The Book of Common Prayer
United States England Scotland Ireland Wales Canada World

    Chuo cha Sala ya Umoja (1662)
The 1662 Book of Common Prayer in Swahili

 

TARATIBU YA KUWABATIZA WATOTO MBELE YA WATU,

ambayo hutumiwa msikitini.

Watu na waonywe kwamba, ni la kufaa zaidi Ubatizo kutousongeza isipokuwa kwa siku za Jumapili au Idi nyingine, maana, waabuduo huzidi kukutanika kuwa tele kwa siku hizo; nalo neno hili liliagizwa, huku ili kwamba mkutano upate kuwashuhudia wabatizwao hapo wapokewapo katika jumla ya Kanisa la Kristo; huku kwamba katika kubatizwa kwao wale watoto jamii ya watu wazima waliopo wapate kukumbus1zwa walivyoahidi wenyewe kwa Mwenyezi Mungu kila mmoja katika kubatizwa kwake. Kwa ajili ya hayo yafaa Ubatizo kuusongeza kwa kutumia lugha hiyo itumikayo sana katika nchi. Pamoja na haya (kwa wakati wa kufaa), hubatizwa watoto kwa siku nyingine iwayo yote.

Nawe angalia, kila mtoto atakayebatizwa, wa kiume huwa na madhamini watatu, wawili waume, mmoja mke ; na mtoto wa kike, huwa na madhamini watatu, wawili wake, mmoja mume.

Na wakipatikana watoto watakao kubatizwa, wazazi wao humpa habari yule Padre kabla ya usiku wa kuamkia siku yake, au asubuhi yake, mbele ya Sala ya Asubuhi. Ndipo hapo wale madhamini na wenye nao watoto huenda na hukaa karibu ya fonti, ili kuwapo tayari; kwamba ni Sala ya Asubuhi, baada ya kusoma Somo la pili; kwamba ni Sala ya Jioni, baada ya kusoma Somo la pili; kama atakavyoona vyema yule Padre kuyaamrisha. Na yule Padre huenda penye fonti (nayo hujazwa maji safi wakati huo), akiisha kusimama husema:

JE, watoto hawa wamebatizwa tangu hapo, hawajabatizwa?

Wakisema, La, hawajabatizwa, ndipo hapo yule Padre huendelea kunena:

ENYI mpendwao sana, kwa ajili ya vile watu wote walivyo chukuliwa mimba na kuzaliwa katika dhambi, na kwa kuwa Mwokozi wetu Kristo alinena, Hakuna mtu awezaye kuingia katika ufa1me wa Mungu ila aliyezaliwa mara ya pili, aliyezaliwa uzazi mpya kwa maji na Roho Mtakatifu: mimi nawataka sana ninyi mmlingane Mungu Baba kwa Bwana wetu Yesu Kristo, apate kuwapa watoto hawa kwa rehema zake zisizo mpaka neno moja ambalo kwa asili yao hawawezi kuwa nalo: nalo ni la wao kubatizwa kwa maji na Roho Mtakatifu, na kukaribishwa katika Kanisa lake Kristo lililo takatifu, na kufanywa kuwa via viliyo hai vya mumo Kanisani.

Ndipo hapo Padre hunena,

Na tuombe.

EWE Mungu Mweza-wa-yote huna mwanzo huna mwisho: wewe kwa rehema zako kuu ulimwokoa Nuhu uliwaokoa na wa nyumbani mwake kwa ile safina, ukawa ponya wao na kule kuangamia majini; nawe uliwaongoza salama watu wako wana wa Isiraeli katikati ya Bahari Nyekundu, kwa kuonya humo mfano wa ubatizo wako mtakatifu: kisha kwa kubatizwa kwake Mwanayo Mpenzi wako sana Yesu Kristo, katika mto wa Yorodani, uliyatakasa maji kwa kuosha dhambi kwa maana ya ndani: sisi tuliopo twakuomba kwa ajili ya rehema zako zisizo mpaka, uwaangalie watoto hawa kwa rehema, uwaoshe na kuwatakasa kwa Roho Mtakatifu: ili kwamba pamoja na kuokoka kwao na ghadhabu zako wakaribishwe na safinani mwa Kanisa lake Kristo; kisha, kwa vile watakavyokaa katika imani, na kuwa hali ya furaha kwa kutumaini, na kukazwa shina lao katika kupendana, huku kuyavuka kwao mawimbi ya ulimwengu huu wa dhiki na taabu, wafikilie mwisho katika nchi ya maisha yaendeleayo milele, wapate kutawala pamoja na wewe katika nchi hiyo milele na milele: kwa Bwana wetu, Yesu Kristo. Amina.

EWE Mwenyezi Mungu, mambo yote wayaweza wewe, wala hushindwi na kifo; Msaada wao wote walio na uhitaji, Auni yao jamii ya wakukimbiliao, Maisha yao waaminio, Kufufuliwani kwao waliokufa, pia hayo ni wewe: sisi twakulingana, twawaombea watoto hawa, ili hivi wajavyo katika ubatizo wako mtakatifu, walipate ondoleo la madhambi yao kwa uzazi mpya wa rohoni. Uwapokee, ewe Bwana, kama ulivyoahidi kwa Mwanayo Mpenzi wako sana, pale aliponena, Ombeni mtapewa: tafuteni mtaona: bisheni mtafunguliwa. Na sasa na iwe vivyo: utupe tukuombao: tutafutao na tuone: utufungulie mlango sisi tubishao: ili kwamba watoto hawa wafurahie baraka iendeleayo milele ya josho lako la mbinguni, na kupata kuufikilia ufalme wa milele uliotuahidi kwa Kristo, Bwana wetu. Amina.

Ndipo hapo husimama wale watu, Padre hunena,
 

Public Baptism of Infants

Yasikizeni maneno ya Injili iliyoandikwa na mtakatifu Mariko, Mlango wa kumi, Kifungu cha kumi na tatu.

IKAWA watu kumpelekea watoto apate kuwagusa; wale wanafunzi wakiwakemea waliowaleta. Yesu akiona yale yakamchukiza, akawaambia, Waacheni watoto wanijilie, msiwakanyeni: kwani ufalme wa Mwenyezi Mungu ni wa kama hawa. Ni kweli nawaambia, asiyeupokea ufalme wa Mwenyezi Mungu kama vile mtoto, haingii ndani yake kamwe, awaye yote. Kisha akawachukua mikononi mwake, ikawa kuwa barikia, huku akiwawekea mikono.

Baada ya kwisha kusomwa Injili hii, yule Padre huonya maonyo hayo kwa kufupiza, katika maneno ya hiyo Injili.

ENYI wapenzi, katika Injili hii mmeyasikia maneno ya Mwokozi wetu Kristo; alivyoamuru kuletewa kwake watoto, na alivyowalaumu wale waliotaka kuwatenga naye; na awatakavyo watu wote wafuate mambo yao yasiyokuwa na uovu. Mmeona jinsi alivyoweka wazi kwa ishara zake na vitendo vyake vya nje kuwa yu radhi moyo wake na watoto wale, kwani aliwachukua mikononi mwake, akawawekea mikono na kuwa barikia. Basi, msitie shaka, aminini tu ndani ya mioyo yenu, ya kuwa atawawele a radhi watoto hawa nao kuwakaribisha kwake; tena atawachukua kwa mikono ya rehema zake; atawapa na baraka ya maisha ya milele, na kuwafanya wawe washirika wa ufalme wake usio mwisho. Kwa ajili ya hayo, sisi ambao tu watu tuliopewa hakika hivi ya kuwapenda kwake watoto hawa Babaetu wa mbinguni kama ilivyowekwa wazi na Yesu Kristo Mwanawe, nasi hatuna shaka ya kuikubali kwake hii kazi yetu ya mapenzi, katika kuwaleta watoto hawa hata katika ubatizo wake mtakatifu; na tumshukuru kwa imani na ibada ya kweli, tuseme,

EWE Mungu Mweza-wa-yote, huna mwanzo huna mwisho; nawe ndiwe Babaetu wa mbinguni; sisi tu miguuni pako, twakuambia asante kwa ulivyotukirimu ya kutuita hata tukapata kuijua neema yako, na kuamini kwako: utuongeze ujuzi huo, uikaze mioyoni mwetu imani hiyo milele. Watoto hawa uwape Roho wako Mtakatifu, wapate kuzawa uzazi ulio mpya, na kufanywa kuwa watu wa kuurithi wokofu usio mwisho: kwa ajili yake yeyule Bwana wetu, Yesu Kristo, aishiye na kutawala pamoja nawe na Roho Mtakatifu, sasa na hata milele. Amina.

Ndipo hapo yule Padre husema na wale madhamini maneno haya:

ENYI niwapendao sana, watoto hawa mmewaleta hapa, wapate kubatizwa, mmeomba ya kwamba Bwana wetu Yesu Kristo awe radhi kuwapokea awaondolee dhambi zao, awatakase kwa Roho Mtakatifu, awape na ufalme wa mbingu, na uzima wa milele. Nanyi mmesikia jinsi alivyoahidi Bwana wetu Yesu Kristo, humo katika Injili yake, kwamba atatupa mambo hayo yote mliyoomba: naye ahadi hiyo hakosi yeye kwa upande wake, ataishika na kuitimiza. Basi kwa ajili ya hayo, baada ya ahadi aliyoahidi Kristo, inawapasa watoto hawa nao kwa upande wao, kuahidi kwa ndimi zenu madhamini, ya kwamba, wakiisha kufikilia umri wa kujitweka wenyewe ahadi hii, watoto hawa watamkataa Shetani na kazi zake zote, na kuliamini daima Neno lake Mwenyezi Mungu lililo takatifu, na kuyashika maagizo yake kwa kutii.

Basi kwa ajili ya hayo nakuuliza:
 

Mark 10:13

JE, wewe kwa jina lake mtoto huyu, wamkataa Shetani na kazi zake zote, na furaha na utukufu visivyofaa vya ulimwengu huu, na kule kuyatamani-tamani mambo hayo yote kwa shauku; pamoja na tamaa za mwilini, hata uwe wewe kukataa kuvifuata na kuchukuliwa navyo?
    Hujibu. Navikataa vyote.

Padre

JE, wewe waamini kwa Mungu Baba Mwenyezi, Muumba mbingu na nchi?
    Na kwa Yesu Kristo, Mwanawe mzaliwa pekee, Bwana wetu? Na ya kuwa alitungishwa mimba na Roho Mtakatifu, akazaliwa na Mwanamwali Mariamu; tena kuwa aliteswa katika enzi ya Pontio Pilato; akasalibiwa, akafa, akazikwa; akashuka na kuingia kuzimu, hata siku ya tatu akasimama tena, ametoka kwa wafu; kisha akapaa na kuingia mbinguni; tena ameketi upande wa mkono wa kuume wa Mwenyezi Mungu Baba; ndiko atakakotoka kuja tena, katika mwisho wa ulimwengu, kuwaamua walio hai hata waliokufa?
    Nawe waamini kwa Roho Mtakatifu; Kanisa takatifu lililo ulimwenguni mote; Ushirika wa watakatifu; Madhambi kusamehewa; Mwili kufufuka; na Maisha ya milele baada ya mauti?
    Hujibu. Haya yote ninayakubali sana kuyaamini.

Padre

JE, wataka ubatizwe katika imani hii?
    Hujibu. Nataka.

Padre

BASI, wataka kuyafuata mapenzi matakatifu ya Mwenyezi Mungu kwa kuyatii, na kuyashika maagizo yake; uyaandame hayo tu siku zote utakazokuwa hai?
    Hujibu. Nataka.

Ndipo hapo Padre hunena,

EWE Mwenyezi Mungu mwenye rehema, watoto hawa uwajalie ya kwamba kwa vile atakavyo zikwa Adamu wa kale aliye ndani yao, wapewe mtu mpya kufufuka ndani yao. Amina.
    Uwajalie shauku zote za mwili zife ndani yao; na mambo yote yatakwayo na Roho yawe hai, yaongezeke daima ndani yao. Amina.
    Uwajalie kuwa na uwezo na nguvu, wapate kushinda kwa furaha Shetani na ulimwengu na mwili. Amina.
    Umjalie kila mmoja atakayewekwa nafsi yake kwako wewe pahali hapa kwa utumishi wetu sisi na usongezi wetu sisi, kuvikwa neema za mbinguni na kupewa thawabu ya milele, kwa rehema zako, ewe Bwana Mungu utukuzwaye, uishiye hali umetawala mambo yote, milele. Amina.

EWE Mungu, Mweza-wa-yote, wewe uli hai milele; huyo Mwanayo Mpenzi wako sana sana Yesu Kristo, kwa kutusamehe madhambi yetu, alitokwa na damu na maji sambamba katika ubavu wake ulio wa thamani sana, akawapa na amri wanafunzi wake, ya kwenda kuwafanya wanafunzi mataifa wote, na kuwabatiza, kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu; twakuomba utege masikio yako kwetu mkutano wako; nawe uyatakase maji haya yawe njia ya kuosha dhambi kwa maana ya ndani; uwajalie watoto hawa waendao kubatizwa humo hivi sasa, wawe wenye kupokea neema yako iliyo timia, na kukaa daima miongoni mwa wanayo waaminifu wateule wako; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Ndipo hapo yule Padre huwachukua wale watoto mmojammoja mikononi mwake, akiwaambia wale madhamini,

Mpeni jina mtoto huyu
 

Questions of godparents

Naye Padre humtaja jina lake kwa kufuata lile wamwambialo, kisha (wakiwa wanampa hakika ya kuwa atayaweza bila shaka), humtia mle ndani ya maji kwa kumwangalia asije akapatikana na madhara, akinena,

FULANI, mimi nakubatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina.

Lakini watakapompa hakika ya kuwa hana nguvu sawasawa yule mtoto, hutosha kumwagia yale maji, huku yuanena kama yaliyotangulia,

FULANI, mimi nakubatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina.

Ndipo hapo hunena yule Padre,

SISI twampokea mtoto huyu katika mkutano wa kundi lake Kristo, * nasi twamtia alama ya msalaba ya kuonyesha kwamba baadaye hataona haya kuikiri imani ya Kristo msalibiwa, na kupigana kiume na dhambi na ulimwengu na Shetani, chini ya beramu yake; na kwendelea kuwa askari mwaminifu na utumishi wa Kristo, hata maisha yake ya duniani yaishe. Amina.
 

The Baptism

 

* Ndipo hapo yule Padre humpiga alama ya msalaba yule mtoto katika japa la uso.
 

 

Ndipo hapo Padre hunena,

HIVI, enyi ndugu zangu mpendwao sana, tuwaonavyo watoto hawa kuwa wamezaliwa uzazi mpya, na kutuliwa katika mwili wa Kanisa la Kristo, na tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa mambo hayo mema: nasi tumwombe kwa umoja wa hali, watoto hawa wayapishe maisha yao yanayosalia duniani kwa mfano wa mwanzo huu.

Ndipo hapo hupiga magoti pia wote na kusema,
 

 

BABAETU uliye mbinguni, Jina lako litakaswe, Ufalme wako na uje, Mapenzi yako yatendeke juu ya nchi, Kama yatendekavyo mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kututosha. Nawe utusamehe makosa yetu, Kama nasi tulivyowasamehe watukosao. Nawe usitupeleke katika kujaribiwa, Utuokoe maovuni. Amina.

Ndipo hapo hunena yule Padre,

TWAKUSHUKURU sana, ewe Baba mwingi wa rehema, kwa kuwa watoto hawa umeridhia kuwapa uzazi mpya kwa Roho wako Mtakatifu, na kuwakubali kuwa wanao wewe kwa ulezi wako ukawatia katika Kanisa lako lililo takatifu. Nasi hivi tulivyo miguuni pako twaomba kwako kwa unyenyekevu, kwamba watoto hawa, wali hali ya kufa na kutokana na dhambi, na kuwa hai kwa kuilekea haki, na kuwa ni watu waliozikwa pamoja na Kristo katika mauti yake: uwape kumsalibu yule mtu wa kale, na kukomesha kabisa mwili wote wa dhambi pia : na ya kwamba, hivyo walivyopewa kuwa washirika wa kufa kwake Mwanayo, na wawe vivyo washirika wa kufufuka kwake; hata iwe mwishowe, baada ya haya, pamoja na waliobaki katika Kanisa lako takatifu, wao nao wapate kuwa watu wa kuurithi ufalme wako usiokuwa na mwisho: kwa Bwana wetu, Yesu Kristo. Amina.

Hapo ndipo husimama wote; Padre huwaambia wale madhamini maonyo haya:
 

Lord's Prayer

KWA maana ya vile walivyoahidi watoto hawa kwa ndimi zenu ninyi madhamini wao, ya kumkataa Shetani na kazi zake zote, na kuamini kwa Mwenyezi Mungu na kumtumikia, inawapasa ninyi kukumbuka kwamba fungu lenu lililowapasa kila mmoja, ni kuangalia kwamba watoto hawa wafunzwe hapo watakapokwisha kuwa ni watu wa kuelewa nayo, jinsi zilivyo kubwa hizo nadhiri na ahadi na amana walizozikiri hapa kwa ndimi zenu. Nao kwamba wapate kuyajua zaidi mambo hayo, sharti ni kuwataka wasikize hotuba; na sana ni kuwatengezea ya wao kujifunza Imani ya Mitume, na Sala ya Bwana, na zile Amri Kumi, kwa lugha ya nchi waketiyo, na kujifunza mambo yote yaliyobaki ambayo yampasa mtu wa Kikristo kuyajua na kuyaamini, wapate kuwa hali njema roho zao; tena ni kuwalea hali ya heshima wapate kuishi maisha yao katika kicho cha Mungu na dini ya Ukristo; huku mkikumbuka kuwa huu ubatizo watuonya mfano wa hali yetu tuikiriyo; nayo ni ya kumwandama Mwokozi wetu Kristo kwa kielelezo chake alichotuonya, na kufananishwa hali zetu na hali yake; ili kwamba, kama yeye alivyokufa na kufufuka kwa ajili yetu, sisi nasi tulio-batizwa tuwe watu wa kufa na kutokana na dhambi, na kufufukia haki; huku tukiendelea katika kuzifisha tamaa zetu mbovu na uharibifu wetu, na kuongea kila siku katika kila lipasalo heshima na uchaji-wa-Mungu wa maisha.

Hapo ndipo atakapoongeza kusema haya,

NINYI sharti ni kutunza kwamba watoto hawa wapelekwe kwa Bishopu wapate kuwekewa mikono na yeye, hapo watakapokwisha kujua kuisema Imani, na Sala ya Bwana, na zile Amri Kumi, kwa lugha ya nchi waketiyo; na kuongezewa mafunzo yaliyo katika Katekisimo ya kanisa yaliyotengezwa tangu hapo kwa ajili ya hayo.

Nao Ubatizo ukile twa wakati usio wa Sala ya Asubuhi au ya Jioni, Padre awafumue wale watu waliokutanika kwa kunena,

BWANA na awabarikie na 'kuwalinda, Bwana na awaangazie uso wake, awape neema, Bwana na awainulie nuru ya uso wake, na kuwapa amani, sasa na hata milele. Amina.

Ni yakini sana, kwa Neno la Mungu, ya kuwa watoto walio-batizwa, wakija hawajatenda dhambi za matendoni, wameokoka watoto hawa hawana shaka.

Ili kuondoa kila shida na tashwishi katika itumiwavyo alama ya msalaba katika kubatiza: mafunuo ya hakika ya maana yake, na sababu zilizoiacha ikahifadhiwa mumo alama hiyo hupatikana katika Kanuni ya Thelathini, iliyoanza kutangazwa mwaka elfu mia sita na nne.
 


 

Exhortation to godparents

UBATIZO WA FARAGHA KUWASONGEZEA WATOTO WACHANGA NYUMBANI

Mapadre wa kila msikiti na wawaonye wenyeji mara kwa mara ya kwamba wasikawishe ubatizo wa watoto wao baada ya Jumapili ya kwanza au ya pili iandamayo siku ya kuzaliwa kwake, au baada ya Idi nyingine iandamayo katikati, isipoonekana sababu ambayo ni kubwa na maana, kama atakavyoiona ina haja yule Padre.

Nao wawaonye ya kwamba, watakapokuwa hawana sababu kubwa au haja kubwa kama hiyo wasiwatakie watoto wao kubatizwa nyumbani mwao. Lakini watakapopatikana na udhuru, hapo husongezwa ubatizo kwa kufuata namna hii :

Kwanza, yeye Padre wa msikiti (au asipopatikana huyu, ni Padre mwingine aliye na amri sheriani apatikanaye awaye yote) na waliopo wote na wamlingane Mwenyezi Mungu, wasome Sala ya Bwana, na katika zile sala zilizoamriwa kusomwa hapo mbele katika Kawaida ya Kuwabatiza Watoto mbele ya Watu, kadiri ya watakazopata kuzisoma, kama watakazowahi kwa majira waliyo nayo na haja iliyopo. Kisha baadaye yule mtoto hupewa jina na mmojawapo wale waliopo, Padre akamwagia maji, kwa kunena maneno haya:
 

Private Baptism of Children

FULANI, mimi nakubatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina.

Ndipo hapo hupiga magoti jamii ya waliopo, yule Padre humshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kunena:

TWAKUSHUKURU sana, ewe Baba mwingi wa rehema, kwa kuwa mtoto huyu umeridhia kumpa uzazi mpya kwa Roho wako Mtakatifu, na kumkubali kuwa mwanayo kwa ulezi wako, na kumtia katika mwili wa Kanisa lako lililo takatifu. Nasi hivi tulivyo miguuni pako, twaomba kwako kwa unyenyekevu ya kwamba hivi alivyopewa kuwa mshirika wa kufa kwake Mwanayo, na awe vivyo mshirika wa kufufuka kwake: hata iwe mwishowe baada ya haya, pamoja na waliobaki katika watakatifu wako wateule, apate kuurithi ufalme wako usio mwisho; kwa yeye huyo Mwanayo Bwana wetu, Yesu Kristo. Amina.

Nao wasitie shaka ya mtoto aliyebatizwa hivyo kuwa amebatizwa kama ifaavyo sheriani na itoshavyo katika haki, hata amekuwa hafai kubatizwa mara ya pili aliyebatizwa hivyo. Ila pamoja na haya, atakapojaliwa kuishi na kukua, mtoto aliyebatizwa kwa kufuata kawaida hii, afaa kuchukuliwa msikitini ili kwamba, akiwa ni Padre wa msikiti aliyembatiza mtoto yule, upewe hakika dhahiri ule mkutano wa kanisani ya kweli ya kawaida ya ubatizo iliyo tangulia kutumiwa faragha: na mambo yawapo ni hayo husema hivi :
 

The Baptism

MIMI nawapa hakika ya mtoto huyu kuwa nilimbatiza, kama ilivyo pasa na kuagizwa na kawaida ya Kanisa, majira kadhawakadha, pahali kadhawakadha, mbele ya mashahidi kadhawakadha.

Lakini ikiwa mtoto yule alibatizwa na Padre mwingine afaaye sheriani awaye yote, ndipo hapo yule Padre wa msikiti wa pahali alipozaliwa na kubatizwa mtoto yule huuliza na kujaribu, apate kutambua kuwa alibatizwa kwa njia ya' sheria, au hakubatizwa. Na hapo, hao wamletao mtoto awaye yote msikitini, watakapojibu kwamba mtoto amekwisha kubatizwa, basi wakati huo yule Padre na azidi kuwauliza, anene,

MTOTO huyu alibatizwa na nani?
    Waliokuwapo ni nani na nani, wakati aliobatizwa mtoto huyu?
    Kwa ilivyowezekana mambo mengine yapasayo Sakramenti hii kukosekana, kwa sababu ya fadhaa au haraka watu waliyo nayo zamani za dhiki kama hizo, mimi kwa ajili ya hayo nawauliza tena:
    Mtoto huyu alibatizwa kwa kutumia kitu gani?
    Mtoto huyu alibatizwa kwa kutumia maneno gani?

Hata ikiwa, kwa vile wamjibuvyo masiala haya wale waliomleta mtoto yule, ameyaona mambo yale yote kuwa yalitendeka kama ipasavyo, ndipo hapo yeye hambatizi mtoto yule mara ya pili, ila humkaribisha kama aliye katika kundi la Wakristo wa kweli, kwa kunena maneno haya,

MIMI nawapa hakika ya jambo hili kuwa lilitendeka vyema lote kwa kufuata taratibu yake kama ambavyo yafaa katika kubatizwa kwake huyu mtoto: naye angawa alizaliwa hali yuna dhambi ya asili, hali yu chini ya ghadhabu zake Mwenyezi Mungu: lakini sasa kwa josho la kuzawa uzazi mpya katika ubatizo amekaribishwa mtoto huyu katika miongoni mwa wana wa Mungu walio na urithi wa maisha ya milele: kwani Bwana wetu Yesu Kristo hawakatai watoto namna hii kuwarehemu na kuwaneemesha, ila kuwaita waje kwake kwa mwito wa mapenzi yake yaliyozidi sana, kama Injili takatifu ilivyo-shuhudia kwa kutuza mioyo yetu, kwa kutumia maneno kama haya:
 

Clergy certification

Mariko 10. 13-16

IKAWA watu kumpelekea watoto apate kuwagusa; wale wanafunzi wakiwakemea waliowaleta. Yesu akiona yale yakamchukiza, akawaambia, Waacheni watoto wanijilie, msiwakanyeni: kwani ufalme wa Mwenyezi Mungu ni wa kama hawa. Ni kweli nawaambia asiyeupokea ufalme wa Mwenyezi Mungu kama vile mtoto, haingii ndani yake kamwe, awaye yote. Kisha akawachukua mikononi mwake, ikawa kuwabarikia, huku akiwawekea mikono.

Baada ya kwisha kusomwa Injili, yule Padre huonya maonyo haya, kwa kufupiza, katika maneno ya hiyo Injili.:

ENYI wapenzi, katika Injili hii mmeyasikia maneno ya Mwokozi wetu Kristo; alivyoamuru kuletewa kwake watoto na alivyowalaumu wale waliotaka kuwatenga naye; na awa taka vyo watu wote kufuata mambo yao yasiyokuwa na uovu. Mmeona jinsi alivyoweka wazi kwa ishara zake na vitendo vyake vya nje kuwa yu radhi moyo wake na watoto wale: kwani aliwachukua mikononi mwake, akawawekea mikono, na kuwabarikia. Basi, msitie shaka, aminini tu ndani ya mioyo yenu, ya kuwa amemwelea radhi mtoto huyu naye kumkaribisha kwake: amempiga na pambaja kwa mikono ya rehema zake; (kama alivyoahidi katika Neno lake takatifu), atampa baraka ya maisha ya milele na kumfanya kuwa mshirika wa ufalme wake usio mwisho. Kwa ajili ya hayo, sisi ambao tu watu tuliopewa hakika hivi, ya kumpenda kwake mtoto huyu Babaetu wa mbinguni kama ilivyowekwa wazi na Yesu Kristo Mwanawe: na tumshukuru kwa imani na ibada ya kweli, tuiseme sala aliyotufunza Bwana wetu nafsi yake:
    Babaetu uliye mbinguni, Jina lako litakaswe, Ufalme wako na uje, Mapenzi yako yatendeke juu ya nchi, Kama yatendekavyo mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kututosha. Nawe -utusamehe makosa yetu, Kama nasi tulivyowasamehe watukosao. Nawe usitupeleke katika kujaribiwa, Utuokoe maovuni. Amina.

EWE Mungu Mweza-wa-yote, huna mwanzo huna mwisho; nawe ndiwe Babaetu wa mbinguni; sisi tu miguuni pako, twakuambia asante kwa ulivyotukirimu ya kutuita hata tukapata kuijua neema yako, na kuamini kwako: utuongeze ujuzi huo, uikaze mioyoni mwetu imani hiyo milele. Mtoto huyu umpe Roho wako Mtakatifu, apate kuzawa uzazi ulio mpya, na kufanywa kuwa mtu wa kuurithi wokofu usio mwisho: kwa ajili yake yeyule Bwana wetu, Yesu Kristo, aishiye na kutawala pamoja nawe na Roho Mtakatifu, sasa na hata milele. Amina.

Ndipo hapo yule Padre huuliza jina lake mtoto yule, hata wakiisha kulitamka palepale wale madhamini jina lake, yule Padre hunena,
 

Mark 10:13

JE, wewe, kwa jina la mtoto huyu, wamkataa Shetani na kazi zake zote, na furaha na utukufu visivyofaa vya ulimwengu huu, na kule kuyatamani-tamani mambo hayo· yote kwa shauku: pamoja na tamaa za mwilini, hata uwe wewe kukataa kuvifuata na kuchukuliwa navyo?
    Hujibu. Navikataa vyote.

Padre

JE, wewe waamini kwa Mungu Baba, Mwenyezi,. Muumba mbingu na nchi ?
    Na kwa Yesu Kristo, Mwanawe mzaliwa pekee, Bwana wetu? Na ya kuwa alitungishwa mimba na Roho Mtakatifu, akazaliwa na Mwanamwali Mariamu: tena kuwa aliteswa katika enzi ya Pontio Pilato: akasalibiwa, akafa, akazikwa; akashuka na' kuingia kuzimu; hata siku ya tatu akasimama tena ametoka kwa wafu; kisha aka paa na kuingia mbinguni; tena ameketi upande wa 'mkono wa kuume wa Mwenyezi Mungu Baba; ndiko atakakotoka kuja tena, katika mwisho wa ulimwengu, kuwaamua walio hai hata waliokufa?
    Nawe waamini kwa Roho Mtakatifu: Kanisa takatifu lililo ulimwenguni mote: Ushirika wa watakatifu: Madhambi kusamehewa: Mwili kufufuka: na Maisha ya milele baada ya mauti?
    Hujibu. Haya yote ninayakubali sana kuyaamini.

Padre

BASI, wataka kuyafuata mapenzi matakatifu ya Mwenyezi Mungu kwa kuyatii, na kuyashika maagizo yake; uyaandame hayo tu siku zote utakazokuwa hai?
    Hujibu. Nataka.

Ndipo hapo yule Padre hunena,
 

Questions of godparents

SISI twampokea mtoto huyu katika mkutano wa kundi la Kristo, nasi twamtia alama ya msalaba* ya kuonyesha ya kwamba baadaye hataona haya kuikiri imani ya Kristo msalibiwa, na kupigana kiume na dhambi na ulimwengu na Shetani, chini ya beramu yake, na kwendelea kuwa askari mwaminifu na utumishi wa Kristo, hata maisha yake ya duniani yaishe. Amina.

Ndipo hapo yule Padre hunena,

HIVI, enyi ndugu zangu mpendwao sana, tumwonavyo mtoto huyu kuwa amezaliwa uzazi mpya, na kutuliwa katika mwili wa Kanisa la Kristo, na tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa mambo hayo mema, nasi tumwombe kwa umoja wa hali, mtoto huyu ayapishe maisha yake yanayosalia duniani kwa mfano wa mwanzo huu.

Ndipo hapo yule Padre hunena,

TWAKUSHUKURU sana, ewe Baba mwingi wa rehema, kwa kuwa mtoto huyu umeridhia kumpa uzazi mpya kwa Roho wako Mtakatifu, na kumkubali kuwa mwanayo wewe kwa ulezi wako, ukamtia katika mwili wa Kanisa lako lililo takatifu. Nasi hivi tulivyo miguuni pako, twaomba kwako kwa unyenyekevu, kwamba mtoto huyu, ali hali ya kufa na kutokana na dhambi, na kuwa hai kwa kuilekea haki, na kuwa ni mtu aliyezikwa pamoja na Kristo katika mauti yake: umpe kumsalibu yule mtu wa kale, na kuukomesha kabisa mwili wote wa dhambi : na ya kwamba, hivyo alivyopewa kuwa mshirika wa kufa kwake Mwanayo, na awe vivyo mshirika wa kufufuka kwake; hata iwe mwishowe, baada ya haya, pamoja na waliobaki katika Kanisa lako takatifu, yeye naye apate kuwa mtu wa kuurithi ufalme wako usiokuwa na mwisho: kwa Bwana wetu, Yesu Kristo. Amina.

Hapo ndipo husimama wote; Padre huwaambia wale madhamini maonyo haya:
 

Reception

* Ndipo hapo yule Padre humpiga alama ya msalaba yule mtoto katika japa la uso.

KWA maana ya vile alivyoahidi mtoto huyu kwa ndimi zenu ninyi madhamini wake, ya kumkataa Shetani na kazi zake zote, na kuamini kwa Mwenyezi Mungu na kumtumikia, inawapasa ninyi kukumbuka kwamba fungu lenu lililowapasa kila mmoja, ni kuangalia kwamba mtoto huyu afunzwe, hapo atakapokwisha kuwa ni mtu wa kuelewa nayo, jinsi zilivyo kubwa hizo nadhiri na ahadi na amana alizozikiri hapa kwa ndimi zenu. Naye kwamba apate kuyajua zaidi mambo hayo, sharti ni kumtaka asikize hotuba; na sana ni kumtengezea ya yeye kujifunza Imani ya Mitume, na Sala ya Bwana, na zile Amri Kumi, kwa lugha ya nchi aketi yo, na kujifunza mambo yote yaliyobaki ambayo yampasa mtu wa Kikristo kuyajua na kuyaamini apate kuwa hali njema roho yake; tena ni kumlea hali ya heshima apate kuishi maisha yake katika kicho cha Mungu na dini ya Ukristo; huku mkikumbuka kuwa huu ubatizo watuonya mfano wa hali yetu tuikiriyo: nayo ni ya kumwandama Mwokozi wetu Kristo kwa kielelezo chake alichotuonya, na kufananishwa hali zetu' na hali yake: ili kwamba, kama yeye alivyokufa na kufufuka kwa ajili yetu, sisi nasi tuliobatizwa tuwe wa kufa na kutokana na dhambi, na kufufukia haki; huku tukiendelea katika kuzifisha tamaa zetu mbovu na uharibifu wetu, na kuongea kila siku katika kila lipasalo heshima na uchaji-wa-Mungu wa maisha.
 
Exhortation to godparents

Isipokuwa wale waliomleta kanisani mtoto yule watakapomjibu masiala yake yule Padre kwa kutohakikisha sawasawa, kuwa alibatizwa yule mtoto kwa maji, kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu, (nayo ni mafungu yaliyo lazima katika ubatizo;) ndipo hapo yule Padre humbatiza kwa kuifuata kawaida itanguliayo kabla ya hii, iliyoamriwa ya Kuwa-batiza Watoto mbele ya Watu, isipokuwa zamani za kumtia yule mtoto katika fonti, hutumia maneno haya,

UKIWA hujabatizwa bado, Fulani, mimi nakubatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina.
 


 

 
Conditional Baptism

TARATIBU YA KUBATIZA WATU WAZIMA,

maana, ambao kwamba waweza kujibu wenyewe.

Watakapopatikana watu ambao kwamba wataka kubatizwa, nao' ni watu wazima, ndipo hapo hupewa habari Bishopu, au mtu atakayewekwa kwa kuangalia mambo hayo, kabla ya siku yake muda wa juma moja zima usipungue; na watakaompa habari ni wale wazazi wao, au watu wengine ambao kwamba ni watu wenye akili; ili kwamba iwe. kama ipasavyo, wapate kujulikana kuwa wamefunzwa ya kutosha katika asili za dini ya Kikristo, tena watu hao wahimizwe kujiweka tayari kwa kuomba na kufunga, wapate kupokea Sakramenti hii iliyo takatifu.

Nao watakapoonekana kuwa wafaa, ndipo hapo wale madhamini huwapo tayari (watu wakiisha kutanika kwa siku ya Jumapili waliyoagana yote), wapate kuwaleta karibu ya fonti baada ya kwisha kusomwa Somo la pili, kwamba ni la Sala ya Asubuhi, kwamba ni la Sala ya Jioni, kama atakavyoona yule Padre.

Padre akiisha kusimama palepale, huuliza, kwamba hapa pana mtu aliyebatizwa tangu hapo au hapana: watakapomwambia, Hapana, ndipo hapo yule Padre husema hivi,

ENYI niwapendao sana, kwa hivyo ambavyo watu wote wametungwa mimba na kuzaliwa katika dhambi (nacho kilichozaliwa kwa mwili huwa mwili), na walio katika mwili hawawezi kumpendeza Mwenyezi Mungu, ila wao waishi katika hali ya dhambi, huku wakifanya madhambi mengi ya vitendo; na kwa vile Bwana wetu Kristo asemavyo kwamba, Hawezi mtu kuingia ufalme wake Mwenyezi Mungu asipokuwa ni mtu aliyezaliwa mara ya pili aliyezaliwa uzazi mpya kwa maji na Roho Mtakatifu: mimi hivi nawataka sana mmlingane Mwenyezi Mungu Baba kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ili kwamba kwa wema wake wa ukarimu awajalie watu hawa kupata neno moja ambalo kwa tabia yao ya asili hawawezi kulipata: nalo ni la wao kubatizwa kwa maji na Roho Mtakatifu, na kukaribishwa katika Kanisa lake Kristo, na kufanywa kuwa via vilivyo mumo Kanisani.

Ndipo hapo Padre hunena,

Na tuombe

Ndipo hapo jamii ya waliokutana hupiga magoti.)

EWE Mungu, Mweza-wa-yote, huna mwanzo huna mwisho, wewe kwa rehema zako kuu ulimwokoa Nuhu, uliwaokoa na wa nyumbani mwake, kwa ile safina, ukawaponya wao na kule kuangamia majini: tena uliwaongoza salama watu wako wana wa Isiraeli katikati ya Bahari Nyekundu, kwa kuonya humo mfano wa ubatizo wako mtakatifu: kisha kwa kubatizwa kwake Mwanayo Mpenzi wako sana Yesu Kristo katika mto wa Yorodani, uliyatakasa maji kwa kuosha dhambi kwa maana ya ndani: sisi tuliopo twakuomba sana kwa ajili ya rehema zako zisizo mpaka, uwaangalie watu hawa kwa rehema, uwaoshe na kuwatakasa kwa Roho Mtakatifu: ili kwamba pamoja na kuokoka kwao na ghadhabu zako, wakaribishwe na safinani mwa Kanisa lake Kristo: kisha, kwa vile watakavyokaa katika imani, na kuwa hali ya furaha kwa kutumaini, na kukazwa mashina yao katika kupendana, huku kuyavuka kwao mawimbi ya ulimwengu huu wa dhiki na taabu, wafikilie mwisho katika nchi ya maisha yaendeleayo milele, wapate kutawala pamoja na wewe katika nchi hiyo milele na milele: kwa Bwana wetu, Yesu Kristo. Amina.

EWE Mwenyezi Mungu, mambo yote wayaweza wewe, wala hushindwi na kifo: Msaada wao wote walio na uhitaji, Auni yao jamii ya wakukimbiliao, Maisha yao waaminio, Kufufuliwa kwao waliokufa, pia hayo ni wewe: sisi twakulingana, twawaombea watu hawa, ili hivi wajavyo katika ubatizo wako mtakatifu walipate ondoleo la madhambi yao kwa uzazi mpya wa rohoni. Uwapokee, ewe Bwana kama ulivyoahidi kwa Mwanayo Mpenzi wako sana, pale aliponena, Ombeni mtapewa: tafuteni mtaona: bisheni mtafunguliwa. Na sasa iwe vivyo: utupe sisi tukuombao: tutafutao na tuone: utufungulie mlango sisi tubishao: ili kwamba watu hawa wafurahie baraka iendeleayo milele ya josho lako la mbinguni, na kupata kuufikilia ufalme wa milele uliotuahidi kwa Kristo Bwana wetu. Amina.

Ndipo hapo husimama wale watu, Padre hunena,
 

Baptism of Such as are of Riper Years

Yasikizeni maneno ya Injili iliyoandikwa na mtakatifu Yohana, Mlango wa tatu, mwanzo Kifungo cha kwanza.

PALIKUWA na mtu mmoja katika Mafarisayo jina lake akiitwa Nikodemo, naye ni mkubwa katika Mayahudi. Huyo akamwendea Yesu usiku, akamwambia, Ewe Rabii, twakujua u mwalimu, umekuja kutoka kwa Mungu, kwani hapana awezaye kuzifanya ishara hizo ufanyazo wewe isipokuwa Mwenyezi Mungu yu pamoja naye. Yesu akamjibu akamwambia, Ni kweli, ni kweli, nakuambia, asipozaliwa mtu uzazi utokao juu, asipozaliwa upya mtu, hawezi kuuona ufalme wa Mwenyezi Mungu. Nikodemo akamwambia, Huwaje mtu kuzaliwa ali mzee? Aweza kuingia mara ya pili tumboni mwa mamaye akazaliwa? Yesu akamjibu, Ni kweli, ni kweli, nakuambia, asipozaliwa mtu kwa maji na Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mwenyezi Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili, na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. Sione ajabu ya kuwa nimekuambia, Imewapasa kuzaliwa uzazi utokao juu, kuzaliwa upya. Upepo huvumia upendako, na sauti yake waisikia, ila huuoni utokeako, wala uendeako. Ndivyo awavyo kila aliyezaliwa kwake Roho.

Kisha baadaye husema maneno ya maonyo haya yafuatanayo:

ENYI wapenzi, katika Injili hii mmeyasikia maneno yake halisi Mwokozi wetu Kristo, ya kwamba, asipozaliwa binadamu kwa maji na Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. Nanyi kwa neno hilo mwaweza kutambua Sakramenti hii kuwa haina budi, iwapo yapatikana. Ni kama vile, na wakati wa kupaa kwake mbinguni (kama tusomavyo katika Mlango wa mwisho wa Injili yake mtakatifu Mariko) aliwaagiza wanafunzi wake, akawaambia, Enendeni ulimwenguni mote, mkavihubiri Injili viumbe vyote. Mwenye kuamini na kubatizwa ataokoka: na mwenye kutoamini atahuhukumiwa. Tena neno hilo latuonya wazi manufaa yake yalivyo makuu tuyapatayo mumo kwa ajili ya hayo. Ndiyo maana yake alivyojibu mtakatifu mtume Petero, wakati alipoanziza kuihubiri kwake Injili wengi walichomwa mioyoni mwao, wakamuuliza yeye na mitume wenziwe, Enyi waume ndugu zetu, tufanyeje? akawaambia, Tubieni mkabatizwe kila mtu katika jina la Yesu Kristo, mpate msamaha wa dhambi zenu; nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwani ahadi hiyo ni kwa ajili yenu na kwa ajili ya watoto wenu, na kwa ajili ya wote walio mbali sana, kadiri ya watakaoitwa na Bwana Mungu wetu waje kwake. Tena akawaonya kwa maneno mengine mengi, na kuwasihi, akisema, Jiokoeni wenyewe na kizazi hiki kilicho kombo. Kwani (kama ashuhudiavyo mtume yeyule pahali pengine), ubatizo huo hutuokoa sisi sasa, maana, si kuziepua taka za mwili, bali ni kule kutaka jawabu ya moyo ulio mwema kwa upande wa Mungu, kwa njia ya kufufuliwa kwake Yesu Kristo. Basi msiyatilie shaka kwa lolote, aminini tu ndani ya mioyo yenu, ya kuwa atawakaribisha na kuwawelea radhi watu hawa nao, waliopo hapa wenye kutubu kwa kweli na kumwendea kwa imani; atawajalia kusamehewa madhambi yao na kupewa Roho Mtakatifu: naye atawapa baraka ya uzima wa milele, atawafanya wawe washirika wa ufalme wake wa milele.
    Kwa ajili ya hayo, sisi ambao tu watu tuliopewa hakika hivi, ya. Babaetu aliye mbinguni alivyowawelea radhi watu hawa, kama ilivyowekwa wazi na Yesu Kristo Mwanawe, na tumshukuru kwa imani na ibada ya kweli, tunene,

EWE Mungu Mweza-wa-yote, huna mwanzo huna mwisho: nawe ndiwe Babaetu wa mbinguni; sisi tu miguuni pako, twakuambia asante kwa ulivyotukirimu ya kutuita hata tukapata kuijua neema yako na kuamini kwako; utuongeze ujuzi huo, uikaze mioyoni mwetu imani hiyo milele. Watu hawa uwape Roho wako Mtakatifu, wapate kuzawa uzazi ulio mpya, na kufanywa kuwa watu wa kuurithi wokofu usio mwisho: kwa Bwana wetu Yesu Kristo, aishiye na kutawala pamoja nawe na Roho Mtakatifu, sasa na hata milele. Amina.

Ndipo hapo yule Padre husema na wale watakao kubatizwa maneno haya :

ENYI mpendwao sana, mliokuja hapa kutaka kuupata ubatizo mtakatifu, mmekwisha kusikia mlivyoombewa na waliokutana hapa, ya kwamba Bwana wetu Yesu Kristo akubali kuwakaribisha na kuwabarikia, na kuwaondolea madhambi yenu, na kuwapa ufalme wa mbingu na uzima wa milele. Nanyi mmesikia kwamba Bwana wetu Yesu Kristo ameahidi katika Neno lake lililo takatifu, kuwa atatupa mambo yale yote tuliyomwomba; naye ahadi hiyo hakosi yeye kwa upande wake, ataishika na kuitimiza. Basi kwa ajili ya hayo, baada ya ahadi hiyo akiyoahidi Kristo, imewapasa ninyi kwa upande wenu kuahidi mbele ya mashahidi yenu na jamii ya waliokutana hapa, ya kwamba mtamkataa Shetani na kazi zake zote, na kuliamini daima Neno lake Mwenyezi Mungu lililo takatifu, na kuyashika maagizo yake kwa kutii.

Ndipo hapo yule Padre huwauliza watu watakaobatizwa kila mmoja masiala haya:
 

John 3:1 & Exhortation

Huuliza

JE, wewe wamkataa Shetani na kazi zake zote, na furaha na utukufu visivyofaa vya ulimwengu huu, na kule kutamani-tamani mambo hayo yote kwa shauku; pamoja na tamaa za mwilini, hata uwe wewe kukataa kuvifuata wala kuchukuliwa navyo?
    Hujibu. Navikataa vyote.

Huuliza

JE, wewe waamini kwa Mwenyezi Mungu Baba, Muumba mbingu na nchi?
    Na kwa Yesu Kristo, Mwanawe mzaliwa pekee, Bwana wetu? Na ya kuwa alitungishwa mimba na Roho Mtakatifu, akazaliwa na mwanamwali Mariamu; tena kuwa aliteswa katika enzi ya Pontio Pilato; akasalibiwa, akafa, akazikwa; akashuka akaingia kuzimu, hata siku ya tatu akasimama tena: kisha akapaa na kuingia mbinguni; tena ameketi upande wa mkono wa kuume wa Mwenyezi Mungu Baba, ndiko atakakotoka kuja tena, katika mwisho wa ulimwengu, kuwaamua walio hai hata waliokufa?
    Nawe waamini kwa Roho Mtakatifu; Kanisa takatifu lililo ulimwenguni mote; Ushirika wa watakatifu; Madhambi kusamehewa; Mwili kufufuka; na Maisha ya milele baada ya mauti?
    Hujibu. Haya yote nayaamini sana.

Huuliza

JE, wataka ubatizwe katika imani hii?
    Hujibu. Nataka.

Huuliza

BASI, wataka kuyafuata mapenzi matakatifu ya Mwenyezi Mungu kwa kuyatii, na kuyashika maagizo yake; uyaandame hayo tu siku zote utakazokuwa hai?
    Hujibu. Nitafanya bidii kuyafanya, Mwenyezi Mungu akinisaidia.

Ndipo hapo yule Padre hunena,

EWE Mwenyezi Mungu mwenye rehema, watu hawa uwajalie ya kwamba kwa vile atakavyozikwa Adamu wa kale aliye ndani yao, wapewe mtu mpya kufufuka ndani yao. Amina.
    Uwajalie shauku zote za mwili zife ndani yao; na mambo yote yatakwayo na Roho yawe hai, yaongezeke daima ndani yao. Amina.
    Uwajalie kuwa na uwezo na nguvu, wapate kushinda kwa furaha Shetani na ulimwengu na mwili. Amina.
    Umjalie kila mmoja atakayewekwa nafsi yake kwako wewe pahali hapa kwa utumishi wetu sisi na usongezi wetu sisi, kuvikwa neema za mbinguni na kupewa thawabu ya milele, kwa rehema zako, ewe Bwana Mungu utukuzwaye, uishiye hali umetawala mambo yote, milele. Amina.

EWE Mungu Mweza-wa-yote, wewe uli hai milele; huyo Mwanayo Mpenzi wako sana sana Yesu Kristo, kwa kutusamehe madhambi yetu, alitokwa na maji na damu sambamba katika ubavu wake ulio wa thamani sana, akawapa na amri wanafunzi wake, ya kwenda kuwafanya wanafunzi mataifa wote, na kuwabatiza, kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu; twakuomba utege masikio yako kwetu mkutano wako; nawe uyatakase maji haya yawe njia ya kuosha dhambi kwa maana ya ndani ; uwajalie watu hawa waendao kubatizwa humo hivi sasa, wawe wenye kupokea neema yako iliyotimia, na kukaa daima miongoni mwa wanayo waaminifu wateule wako; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.

Ndipo hapo yule Padre humshika mkono wake wa kuume kila mtu atakaye kubatizwa, hata akiisha kumweka kando ya fonti, pahali pafaapo, kama aonavyo ni vyema, huwataka jina wale madhamini, kisha humvika majini au hummiminia, kwa kunena,
 

Questions of the candidate(s)

FULANI, mimi nakubatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina.

Ndipo hapo yule Padre hunena,

SISI twampokea mtu huyu katika mkutano wa kundi lake Kristo, nasi* twamtia alama ya msalaba, ya kuonyesha kwamba baadaye hataona haya kuikiri imani ya Kristo msalibiwa, na kupigana kiume na dhambi na ulimwengu na Shetani, chini ya beramu yake; na kwendelea kuwa askari mwaminifu na utumishi wa Kristo, hata maisha yake ya duniani yaishe. Amina.

¶ Ndipo hapo yule Padre hunena,

HIVI, enyi ndugu zangu mpendwao sana, tuwaonavyo watu hawa kuwa wamezaliwa uzazi mpya, na kutuliwa katika mwili wa Kanisa la Kristo, na tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa mambo haya mema: nasi tumwombe kwa umoja wa hali, watu hawa wapishe maisha yao yanayosalia duniani kwa mfano wa mwanzo huu.

Ndipo hapo hupiga magoti pia wote na kusema,
 

The Baptism

 

 

* Ndipo hapo yule Padre humpiga alama ya msalaba yule mtu katika japa la uso.

BABAETU uliye mbinguni, Jina lako litakaswe, Ufalme wako na uje, Mapenzi yako yatendeke juu ya nchi, Kama yatendekavyo mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kututosha. Nawe utusamehe makosa yetu, Kama nasi tulivyowasamehe watukosao. Nawe. usitupeleke katika kujaribiwa, Utuokoe maovuni. Amina.

SISI tu miguuni pako twakushukuru wewe, Babaetu wa mbinguni, kwa vile ulivyotujalia ya kuitwa kuja kuijua neema yako na kuamini kwako wewe; utuongoze kujua huku, ututhubutishe katika kuamini huku daima. Watu hawa uwape Roho wako Mtakatifu, ili kwamba, kwa walivyozawa upya na kufanywa kuwa warithi wa wokofu wa milele kwa Bwana wetu Yesu Kristo, waendelee kuwa watumishi kwako, wazifikilie na ahadi zako, kwa yeyule Yesu Kristo Mwanayo, aishiye na kutawala pamoja nawe katika umoja wa yeyule Roho Mtakatifu, milele. Amina.

Wakiisha kusimama wote, yule Padre huwaambia wale madhamini,
 

Lord's Prayer

KWA vile walivyoalhidi watu hawa mbele yenu ninyi madhamini wao, ya kumkataa Shetani na kazi zake zote, na kuamini kwa Mwenyezi Mungu na kumtumikia; inawalazimu ninyi kukumbuka kwamba fungu lenu lililowapasa kila mmoja ni kuwakumbusha jinsi zilivyo kuu nadhiri na ahadi na amana walizozikiri hivi sasa mbele yenu ninyi mashahidi wao mlioteuliwa na wao; nanyi imewapasa kuwataka wajitahidi kujitia katika mafunzo sawasawa na Neno lake Mwenyezi Mungu lililo takatifu; ili kwamba kwa kufanya hivyo wakue na kuongea katika neema na ujuzi wa Bwana wetu Yesu Kristo, na katika ulimwengu huu wa sasa kuishi hali ya kumcha Mungu, na haki, na makini.

Ndipo hapo huendelea kusema, na wale waliobatizwa hapo, akinena,

NANYI mliomvaa Kristo hivi kwa ubatizo, fungu lenu liwapasalo sana (kwa mlivyofanywa ninyi kuwa wana wa Mungu na wa ule mwanga, kwa imani mliyo nayo katika Yesu Kristo) ni la kwenenda kama kutakavyolingamana na mwito wenu wa Kikristo, na kama ilivyowapasa wana wa mwanga; huku mkikumbuka daima ya kuwa huo ubatizo watuonya namna ya dini yetu tuliyoikiri; nayo ni kufuata kielelezo cha Mwokozi wetu Kristo na kulinganishwa naye; hata imekuwa, kama vile yeye alivyokufa akafufuka kwa ajili yetu, imetupasa sisi nasi tuliobatizwa tufe kutokuwa na dhambi, na kufufukia haki, kwa kuyaua daima mambo yetu yote ya tamaa mbovu yaliooza, na kwendelea daima katika mambo ya heshima yote na hali ya kuishi katika kicho cha Mungu kabisa kabisa.

Kila mtu aliyebatizwa kwa jinsi hii ni vyema athubutishwe na Bishopu baada ya kubatizwa kwake akiisha kuwa tayari; ili kwamba apate kukaribishwa Ushirika Mtakatifu.

Na pakiwa na watu ambao kwamba hawakubatizwa katika utoto wao waletwa ili kubatizwa, hawajafika miaka ya kuwa na akili na kutwaa daraka ya nafsi zao, yatosha itumiwapo kawaida ya Kuwabatiza Watoto mbele ya Watu, au (pachelewapo hatari) hutumia kawaida ya Ubatizo wa Faragha Kuwasongezea Watoto Wachanga Nyumbani, isipokuwa hugeuza neno la mtoto palipoandikwa hilo, na kulibadili kuwa mtu kila palipo na haja.

Exhortations

 

Return to the 1662 Book of Common Prayer in Swahili

Web author: Charles Wohlers U. S. EnglandScotlandIrelandWalesCanadaWorld