TARATIBU YA KUZIKA MAITI
¶ Hapa ni kuangaliwa kwamba Taratibu hii haitumiwi kwa kuzika waliokufa hawajabatizwa, wawao wote, wala waliopigwa marufuku ya kanisa, wala waliojiua wenyewe.
¶ Yule Padre na makatibu humwendea yule maiti na kukutana naye langoni pa uwanda wa mazishi, humtangulia, kwamba ni kuingia msikitini, kwamba ni kwenda upande wa kaburi lake, huku wanena (au kuimba),
YESU akamwambia, Mimi ndimi huko kufufuliwa, nami ndimi maisha. Aaminiye kwangu ajapokuwa amekufa, ataishi. Na kila mtu aishiye na kuamini kwangu, hafi milele. Yohana 11. 25-26.
MIMI najua ya kuwa Mkombozi wangu yu hai, na mwisho atasimama juu ya nchi: hata 'ngovi yangu itakapokwisha kuharibika hivi, pasipokuwa na mwili wangu nitamwona Mwenyezi Mungu: naye nitamwona nafsi yangu, tena macho yangu yatamwangalia, wala si kana mgeni. Ayubu 19. 25-27.
KWANI hatukuingiana kitu ndani ya ulimwengu, kwa kuwa hata kutoka na kitu hatuwezi. 1 Timotheo 6. 7.
YEHOVA alitoa, na Yehova ametwaa; jina la Yehova na libarikiwe. Ayubu 1. 21.
¶ Hata wakiisha kuingia ndani ya msikiti, husomwa Zaburi hizi mojawapo, au zote mbili.
Dixi custodiam. Zaburi 39
NILISEMA, Nitazitunza njia zangu, nisije nikakosa kwa ulimi wangu : nitazuia kinywa changu kwa ukanda, akiwapo mbele yangu yule mbaya.
2. Nilikuwa sisemi, nilinyamaa kimya, nisitamke hata neno jema : maumivu yangu yakazidi.
3. Moyo wangu ukawa moto ndani yangu, na katika kuwaza kwangu moto ukawaka : nilisema kwa ulimi wangu.
4. Ewe Yehova, unijulishe mwisho wangu, na kiasi cha siku zangu ni kiasi gani : nijue jinsi nilivyo dhaifu.
5. Tazama, umefanya siku zangu kuwa mashubiri, maisha yangu kama si kitu mbele zako : ubatili tu ni kila mwanadamu ingawa amesitawi.
6. Binadamu huenda tu huko na huko kama kivuli, hufanya ghasia tu kwa ajili ya ubatili : huweka akiba wala hajui ni nani atakayeichukua.
7. Na sasa ninangojea nini, ewe Yehova : matumaini yangu ni kwako.
8. Uniokoe na maasi yangu yote : usinifanye laumu ya wapumbavu,
9. Nilinyamaza sikufumbua kinywa changu : kwani wewe ndiwe uliyeifanya.
10. Uniondolee pigo lako : kwa uadui wa mkono wako nimeangamia.
11. Ukimrudi mtu kwa kumkemea kwa ajili ya uovu wake, watowesha uzuri wake kama nondo : ubatili tu ni kila mwanadamu.
12. Usikie maombi yangu, ewe Yehova; utege sikio lako niliapo, usiyanyamalie machozi yangu : kwa maana mimi ni mgeni wako, msafiri kama baba zangu wote.
13. Uniachilie nipate nafuu: kabla sijaondoka nisiwepo tena.
Utukufu uwe kwa Baba, na kwa Mwana: na kwa Roho Mtakatifu ;
Kama vile mwanzo, na sasa : hata milele ni vivyo. Amina.
Domine refugium. Zaburi 90
EWE Bwana, wewe umekuwa makao yetu : kizazi baada ya kizazi.
2. Kabla haijazaliwa milima, kabla hujaiumba dunia : na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.
3. Wamrudisha mtu mavumbini : ukisema, Rudini, enyi wanadamu.
4. Kwani miaka elfu machoni pako ni kama siku ya jana ikiisha kupita : na kama kesha la usiku.
5. Wawagharikisha, huwa kama usingizi : asubuhi wa kama majani yameayo.
6. Asubuhi yachipka na kumea : jioni yakatika na kukauka.
7. Kwani tumetoweshwa kwa hasira yako : na kwa ghadhabu yako tumefadhaishwa.
8. Umeyaweka maovu yetu mbele zako : siri zetu katika mwanga wa uso wako.
9. Kwani siku zetu zote zimepita katika hasira yako : tumetoweshwa miaka yetu kama hadithi.
10. Siku za miaka yetu ni miaka sabuini, na ikiwa tuna nguvu miaka themanini : kiburi chake ni taabu na ubatili, kwani chapita upesi tukatokomea mara.
11. Ni nani aujuaye uwezo wa hasira yako : na ghadhabu yako kiasi cha kicho kilicho haki yako?
12. Basi utujulishe kuzihesabu siku zetu : nijipatie moyo wa hekima.
13. Urudi, ewe Yehova; hata lini? uwahurumie watumishi wako.
14. Utushibishe asubuhi kwa fadhili zako : nasi tutashangiria na kufurahi siku zetu zote.
15. Utufurahishe kwa kadiri ya siku ulizotutesa : kama miaka ile tuliyoona mabaya.
16. Matendo yako na yaonekane kwa watumishi wako : na adhama yako kwa watoto wao.
17. Na uzuri wa Yehova Mungu wetu uwe juu yetu : na kazi ya mikono yetu utufanyie thabiti, naam, kazi ya mikono yetu uifanye thabiti.
Utukufu uwe kwa Baba, na kwa Mwana: na kwa Roho Mtakatifu;
Kama vile mwanzo, na sasa : hata milele ni vivyo. Amina.
¶ Ndipo hapo hufuatana lile Somo, limetwaliwa katika Waraka wa kwanza wa mtakatifu Paulo aliowaandikia Wakorintho, Mlango wa kumi na tano.
|
1 Wakorintho 15. 20-58
ILA sasa Kristo amefufuliwa kutoka kwa wafu, naye amekuwa ni malimbuko ya hao waliolala. Kwani, kwa kuwa mauti yakaja kwa njia ya binadamu, kufufuka kwa wafu vivyo huja kwa njia ya binadamu. Kwani vivile kama wote wafavyo katika Adamu, vivyo katika Kristo wote watafanywa kuwa hai. Ila ni kila mmoja katika pahali pake mwenyewe; Kristo ni malimbuko; baadaye ni hao ambao ni wa Kristo katika kuja kwake. Kisha huja ule mwisho, hapo Kristo atakapompa Mwenyezi Mungu, yeye Baba, ule ufalme; hapo atakapoyabatilisha kila mamlaka na kila amri na uwezo. Kwani yapasa kwamba atawale yeye hata atakapowatia adui zake wote chini ya nyayo zake. Adui wa mwisho wa kutoweshwa ni mauti. Kwani, Aliviweka vitu vyote viwe chini ya nyayo zake. Ila hapo asemapo ya kwamba, Vitu vyote vimewekwa viwe chini, ni dhahiri ya kwamba yeye aliyeviweka vitu vyote viwe chini yake, hamo. Na hapo vitu, vyote vitakapowekwa viwe chini yake, ndipo hapo Mwana naye mwenyewe atawekwa chini ya huyo aliyeviweka vitu vyote chini yake, ili kwamba Mwenyezi Mungu awe vyote katika vyote.
Auje, watafanya nini hao wabatizwao kwa ajili ya wafu? Kwamba wafu hawafufuki kabisa, wamebatizwa kwa ajili ya wafu kwa maana gani? na sisi tumo katika hatari kila saa kwa maana gani? Kila siku nafa, naam, kwa majivuno yangu kwa ajili yenu, ndugu zangu, niliyo nayo katika Kristo Yesu Bwana wetu. Kwamba kwa hali ya ki-binadamu nilipigana na nyama za mwitu huko Efeso, nina, faida gani? Kwamba wafu hawafufuki, na tule, na tunywe, kwa kuwa kesho twafa. Msidanganyike; vikao vibaya huharibu tabia njema. Levuka kwa kutenda mema, nanyi msifanye dhambi; kwani wengine hawana kumjua Mungu; nanena haya kuwatahayarisha ninyi.
Kwenda mtu mmoja atanena, Je, wafu wafufuliwaje? Nao huja na mwili namna gani? Ewe mpumbavu, kile upandacho wewe hakipewi uhai, kikiwa hakijakufa; na hicho upandacho, hupandi ule mwili utakaokuwapo, lakini ni tembe tupu, huenda ikawa ni ya nganu, au nyingineyo yoyote; ila Mwenyezi Mungu huipa mwili vivile kama alivyopenda, na kila mbegu hupewa mwili wake mwenyewe.
Nyama zote si nyama moja: lakini iko nyama ya binadamu, na nyama nyingine ni ya nyama wa miguu minne, na nyingine ni ya nyuni, na nyingine ni ya samaki. Tena iko miili ya mbinguni, na miili ya nchi: lakini utukufu wa ile ya mbinguni ni aina mbali, na utukufu wa ile ya nchi ni aina mbali. Kuna utukufu wa jua, na mwingine wa mwezi, na mwingine wa nyota, kwani hufadhiliana nyota na nyota kwa utukufu. Na kufufuka kwao wafu ni vivyo hivyo. Hupandwa katika kuharibika, hufufuliwa katika hali isiyo ya kuharibika: hupandwa katika unyonge; hufufuliwa katika utukufu: hupandwa katika udhaifu; hufufuliwa katika nguvu: hupandwa mwili wa nafsi; hufufuliwa mwili wa roho. Kwamba kuna mwili wa nafsi na mwili wa roho pia uko. Ndipo yakaandikwa na haya, Mtu wa kwanza huyo Adamu akawa nafsi iliyo hai. Adamu wa mwisho akawa roho ihuishayo. Lakini ule uliokuwa wa roho, sio wa kwanza, lakini ni ule wa nafsi uliokuwa wa kwanza, baadaye ule ulio. wa roho. Mtu wa kwanza alitoka katika nchi; ni wa udongo; mtu wa pili alitoka mbinguni, naye ni Bwana. Jinsi alivyo huyo wa udongo, na hao wa udongo ni vivyo; na jinsi alivyo huyo wa mbinguni, na hao wa mbinguni ni vivyo. Tena, vivile kama tulivyochukua sura za huyo wa udongo, nasi vivyo tutachukua sura za huyo wa mbinguni.
Basi nanena neno hili, ndugu zangu, ya kwamba nyama na damu haviwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala kiharibikacho hakiwezi kukirithi hicho kisichoharibika. Hili ndilo, nawaambia ninyi jambo lililofichamana : Sisi hatutalala sote, ila sote tutabadilika, mara, kama kupesa na kufumbua, ipigwapo parapanda ya mwisho: kwani parapanda itavuma, na wafu watafufuliwa katika hali isiyo ya kuharibika, na sisi tutabadilika. Kwani imepasa huu uharibikao uvikwe kutoharibika, na huu upatikanao na mauti uvikwe kutokufa. Ila hapo huu uharibikao utakapovikwa kutoharibika, na huu upatikanao na mauti utakapovikwa kutokufa, ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, nalo ni hili, Mauti yamemezwa katika kushindwa. Ku wapi, ewe mauti, kushinda kwako? ki wapi, ewe mauti, chembe chako cha ushungu? Ushungu wa mauti ni dhambi; na nguvu za dhambi ni ile sheria: ila asante ni yake Mwenyezi Mungu atupaye kushinda kwa njia ya Yesu Kristo Bwana wetu. Kwa ajili ya hayo, ndugu zangu, wapenzi wangu, thubutikeni, msiweze kuondolewa, mfanye kazi kwa wingi katika Bwana kila wakati, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu si ya bure katika Bwana.
|
1 Corinthians 15:20 |
¶ Badala ya Zaburi hizi na Somo hili, moja katika Masomo yafuatanayo laweza kusomwa.
2 Wakorintho 4. 16-18 na 5. 1-10
Ufunuo 7. 9-17
Ufunuo 21. 1-7
|
Alternative Biblical texts (as in 1928 C of E Burial rite) |
¶ Hata wakifika Kaburini, wakati wa kumtengeneza yule maiti ili kumlaza ndani ya nchi, yule Padre hunena maneno haya, au yule Padre na wale makatibu huyaimba :
BINADAMU aliyezawa na mwanamke siku zake atakazoishi ni haba, nazo zilizojaa taabu. Yeye hutepuza kama vile ua, kisha huka twa : hukimbia kama kivuli kikimbiavyo, wala hasimami.
Tuwapo hai tu katika kufa; tumwendee nani tupate msaada tusipokuja kwako, ewe Bwana? nawe uliye na haki kuchukiwa kwa makosa yetu.
Na haya yote, ewe Bwana Mungu uliye mtakatifu sana, ewe Mola mwingi wa uwezo, ewe Mwokozi mtakatifu, mwenye rehema zote; usitutie katika maumivu ya uchungu ya kufa kwa milele.
Wewe, Bwana, wajua siri za mioyoni mwetu; usituzibie masikio yako ya rehema tukuombao, nawe utusamehe, ewe Bwana uliye mtakatifu kabisa, ewe Mwenyezi Mungu mwingi wa uwezo, ewe Mwokozi mtakatifu mwenye rehema, nawe ndiwe Mwamuzi mwenye haki wa milele, usituache saa yetu ya kufa kwa maumivu ya mauti yawayo yote tukatengwa nawe.
¶ Ndipo hapo, muda ule mwili ukitupiwa mchanga juu yake na wengine waliosimama kando, yule Padre hunena,
KWA maana ya hivyo alivyopendezewa Mwenyezi Mungu na kuitwaa roho yake huyu ndugu yetu mpenzi aliyefariki, sisi kwa ajili ya neno hili, twauweka mwili wake katika nchi: kilicho mchanga kirejee mchanga, kilicho ivu kirejee ivu, kilicho uvumbi kirejee uvumbi, kwa tumaini lililo yakini na imara la kufufuliwani kwa maisha ya milele, kwa Bwana wetu Yesu Kristo, atakayeugeuza mwili huu wa unyonge wetu uwe mfano mmoja na mwili wa utukufu wake, kwa kadiri ya kutenda kwake yeye awezavyo hata kuvitweza vitu vyote chini yake.
¶ Kisha husomwa au huimbwa,
NILISIKIA sauti iliyotoka mbinguni, ikineria, Andika, Heri ni yao wafu wafao katika Bwana tokea sasa; naam, yuanena huyo Roho, ya kwamba wapate kupumzika baada ya taabu zao za kazi.
¶ Kisha husoma yule Padre,
Bwana, uturehemu.
Kristo, uturehemu.
Bwana, uturehemu.
|
|
BABAETU uliye mbinguni, Jina lako litakaswe, Ufalme wako na uje, Mapenzi yako yatendeke juu ya nchi, Kama yatendekavyo mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kututosha. Nawe utusamehe makosa yetu, Kama nasi tulivyowasamehe watukosao. Nawe usitupeleke katika kujaribiwa, Utuokoe maovuni. Amina.
Padre
EWE Mungu, Mweza-wa-yote, zi hai pamoja nawe roho za waondokao huku katika Bwana; tena roho zao waaminifu waliopona katika taabu ya miili zi pamoja na wewe katika furaha na raha; sisi twakushukuru sana kwa kuwa umependa kumponya huyu ndugu yetu, umemwokoa na mashaka ya ulimwengu huu wa madhambi; na huku twaomba upende kwa fadhili za wema wako kufanya haraka kuitimiliza hesabu ya wateule wako, ili kwamba sisi tulio hai huku, pamoja 'na hao wenzetu wote waliokwisha kufariki dunia wenye imani ya kweli ya jina lako· takatifu pia sote, tupate kukamilika katika utimilifu wa heri, miili yetu na roho zetu, katika utukufu wako wa milele: kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
Sala
EWE Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, ndiwe Babaye Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye ndiye huko kufufuliwa, tena ndiye maisha: naye aaminiye kwake, ajapokuwa amekufa, ataishi; kisha kila mtu aishiye na kuamini kwake hafi kifo cha milele; tena ndiye aliyetufunza, kwa mtume wake mtakatifu yule Paulo, ya kwamba, tusisikitike kama watu wasiokuwa na tumaini wasikitikavyo, kwa ajili ya hao waliolala ndani yake; sisi twakunyenyekea sana, twaomba kwako, ewe Baba, kwamba utufufue sisi katika hiki kifo cha dhambi, ututie katika maisha ya haki; ili kwamba wakati tutakapofariki dunia hii, tupate kupumzika ndani yake yeye; nasi ndivyo ambavyo twatumaini kuwa amepumzika huyu ndugu yetu naye: hata iwe, katika kule kufufuliwa kwa watu wote, katika siku ya mwisho, kuwa sisi kupata radhi machoni pako; tupate na hiyo baraka, Mwanayo mpenzi wako umpendaye sana atakayowabarikia watu wote wakupendao na kukucha wewe, kwa kuwaambia, Njoni, enyi mliobarikiwa na Babaangu, mje muurithi ufalme mliotengezewa ninyi tokea kupigwa msingi ulimwengu: utuneemeshe hayo, Baba mwingi wa rehema, kwa Yesu Kristo, Mwombezi wetu aliyetukomboa. Amina.
|
Lord's Prayer |
¶ Sala iwezayo kutumiwa mbele ya Baraka.
EWE Mwenyezi Mungu, Baba wa rehema zote, Mpaji wa faraja yote; twakuomba uwahurumie wao waliao, ili kwa kukutwika wewe taabu zao zote, wajue faraja ya mapenzi yako; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
|
Alternative Blessing |
NEEMA ya Bwana wetu Yesu Kristo, na mapenzi ya Mwenyezi Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu, viwe pamoja nasi sote milele. Amina.
|
|
SIDJKRANI ZA WANAWAKE BAADA YA KWISHA KUZAA
¶ Wale wanawake, ukifika wakati wao wa kutoka kutawa kwao baada ya kujifungua, huingia msikitini hali wamevaa mavao ya heshima, huenda na kupiga magoti pahali pafaapo, kama ilivyo ada ya msikiti ule: au kama atakavyoamuru mwenye amri ya mambo haya:
KWA maana ya hivyo alivyopenda Mwenyezi Mungu kuwapa kwa wema wake ya' kujifungua salama, na alivyowaponya katika hiyo hatari kubwa mno ya uzazi : kwa ajili ya hayo ninyi mshukuruni Mwenyezi Mungu shukrani ya mioyoni sana, mseme,
¶ Ndipo hapo Padre husoma,
Dilexi quoniam. Zaburi 116
NAMPENDA Yehova kwa kuwa amesikiliza: sauti zangu na sala zangu.
2. Kwa maana amenitegea sikio lake : kwa hiyo niramlingana siku zangu zote.
3. Kamba za mauti zilinizunguka, shida za kuzimu zilinipata : niliona taabu na huzuni.
4. Nikalilingana jina la Yehova : ewe Yehova, nakuomba sana, uniokoe nafsi yangu.
5. Yehova ni mwenye neema na haki : naam, Mungu wetu ni mwenye rehema.
6. Yehova huwalinda wasio hila : nilidhilika akaniokoa.
7. Urudi, ewe nafsi yangu, rahani mwako : kwa kuwa Yehova amekutendea kwa ukarimu.
8. Kwani umeniponya nafsi yangu na mauti, macho yangu na machozi : na miguu yangu na kuanguka.
9. Nitaenenda mbele za Yehova : katika nchi ya walio hai.
10. Naamini, kwani nitasema : mimi niliteswa sana.
11. Mimi nilisema katika haraka yangu : wanadamu wote ni waongo.
12. Nimrudishie Yehova nini : kwa ukarimu wake wote alionitendea ?
13. Nitakipokea kikombe cha wokofu : nitalilingana jina la Yehova.
14. Nitaziondoa nadhiri zangu kwa Yehova : naam, mbele ya watu wake wote.
15. Ina thamani machoni pa Yehova : mauti ya watakatifu wake.
16. Ewe Yehova, hakika -mimi ni mtumishi wako : mtumishi wako, mwana wa kijakazi chako; umefungua vifungo vyangu.
17. Nitakutolea dhabihu ya kushukuru : nitalilingana jina la Yehova.
18. Nitaziondoa nadhiri zangu kwa Yehova : naam, mbele ya watu wake wote;
19. Katika nyua za nyumba ya Yehova : ndani yako, ewe Yerusalemu. Aleluya.
Utukufu uwe kwa Baba, na kwa Mwana: na kwa Roho Mtakatifu;
Kama vile mwanzo, na. sasa : hata milele ni vivyo. Amina.
Au hii, Zaburi 127
YEHOV A asipoijenga nyumba, waijengao wafanya kazi bure : Yehova asipoulinda mji, yeye aulindaye akesha bure.
2. Kazi yenu ni bure, ninyi mnao amka mapema na kukawia kwenda kulala, mnapokula chakula cha taabu : humpa mpenzi wake usingizi.
3. Wana ndio walio urithi wa Yehova : uzao wa tumbo ni thawabu.
4. Kama mishare mkononi mwa shujaa : ndivyo walivyo wana wa ujanani.
5. Yuna heri mtu yule aliyelijaza podo lake hivyo : naam, hawataona aibu wanapokuwa wakisema na adui langoni.
Utukufu uwe kwa Baba, na kwa Mwana: na kwa Roho Mtakatifu ;
Kama vile mwanzo, na sasa : hata milele ni vivyo. Amina.
¶ Ndipo hapo yule Padre hunena, Na tuombe.
Bwana, uturehemu.
Kristo, uturehemu.
Bwana, uturehemu.
|
BABAETU uliye mbinguni, Jina lako litakaswe, Ufalme wako na uje, Mapenzi yako yatendeke juu ya nchi; Kama yatendekavyo mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kututosha. Nawe utusamehe makosa yetu, Kama nasi tulivyowasamehe watukosao. Nawe usitupeleke katika kujaribiwa, Utuokoe maovuni. Amina.
Padre. Ewe Bwana, uwaokoe hawa vijakazi vyako;
Huitika. Wakutumainio wewe.
Padre. Uwe kwao ngome iliyo imara;
Huitika. Penye uso wa adui wao.
Padre. Ewe Bwana, utusikize maombi yetu;
Huitika. Kilio chetu kikufikilie uliko.
Padre.
Na tuombe.
EWE Mungu, Mweza-wa-yote, sisi tu miguuni pako twakushukuru kwa ajili ya ulivyopenda kuwaokoa hawa vijakakazi vyako na mambo ya uzazi, ambayo maumivu yake ni mengi na hatari yake ni kubwa mno; nasi twakunyenyekea, ewe Baba uliye na rehema, twakuomba, uwajalie huku katika maisha haya ya sasa kuwa waaminifu wa maisha, na kuwa watu wa kwenenda katika mwendo wao kama upendavyo wewe; na katika maisha yajayo, wawe washirika wa utukufu usio ukomo; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
¶ Wale wanawake wajao kumpa Mwenyezi Mungu shukrani na asante, hawana budi na kutoa ada; na pakishirikanwa Ushirika, yafaa waupokee Ushirika Mtakatifu.
|
Lord's Prayer |