KAWAIDA YA KUWAPA WATU
KIPA IMARA,
AU KUWEKA MIKONO JUU YA VICHWA VYAO WALIOBATIZWA NA KUPATA UMRI WA KUCHAGUA KATIKA MEMA NA MABAYA.¶ Siku iliyochaguliwa, wote watakaopewa Kipa Imara, wapangwe tayari, wasimame mbele ya Askofu; Yeye mwenyewe asome Dibaji hii ifuatayo (au Mkhudumu mwingine atakaemwamuru).
Kusudi Kipa Imara ipate kukhudumiwa kwa jinsi ya kuwafaa zaidi watu watakaopewa, Kanisa limeona vema kuamuru, Mtu asiletwe kupewa Kipa Imara, asipojua kusema Imani, na Sala ya Bwana, na Amri kumi; na kujibu Maswali, yaliyomo katika Katekisimo. Amri hii yafaa sana ishikwe, illi watoto, wakiisha kupata akili, na kujifunza mambo waliyoahidi Wadhamini wao wakati wa Ubatizo, wao wenyewe wayathubutishe kwa vinywa vyao, wakiyakubali kwa wazi mbele ya Kanisa; tena waahidi ya kuwa watajitahidi siku zote, kwa msaada wa Mungu, kuyashika kwa kweli mambo waliyoyakiri na kuyakubali.
¶ Kiisha, Askofu aseme, Nawaulizeni ninyi, mbele ya Mungu, na machoni pa kusanyiko hili, mnafanya tena ile ahadi na nadbiri iliyofanywa kwa jina lenu wakati wa Ubatizo wenu. Mnaithubutisha ninyi wenyewe, inkikiri ya kuwa imewapasani kuyaamini, na kuyatenda, mambo yale yote waliyoahidi Wadhamini wenu?
¶ Killa, mtu ajibu kwa sauti ya kusikiwa, Nafanya ahadi. ¶ [Kama walibatiziva wangali watu wazima, waulizwe hivi,
Nawaulizeni ninyi, mbele ya Mungu, na machoni pa kusanyiko hili, mnafanya tena ile ahadi mliyofanya wakati wa Ubatizo wenu?
¶ Na killa mtu ajibu, Nafanya ahadi.] Askofu. Msaada wetu u katika Jina la Mungu;
Watu. Aliyeumba mbingu na inchi.
Askofu. Jina la Mungu litukuzwe;
Watu. Tangu leo hatta milele.
Askofu. Mungu, usikie sala zetu.
Watu. Kilio chetu kikufikie.¶ Askofu. Tuombe: Mwenyiezi Mungu uishiye milele, ulipenda hawa watumishi wako wazaliwe marra ya pili kwa Maji na kwa Roho Mtakatifu, ukawapa masamaha ya dhambi zao zote; Bwana, twakusihi, uwatie nguvu kwa Roho Mtakatifu aliye Mfariji, uwazidishie killa siku karama za neema yako; roho ya hekima ca akili; roho ya shauri na nguvu za rohoni; roho ya elimu na utawa; uwajaze, Mungu, roho ya kicho chako kitakatifu, leo na siku zote. Amin.
¶ Kiisha, wutu wakipiga magoti kwa taratibu iribele ya Askofu, awatie mikono Mchivani mmoja mmojci, akinena,
Bwana, umlinde Mtoto wako huyu kwa neema yako ya mbinguni, adumu kuwa wako milele; akazidi killasiku kupewa Roho yakoMtakatifu, hatta aufikie ufalme wako wa milele. Amin.
¶ Kiisha Askofu aseme, Bwana akae nanyi. Watu. Akae na roho yako.
¶ Wote wapige magoti, na, Askofu azidi kusema, Tuombe. Baba yetu, uliye mbinguni, Jina lako liwe takatifu. Ufalme wako uje. Mapenzi yako yatimizwe duniani, Kama yatirnizwavyo mbinguni. Utupe leo riziki zetu. Utusatnehe makosa yetu. Kama sisi tunavyowasamehe waliotukosa. Usitutie majaribuni; Lakini utuokoe maovuni. Amin.
¶ Na Sala liii. Mwenyiezi Mungu uishiye milele, wewe ndiwe ufcutiae moyo tutake na tutende mambo yaliyo mema, na yakupendezayo wewe uliye Mwenyiezi; Tunawaombea hawa watumishi wako; tukiwafuatisha Mitume wako watakatifu, tumeweka mikono yetu juu ya vichwa vyao, illi kuwajulisha kwa ishara bli upendeleo na wema wako kwao. Mkono wako, Baba, uwe juu yao daima; Roho yako Mtakatifu awe nao siku zote; uwaongoze walijue na kulif uata Neno lako takatifu, illi mwisho waupate uzima wa inilele; kwa Yesu Kristo Bwana wetu, aishiye na amilikiye pamoja nawe, na Koho Mtakatifu, Mungu mmoja, sasa na milele. Amin.
Bwana Mwenyiezi, Mungu wa milele, ukubali, twakusihi, kutuongoza, kututakasa, na kututawala, miili yetu na roho zetu, katika njia ya sharia zako, na katika kutenda uliyotuagiza; illi, kwa ulinzi wako, tuhifadhike mwili na roho, hapa duniani na akhera; kwa Bwana na Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Amin.
¶ Kiisha Askofti, aivabariki, akisema, Baraka ya Mungu Mwenyiezi, Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, iwe kwenu, ikae nauyi daima. Amin.
¶ Mtu asikaribishwe katika Ushirika Utakatifu, mpaka aishe kupewa Kipa Imara, au yu tayari, tena anataha kupewa Kipa Imara.
Project Canterbury