga na adui zetu wawao wote; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. Waefeso 5. 1-14
Injili. Luka 11. 14-28
 

3 Lent

JUMAPILI YA NNE KATIKA SAUMU

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, ukubali, twakuomba, ya kwamba tungawa twafaa mno sisi kuadhibiwa kwa maovu yetu, lakini kwa kutulizwa mioyo yetu kwa neema yako, tupate kuponywa kwa rehema zako; kwa Bwana wetu Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Amina.

Waraka. Wagalatia 4. 21-31
Injili. Yohana 6. 1-14
 

4 Lent

JUMAPILI YA TANO YA SAUMU

Sala

TWAKUOMBA, ewe Mwenyezi Mungu, uwaangalie kwa rehema hawa watu wako; ili kwamba wapate kutawaliwa na wewe kwa wema wako mwingi, na kuwekwa salama daima, miili yao na roho zao; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. Wahibirania 9. 11-15
Injili. Yohana 8. 46-59
 

5 Lent

JUMAPILI ITANGULIAYO MBELE YA IDI YA UFUFUO

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, Mkazi wa milele, wewe jinsi ulivyowapenda wanadamu kwa mapenzi ya ndani sana, ulimtuma Yesu Kristo Mwanayo Mwokozi wetu, kuja kuutwaa mwili wetu, hata akapatikana na mauti msalabani; ili kwamba wote walio katika mbegu ya kibinadamu wafuate kielelezo chake alichotupa cha unyenyekevu mkuu: ukubali kwa rehema ya kwamba sisi tupate kufuata kielelezo chake cha kuvumilia na kuwa washirika naye katika kufufuka kwake; kwa yeye Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. Wafilipi 2. 5-11
Injili. Mathayo 27. 1-54
 

Sunday next before Easter
(Palm Sunday)

JUMATATU MBELE YA UFUFUO

Badala ya Waraka. Isaya 63. 1-19
Injili. Mariko 14. 1-72
 

Monday before Easter

JUMANNE MBELE YA UFUFUO

Badala ya Waraka. Isaya 50. 5-11
Injili. Mariko 15. 1-39
 

Tuesday before Easter

JUMATANO MBELE YA UFUFUO

Waraka. Wahibirania 9. 16-28
Injili. Luka 22. 1-71
 

Wednesday before Easter

ALHAMISI MBELE YA UFUFUO

Waraka. 1 Wakorintho 11. 17-34
Injili. Luka 23. 1-49
 

Maundy Thursday

IJUMAA NJEMA
(au, Siku ya Kuteseka kwake Bwana wetu)

Sala

TWAKUOMBA sana, ewe Mwenyezi Mungu, uiangalie kwa rehema hii nyumba yako, ambayo kwa ajili yake Bwana wetu Yesu Kristo alikuwa radhi kusali tiwa na kutiwa mikononi mwa watu waovu, hata akapatikana na mauti msalabani; naye sasa amekuwa yuaishi na kutawala pamoja nawe na Roho Mtakatifu, Mungu mmoja, milele. Amina.

EWE Mwenyezi Mungu, Mkazi wa milele, ambaye kwa Roho wako kanisa lote limetawaliwa na kutakaswa ;. twakuomba uyasikize hayo maombi yetu na hizi sala zetu tukuleteazo wewe sasa, kwa kuwaombea watu wa kila daraja katika kanisa lako takatifu, kila mtu katika kazi yake akutumikie kwa kweli na haki, kwa Bwana wetu, Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Amina.

EWE Mungu mwenye huruma, Muumba wa watu wote, huchukii ulivyovifanya hata kimoja, wala hutaki mauti ya mwenye dhambi, waona ni vyema afadhali ageuke na kuishi: uwarehemu wote Mayahudi, na Waislamu, na Makafiri, na waipingao dini ya kweli, uwaondolee ujinga uwao wote, na uzito wote walio nao wa moyo, uwatoe na dharau ya neno lako, nawe uwaongoze, ewe Bwana wa rehema, uwalete kwao, maana, ndani ya kundi lako, na iwe wao kuupata wokofu pamoja na wote wateule Waisiraeli wa kweli, liwe zizi moja, Mchunga mmoja, naye ni Yesu Kristo, Bwana wetu, aishiye na kutawala pamoja na wewe na Roho Mtakatifu, Mungu mmoja, milele. Amina.

Waraka. Wahibirania 10. 1-25
Injili. Yohana 19. 1-37
 

Good Friday

MATENGEZO YA IDI YA UFUFUO

Sala

UKUBALI, ewe Bwana, ya kwamba, kama vile tubatizwavyo sisi ndani ya mauti ya Mwanayo Mwenye-baraka Mwokozi wetu Yesu Kristo, tupate na kuzikwa pamoja naye vilevile, kwa kuyatia mautini daima mambo yetu mabovu ya tamaa, ili kwamba kwa kupita ndani ya kaburi, ndani ya mlango wa mauti, tufikilie katika kufufuliwani kwetu kwenye furaha; kwa ajili ya kustahili kwake yeye, ambaye alikufa, akazikwa, akafufuka, kwa ajili yetu, Mwanayo Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. 1 Petero 3. 17-22
Injili. Mathayo 27. 57-66
 

Easter Even

IDI YA UFUFUO

Katika Sala ya Asubuhi, badala ya Zaburi ya, Haya, na tumwimbie, w.k., husomwa au huimbwa Nyimbo hizi.

PASAKA wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka kwa ajili yetu, naye ni Kristo: basi na tuifanye karamu;
    Si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uadui na uovu: ila kwa mkate usio chachu wa weupe wa moyo na kweli.   1 Wakorintho 5. 7-8.

    Kristo kwa kuwa amekwisha kufufuliwa kutoka kwa wafu, hafi tena: mauti hayatawali juu yake tena.
    Kwani vile alivyokufa, alizifilia dhambi mara moja, basi: na vile aishivyo', yuaishi kwa Mwenyezi Mungu.
    Nanyi ni vivyo jihesabuni wenyewe kuwa mu wafu kweli-kweli kwa zile dhambi: kisha mu hai kwa Mwenyezi Mungu, katika Kristo Yesu Bwana wetu.   Warumi 6.9-11.

    Ila sasa Kristo amefufuliwa kutoka kwa wafu: naye amekuwa ni malimbuko ya hao waliolala.
    Kwani kwa kuwa mauti yakaja kwa njia ya binadamu: kufufuka kwa wafu vivyo huja kwa njia ya binadamu.
    Kwani vivile kama wote wafavyo katika Adamu: vivyo katika Kristo wote watafanywa kuwa hai.   1 Wakorintho 15. 20-22.

    Utukufu uwe kwa Baba, na kwa Mwana: na kwa Roho Mtakatifu;
    Kama vile mwanzo, na sasa: hata milele ni vivyo. Amina.

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, wewe kwa Mwanayo mzaliwa pekee Yesu Kristo umeyashinda mauti, umetufungulia na lango la maisha ya milele; sisi tu miguuni pako, twakutaka ya kwamba, kama neema yako ituongozavyo, wewe hututilia mioyoni mwetu tamaa zilizo njema, tuwe sisi nasi kwa msaada wako wa daima kuzitimiliza sawasawa hizo tamaa; kwa ajili ya Yesu Kristo, Bwana wetu, aishiye na kutawala pamoja nawe na Roho Mtakatifu, uli Mungu mmoja, milele. Amina.

Waraka. Wakolosai 3. 1-7
Injili. Yohana 20. 1-10
 

Easter Day

JUMATATU BAADA YA IDI YA UFUFUO

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, wewe kwa Mwanayo mzaliwa pekee Yesu Kristo umeyashinda mauti, umetufungulia na lango la maisha ya milele; sisi tu miguuni pako, twakutaka ya kwamba, kama neema yako ituongozavyo, wewe hututilia mioyoni mwetu tamaa zilizo njema, tuwe sisi nasi kwa msaada wako wa daima kuzitimiliza sawasawa hizo tamaa; kwa ajili ya Yesu Kristo, Bwana wetu, aishiye na kutawala pamoja nawe na Roho Mtakatifu, uli Mungu mmoja, milele. Amina.

Badala ya Waraka. Vitendo vya Mitume 10. 34-43
Injili. Luka 24. 13-35
 

Monday in Easter Week

JUMANNE BAADA YA UFUFUO

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, wewe kwa Mwanayo mzaliwa pekee Yesu Kristo umeyashinda mauti, umetufungulia na lango la maisha ya milele; sisi tu miguuni pako, twakutaka ya kwamba, kama neema yako ituongozavyo, wewe hututilia mioyoni mwetu tamaa zilizo njema, tuwe sisi nasi kwa msaada wako wa daima kuzitimiliza sawasawa hizo tamaa; kwa ajili ya Yesu Kristo, Bwana wetu, aishiye na kutawala pamoja nawe na Roho Mtakatifu, uli Mungu mmoja, milele. Amina.

Badala ya Waraka. Vitendo vya Mitume 13. 26-41
Injili. Luka 24· 36-48
 

Tuesday in Easter Week

JUMAPILI YA KWANZA BAADA YA IDI YA UFUFUO

Sala

EWE Baba Mwenyezi, Mwanayo mzaliwa pekee ulitupa afe kwa makosa yetu, akasimame tena kwa kutupa haki; ukubali ya kwamba tuitupe chachu ya uadui na uovu, hata iwe sisi kukutumikia daima kwa maisha safi katika kweli, kwa kustahili kwake yeye huyo Mwanayo, Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. 1 Yohana 5. 4-12
Injili. Yohana 20. 19-23
 

1st Sunday after Easter

JUMAPILI YA PILI BAADA YA IDI YA UFUFUO

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, ulitupa Mwanayo mzaliwa pekee awe kwetu dhabihu kwa ajili ya dhambi, na kielelezo cha maisha ya uchaji-wa-Mungu; utupe neema tupate kwendelea katika kuyapokea manufaa yake yasiyothaminika kwa asante nyingi sana, kisha ria iwe sisi siku zote kujitia bidii ya kuzifuata hatua zilizobarikiwa za maisha yake matakatifu sana; kwa mwenyewe Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. 1 Petero 2. 19-25
Injili. Yohana 10. 11-16
 

2 Easter

JUMAPILI YA TATU BAADA YA IDI YA UFUFUO

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, uwaonyeshaye mwanga wa kweli yako hao wakosao, ili wapate kurejea katika njia ya haki; uwape wote waliokubaliwa katika ushirika wa Dini ya Kikristo, wapate kukataa mambo yote yapingamanayo na ufuasi huo waufuatao, uwape na kuyaendelea yote ambayo kwamba yalingana nao; kwa ajili ya Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Amina.

Waraka. 1 Petero 2. 11-27
Injili. Yohana 16.16-22
 

3 Easter

JUMAPILI YA NNE BAADA YA IDI YA UFUFUO

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, ni wewe pekeo uwezaye kuitawala mioyo ya ukaidi na mapenzi ya utukutu ya wanadamu wenye dhambi; uwape watu wako kuyapenda uliyowaagiza, na kuvitamani ulivyowapa ahadi, ili hivyo, hata humu katika mageule yote mbali-mbali ya ulimwengu, tuwe sisi kuituliza sana mioyo yetu huko kwenye furaha za kweli; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. Yakobo 1. 17-21
Injili. Yohana 16. 5-15
 

4 Easter

JUMAPILI YA TANO BAADA YA IDI YA UFUFUO

Sala

EWE Bwana, ni wewe asili ya mema yote: basi utukirimu sisi waja wako tulio miguuni pako, tuvuviwe na wewe uliye Mtakatifu, ili tupewe kuyawaza mambo mema; utukirimu na kuongozwa na rehema yako, ili tupate kuyatenda: kwa Bwana wetu,' Yesu Kristo. Amina.

Waraka. Yakobo 1. 22-27
Injili. Yohana 16. 23-33
 

5 Easter

IDI YA KUPAA BWANA WETU

Sala

TWAKUOMBA, ewe Mwenyezi Mungu, utupe ya kwamba, kama hivyo sisi tulivyoamini ya kuwa Mwanayo mzaliwa pekee Bwana wetu, Yesu Kristo, amepaa juu ameingia na mbinguni, iwe sisi nasi wenyewe kupaa vivyo kwa mioyo yetu na nia zetu, na kukaa huko pamoja naye daima; ambaye yuaishi na kutawala pamoja nawe na Roho Mtakatifu, uli Mungu mmoja milele. Amina.

Badala ya Waraka. Vitendo vya Mitume 1. 1-11
Injili. Mariko 16. 14-20
 

Ascension Day

JUMAPILI ILIYOANDAMA BAADA YA IDI YA KUPAA

Sala

EWE Mungu, Mfalme wa Utukufu, wewe umemkuza Yesu Kristo Mwanayo mzaliwa pekee, umempaza hata ufalme wako wa mbinguni kwa furaha kuu ya kushinda; twakuomba usituache pasipo na msaada, bali utuletee Roho wako Mtakatifu, aje atutu1ize, apate kutuinua na kututia utukufuni mle mle, alimotangulia kupaa yeye Mwokozi wetu Kristo; naye ndiye aishiye na kutawala pamoja nawe na Roho Mtakatifu, uli Mungu mmoja, milele. Amina.

Waraka. 1 Petero 4. 7-11
Injili. Yohana 15.26-16.4
 

Sunday after Ascension

IDI YA PENTECOST

Sala

EWE Mungu, wewe kwa majira kama haya uliwafunza mioyo yao watu wako waaminifu kwa kuwaletea mwanga wa Roho wako Mtakatifu; utupe nasi kwa yeye Roho, tuwe na fahamu njema kwa mambo yote, na siku zote tuufurahie utulizi wake mtakatifu; kwa kustahili kwake Yesu Kristo, Mwokozi wetu, ambaye yuaishi na kutawala pamoja nawe katika umoja wa yeye Roho, uli Mungu mmoja, milele. Amina.

Badala ya Waraka. Vitendo vya Mitume 2. 1-11
Injili. Yohana 14. 15-31
 

Pentecost (Whitsunday)

JUMATATU BAADA YA PENTECOST

Sala

EWE Mungu, wewe kwa majira kama haya uliwafunza mioyo yao watu wako waaminifu kwa kuwaletea mwanga wa Roho wako Mtakatifu; utupe nasi kwa yeye Roho tuwe na fahamu njema kwa mambo yote, na siku zote tuufurahie utulizi wake mtakatifu; kwa kustahili kwake Yesu Kristo, Mwokozi wetu, ambaye yuaishi na kutawala pamoja nawe katika umoja wa yeye Roho, uli Mungu mmoja, milele. Amina.

Badala ya Waraka. Vitendo vya Mitume 10. 34-48
Injili. Yohana 3. 16-21
 

Monday after Pentecost

JUMANNE BAADA YA PENTECOST

Sala

EWE Mungu, wewe kwa majira kama haya uliwafunza mioyo yao watu wako waaminifu kwa kuwaletea mwanga wa Roho wako Mtakatifu, utupe nasi kwa yeye Roho tuwe na fahamu njema kwa mambo yote, na siku zote tuufurahie utu1izi wake mtakatifu: kwa kustahili kwake Yesu Kristo, Mwokozi wetu, ambaye yuaishi na kutawala pamoja nawe katika umoja wa yeye Roho, uli Mungu mmoja, milele. Amina.

Badala ya Waraka. Vitendo vya Mitume 8. 14-17
Injili. Yohana 10. 1-10
 

Tuesday after Pentecost

JUMAPILI YA UTATU

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, Mkazi wa milele, wewe huna mwanzo huna mwisho; nawe umetupa neema' sisi watu wako, ya kuukubali utukufu wa Utatu wako usio mwanzo wala mwisho, kwa tulivyoikiri imani ya kweli; umetupa na kuuabudu ule Umoja kwa tulivyovikwa uwezo wa Uungu mtukufu; twakuomba sana, utudumishe mumu katika imara ya imani hii, utukinge daima na kila uovu ; nawe ndiwe uishiye na kutawala, uli Mungu mmoja, milele. Amina.

Badala ya Waraka. Ufunuo 4. 1-11
Injili. Yohana 3. 1-15
 

Trinity Sunday

JUMAPILI YA KWANZA BAADA YA UTATU

Sala

EWE Mungu, wewe ndiwe nguvu za wakutumainio ; uzikubali sala zetu kwa rehema: nawe kwa vile huu udhaifu wa binadamu usivyoweza kutenda neno jema liwalo lote pasipokuwa na wewe, utupe msaada wa neema yako, ili kwamba sisi kwa kuyatimiza maagizo yako, tukupendeze huku kwa maombi yetu na huku kwa vitendo vyetu; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. 1 Yohana 4.7-21
Injili. Luka 16. 19-31
 

1st Sunday after Trinity

JUMAPILI YA PILI BAADA YA UTATU

Sala

EWE Bwana, wewe huachi daima kuwasaidia na kuwaongoza hao uwakubalio kuwalea katika imara ya hofu yako na mapenzi yako: utulinde sisi, twakuomba, katika hifadhi ya uangalizi wako wema, utuweke hali ya kulihofu na kulipenda daima jina lako takatifu; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. 1 Yohana 3. 13-24
Injili. Luka 14. 16-24
 

2 Trinity

JUMAPILI YA TATU BAADA YA UTATU

Sala

EWE Bwana, twakuomba sana utusikize kwa rehema, nawe uliotutia tamaa isiyo shaka ya kukuomba, utupe sisi kulindwa na kutulizwa kwa msaada wako wa nguvu katika hatari zote na mashaka yote: kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. 1 Petero 5. 5-11
Injili. Luka 15. 1-10
 

3 Trinity

JUMAPILI YA NNE BAADA YA UTATU

Sala

EWE Mungu, uwalindaye wote wakutumainio, pasipokuwa na wewe hakuna kilicho na nguvu, hakuna kitakatifu; utuongezee rehema zako uzifanye nyingi kwetu, ili kwamba, kwa kuwa wewe ndiwe mtawala wetu na kiongozi chetu tupite katika mambo ya dunia kisha tusipotewe na mambo ya milele. Uyakubali haya, ewe Baba wa mbinguni, kwa ajili ya Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. Warumi 8. 18-23
Injili. Luka 6. 36-42
 

4 Trinity

JUMAPILI YA TANO BAADA YA UTATU

Sala

UKUBALI, ewe Bwana, twakuomba sana, ya kwamba mwendo wa ulimwengu ulekezwe na uongozi wako katika utulivu, hata hili kanisa lako likutumikie kwa furaha, katika hali ya uchaji-wa-Mungu na utulivu; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. Petero 3. 8-15
Injili. Luka 5. 1-11
 

5 Trinity

JUMAPILI YA SITA BAADA YA UTATU

Sala

EWE Mungu, umewatengezea hao wakupendao mambo ambayo kwamba wema wake umepita fahamu za binadamu, utumiminie ndani ya mioyo yetu mapenzi, namna ambayo kwa kukupenda wewe zaidi ya vyote tupate kuzifikilia ahadi zako, nazo zapita yote tuwezayo kuyatamani; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. Warumi 6. 3-11
Injili. Mathayo 5. 20-26
 

6 Trinity

JUMAPILI YA SABA BAADA YA UTATU

Sala

EWE Bwana, uliye na uwezo wote na nguvu zote, mwenye kuanziliza na kukirimu vitu vyema vyote: uyatie mapenzi ya jina lako ndani ya mioyo yetu; uikuze ndani yetu dini ya kweli, na kutulea katika hali ya wema uliotimia, nawe utuweke vivyo hivyo, kwa rehema zako kuu; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. Warumi 6. 19-23
Injili. Mariko 8. 1-9
 

7 Trinity

JUMAPILI YA NANE BAADA YA UTATU

Sala

EWE Mungu, uangalizi wako usiopungua ndio upangao mambo yote, ya mbinguni na ya duniani; sisi tulio miguuni pako twakuomba utuepushie mambo yote yatakayotudhuru; utupe na vitu vyote vitakavyotufaa; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. Warumi 8. 12-17
Injili. Mathayo 7. 15-21
 

8 Trinity

JUMAPILI YA TISA BAADA YA UTATU

Sala

TWAKUOMBA sana Bwana, utupe moyo wa kuyawaza yafaayo yote na kuyatenda daima; ili kwamba tungawa sisi hatuwezi kufanya neno lolote la haki pasipokuwa na wewe, lakini kwa kuwezeshwa na wewe tuishi kama upendavyo; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. 1 Wakorintho 10. 1-13
Injili. Luka 16. 1-9
 

9 Trinity

JUMAPILI YA KUMI BAADA YA UTATU

Sala

MASIKIO ya rehema zako, ewe Bwana, na yategeke kwa sala za watumishi wako walio miguuni pako; kisha, ili kwamba wayapate wakuombayo, uwafanye wawe watu wa kukuomba kama yakupendezayo; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. 1 Wakorintho 12. 1-11
Injili. Luka 19. 41-48
 

10 Trinity

JUMAPILI YA KUMI NA MOJA BAADA YA UTATU

Sala

EWE Mungu, wewe huonyesha hizo nguvu zako zisizo-wezekana katika rehema zako na huruma zako; utupe kwa rehema kiasi hicho cha neema yako, ambacho kwamba kitatupa sisi kwenenda mbio katika njia ya maagizo yako, hata tuzifikilie ahadi za neema yako, na kufanywa tuwe na fungu katika mali zako za mbinguni, kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. 1 Wakorintho 15. 1-11
Injili. Luka 18. 9-14
 

11 Trinity

JUMAPILI YA KUMI NA MBILI BAADA YA UTATU

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, huna mwanzo huna mwisho, . wewe siku zote u mwepesi zaidi wa kusikia kuliko sisi wa kukuomba, umezoea kutupa zaidi ya tutakavyo na yatufaavyo kupewa; utumwagie juu yetu wingi wa rehema yako, utusamehe hayo tuyachayo kwa kujijua kuwa na makosa, utupe na hivyo vitu vyema ambavyo sisi hatufai kuviomba, ila kwa afaavyo na atuombeavyo Mwanayo, Bwana wetu, Yesu Kristo. Amina.

Waraka. 2 Wakorintho 3. 4-9
Injili. Mariko 7. 31-37
 

12 Trinity

JUMAPILI YA KUMI NA TATU BAADA YA UTATU

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, mwenye huruma, kwa kuwa ni kwa ihisani yako tu, wapatavyo watu wako waaminifu kukutumikia kwa kufaa na kusifiwa; utupe sisi, twakuomba sana, ya kukutumikia kwa uaminifu sana hapa duniani, hata mwisho tusikose kuzifikilia ahadi zako za mbinguni; kwa kustahili kwake Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. Wagalatia 3. 16-22
Injili. Luka 10. 23-37
 

13 Trinity

JUMAPILI YA KUMI NA NNE BAADA YA UTATU

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, huna mwanzo huna mwisho; utupe sisi kuongea imani, na matumaini, na kupendana ; tena kwamba tuvipate ulivyoviahidi, utupe kuyapenda uliyoyausia; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. Wagalatia 5. 16-24
Injili. Luka 17. 11-19
 

14 Trinity

JUMAPILI YA KUMI NA TANO BAADA YA UTATU

Sala

ULILINDE kanisa lako, twakuomba sana, ewe Bwana, kwa rehema zako za daima, na kwa kuwa unyonge wa binadamu pasipokuwa na wewe hauna budi kuanguka, utuweke salama daima kwa msaada wako, tupate kulindwa na kila uovu, utuongoze tuvifikilie vyote vitakavyotufaa kwa wokofu wetu; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. Wagalatia 6. 11-18
Injili. Mathayo 6. 24-34
 

15 Trinity

JUMAPILI YA KUMI NA SITA BAADA YA UTATU

Sala

TWAKUOMBA sana, ewe Bwana, huruma zako za daima na zilisafi kanisa lako na kuliweka salama; kisha kwa vile lisivyoweza kulindwa pasipokuwa na msaada wako, uzidi wewe kulilinda kwa kulipenda na kulitetea daima; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. Waefeso 3. 13-21
Injili. Luka 7. 11-17
 

16 Trrinity

JUMAPILI YA KUMI NA SABA BAADA YA UTATU

Sala

TWAKUOMBA, ewe Bwana, neema yako na idumu katika kututangtilia na kutuandama, kisha na itutie bidii tuwe wenye kufanya kazi njema zote daima; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. Waefeso 4. 1-6
Injili. Luka 14. 1-11
 

17 Trinity

JUMAPILI YA KUMI NA NANE BAADA YA UTATU

Sala

TWAKUOMBA, ewe Bwana, uwape watu wako neema ya kuyashinda majaribu ya ulimwengu na mwili na Ibilisi, na kukufuata wewe tu, Mungu pekeo wa kweli, kwa mioyo iliyotakata na nia zilizosafika : kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. 1 Wakorintho 1. 4-8
Injili. Mathayo 22. 34-46
 

18 Trinity

JUMAPILI YA KUMI NA KENDA BAADA YA UTATU

Sala

EWE Mungu, kwa kuwa pasipokuwa na wewe hatuwezi kukupendeza, utupe kwa rehema ya kwamba Roho wako Mtakatifu atuongoze na kututawala mioyo yetu katika mambo yote, kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. Waefeso 4. 17-32
Injili. Mathayo 9. 1-8
 

19 Trinity

JUMAPILI YA ISHIRINI BAADA YA UTATU

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, wewe u mwingi wa rehema; kwa .ihisani yako nyingi utulinde, twakuomba sana, na mambo yote yenye kutudhuru, hata sisi tukiwa tayari katika miili yetu na mioyo yetu, tutimize yote kwa furaha uyatakayo wewe kwetu; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. Waefeso 5. 15-21
Injili. Mathayo 22. 1-14
 

20 Trinity

JUMAPILI YA ISHIRINI NA MOJA BAADA YA UTATU

Sala

TWAKUOMBA, ewe Bwana, uliye mwingi wa rehema, utupe watu wako waaminifu msamaha na amani, ili kwa kusafiwa na makosa yetu yote, tupate kukutumikia kwa utulivu wa moyo; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. Waefeso 6. 10-20
Injili. Yohana 4· 46-54
 

21 Trinity

JUMAPILI YA ISHIRINI NA MBILI BAADA YA UTATU

Sala

HILO kanisa lako, nalo ndilo watu wa nyumba yako, twakuomba, ewe Bwana, ulilinde katika hali ya kukucha daima; lipate kulindwa na wewe na mashaka yawayo yote, kisha na liwe na bidii 'nyingi ya uchaji-wa-Mungu katika kukutumikia wewe kwa kazi njema, ili kulitukuza jina lako; kwa ajili ya Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. Wafilipi 1. 3-11
Injili. Mathayo 18. 21-35
 

22 Trinity

JUMAPILI YA ISHIRINI NA TATU BAADA YA UTATU

Sala

EWE Mungu, makimbilio yetu ni wewe, nguvu zetu ni wewe, nawe ndiwe asili ya wema wote; twakuomba sana uwe radhi kuyasikia kwa wepesi hayo likuombayo kanisa lako kwa kutii, utupe ya kwamba tuyatakayo kwa uaminifu tuyapate kwa ukamilifu: kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. Wafilipi 3. 17-21
Injili. Mathayo 22. 15-22
 

23 Trinity

JUMAPILI YA ISHIRINI NA NNE BAADA YA UTATU

Sala

TWAKUOMBA sana, ewe Bwana, utuondolee hatia zetu watu wako, ili sisi sote kwa wingi wa ihisani yako tufunguliwe vifungo vya makosa yetu yote tuliyokukosa kwa huu unyonge wetu. Utujalie haya, ewe Baba wa mbinguni, kwa ajili ya Yesu Kristo, Bwana wetu, Mwokozi wetu Mwenye-baraka. Amina.

Waraka. Wakolosai 1. 3-12
Injili. Mathayo 9. 18-26
 

24 Trinity

JUMAPILI YA ISHIRINI NA TANO BAADA YA UTATU

Sala

EWE Bwana, twakuomba sana, uwaamshe hao watu wako waaminifu, ili kwamba, kwa vile watakavyozaa kwa wingi matunda ya kazi njema, iwe wao kupata kufurahishwa na wewe vivyo kwa wingi; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Badala ya Waraka. Yeremia 23. 5-8
Injili. Yohana 6. 5-14

Kadiri ya siku za Jumapili zilizobaki, kabla isijafika Jumapili ya Wakati wa Kuja, hutwaliwa Maweko ya Ibada ya Jumapili zile zilizorukizwa baada ya Idi ya Mafunuo, kwa hesabu ya zilizopungua hapa. Na Jumapili zikipungua, hayo yaliyozidi humu hurukizwa. Lakini Sala hii na Waraka huu na Injili hii hutumiwa daima katika siku ya Jumapili itanguliayo mbele ya Wakati wa Kuja.
 

25 Trinity

IDI YA MTAKATIFU ANDAREA

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, wewe ndiwe uliyempa neema yule mtume wako mtakatifu, Andarea, nayo ikampa kuitika mwito wa Mwanayo Yesu Kristo kwa upesi, akamfuata pasipo kukawia; utujalie sisi sote, ya kwamba kwa hivyo tulivyoitwa na Neno lako takatifu, mwanzo wa sasa tujitoe nafsi zetu tuyatimize maagizo yako matakatifu : kwa yeye huyo Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. Warumi 10. 9-21
Injili. Mathayo 4. 18-22
 

St. Andrew

IDI YA MTAKATIFU THOMA MTUME

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, huna mwanzo huna mwisho, ni kwa ajili ya kuithubutisha zaidi hii imani wewe ulivyomwacha yule Thoma, mtume wako mtakatifu, aingiwe, na shaka juu ya kufufuka kwake Mwanayo; utupe ya kwamba, jinsi tutakavyomwamini Mwanayo Yesu Kristo kwa ukamilifu sana, tusifanye tashwishi kwa neno liwalo lote: ili kwamba imani yetu isilaumiwe majira yoyote mbele zako. Nawe Bwana, utusikize kwa haya kwa ajili yake yeye huyo Yesu Kristo, ambaye huheshimiwa na kutukuzwa pamoja na wewe na Roho Mtakatifu, sasa na milele. Amina.

Waraka. Waefeso 2. 19-22
Injili. Yohana 20. 24-31
 

St. Thomas

IDI YA KUONGOKA KWAKE MTAKATIFU PAULO

Sala

EWE Mungu, dunia nzima umeieneza mwanga wa Injili kwa kuhubiri kwake yule Paulo mtume wako mbarikiwa; utujalie sisi, twakuomba sana, ya kwamba kwa vile tutakavyoikumbuka daima ile ajabu ya kuongoka kwake, tuwe wenye kukushukuru kwa jambo hilo kwa kuyafuata mafunzo yale ya utakatifu aliyokuwa akiyafunza yeye; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Badala ya Waraka. Vitendo vya Mitume 9. 1-22
Injili. Mathayo 19. 27-30
 

Conversion of St. Paul

IDI YA KUHUDHURISHWA KWAKE KRISTO HEKALUNI,
nayo huitwa

KUTAKATA KWAKE MTAKATIFU MARIAMU MWANAMWALI
baada ya kuzaa

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, huna mwanzo huna mwisho, twajinyenyekeza tukikuomba uliye Mfalme wetu ya kwamba, kama vile Mwanayo pekee alivyoletwa ndani ya hekalu kama wakati wa hii siku ya leo, naye alikuwa na mwili mfano wetu, iwe vivyo nasi kuletwa kwako tuli na mioyo iliyosafiwa na kutakaswa: kwa yeye huyo Mwanayo Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Badala ya Waraka. Malaki 3. 1-5
Injili. Luka 2. 22-40
 

Purification of St. Mary

IDI YA MTAKATIFU MATHIA

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, hapo kale badala ya yule salata yule Yudasi, wewe ulimchagua mtumwa wako mwaminifu Mathia, akawa ni mmoja katika hesabu ya mitume kumi na wawili; utupe ya kwamba hili kanisa lako liwe hali ya kulindwa siku zote lisiingiwe na mitume ya uwongo, bali litunzwe na kuongozwa na walisha wa kweli waaminifu; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Badala ya Waraka. Vitendo vya Mitume 1. 15-26
Injili. Mathayo 11. 25-30
 

St. Matthias

IDI YA KUPEWA HABARI KWAKE MBARIKIWA MARIAMU MWANAMWALI

Sala

EWE Bwana, twakuomba sana, utumiminie neema yako mioyoni mwetu; ili kwa vile sisi tulivyopata habari ya kufanywa mwili Mwanayo Yesu Kristo kwa ujumbe uliokuja na malaika, sasa kwa kusalibiwa na kuteseka kwake tuwe wenye .kupelekwa mbele vivyo hivyo hata utukufu wa kufufuka kwake; kwa yeye huyo Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Badala ya Waraka. Isaya 7. 10-15
Injili. Luka 1. 26-38
 

The Annunciation

IDI YA MTAKATIFU MARIKO

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, umetufundisha sisi watu wa kanisa lako takatifu kwa elimu ya mbinguni, hiyo aliyokuwa nayo yule mhubiri wako, yule mtakatifu Mariko; utupe neema hiyo, ya kwamba tusiwe mfano wa watoto, tukachukuliwa na kila upepo wa elimu ya upuzi; bali daima tuwe na uwezo katika kweli ya Injili yako takatifu; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. Waefeso 4.7-16
Injili. Yohana 15. 1-11
 

St. Mark

IDI YA WATAKATIFU FILIPU NA YAKOBO

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, kukujua kweli wewe ndiko kuishi milele; utupe sisi kumjua kwa utimilifu Mwanayo Yesu Kristo, kuwa ndiye Njia, ndiye Kweli, naye ndiye Uzima; ili kwamba kwa kuzifuata nyayo zao wale mitume wako watakatifu, mtakatifu Filipu na mtakatifu Yakobo, tuwe sisi watu wa kwenenda kwa kujikaza katika njia ifikishayo maisha ya milele; kwa yeye Mwanayo Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. Yakobo 1. 1-12
Injili. Yohana 14. 1-14
 

St. Philip & St. James

IDI YA MTAKATIFU BARANABA

Sala

EWE Bwana Mwenyezi Mungu, yule mtume wako mtakatifu, Baranaba, ulimvika vipawa vikubwa vya Roho Mtakatifu; twakuomba sana usituache sisi tukavikosa vipawa vyako namna namna, wala tusikose neema yako, tupate kuvitumia daima vipawa hivyo kwa kukuheshimu na kukutukuza; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Badala ya Waraka. Vitendo vya Mitume 11. 22-30
Injili. Yohana 15. 12-16
 

St. Barnabas

IDI YA MTAKATIFU YOHANA MBATIZAJI

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, uangalizi wako ndilo lililompa mtumwayo mtakatifu Yohana kuzaliwa kwa ajabu, likamtuma kumtengezea njia Mwanayo Mwokozi wetu, kwa kuhubiri watu ya kutubia; utupe sisi kufuata mafunzo yake na maisha yake matakatifu sana, hata tuwe sisi watu wa kutubu kweli kama vile alivyokuwa akifunza yeye; kisha na kama vile alivyotupa kielelezo, tuwe siku zote wenye kusema ambayo ni kweli, tuukemee na uovu pasina kucha watu, nasi tuvumilie katika mateso kwa ajili ya ile kweli; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Badala ya Waraka. Isaya 40. 1-11
Injili. Luka 1. 57-80
 

St, John the Baptist

IDI YA MTAKATIFU PETERO

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, wewe kwa Mwanayo Yesu Kristo ndiwe uliyempa yule mtume wako mtakatifu Petero vipawa vingi vizuri, ukamuusia sana kulilisha kundi lako; twakuomba sana uwawezeshe mabishopu wote, na wachungaji wote, wawe wenye kulihubiri kwa bidii Neno lako takatifu; na wale watu nao wawe wenye kulifuata kwa kutii lile Neno; ili kwamba apate kupewa kila mmoja taji ya utukufu usio mwisho; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Badala ya Waraka. Vitendo vya Mitume 12. 1-11
Injili. Mathayo 16. 13-19
 

St. Peter

IDI YA MTAKATIFU YAKOBO MTUME

Sala

UTUPE, ewe Mungu mwingi wa rehema, ya kwamba kama vile yule mtakatifu Yakobo mtume wako, alivyomwacha mzee wake na alivyokuwa navyo vyote, akautii mwito wake Mwanayo Yesu Kristo pasipo kukawia, akamfuata; iwe sisi nasi kuziacha tamaa za' ulimwengu na mwili zote pia, tupate kukaa tayari daima kuyafuata maagizo yako matakatifu; kwa Bwana wetu, Yesu Kristo. Amina.

Badala ya Waraka. Vitendo vya Mitume 11. 27-12. 3
Injili. Mathayo 20. 20-28
 

St. James the Apostle

IDI YA MTAKATIFU BARITOLOMAYO MTUME

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, huna mwanzo huna mwisho, wewe ulimpa neema yule mtume wako Baritolomayo, kuliamini kweli hilo Neno lako na kulihubiri; twakuomba sana ulipe kanisa lako kulipenda Neno hilo aliloamini yeye, na kulihubiri na kulikubali ; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Badala ya Waraka. Vitendo vya Mitume 5. 12-16
Injili. Luka 22. 24-30
 

St. Bartholomew

IDI YA MTAKATIFU MATHAYO MTUME

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, wewe kwa kinywa cha Mwanayo Mwenye-baraka ulimwita yule Mathayo, ili aache kutoza ushuru awe mtume na mhubiri; utuneemeshe nasi ya kuacha mambo ya kutamani-tamani, na kule kupenda mno mali ya dunia, kwamba nasi tupate kumfuata yeye huyo Mwanayo, Yesu Kristo; aishiye na kutawala pamoja nawe na Roho Mtakatifu, uli Mungu mmoja milele. Amina.

Waraka. 2 Wakorintho 4. 1-6
Injili. Mathayo 9. 9-13
 

St. Matthew

IDI YA MTAKATIFU MIKAELI NA MALAIKA PIA WOTE

Sala

EWE Mungu, Mkazi wa milele, huo utumishi wa malaika na binadamu umeuanziliza, umeupanga kwa taratibu ya ajabu; utujalie sisi kwa rehema zako, ya kwamba, kama hivyo wakutumikiavyo daima malaika zako watakatifu huko mbinguni, nasi watusaidie na kutulinda hapa duniani kwa utakavyowaagiza, kwa ajili ya Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Badala ya Waraka. Ufunuo 12. 7-12
Injili. Mathayo 18. 1-10
 

St. Michael & all Angels

IDI YA MTAKATIFU LUKA MHUBIRI

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, yule tabibu Luka, ambaye sifa yake i katika Injili, ulimwita wewe apate kuwa mhubiri wa Injili, na kupoza roho zao wanadamu: twakuomba ya kwamba tupozwe sisi maradhi yote ya roho zetu kwa dawa za afya za mafunzo aliyofunza yeye; kwa kustahili kwake Mwanayo Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. 2 Timotheo 4. 5-15
Injili. Luka 10. 1-7
 

St. Luke

IDI YA WATAKATIFU SIMONI NA YUDA MITUME

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, hili kanisa lako umelijenga juu ya misingi ya mitume na manabii, nalo jiwe lake kuu la pembeni ni yeye Yesu Kristo; utupe kuungamanishwa sana katika umoja wa roho, kwa yale mafunzo yao, hata tufanywe sisi hekalu takatifu lenye kukubaliwa na wewe; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. Yuda 1-8
Injili. Yohana 15. 17-27
 

St. Simon & St. Jude

IDI YA WATAKATIFU PIA WOTE

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, wewe umewaungamanisha wateule wako wote kwa maungamano ya umoja na shirika iliyo katika mwili wake wa siri yeye Mwanayo Kristo Bwana wetu; utupe nasi neema kuwafuata watakatifu wako wote waliobarikiwa kwa wema wa kila namna na mwendo wa haki, hata tuzifikilie na sisi furaha zisizosemeka, nazo ndizo ulizowatengezea hao wakupendao kweli; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Badala ya Waraka. Ufunuo 7. 2-12
Injili. Mathayo 5. 1-12
 

All Saints' Day

IDI YA MTAKATIFU MARIAMU MMAGIDALA
(July 22)

Sala

EWE Mwenyezi Mungu, Mwanayo Mwenyebaraka alimwita na kumtakasa Mariamu Mmagidala awe shahidi wa kufufuka kwake: uturehemu na kutujalia kwa neema yako tupozwe katika unyonge wetu wote, na kukutumikia siku zote katika uwezo wa maisha ya milele ya Mwokozi wetu, ambaye pamoja na wewe na Roho Mtakatifu huishi na kutawala, Mungu mmoja milele. Amina.

Waraka. 2 Wakorintho 5. 14-17
Injili. Yohana 20. 11-18
 

St. Mary Magdalene

This and the following commemoration are additions to the 1662 text, and are optional.

IDI YA KUGEUKA SURA
(August 6)

Sala

EWE Mungu, mbele ya kuteswa kwake Mwanayo mzaliwa pekee, ulifunua utukufu wake juu ya mlima mtakatifu; utujalie sisi watumishi wako kwamba tukiangalia kwa imani mwanga wa uso wake, tutiwe nguvu kuchukua msalaba, na kubadilishwa tuwe mfano mmoja na yeye, kutoka utukufu kufikilia utukufu; kwa yeye Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Waraka. 1 Yohana 3. 1-3
Injili. Mariko 9. 2-7

Transfiguration

 

Return to the 1662 Book of Common Prayer in Swahili

Web author: Charles Wohlers U. S. EnglandScotlandIrelandWalesCanadaWorld